![Majadiliano Ya Bunge ______](https://data.docslib.org/img/3a60ab92a6e30910dab9bd827208bcff-1.webp)
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Saba – Tarehe 17 Juni, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Halmashauri ya Biashara ya Nje kwa Miaka ya Fedha ya 2005/2006 na 2006/2007 (The Annual Report and Audited Accounts of the Board of External Trade (BET) for the Financial Years 2005/2006 and 2006/2007). MASWALI NA MAJIBU Na. 65 Ujenzi wa Barabara za Lami Singida Mjini MHE. DIANA M. CHILOLO (K.n.y. MHE. MOHAMMED G. DEWJI) aliuliza:- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea Mkoa wa Singida kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 4 Agosti, 2009 aliahidi kuunga mkono juhudi za Manispaa ya Singida Mjini, katika ujenzi wa barabara za lami ndani ya Manispaa. Je, ahadi hiyo itatekelezwa lini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Gulam Dewji, Mbunge wa Singida Mjini, kama ituatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea Mkoa wa Singida tarehe 4 Agosti, 2009 alitoa ahadi ya kuunga mkono juhudi za Manispaa ya Singida katika ujenzi wa barabara za lami. Katika mwaka 2010/2011 Halmashauri ilituma maombi maalum ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo. Hadi sasa shilingi milioni 300 zimetolewa na kazi zilizofanyika ni ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 1.07 na kazi zinazoendelea ni kuimarisha mifereji katika barabara zilizokamilika. Ufuatiliaji wa fedha shilingi milioni 300 unaendelea ili kuendelea na ujenzi wa barabara kilomita 1 kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Salmin na Lumumba iliyoko katika Kata ya Itende. Barabara zilizojengwa ni kama zifuatazo:- (i) Mtaa wa Msikiti km. 0.450 (ii) Mtaa wa Kanisa Katoliki km 0.310 (iii) Mtaa wa Mwenge km 0.165 (iv) Mtaa wa Faraja km 0.145 Jumla km 1.070 Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Bajeti ya mwaka 2011/2012 Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeidhinishiwa shilingi milioni 745 toka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ya barabara. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kujenga barabara za Halmashauri, hususan za Manispaa ikiwemo ya Singida kwa kiwango cha lami kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu. MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina swali moja dogo la nyongeza. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba ombi la Manispaa ilikuwa ni shilingi milioni 600 na wameshatuma shilingi milioni 300. Na kwa kuwa katikati ya Manispaa barabara ni nyingi na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo amejitahidi kuweka taa za barabarani mji wote. Na kwa kuwa barabara za lami bado nyingi ambazo hazijatengenezwa mjini kati ili hadhi ya taa hizo ziendane na barabara. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuwaambia wananchi wa Singida Mjini kwamba kupitia Bajeti hii shilingi milioni 300 zilizobakia zitatengwa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru na kumpongeza sana Mbunge Dewji kwa kazi 2 nzuri ambayo ameifanya katika Manispaa ile ya Singida na wenzake wote ambao anashirikiana nao. Leo asubuhi nilikuwa nazungumza na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Paschal Mabiti wananchi wa Singida wenyewe wanasema wanamshukuru sana Rais kwamba ametekeleza ahadi yake kwa maana ya kazi iliyofanyika pale na ndiyo maana tumezungumza hapa. Shilingi milioni 300 ambazo zinadaiwa hakuna ubishi hapa huwezi ku-debate hapa maelekezo ya Rais, sina ubavu huo. Hizo fedha tutazitafuta tutazipeleka pale kwenda kumalizia kazi iliyobakia pale. Hapa sisi tunatekeleza maelekezo ya Rais kama ilivyotamkwa. Kwa hiyo Mheshimiwa Diana Chilolo uwe na amani moyoni mwako. Hii kazi itafanyika, tena itafanyika vizuri mpaka mwenyewe utafurahi. (Makofi) MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri kuonyesha dhamira ya kufuatilia ahadi za Rais. Kwa kuwa swali la msingi lilitokana na ahadi ya Rais aliyoitoa kwenye Mkutano wa hadhara na kwa kuwa kwa spirit hiyo hiyo ya Mheshimiwa Naibu Waziri ya kufuatilia kwa karibu ahadi za Mheshimiwa Rais. Je, Naibu Waziri yuko tayari vile vile kufuatilia ahadi ya Mheshimiwa Rais ya tarehe 24 Mei, 2010 aliyoitoa kwenye Mkutano wa hadhara Kimara Mavurunza ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kimara mpaka Segerea kupitia Bonyokwa ambayo iko chini ya Manispaa inayounganisha Manispaa mbili za Kinondoni na Ilala yeye kama Kiongozi wa TAMISEMI? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hakika kabisa kwamba kila akisimamishwa hapa kila mmoja atasema kwamba kuna ahadi za Serikali kwa maana ya Rais. Nimesema na juzi tumejibu tena hapa sisi hapa hatumfuati Rais tukamwambia fedha ziko wapi. Rais ameshapitisha bajeti tumeileta hapa ndiyo hii. Nyie tusaidieni kupitisha bajeti hapa, ndiyo kazi inayotakiwa hapa. Sisi tuna orodha na kitabu kimetengenezwa cha ahadi zote zilizotolewa na Rais nchi nzima. Kama nilivyosema Rais akishatoa ahadi sisi kazi yetu ni kutekeleza ahadi za Rais. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mnyika kama unataka tukitoka hapa twende Ubungo ili unipeleke kwenye hiyo barabara lakini nitakwenda kuangalia kwenye Bajeti yenu nyinyi kama mmeliangalia hili ili tuweze kujua jinsi tutakavyofanya. Lakini nataka nimthibitishie kwamba hatuna tatizo na ahadi yoyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais. MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na swali lililofuata nalo linaulizwa na Mheshimiwa Vicky Paschal Kamata, Mbunge wa Viti Maalum na linaelekezwa tena kwenye Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Na. 66 3 Mikoa Mipya Kuanza Kazi Rasmi na Wakuu wa Mikoa Kuteuliwa MHE. VICK P. KAMATA aliuliza:- Mheshimiwa Rais ameridhia kuanzishwa kwa Mikoa mipya ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Geita; wananchi wa Geita wameupokea uamuzi huo kwa furaha na matumaini makubwa sana. (a) Je, ni lini Mikoa hiyo itaanza kazi rasmi na Viongozi wa Mikoa kuteuliwa? (b) Je, Serikali imejiandaa vipi kuiendeleza Miji Mikuu ya Mikoa mipya katika maeneo ya huduma za kijamii, kiuchumi na miundombinu ambayo awali ilikuwa Miji Mikuu ya Wilaya? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vicky Paschal Kamata, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutumia fursa hii kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba wakati Serikali inatangaza kuanzishwa kwa Mikoa na Wilaya mpya ilikuwa ni kusudio la kuanzisha maeneo mapya ya utawala ambayo hatimaye yatawezesha kuanza rasmi kwa Mikoa na Wilaya hizo. Hatua iliyokwishafikiwa ni kuhakiki mipaka ya maeneo yote yanayopendekezwa kuanzishwa ikiwa ni pamoja na wananchi wa maeneo hayo kushirikishwa kuhusu dhamira hiyo ya Serikali. Hivyo, Mikoa na Wilaya mpya zitaanza rasmi Serikali itakapotoa Tangazo la kuanzishwa kwake (Government Establishment Notice). Uteuzi wa Viongozi na watumishi utafanyika zitakapokamilika taratibu za kisheria za uanzishaji Mikoa na Wilaya. Aidha, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Mheshimiwa Rais Mamlaka na Madaraka ya kuanzisha mamlaka mpya za Wilaya na Mikoa kwa wakati na namna ambavyo atakavyoona inafaa. (c) Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukidhi huduma za kijamii, kiuchumi na miundombinu katika maeneo yanayohusika, Serikali, Benki ya Dunia pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo imeandaa Mpango wa Muda Mfupi na wa Kati wa uendelezaji wa Majiji 3, Manispaa 15 na Miji Midogo 14 nchini. Geita ni moja ya maeneo ambayo yamefanyiwa maandalizi ya ukuaji wa Miji yenye hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa. Shughuli zitakazozingatiwa ni pamoja na upangaji Miji, mazingira na usafi, barabara, mifereji na uboreshaji wa mapato ya Miji hiyo. 4 MHE. VICK P. KAMATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa taarifa zisizo rasmi ilikuwa inafahamika kwamba kuanzishwa kwa mikoa hii kunasubiri Bajeti. Je, hiki kigugumizi cha Serikali ni kwa sababu hakuna fungu maalum lililotengwa kwa ajili ya kuanzishwa kwa mikoa hiyo? Pili, je, Serikali inawaambia nini wananchi wa Geita waliokuwa na matumaini makubwa sana ya kuanza kupata huduma zao za kimkoa na sasa kumbe uanzishaji wa mikoa hii unasuasua? Ahsante sana. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri nafikiri ujibu tu kwa mikoa yote ambayo inaanzishwa kwa utaratibu huo. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kama Mbunge mpya wa Viti Maalum anayekuja hapa. Nampongeza kwamba anafuatilia mambo haya kwa karibu sana. Yaani kwa kweli hilo hatuna tatizo nalo tunampongeza kwamba anafuatilia ni Mbunge wetu anatoka kule Geita. Yeye hakupata nafasi ya kuwa Mbunge wa Viti Maalum ni kwa tiketi ya Geita, sasa huko ni kusuasua. Yaani mkoa ule wa Geita ambao unazungumzwa hapa na ndio umemleta humu ndani. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, dada yangu Vicky Kamata nataka nikuthibitishie Rais tumemsikia, Waziri Mkuu tumemsikia, Mkuchika tumemsikia sisi wote Taifa zima tumesikia lile lilikuwa ni kusudio linatolewa notice yake. Sasa kuna establishment ukiingiza voti humu ndani Mheshimiwa Mkulo atakuambia hivi,
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages111 Page
-
File Size-