Majadiliano Ya Bunge ______

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Majadiliano Ya Bunge ______ Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Saba – Tarehe 17 Juni, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Halmashauri ya Biashara ya Nje kwa Miaka ya Fedha ya 2005/2006 na 2006/2007 (The Annual Report and Audited Accounts of the Board of External Trade (BET) for the Financial Years 2005/2006 and 2006/2007). MASWALI NA MAJIBU Na. 65 Ujenzi wa Barabara za Lami Singida Mjini MHE. DIANA M. CHILOLO (K.n.y. MHE. MOHAMMED G. DEWJI) aliuliza:- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea Mkoa wa Singida kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 4 Agosti, 2009 aliahidi kuunga mkono juhudi za Manispaa ya Singida Mjini, katika ujenzi wa barabara za lami ndani ya Manispaa. Je, ahadi hiyo itatekelezwa lini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Gulam Dewji, Mbunge wa Singida Mjini, kama ituatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea Mkoa wa Singida tarehe 4 Agosti, 2009 alitoa ahadi ya kuunga mkono juhudi za Manispaa ya Singida katika ujenzi wa barabara za lami. Katika mwaka 2010/2011 Halmashauri ilituma maombi maalum ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo. Hadi sasa shilingi milioni 300 zimetolewa na kazi zilizofanyika ni ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 1.07 na kazi zinazoendelea ni kuimarisha mifereji katika barabara zilizokamilika. Ufuatiliaji wa fedha shilingi milioni 300 unaendelea ili kuendelea na ujenzi wa barabara kilomita 1 kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Salmin na Lumumba iliyoko katika Kata ya Itende. Barabara zilizojengwa ni kama zifuatazo:- (i) Mtaa wa Msikiti km. 0.450 (ii) Mtaa wa Kanisa Katoliki km 0.310 (iii) Mtaa wa Mwenge km 0.165 (iv) Mtaa wa Faraja km 0.145 Jumla km 1.070 Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Bajeti ya mwaka 2011/2012 Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeidhinishiwa shilingi milioni 745 toka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ya barabara. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kujenga barabara za Halmashauri, hususan za Manispaa ikiwemo ya Singida kwa kiwango cha lami kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu. MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina swali moja dogo la nyongeza. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba ombi la Manispaa ilikuwa ni shilingi milioni 600 na wameshatuma shilingi milioni 300. Na kwa kuwa katikati ya Manispaa barabara ni nyingi na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo amejitahidi kuweka taa za barabarani mji wote. Na kwa kuwa barabara za lami bado nyingi ambazo hazijatengenezwa mjini kati ili hadhi ya taa hizo ziendane na barabara. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuwaambia wananchi wa Singida Mjini kwamba kupitia Bajeti hii shilingi milioni 300 zilizobakia zitatengwa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru na kumpongeza sana Mbunge Dewji kwa kazi 2 nzuri ambayo ameifanya katika Manispaa ile ya Singida na wenzake wote ambao anashirikiana nao. Leo asubuhi nilikuwa nazungumza na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Paschal Mabiti wananchi wa Singida wenyewe wanasema wanamshukuru sana Rais kwamba ametekeleza ahadi yake kwa maana ya kazi iliyofanyika pale na ndiyo maana tumezungumza hapa. Shilingi milioni 300 ambazo zinadaiwa hakuna ubishi hapa huwezi ku-debate hapa maelekezo ya Rais, sina ubavu huo. Hizo fedha tutazitafuta tutazipeleka pale kwenda kumalizia kazi iliyobakia pale. Hapa sisi tunatekeleza maelekezo ya Rais kama ilivyotamkwa. Kwa hiyo Mheshimiwa Diana Chilolo uwe na amani moyoni mwako. Hii kazi itafanyika, tena itafanyika vizuri mpaka mwenyewe utafurahi. (Makofi) MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri kuonyesha dhamira ya kufuatilia ahadi za Rais. Kwa kuwa swali la msingi lilitokana na ahadi ya Rais aliyoitoa kwenye Mkutano wa hadhara na kwa kuwa kwa spirit hiyo hiyo ya Mheshimiwa Naibu Waziri ya kufuatilia kwa karibu ahadi za Mheshimiwa Rais. Je, Naibu Waziri yuko tayari vile vile kufuatilia ahadi ya Mheshimiwa Rais ya tarehe 24 Mei, 2010 aliyoitoa kwenye Mkutano wa hadhara Kimara Mavurunza ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kimara mpaka Segerea kupitia Bonyokwa ambayo iko chini ya Manispaa inayounganisha Manispaa mbili za Kinondoni na Ilala yeye kama Kiongozi wa TAMISEMI? