Tarehe 9 Aprili, 2021

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Tarehe 9 Aprili, 2021 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Sita – Tarehe 9 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Taarifa za Matoleo y a gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo: - 1. Toleo Na. 06 la tarehe 05 Februari, 2021; 2. Toleo Na. 07 la tarehe 12 Februari, 2021; 3. Toleo Na. 08 la tarehe 19 Februari, 2021; 4. Toleo Na. 09 la tarehe 26 Februari, 2021; 5. Toleo Na. 10 la tarehe 05 Machi, 2021; 6. Toleo Na. 11 la tarehe 12 Machi, 2021; 7. Toleo Na. 12 la tarehe 19 Machi, 2021; na 8. Toleo Na. 13 la tarehe 26 Machi, 2021. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge maswali tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini sasa aulize swali lake. Na. 38 Upungufu wa Walimu Shule za Msingi na Sekondari Maeneo ya Vijijini MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, Serikali inachukua hatua gani kumaliza tatizo la upungufu wa Walimu nchini, hasa shule zilizopo maeneo ya vijijini? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa David Ernest Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deodatus Phillip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo: - Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari, kuanzia Disemba 2015 hadi Septemba 2020, Serikali imeajiri walimu 10,666 wa shule za msingi na walimu 7,515 wa shule za sekondari na kuwapanga kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa. Aidha, kuanzia mwezi Desemba 2015 hadi 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Septemba 2020, Halmashauri ya Mji Njombe imeajiri walimu 21 wa shule za msingi na walimu 111 wa shule za sekondari. Vilevile Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaajiri walimu wapya 6,000 wa shule za msingi na sekondari ifikapo Juni 2021 ili kujaza nafasi zilizoachwa na walimu waliofariki ama kustaafu kazi. Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kupitia ofisi za wakuu wa mikoa imekuwa ikifanya uhamisho wa ndani kwa kuwahamisha walimu waliozidi hasa kwenye maeneo ya mijini na kuwapanga kwenye shule zenye uhaba mkubwa wa walimu ambazo nyingi zipo maeneo ya vijijini. Serikali itaendelea kuajiri na kuwapanga walimu kwenye shule za msingi na sekondari hasa zenye mahitaji makubwa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Deodatus Mwanyika, swali la nyongeza. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya swali la msingi lakini niulize swali la kwanza. Kwanza tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, mama yetu Samia Suluhu Hassan, kwa maamuzi aliyoyatoa siku ya Jumatatu ya kuruhusu kuajiriwa kwa walimu 6,000 kwa haraka, tunamshukuru sana. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni ukweli kwamba walimu 6,000 wanaokwenda kuajiriwa bado wanakwenda kufanya replacement; mahitaji ya walimu katika shule bado ni makubwa sana. Maamuzi ya Serikali ya kutoa elimu bure kwa nia njema yamefanya kuwe na uhaba mkubwa sana wa walimu katika maeneo hasa ya vijijini. Kwa hiyo, pamoja na mipango ambayo imeelezewa lakini bado kuna tatizo kubwa na ninapenda kujua, je, Serikali inaweza 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) bado ikatoa commitment kwamba itaajiri walimu wa kutosha? Kwasababu hii namba iliyotajwa hapa bado haitoshi. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; naelewa kuna vigezo ambavyo vinatumika kwenye ugawaji wa walimu kwenye maeneo mbalimbali. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa yale maeneo ambayo ni miji ambayo iko ndani ya halmashauri vigezo ambavyo vinatumika kwa kweli havina uhalisia kwasababu maeneo hayo unakuta yanaangaliwa sana kwasababu yana miji lakini vilevile yana maeneo mengi sana yenye shule nyingi sana ambayo wananchi wamejitoa wakajenga shule ambazo zipo katika maeneo ya vijijini. Wanapoangalia vigezo vya reallocation unakuta kwamba hawaangalii hivyo. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali; je, Wizara itakuwa tayari kupitia upya vigezo vya ku-allocate walimu ili maeneo ya halmashauri za miji ambayo yana maeneo makubwa ya zaidi ya kilometa 25 yaweze kupata walimu ili elimu yetu iwe na tija? Ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikiri wazi kabisa kwamba alichozungumza Mheshimiwa Mbunge ya uhaba wa walimu nchini pamoja na replacement ya walimu 6,000 ambayo tunakwenda kuifanya hivi karibuni bado upo. Na Serikali imeji-commit hapa katika statement yangu ya awali kwamba tutaendelea kuajiri kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Na mpango huo upo na ni endelevu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge ondoa wasiwasi kwenye hilo kwa sababu Serikali iko makini, na Serikali ya Rais wa Sita, mama Samia Hassan Suluhu, imejipanga kuhakikisha tunaondoa kabisa tatizo hilo. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, amezungumzia kuhusu Wizara kama tutakuwa tayari kupitia vigezo vya 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ugawaji wa walimu upya. Nikubali kabisa hilo tumelipokea, moja, ni kama ushauri, lakini pili, tutaendelea kulizingatia kuhakikisha kabisa ugawanyaji wa walimu wote nchini unafuata usawa na haki katika maeneo yote. Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masache Kasaka, swali la nyongeza. MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Tatizo ambalo linaikumba Njombe Mjini la uhaba wa walimu, ndilo tatizo hilohilo ambalo linaikumba Wilaya ya Chunya kwa uhaba wa walimu. Ajira mara ya mwisho iliyopita Wilaya ya Chunya tulipata takribani walimu 26 tu ambao ni idadi ndogo ukilinganisha na ukubwa wa Wilaya ya Chunya. Je, Serikali inatuhakikishia vipi kwamba kwenye awamu hii ya ajira itakayokuja tutapata walimu wa kutosha, hasa maeneo ya vijijini, ili kuweza kukidhi mahitaji ya watu wa Wilaya ya Chunya? Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, moja, nikubaliane na yeye kwamba kweli hata Chunya nakufahamu vizuri. Eneo ni kubwa na kuna idadi ndogo sana ya walimu. Lakini kwa sababu ameleta hapa ombi na sisi kama Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI tumelipokea hilo ombi na katika mgawanyo wa walimu 6,000 tutalizingatia hilo. Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, taratibu zile za Bunge la Bajeti zimeshaanza, kwa hiyo, ntakuwa nakata mtu yeyote anayeuliza swali kwa kuchangia. Maswali yawe mafupi muda wetu wa maswali ni mfupi. Kwa hiyo, ukipewa fursa uliza swali, usianze kutoa mchango mrefu, ikiwa ni pamoja na wale wenye maswali yao ya msingi, uliza swali ulilojiandaa nalo. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, swali la nyongeza. MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kumekuwa na tatizo kubwa la walimu katika nchi nzima, na kuna walimu ambao wanajitolea kufanya kazi za kufundisha katika maeneo mbalimbali nchini, zinapojitokeza ajira walimu hawa hawapewi nafasi; je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha walimu wanaojitolea wanapewa kipaumbele pale nafasi zinapotoka? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya vigezo ambavyo sasa hivi Serikali imekuwa ikitumia katika kuajiri walimu ni pamoja na kuzingatia walimu wote ambao wamejitolea kwa muda mrefu katika shule wanazofundisha. Kwa hiyo, hata katika hizi nafasi 6,000 ambazo tunakwenda kuzijaza zitazingatia vigezo hivyo. Na tumetoa maelekezo kwa maafisa elimu wote ngazi za wilaya kuleta taarifa za walimu wote wanaojitolea katika shule zao ili tuweze kuwazingatia katika ajira mpya. Ahsante sana. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rose Tweve, swali la nyongeza. MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Mheshimiwa Naibu Waziri katika majibu yako ya msingi ameonesha kabisa changamoto ya walimu pamoja na kuajiri hawa waliopo bado changamoto itakuwepo, hasa kwenye walimu wetu wa sayansi. Na technology inakua, hasa matumizi yetu ya simu. Sasa kama Serikali, mna mkakati gani wa kuhakikisha sasa tuna-link, hasa zile shle zilizopo vijijini tukatumia hii mitandao ili wakawa na access ya wale walimu wanaofundisha wenzao mjini wapate elimu sawa na kule vijijini? Nakushukuru sana. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kwamba kwenye masuala haya ya TEHAMA bado kuna changamoto kubwa sana hususan vijijini, na hata kwenye mitandao ya simu sisi wote ni mashuhuda kabisa kwamba networking
