Majadiliano Ya Bunge ______
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha kumi na Sita – Tarehe 29 Juni, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta ) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO:- Hotuba ya bajeti ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2009/2010. MHE. RAMADHANI A. MANENO (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI WA KATIBA SHERIA NA UTAWALA):- Taarifa ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka 2008/2009 pamoja na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya mwaka wa fedha 2009/2010. MHE. RIZIKI OMAR JUMA - MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA MAKAMU WA RAIS:- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya ya Makamu wa Rais, kwa mwaka 2009/2010. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA:- Randama za Makadirio ya Mafungu na Kasma za Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2009/2010. 1 MASWALI NA MAJIBU Na. 119 Miji Midogo ya Kongwa na Kibaigwa kuwa Mamlaka ya Miji Midogo. MHE. JOB Y. NDUGAI aliuliza:- Kwa kuwa Serikali ilishaamua na kuagiza kuwa Miji Midogo ya Kongwa na Kibaigwa sasa iwe na hadhi ya Mamlaka ya Miji Midogo. Je, kwa nini hadi sasa Mji wa Kongwa ambao ni Makao Makuu ya Wilaya haujawa Mamlaka ya Mji Mdogo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Mbunge wa Kongwa, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mamlaka za Miji Midogo ya Kongwa na Kibaigwa zilitangazwa katika Tangazo la Serikali Na. 353 la tarehe 17/9/2004. Baada tangazo hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambamo Mamlaka za Miji midogo hiyo imo iliteua Wajumbe waliokwenda Wilaya ya Kondoa kujifunza namna ya kuunda na kuendesha Mamlaka za Miji midogo. Aidha hoja ya kuanzisha Mamlaka za Miji midogo ya Kongwa na Kibaigwa ilijadiliwa katika kikao cha Kamati ya Uchumi, ujenzi na mazingira na kisha kuwasilishwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani mwezi Machi, 2006. Kikao hicho kiliweka azimio la kuanzisha Mamlaka hizo kwa awamu, kwa kuanza na Mamlaka ya Mji mdogo wa Kibaigwa na baadae Kongwa. Mheshimiwa Spika, uamuzi huo ulifanyika kwa kuzingatia kwamba kuanzisha Mamlaka mbili za Miji midogo kwa wakati mmoja ulikuwa mzigo mkubwa kwa Halmashauri ya Wilaya ambayo mapato yake wakati huo yalikuwa chini ya shilingi milioni 80/- kwa mwaka na upungufu mkubwa wa watumishi na miundombinu mingine kama vile majengo ambayo yanahitajika kwa ajili ya Ofisi za Mamlaka hizo. Mheshimiwa Spika, baada ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mji mdogo wa Kibaigwa ni vema sasa , Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ikaagiza kuanza mchakato wa kuanzisha Mamlaka ya Mji mdogo wa Kongwa. Aidha inashauriwa kutumia uzoefu 2 ulipatikana katika uanzishwaji wa Mamlaka ya Mji wa Kibaigwa katika kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kongwa ambao ni Makao Makuu ya Wilaya. MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana nina maswali mawili madogo ya nyongeza,la kwanza inaelekea Serikali imeiachia Halmashauri ya Kongwa peke yake jukumu na mzigo wa kuanzisha mamlaka ya mji mdogo, lakini swali langu haswa ni kwamba kwa kuwa tuna Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi wa kumi mwaka huu na Uchaguzi wa miji midogo unahusisha katika muundo wake mitaa, na siyo vitongoji kama ilivyo sasa kwa vijiji kwa maana ya mji wa Kongwa kama unakuwa mji mdogo. Je kati ya sasa na mwezi wa kumi maandalizi haya yanatosha kwa maana ya kukubalika mitaa yake ili uchaguzi wa mwezi wa kumi wa Kongwa mjini kwa maana ya mamalka ya mji mdogo uwe katika mitaa na siyo vitongoji? La pili, katika miji midogo ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya kama hapa Dodoma Kongwa, Mpwapwa, Kondoa isingekuwa vema kama katika miji midogo hiyo pakawekwa lami angalau ya kilometa tatu nne pale mjini katikati ikizingatiwa kwamba kwa mji wa Kongwa lami ya kwanza iliwekwa katika mji wa Kongwa mwaka 1947, leo hakuna chochote,Kongwa hakuna chochote, Mpwapwa hakuna chochote na Kondoa pia. Je, haiwezi kuwa ni mpango mzuri kwa kilometa tatu,nne, tano zikawekwa lami katikati ya miji hii ili kuifanya miji hiyo midogo iitwe miji kweli? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Job Ndugai, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika liko moja hili la kwanza analozungumzia kwamba Kongwa nayo iweze kuwa mji kamili na kwamba utaratibu huo umekamilika kati ya sasa na mwezi wa kumi, na kwamba sasa uchaguzi wa Serikali za mitaa pale uweze kufanyika. Sijui jinsi ambavyo hii inaweza ikafanyika kwa sababu hili lilikuwa linakiwa liwe limeshafika, limeshakamilikika. Kipindi kilichobaki hapa sasa hivi ni almost tumemaliza mpangilio wenyewe ninachoweza kabisa labda Kibaigwa, lakini Kongwa kwamba utaiweka katika utaratibu sasa hivi hapa labda niseme vizuri msimamo wa Serikali katika jambo, hili tulisha kubaliana hapa na lilishawekwa wazi wakati wa Mheshimiwa