NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Hamsini na Tatu – Tarehe 26 Juni, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Tukae. Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU WA MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:- Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019). MHE. MASHIMBA M. NDAKI – MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI:- Maoni ya Kamati ya Bajeti kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DAVID E. SILINDE – NAIBU MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO:- Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019). NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. NEEMA MSANGI:- KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali, Waheshimiwa Wabunge tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, sasa aulize swali lake. Na. 459 Mikataba ya Ajira kwa Madereva wa Malori na Mabasi MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itasimamia na kuhakikisha Madereva wa Malori na Mabasi wanapata Mikataba ya Ajira ili kuboresha maslahi yao na kuongeza ufanisi katika Utumishi wao? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kushughulikia haki na maslahi ya Madereva nchini Tanzania, Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kutatua changamoto zinazowakabili madereva ambapo mnamo tarehe 2 Mei, 2015 Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliagiza iundwe Kamati ya Kudumu ya Kutatua Matatizo katika Sekta ya Usafirishaji chini ya Uenyekiti wa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi. Aidha, Kamati ndogo chini wa Uenyekiti wa iliyokuwa Wizara ya Kazi na Ajira iliundwa kwa ajili ya kushughulikia haki, maslahi na mkataba wa ajira wa Madereva. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva na Viongozi wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji nchini waliufanyia marekebisho na kuuboresha Mkataba wa ajira wa Madereva uliokuwepo. Mkataba ulioboreshwa uliidhinishwa na wadau katika kikao kilichofanyika tarehe 23 Juni, 2015 na ilikubalika kwamba Mkataba huo uanze kutumika rasmi tarehe Mosi, Julai, 2015. Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, masharti yamewekwa kwamba kila Mmiliki wa basi au lori anayeomba leseni ya usafirishaji toka SUMATRA ni lazima awasilishe mikataba ya ajira ya Madereva wake ambayo imehakikiwa na Maafisa wa Kazi wa maeneo husika. Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kusimamia majadiliano baina ya Vyama vya Wafanyakazi, Madereva na Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji ili kuwawezesha kufikia muafaka wa viwango vya posho za safari na kujikimu wakati Madereva wanaposafiri ndani na nje ya nchi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, swali la nyongeza. MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya nyongeza. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini bado kuna malalamiko makubwa sana kwa Madereva wa malori na mabasi na karibu asilimia 90 ya Madereva hao hawana mikataba ya kazi na kwa sababu Serikali inasema kwamba Mikataba yao ilitakiwa iboreshwe toka mwaka 2015 na mpaka sasa mikataba yao bado haijaboreshwa na bado hawajapewa mikataba. Je, Serikali ina mpango gani wa kuharakisha jambo hili ili wafanyakazi hao waweze kufanya kazi yao vizuri kwa sababu wakiwa na mawazo sana wanaweza wakasababisha ajali na Watanzania wengi wakapoteza maisha? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa sisi ambao tunaishi mipakani na mmeona kuna migomo mingi sana inatokea pale Tunduma watu Madereva wanapaki malori kwa sababu tu ya migongano kati ya wamiliki wa mabasi na malori kwa ajili ya mikataba hiyo? Sasa Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba jambo hili linakwisha haraka kwa sababu ni muda mrefu sasa na Serikali ipo, inatoa majibu humu Bungeni lakini utekelezaji unakuwa hakuna? Ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Frank Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, maswali yake nitayajibu yote kwa mkupuo. Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na katika ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa akiwa Kahama mwaka 2015 juu ya Mikataba ya Wafanyakazi na hasa Madereva, Serikali inakuja na mpango mkakati ufuatao, hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwataka Wamiliki wote wa Mabasi na Malori ambao watakwenda kuomba SUMATRA leseni ya usafirishaji wahakikishe kwamba 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wanawasilisha na Mikataba ya Wafanyakazi kama eneo la kwanza la kuhakikisha kwamba Madereva hawa wanapata mikataba yao. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza hili, Serikali tumekuja na mkakati tofauti tumeona kwamba mkakati huu ulikuwa una mianya ya utekelezaji wake hivyo, siku mbili hizi zijazo Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, watatoa tamko na maelekezo ya kuanzia tarehe moja mwezi Julai ni hatua gani zitachukuliwa. Kuanzia hapo nina hakika kwa mkakati huo ambao wameuweka ni kwamba kila Dereva wa nchi hii atakuwa na mkataba wake na tutahakikisha kwamba pia kila Mmiliki wa Chombo cha Usafiri anafuata masharti ya sheria kama Kifungu cha 14 cha Sheria za Ajira na Uhusiano Kazini kinavyosema. Kwa hiyo, nimwondoe tu hofu Mbunge kwamba si maneno tu lakini mkakati umeshawekwa vizuri kabisa na tumekaa na wenzetu wa Jeshi la Polisi muda siyo mrefu kuanzia tarehe Mosi, Julai mtaona cheche za Wizara. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo tuna maswali mengi sana, kwa hivyo tutaendelea na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa Manonga, sasa aulize swali lake, kwa niaba yake Mheshimiwa Mwanne Mchemba. Na. 460 Ujenzi wa Vituo vya Afya vya Simbo, Ziba, Choma cha Nkola na Igurubi kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. SEIF K. GULAMALI) aliuliza:- Wilaya ya Igunga ilipata ufadhili wa Benki ya Dunia wa ujenzi wa Vituo vya Afya vya Simbo, Ziba, Chomachankola na Igurubi ambapo Vituo vya Afya vya Ziba, Chomachankola na Igurubi vimekamilika na vifaa tayari vipo japo majengo na vifaa katika Kituo cha Afya cha Chomachankola na 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Igurubi bado havijaanza kufanya kazi; Kituo cha Afya cha Simbo bado hakijakamilika na vifaa havipo na Wafadhii walishakabidhi Halmashauri bila kukamilisha ujenzi huo:- Je, Serikali inachukua hatua gani kujua nini kilichojificha juu ya Mradi huo kukabidhiwa bila kukamilika? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa Manonga, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa Wilaya ya Igunga ilipata ufadhili wa Benki ya Dunia kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya Simbo, Ziba, Chomachankola na Igurubi. Sababu kuu ya kushindwa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati ilitokana na makadirio ya chini ikilinganishwa na gharama halisi za kukamilisha ujenzi. Ili kukamilisha ujenzi wa Vituo hivyo kwa kuzingatia ramani mpya, Serikali ilitoa jumla ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya Simbo na Igurubi ambapo kila kituo kilipatiwa shilingi milioni 400. Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Simbo kimekamilisha ujenzi wa majengo ya upasuaji na nyumba ya mtumishi na sasa vifaa tiba vinaendelea kuletwa. Aidha, Kituo cha Afya Igurubi kinaendelea na ujenzi wa majengo manne ambayo ni Maabara, Jengo la Wazazi, Jengo la Kufulia na Jengo la Kuhifadhia maiti. Majengo yote haya yapo katika hatua za ukamilishaji. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwanne Mchemba, swali la nyongeza. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nami naomba niulize swali dogo la nyongeza, kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali yangu ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri ambayo inafanya kukamilisha Vituo vya Afya ambavyo mimi mwenyewe kama Mjumbe wa Kamati hiyo nimejionea kwa macho yangu mwenyewe. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu sasa, kwa kuwa Kituo cha Afya Simbo kimekamilika na bado hakijaanza kazi, je, ni lini sasa hivyo vifaa tiba vitapelekwa haraka sana ili kuwapunguzia adha wagonjwa ambao wanakimbilia kwenda Hospitali ya Private ya Nkinga? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mchemba,
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages266 Page
-
File Size-