Recommended publications
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ BUNGE LA KUMI NA MOJA ___________ MKUTANO WA KWANZA Kikao cha Kwanza - Tarehe 17 Novemba, 2015 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Naomba tukae. TANGAZO LA RAIS LA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa masharti ya Katiba, Mkutano huu wa Kwanza unaanza kwa Rais kuuitisha. Naomba kuchukua nafasi hii kusoma Tangazo la Rais kama ambavyo tumelipokea. Tangazo la Serikali Na. 513 la tarehe 6 Novemba, 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sura ya Pili, hati iliyotolewa kwa mujibu wa Ibara ya 90(1). Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya. KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; NA KWA KUWA, masharti ya Ibara ndogo ya kwanza ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, yanamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu; NA KWA KUWA, matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 yalitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2015; HIVYO BASI, mimi John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyonayo chini ya Ibara ya 90(1) ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, naitisha Mkutano wa Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ufanyike katika ukumbi wa Bunge uliopo Mjini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016 Magufuli’s “Cleansing” Operation Zanzibar Election Re-run Nyerere Bridge Opens David Brewin: MAGUFULI’S “CLEANSING” OPERATION President Magufuli helps clean the street outside State House in Dec 2015 (photo State House) The seemingly tireless new President Magufuli of Tanzania has started his term of office with a number of spectacular measures most of which are not only proving extremely popular in Tanzania but also attracting interest in other East African countries and beyond. It could be described as a huge ‘cleansing’ operation in which the main features include: a drive to eliminate corruption (in response to widespread demands from the electorate during the November 2015 elections); a cutting out of elements of low priority in the expenditure of government funds; and a better work ethic amongst government employees. The President has changed so many policies and practices since tak- ing office in November 2015 that it is difficult for a small journal like ‘Tanzanian Affairs’ to cover them adequately. He is, of course, operat- ing through, and with the help of ministers, regional commissioners and cover photo: The new Nyerere Bridge in Dar es Salaam (see Transport) Magufuli’s “Cleansing” Operation 3 others, who have been either kept on or brought in as replacements for those removed in various purges of existing personnel. Changes under the new President The following is a list of some of the President’s changes. Some were not carried out by him directly but by subordinates. It is clear however where the inspiration for them came from.
    [Show full text]
  • The South African ‘Secrecy Act’: Democracy Put to the Test
    2015 3 48. Jahrgang VRÜ Seite 257 – 438 Begründet von Prof. Dr. Herbert Krüger (†) Herausgegeben von Prof. Dr. Brun-Otto Bryde (em.), Justus-Liebig-Universität Gießen, Prof. Dr. Dr. h.c. (Univ. Athen) Dr. h.c. (Univ. Istanbul) Philip Kunig, Freie Universität Berlin, Prof. Dr. Thilo Ma- rauhn, Justus-Liebig-Universität Gießen, Prof. Dr. Philipp Dann, Humboldt-Universität zu Berlin, Prof. Dr. Jürgen Bast, Justus-Liebig-Universität Gießen, Prof. Dr. Axel Tschentscher, Universität Bern, Dr. Karl-Andreas Hernekamp, Universität Hamburg im Institut für Inter- nationale Angelegenheiten der Universität Hamburg durch die Hamburger Gesellschaft für Völkerrecht und Auswärtige Politik in Verbindung mit den Regional-Instituten des Ger- man Institute of Global and Area Studies (GIGA) Beirat: Prof. Dr. Rodolfo Arango, Bogota, Prof. Dr. Moritz Bälz, Frankfurt, Prof. Dr. Ece Göztepe, Ankara, Prof. Heinz Klug, Madison, Prof. Dr. Kittisak Prokati, Bangkok/Fukuoka, Prof. Dr. Atsushi Takada, Osaka. Schriftleitung: Prof. Dr. Philipp Dann, E-mail: [email protected] Inhalt Editorial: The Current State of Democracy in South Africa ..... 259 Abhandlungen / Articles Wessel le Roux Residence, representative democracy and the voting rights of migrant workers in post-apartheid South Africa and post-unification Germany (1990-2015) ......... 263 Jonathan Klaaren The South African ‘Secrecy Act’: Democracy Put to the Test ............................ 284 Richard Calland/Shameela Seedat Institutional Renaissance or Populist Fandango? The Impact of the Economic