Ngwilizi, mimi nakumbuka nilikuwa nimekaa pale nasikilza vizuri. Mheshimiwa Spika, kwamba popote pale ambapo pana makao makuu ya Wilaya tulishaanza kupatambua kama mji mdogo. Lakini ukitaka kufika hatua hiyo lazima mkutane wenyewe wenye mji mdogo ule, lazima mkutane wenyewe wenye Halmashauri yenyewe mkae mzungumze mkubaliane, kama tulivyozungumza hapa tuliona kwamba utakuwa ni mzigo Kongwa nayo kuingizwa katika mpango huu kwasababu Kongwa nayo ikiwa mji mdogo Bajeti yake itatokana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. Sasa kama Mheshimiwa Job Ndungai anafikiri kama anaweza aka- fast truck habari zote harakaharaka ikaja bado jambo hili linabakia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, ndiyo inatakiwa iamue lakini mimi natakiwa nimwambie kwamba hatuna 3 objection yoyote wala hatuna tatizo lolote kuanzisha mji wa Kongwa. Kwa sababu kimsingi maamuzi yale yalishafanyika kwa hiyo ni suala tu la kukaa. Mheshimiwa Spika, la pili,kuhusu kwamba tuwe na kilomita mbili au tatu katika miji hii midogo. Hii ni uamuzi wako, mheshimiwa Spika pale kwako Urambo mkiamua ninyi kwamba mnataka kuweka kilomita mbili tatu za lami pale mtapima. Mtaangalia kama mtaona ni kipaumbele mtafanya hivyo lakini mimi nikiangalia bajeti inavyokwenda hapa; na juzi nilimsikia Mheshimiwa Waziri Mkuu akizungumza habari hizi za kilomita mbili tatu kule ndani wakati kuna maeneo mengine yamekuwa hayajaungashwa na nini, nilimsikia akijibu yale. Sasa lakini mimi nasema kama Kongwa wanafika mahali wakaona ni kipaumbele wakaamua kuwa waweke kilomita mbili, tatu hakuna mtu atakaye wapinga kwa sababu wao wamepewa mamlaka ya kufanya hivyo. MHE. MICHAEL L. LAIZER: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kuna Wilaya mpya kama Longodo , Siha na Wilaya zingine ambazo bado hazina hadhi ya kuwa miji ya Wilaya. Je, Naibu Waziri atakubaliana nami kwamba kwa sasa tuwe na mitaa badala ya kuwa vitongoji na uchaguzi ukija tayari umekwisha kamilika kuwa miji midogo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, sijui kama nitakuwa nimempata vizuri sana Mheshimiwa Lekule Laizer, kwa sababu hapa vijiji na vitongoji hivi unavipata tu katika Halmashauri ya Wilaya . Unapoanza kuzungumza habari ya mtaa unaanza kuzungumza habari ya mahali ambapo pamepimwa , mahali ambapo ni pa mji mji tumepakubali kama mamlaka ya mji mdogo, na ndio maana mkishakubalika mnakuwa nyinyi ni mji mdogo na vijiji vinafutika pale na wanaokwenda sasa pale ni madiwani wawili halafu wanakwenda Wenyeviti wa vitongoji ndio wanakwenda pale kwa kweli suala lile linakuwa limekwisha pale. Mheshimiwa Spika, sasa huwezi ukaitisha mkutano wa mtaa na waende wakafanye mkutano wa mtaa na waende wakafanye uchaguzi wa mtaa pale wakati mamlaka ile haijatambullika kama mamlaka ya mji mdogo. Kwahiyo tulikuwa tunashauri hapa na nina mshukuru sana kwamba anaizungumzia hata na Wilaya yangu ya Siha kwamba turuhusiwe kufanya hivyo lakini lazima tufuate utaratibu huo kwanza tuka – declear pale kwamba ni mji mdogo ndipo sasa paweze kujulikana kama Halmashauri ya mji mdogo na uweze kupata mitaa mle ndani yake lakini hili suala la mchakato wenyewe utakavyokwenda pale Wilayani. Na. 120 Kuchimba Visima vya Mji kwa Matumizi ya Shuleni MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- 4 Kwa kuwa shule ya sekondari ya Kipili ambapo ipo katika Kata ya Kipili Tarafa ya Kilanda Wilaya ya Nkasi haina bomba la maji wala kisima kwa matumizi ya shule , na kwa kuwa hali hiyo husabaisha mlipuko wa magonjwa hatari na kuliwa na mamba. Je ,Serikali ina mpango gani wa kuona wa kuchimba visima katika shule zilizoko Rukwa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe Mbunge wa viti maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa mwaka fedha wa 2008/2009 kupitia mpango wa quick wins Serikali ilianza kutekeleza mpango wa kuchimba kisima kirefu kimoja katika shule ya Sekondari Kipili hali ya uekelezaji hadi sasa imefikia hatua mbalimbali kama ifuatavyo:- .Uchunguzi wa sehemu ya kuchimba kisima (geophisical survey) umekamilika. Ununuzi wa pampu ya mkono (India mark II) umekamilika. .Mkandarasi wa kuchimba amepatikana ambaye ni RWE- Rukwa, maandalizi ya kupeleka mitambo (mobilization )yako kwenye hatua za mwisho. Mheshimiwa Spika, pamoja na mikakati iliyopo ya kuipatia shule ya sekondari Kipili maji kwa kuchimba kisima kirefu kupitia mpango wa quick wins serikali inafanya mpango kuhakikisha kuwa shule zote za sekondari Mkoani zinapata huduma ya maji. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kueleza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika shule za sekondari Wilayani Nkasi . Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ina jumla ya shule sekondari 18 ambapo kati ya hizo sekondari 10 za Nkasi ni Mkole, Mtenga, Kabwe, Chala, Milundikwa, Kipande, Wampembe na Kala zinahuduma ya maji.Huduma ya maji inapatikana kupitia kutumia njia ya Kupitia mifumo ifuatayo:- (i) Visima virefu.