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hakika kabisa kwamba kila akisimamishwa hapa kila mmoja atasema kwamba kuna ahadi za Serikali kwa maana ya Rais. Nimesema na juzi tumejibu tena hapa sisi hapa hatumfuati Rais tukamwambia fedha ziko wapi. Rais ameshapitisha bajeti tumeileta hapa ndiyo hii. Nyie tusaidieni kupitisha bajeti hapa, ndiyo kazi inayotakiwa hapa. Sisi tuna orodha na kitabu kimetengenezwa cha ahadi zote zilizotolewa na Rais nchi nzima. Kama nilivyosema Rais akishatoa ahadi sisi kazi yetu ni kutekeleza ahadi za Rais. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mnyika kama unataka tukitoka hapa twende Ubungo ili unipeleke kwenye hiyo barabara lakini nitakwenda kuangalia kwenye Bajeti yenu nyinyi kama mmeliangalia hili ili tuweze kujua jinsi tutakavyofanya. Lakini nataka nimthibitishie kwamba hatuna tatizo na ahadi yoyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais. MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na swali lililofuata nalo linaulizwa na Mheshimiwa Vicky Paschal Kamata, Mbunge wa Viti Maalum na linaelekezwa tena kwenye Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Na. 66 3 Mikoa Mipya Kuanza Kazi Rasmi na Wakuu wa Mikoa Kuteuliwa MHE. VICK P. KAMATA aliuliza:- Mheshimiwa Rais ameridhia kuanzishwa kwa Mikoa mipya ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Geita; wananchi wa Geita wameupokea uamuzi huo kwa furaha na matumaini makubwa sana. (a) Je, ni lini Mikoa hiyo itaanza kazi rasmi na Viongozi wa Mikoa kuteuliwa? (b) Je, Serikali imejiandaa vipi kuiendeleza Miji Mikuu ya Mikoa mipya katika maeneo ya huduma za kijamii, kiuchumi na miundombinu ambayo awali ilikuwa Miji Mikuu ya Wilaya? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vicky Paschal Kamata, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutumia fursa hii kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba wakati Serikali inatangaza kuanzishwa kwa Mikoa na Wilaya mpya ilikuwa ni kusudio la kuanzisha maeneo mapya ya utawala ambayo hatimaye yatawezesha kuanza rasmi kwa Mikoa na Wilaya hizo. Hatua iliyokwishafikiwa ni kuhakiki mipaka ya maeneo yote yanayopendekezwa kuanzishwa ikiwa ni pamoja na wananchi wa maeneo hayo kushirikishwa kuhusu dhamira hiyo ya Serikali. Hivyo, Mikoa na Wilaya mpya zitaanza rasmi Serikali itakapotoa Tangazo la kuanzishwa kwake (Government Establishment Notice). Uteuzi wa Viongozi na watumishi utafanyika zitakapokamilika taratibu za kisheria za uanzishaji Mikoa na Wilaya. Aidha, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Mheshimiwa Rais Mamlaka na Madaraka ya kuanzisha mamlaka mpya za Wilaya na Mikoa kwa wakati na namna ambavyo atakavyoona inafaa. (c) Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukidhi huduma za kijamii, kiuchumi na miundombinu katika maeneo yanayohusika, Serikali, Benki ya Dunia pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo imeandaa Mpango wa Muda Mfupi na wa Kati wa uendelezaji wa Majiji 3, Manispaa 15 na Miji Midogo 14 nchini. Geita ni moja ya maeneo ambayo yamefanyiwa maandalizi ya ukuaji wa Miji yenye hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa. Shughuli zitakazozingatiwa ni pamoja na upangaji Miji, mazingira na usafi, barabara, mifereji na uboreshaji wa mapato ya Miji hiyo. 4 MHE. VICK P. KAMATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa taarifa zisizo rasmi ilikuwa inafahamika kwamba kuanzishwa kwa mikoa hii kunasubiri Bajeti. Je, hiki kigugumizi cha Serikali ni kwa sababu hakuna fungu maalum lililotengwa kwa ajili ya kuanzishwa kwa mikoa hiyo? Pili, je, Serikali inawaambia nini wananchi wa Geita waliokuwa na matumaini makubwa sana ya kuanza kupata huduma zao za kimkoa na sasa kumbe uanzishaji wa mikoa hii unasuasua? Ahsante sana. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri nafikiri ujibu tu kwa mikoa yote ambayo inaanzishwa kwa utaratibu huo. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kama Mbunge mpya wa Viti Maalum anayekuja hapa. Nampongeza kwamba anafuatilia mambo haya kwa karibu sana. Yaani kwa kweli hilo hatuna tatizo nalo tunampongeza kwamba anafuatilia ni Mbunge wetu anatoka kule Geita. Yeye hakupata nafasi ya kuwa Mbunge wa Viti Maalum ni kwa tiketi ya Geita, sasa huko ni kusuasua. Yaani mkoa ule wa Geita ambao unazungumzwa hapa na ndio umemleta humu ndani. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, dada yangu Vicky Kamata nataka nikuthibitishie Rais tumemsikia, Waziri Mkuu tumemsikia, Mkuchika tumemsikia sisi wote Taifa zima tumesikia lile lilikuwa ni kusudio linatolewa notice yake. Sasa kuna establishment ukiingiza voti humu ndani Mheshimiwa Mkulo atakuambia hivi,
Recommended publications
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 27 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kwa Mwaka 2012/2013 (The Annual Report and Accounts of Arusha International Conference Centre for the Year 2012/2013). Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. BETTY E. MACHANGU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. ABDULKARIM E.H. SHAH (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
    [Show full text]
  • Conference Report
    2 ND GOPAC GLOBAL CONFERENCE Arusha, Tanzania September 19-23, 2006 FINAL REPORT GLOBAL ORGANISATION OF PARLIAMENTARIANS AGAINST CORRUPTION: 2ND GLOBAL CONFERENCE Acknowledgements The Global Organisation of Parliamentarians Against Corruption wishes to thank the following organisations for their contributions to the 2nd Global Conference: Parliament of Tanzania African Parliamentarians Network Against Corruption (APNAC) Barrick Gold Canadian International Development Agency (CIDA) US Agency for International Development (USAID) World Bank Institute (WBI) Events Hosts Dr. Zainab A. Gama, MP, Chair, APNAC – Tanzania Arusha Regional Commissioner Col (Rtd). Samuel Ndomba H.E. Dr. Ali Mohamed Shein the Vice President of the United Republic of Tanzania Hosted by Hon. Samuel Sitta, MP – Speaker of the National Assembly Guest Speakers Deputy Barrister Emmanuel Akomaye, Economic and Financial Crimes Commission of Nigeria Doris Basler, Transparency International Hon. Ruth Kavuma, MP, Vice Chair, APNAC Uganda Mr. Paul Wolfowitz, President, World Bank (Taped message) Conference and Workshop Speakers Conference Chair: John Williams MP (Canada) Edward Doe Adjaho, MP (Ghana) Naser Al Sane, MP (Kuwait) Edgardo Angara, Senator (Philippines) Stella Cittadini, Senator (Argentina) Roy Cullen, MP (Canada) César Jauregui, Senator (Mexico) Edith Mastenbroek, MEP (Netherlands) J.T.K. Green-Harris, MP (Gambia) Mary King, Senator (Trinidad and Tobago) Omingo Magara, MP (Kenya) Augustine Ruzindana, Former MP (Uganda) Willibroad Slaa, MP (Tanzania) Navin Beekarry (IMF) Giovanni Gallo (UNODC) Scott Hubli (UNDP) Latifah Merican Cheong (World Bank) Carmen Lane (DAI) Luis Gerardo Villanueva, Former MP (Costa Murray Michel (Egmont Group and Rica) FATF) Patrick Moulette (IMF) Keith Schulz (USAID) Ingeborg Schwarz (IPU) Emiko Todoroki (WB) Frederick Stapenhurst (WBI) Stuart Yikona (WB) GOPAC wishes to thank the following individuals for their significant contribution to the conference and its administration: Canadian High Commission - Tanzania Parliament of Tanzania H.E.