    [Show full text]
  • Serikali Kwa Maendeleo Ya Wananchi
    ZANZIBAR SERIKALI KWA MAENDELEO YA WANANCHI TOLEO NO. 024 ISSN 1821 - 8253 MACHI - APRILI 2016 Wananchi wa Zanzibar wameamua Wamemchagua tena Dk. Shein kuwa Rais Maoni ya Mhariri Bodi ya Wahariri Mhariri Mkuu Muelekeo wetu uwe kuleta maendeleo Hassan K. Hassan endelevu ananchi wa Zanzibar pamoja wengi waliotarajia kwamba ingemalizika kwa Mhariri Msaidizi na wenzao wa Tanzania Bara amani, utulivu na usalama kama ilivyotokea. Ali S. Hafidh wanastahiki kujipongeza Hii kwa mara nyengine ilidhihirisha namna kufuatiaW kumalizika kwa salama, amani na Wazanzibari walivyokomaa kisiasa na utulivu kwa uchaguzi mkuu ambao ni moja kufahamu maana halisi ya amani na athari za Waandishi kati ya majukumu muhimu ya kikatiba na uvunjifu wa amani. Said J.Ameir kidemokrasia. Hatua hiyo imeliwezesha taifa Kuna msemo wa kiswahili usemao Rajab Y. Mkasaba kupata viongozi halali waliochaguliwa na “iliyopitayo si ndwele, tugange ijayo”. Wakati wananchi kuiongoza nchi kwa kipindi cha umefika sasa kwa wananchi wote kuona haja, Haji M. Ussi miaka mitano ijayo. umuhimu au ulazima wa kuendeleza harakati Said K. Salim Uzoefu wa Tanzania, Barani Afrika na za kuleta maendeleo endelevu badala ya Yunus S. Hassan kwengineko duniani, kipindi cha uchaguzi kuendelea kukaa vijiweni kuzungumzia siasa Mahfoudha M. Ali ndicho kipindi pekee chenye kuvuta hisia ambazo wakati wake umeshamalizika. za watu wengi wakiwemo wanasiasa na Ni ukweli uliowazi kwamba hivi sasa Amina M. Ameir wanajamii wa rika na jinsia tofauti. Katika kumekuwa na fursa nyingi za kuweza kipindi hiki wanasiasa hutumia njia za kujikwamua na umasikini iwapo kila mtu Mpiga Picha aina mbali mbali kuwashawishi wananchi ataamua kufanyakazi kwa bidii. Serikali kuwapigia kura kupitia vyama vyao vya siasa imeshafanya juhudi kubwa za kueneza Ramadhan O.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019 Feathers Ruffled in CCM Plastic Bag Ban TSh 33 trillion annual budget Ben Taylor: FEATHERS RUFFLED IN CCM Two former Secretary Generals of the ruling party, CCM, Abdulrahman Kinana and Yusuf Makamba, stirred up a very public argument at the highest levels of the party in July. They wrote a letter to the Elders’ Council, an advisory body within the party, warning of the dangers that “unfounded allegations” in a tabloid newspaper pose to the party’s “unity, solidarity and tranquillity.” Selection of newspaper covers from July featuring the devloping story cover photo: President Magufuli visits the fish market in Dar-es-Salaam following the plastic bag ban (see page 5) - photo State House Politics 3 This refers to the frequent allegations by publisher, Mr Cyprian Musiba, in his newspapers and on social media, that several senior figures within the party were involved in a plot to undermine the leadership of President John Magufuli. The supposed plotters named by Mr Musiba include Kinana and Makamba, as well as former Foreign Affairs Minister, Bernard Membe, various opposition leaders, government officials and civil society activists. Mr Musiba has styled himself as a “media activist” seeking to “defend the President against a plot to sabotage him.” His publications have consistently backed President Magufuli and ferociously attacked many within the party and outside, on the basis of little or no evidence. Mr Makamba and Mr Kinana, who served as CCM’s secretary generals between 2009 to 2011 and 2012-2018 respectively, called on the party’s elders to intervene.
    [Show full text]
  • THRDC's Report on the Situation of Human Rights Defenders in Tanzania
    THE 2018 REPORT ON THE SITUATION OF HUMAN RIGHTS DEFENDERS AND CIVIC SPACE IN TANZANIA RESEARCHERS ADVOCATES JONES SENDODO, DEOGRATIAS BWIRE, LEOPOLD MOSHA WRITERS ADVOCATES JONES SENDODO, DEOGRATIAS BWIRE, LEOPOLD MOSHA EDITORS PILI MTAMBALIKE ONESMO OLENGURUMWA The 2018 Report on the Situation of Human Rights Tanzania Human Rights Defenders Coalition Defenders and Civic Space in Tanzania ii [THRDC] Table of Contents ABREVIATIONS vi LIST OF STATUTES AND INTERNATIONAL INSTRUMENTS vii ACKNOWLEDGMENT ix PREFACE x VISION, MISSION, VALUES xi THE OVERAL GOAL OF THE THRDC xii EXECUTIVE SUMMARY xiii Chapter One 1 GENERAL INTRODUCTION 1 1.0 Introduction 1 1.1 Protection Mechanisms for Human Rights Defenders 3 1.1.1 Legal Protection Mechanism at International Level 4 1.1.2 Legal Protection Mechanism at Regional Level 7 1.1.3 Legal Protection Mechanism at the National Level 11 1.1.4 Challenges with Both International and Regional Protection Mechanisms for HRDS 13 1.2 Non Legal Protection mechanism 13 1.2.1 Non Legal Protection mechanism at International level 14 1.2.2 Non Legal Protection Mechanism at Regional level 15 1.2.3 Protection Mechanism at National Level 16 Chapter Two 20 VIOLATIONS COMMITTED AGAINST HUMAN RIGHTS DEFENDERS 20 2.0 Overview of the Chapter 20 2.1 Violations Committed against Human Rights Defenders in 2018 21 2.1.1 Arrests and Prosecution against HRDs in 2018 Other Strategic Litigation Cases for HRDs in Tanzania 21 2.2 Physical violence, Attacks, and Torture 30 2.2.1 Pastoralists Land Rights Defenders and the Situation in
    [Show full text]
  • 20 MAY 2019.Pmd
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Moja – Tarehe 20 Mei, 2019 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo kikao cha 31. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nasikitika kuwatangazia kifo cha mwanasiasa mkongwe na kiongozi aliyepata kuhudumia kwa muda mrefu hasa kule kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Ally Juma Shamhuna. Waheshimiwa Wabunge, katika uhai wake, marehemu Ally Juma Shamhuma amepata kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo hizi zifuatazo; amepata kuwa Mkurugenzi wa Mifugo, amewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, amewahi kuwa Katibu Mkuu, Export Processing Zone Zanzibar, amewahi kuwa Waziri wa Mipango, amekuwa Waziri wa Nchi, Afisi ya Waziri Kiongozi, aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na wakati huo huo akiwa ni 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Naibu Waziri Kiongozi, katika uhai wake amekuwa Waziri wa Ardhi, Maji na Nishati na alipata kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali. Aidha, Marehemu Mheshimiwa Shamhuna kwa muda mrefu alikuwa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kutokea Zanzibar na baadhi yenu humu Wabunge mtamkumbuka marehemu Mheshimiwa Shamhuna kama Mbunge wa Bunge la Katiba na alikuwa Mjumbe wa Kamati namba 8 kwenye Bunge la Katiba, Kamati ambayo nilikuwa Mwenyekiti wake. Kwa niaba yenu Waheshimiwa Wabunge, tunatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Tunatoa pole kwa Wazanzibari wote na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia kifo hicho na tunamuomba Mwenyezi Mungu aihifadhi roho yake mahali pema peponi, amina.