    [Show full text]
  • Bunge Newsletter
    BungeNe ewsletter Issue No 008 June 2013 New Budget Cycle Shows Relavance For the first time in recent Tanzania history the engage the government and influence it make sev- Parliament has managed to pass the next financial eral tangible changes in its initial budget proposals. year budget before the onset of that particular year. This has been made possible by the Budget Commit- This has been made possi- tee, another new innovation by Speaker Makinda. ble by adoption of new budget cycle. Under the old cycle, it was not possible to influence According to the new budget cycle, the Parliament the government to make changes in budgetary allo- starts discussing the budget in April as opposed to cations. That was because the main budget was read, old cycle where debate on the new budget started on debated and passed before the sectoral plans. After June and ends in the first or second week of August. the main budget was passed, it was impossible for the MPs and government to make changes in the When the decision was taken to implement the new sectoral budgets since they were supposed to reflect budget cycle and Speaker Anne Makinda announced the main budget which had already been passed. the new modalities many people, including Mem- bers of Parliament, were skeptical. Many stakehold- These and many other changes have been made possi- ers were not so sure that the new cycle would work. ble through the five components implemented under the Parliament five years development plan. “Govern- But Ms Makinda has managed to prove the doubt- ment and Budget Oversight and Accountability is one ers wrong.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • Rumours and Riots: Local Responses to Mass Drug Administration for the Treatment of Neglected Tropical Diseases Among School-Ag
    Rumours and riots: Local responses to mass drug administration for the treatment of neglected tropical diseases among school-aged children in Morogoro Region, Tanzania A thesis submitted for the degree of Doctor of Philosophy by Julie Dawn Hastings Department of Anthropology School of Social Sciences Brunel University January 2013 Abstract In August 2008, a biomedical intervention providing free drugs to school aged children to treat two endemic diseases – schistosomiasis haematobium and soil- transmitted helminths - in Morogoro region, Tanzania, was suspended after violent riots erupted. Parents and guardians rushed to schools to prevent their children taking the drugs when they heard reports of children dying in Morogoro town after receiving treatment. When pupils heard these reports, many of those who had swallowed the pills began to complain of dizziness and fainted. In Morogoro town hundreds of pupils were rushed to the Regional Hospital by their parents and other onlookers. News of these apparent fatalities spread throughout the region, including to Doma village where I was conducting fieldwork. Here, protesting villagers accused me of bringing the medicine into the village with which to “poison” the children and it was necessary for me to leave the village immediately under the protection of the Tanzanian police. This thesis, based on eleven months fieldwork between 2007 and 2010 in Doma village and parts of Morogoro town, asks why was this biomedical intervention so vehemently rejected? By analysing local understandings and responses to the mass distribution of drugs in relation to the specific historical, social, political, and economic context in which it occurred, it shows that there was a considerable disjuncture between biomedical understandings of these diseases, including the epidemiological rationale for the provision of preventive chemotherapy, and local perspectives.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tano - Tarehe 16 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU: Hotuba ya Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MHE. MARGARETH A. MKANGA (k.n.y. MHE. OMAR S. KWAANGW’ - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 239 Majimbo ya Uchaguzi MHE. JAMES P. MUSALIKA (k.n.y. MHE. DR. WILLIAM F. SHIJA) aliuliza:- Kwa kuwa baadhi ya Majimbo ya Uchaguzi ni makubwa sana kijiografia na kwa wingi wa watu; je, Serikali itashauriana na Tume ya Uchaguzi ili kuongeza Majimbo ya Uchaguzi katika baadhi ya maeneo nchini katika Uchaguzi wa mwaka 2005? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (MHE. MUHAMMED SEIF KHATIB) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Dr. William Shija, Mbunge wa Sengerema, naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, lilipokuwa linajibiwa swali la Mheshimiwa Ireneus Ngwatura, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na pia swali la Mheshimiwa Sophia Simba, Mbunge wa Viti Maalum, CCM 1 katika Mikutano ya Saba na Kumi na Moja sawia ya Bungeni, nilieleza kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 75(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungao wa Tanzania 1977, Jamhuri ya Muungano inaweza kugawanywa katika Majimbo ya Uchaguzi kwa idadi na namna itakavyoamuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kupata kibali cha Mheshimiwa Rais.
    [Show full text]
  • Parliamentary Strengthening and the Paris Principles: Tanzania Case Study
    Parliamentary Strengthening and the Paris Principles Tanzania case study January 2009 Dr. Anthony Tsekpo (Parliamentary Centre) and Dr. Alan Hudson (ODI) * Disclaimer: The views presented in this paper are those of the authors and do not necessarily represent the views of DFID or CIDA, whose financial support for this research is nevertheless gratefully acknowledged. Overseas Development Institute 111 Westminster Bridge Road London SE1 7JD UK Tel: +44 (0)20 7922 0300 Fax: +44 (0)20 7922 0399 www.odi.org.uk i Parliamentary strengthening and the Paris Principles: Tanzania case study Acknowledgements We would like to thank all of the people who have shared with us their insights and expertise on the workings of the Parliament of Tanzania and about the range of parliamentary strengthening activities that take place in Tanzania. In particular, we would like to thank those Honourable Members of Parliament who took the time to meet with us, along with members of the Secretariat and staff members from a number of Development Partners and from some of the key civil society organisations that are engaged in parliamentary strengthening work. Our hope is that this report will prove useful to these people and others as they continue their efforts to enhance the effectiveness of Tanzania’s Parliament. In addition, we gratefully acknowledge the financial support provided by the UK’s Department for International Development (DFID) and the Canadian International Development Agency (CIDA). ii Parliamentary strengthening and the Paris Principles: Tanzania
    [Show full text]
  • Country Report Tanzania
    ODA Parliamentary Oversight Project Country Report and Data Analysis United Republic of Tanzania December 2012 © Geoffrey R.D. Underhill, Research Fellow, Amsterdam Institute for International Development and Professor of International Governance, University of Amsterdam © Sarah Hardus, Amsterdam Institute for Social Science Research, University of Amsterdam 2 About AIID About Awepa The Amsterdam Institute for International The Association of European Parliamentarians with Development (AIID) is a joint initiative of the Africa (AWEPA) works in partnership with African Universiteit van Amsterdam (UvA) and the Vrije parliaments to strengthen parliamentary Universiteit Amsterdam (VU). Both universities democracy in Africa, keep Africa high on the have a long history and an outstanding political agenda in Europe, and facilitate African- reputation in scientific education and research European parliamentary dialogue. in a broad range of disciplines. AIID was Strong parliaments lie at the heart of Africa's long- founded in 2000 by the two universities as a term development; they serve as the arbiters of network linking their best experts in peace, stability and prosperity. AWEPA strives to international development and to engage in strengthen African parliaments and promote policy debates. human dignity. For 25 years, AWEPA has served as a unique tool for complex democratisation AIID’s mission is laid down in its official operations, from Southern Sudan to South Africa. mission statement: The pillars that support AWEPA's mission “The Amsterdam Institute for International include: Development (AIID) aims at a comprehensive understanding of international development, A membership base of more than 1500 with a special emphasis on the reduction of former and current parliamentarians, poverty in developing countries and transition from the European Parliament and almost economies.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA MBILI ___Kikao Cha Sita
    Hii ni nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI __________ Kikao cha Sita - Tarehe 18 Juni, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Juma J. Akukweti) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 50 Upungufu wa Watumishi - Hospitali ya Wilaya ya Mbulu MHE. PHILIP S. MARMO aliuliza:- Kwa kuwa siku zilizopita Wizara imekiri upungufu mkubwa wa watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu katika fani zote kama Madaktari, Wauguzi, Wataalam wa X-ray na Famasia na mfano mmoja ukiwa ni kwamba mashine mpya za chumba cha X- ray hazitumiki kwa sababu ya ukosefu wa wataalam. Je, ni lini Serikali itawaajiri wataalam niliowataja ili kutatua tatizo hilo sugu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Philip Marmo, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tarehe 18 Julai, 2002 wakati nikijibu swali Na. 873 la Mheshimiwa Mbunge, nilikiri upungufu wa wataalam wa afya katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu. Naomba kumpongeza kwanza Mheshimiwa Philip Marmo, Mbunge wa Mbulu, kwa juhudi zake kubwa sana anazozichukua katika kutatua matatizo yaliyoko katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi. Halmashauri 1 za Wilaya nyingi hapa nchini bado zina upungufu wa wataalam katika fani mbalimbali. Ofisi ya Rais, pamoja na Idara Kuu ya Utumishi inajitahidi sana kutoa vibali vya ajira, lakini waombaji wa kazi hizo mara nyingi wamekuwa ni wachache. Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Wilaya ya Mbulu ni moja ya Hospitali za Wilaya ambazo zina upungufu wa Madaktari, Wauguzi na wataalam wengine.
    [Show full text]
  • Na Namba Ya Prem Jina La Mwanafunzi Shule Atokayo 1
    ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 WILAYA YA TEMEKE - WASICHANA A.UFAULU MZURI ZAIDI SHULE YA SEKONDARI KILAKALA - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140978513 GIFT JUMANNE MWAMBE SACRED HEART SHULE YA SEKONDARI MSALATO - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20141212460 IQRA SUPHIAN MBWANA ASSWIDDIQ 2 20141196774 HADIJA SAMNDERE ABDALLAH KIZUIANI SHULE YA SEKONDARI TABORA WAS - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140161890 JANETH JASSON RWIZA HOLY CROSS 2 20140142894 CATHERINE JACKSON MUGYABUSO HOLY CROSS 3 20140158817 MARTHA FREDRICK KIULA KAMO 4 20141283912 VANESSA ARISTIDES MSOKA JOYLAND B.UFUNDI BWENI SHULE YA SEKONDARI MTWARA UFUNDI - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140246791 PRINCESSREBECA ALOYCE MOSHA SHALOM 2 20140293569 SUZAN DIOCRES PETER MWANGAZA ENG. MED. SHULE YA SEKONDARI TANGA UFUNDI - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140271585 FATUMA IBRAHIMU NASSORO SOKOINE 2 20141282072 ALAWIA ASHIRI KIBWANGA KIBURUGWA 3 20140813416 LUCY MARTIN NDEU MGULANI C.BWENI KAWAIDA SHULE YA SEKONDARI KAZIMA - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20141358656 ASHURA ISSA NGULANGWA NZASA 2 20140961580 SHUFAA HAMADI TAMBARA UKOMBOZI 3 20140801607 NAIMA RAZACK MCHALAGANYA TAIFA 4 20140437650 HALIMA HASHIMU MPEGEA RUVUMA SHULE YA SEKONDARI LOWASSA- BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20141303924 RAHMA ALLY KWAKWADU MBANDE SHULE YA SEKONDARI LUGOBA-
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • 6 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd
    6 MEI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 6 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Waheshimiwa, mtakuwa mmepata Supplementary Order Paper, halafu na ile paper ya kwanza Supplementary hiki ni Kikao cha 19, wameandika 18 ni Kikao cha 19. Kwa hiyo, mtakuwa na Supplementary Order Paper. Katibu tuendelee? HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatayo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 6 MEI, 2013 MHE. AUGUSTINO M. MASELE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. GRACE S. KIWELU (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MASWALI NA MAJIBU Na. 145 Wajibu wa Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji MHE. MARIAM R. KASEMBE (K.n.y. MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA) aliuliza:- Msingi mkubwa wa Maendeleo ya Jamii huanzia kwenye ngazi ya Mitaa na Vijiji ambapo hutegemea ubunifu na utendaji wa Viongozi wa ngazi husika.
    [Show full text]