    [Show full text]
  • 1 BUNGE LA TANZANIA ___MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao Cha Nne – Tarehe 8 Novemba, 20
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao cha Nne – Tarehe 8 Novemba, 2019 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Taarifa ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini (State of the Environment Report, 3). NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Mwaka ya Tathmini ya Utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2018/2019 (The Annual Performance Evaluation Report on Public Procurement Regulatory Authority for the Financial Year 2018/2019). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante sana. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Linaulizwa na Mheshimiwa Justin Joseph Monko, Mbunge wa Singida Kaskazini. Na. 40 Kuwa na Uchaguzi Mdogo wa Serikali za Mitaa MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:- Inapotokea Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa/Kijiji amefariki au kupoteza sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Mtaa au Kijiji husika huongozwa na Kaimu Mwenyekiti:- Je, kwa nini Serikali haioni umuhimu wa kuwepo uchaguzi mdogo kama ilivyo kwa Madiwani na Wabunge? MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA
    [Show full text]
  • Tarehe 12 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Saba – Tarehe 12 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Saba. Natumaini mlikuwa na weekend njema Waheshimiwa Wabunge, ingawaje weekend ilikuwa na mambo yake hii. Jana nilimtafuta Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba kwa mambo yetu haya ya Bunge kuhusiana na uchangiaji wa Mpango wa Maendeleo akaniambia Mheshimiwa Spika tafadhali niache. Aah! Sasa nakuacha kuna nini tena? Anasema nina stress. Kumbe matokeo ya juzi yamempa stress. (Makofi/Kicheko) Pole sana Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, na Wanayanga wote poleni sana. Taarifa tulizonazo ni kwamba wachezaji wana njaa, hali yao kidogo, maana yake wamelegealegea hivi. Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge baadaye tunaweza tukafanya mchango kidogo tuwasaidie Yanga ili wachezaji… (Kicheko) Katibu, tuendelee. (Kicheko) NDG. EMMANUEL MPANDA – KATIBU MEZANI: 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA NA VIJANA) (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu. Katibu! NDG. EMMANUEL MPANDA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza linaelekea TAMISEMI na litaulizwa na Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, Mbunge kutoka kule Ruvuma. Na. 49 Hitaji la Vituo vya Afya – Tunduru MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga vituo vya afya katika Kata za Tinginya, Muhimba, Kalulu, Mindu, Nalasi Magharibi na Nalasi Mashariki Wilayani Tunduru? SPIKA: Majibu ya Serikali kuhusu ujenzi wa vituo vya afya Ruvuma na nchi nzima, Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI, Mheshimiwa David Silinde, tafadhali.
    [Show full text]
  • Thesis Law 2019 Lihiru Victoria.Pdf
    Participatory Constitutional Reforms vs. Realization of Equal Representation of Men and Women in the Parliaments: A Study of Kenya, Rwanda and Tanzania By Victoria Melkisedeck Lihiru- LHRVIC001/1555440 Thesis Submitted for the Degree of DOCTOR OF PHILOSOPHYTown in the Department of Public Law, Faculty of Law of the UNIVERSITY OF CAPE TOWN. August 2019Cape of University Supervisor: Associate Professor Waheeda Amien The copyright of this thesis vests in the author. No quotation from it or information derived from it is to be published without full acknowledgementTown of the source. The thesis is to be used for private study or non- commercial research purposes only. Cape Published by the University ofof Cape Town (UCT) in terms of the non-exclusive license granted to UCT by the author. University COPYRIGHT The copyright of this thesis vests in the author. No quotation from it or information derived from it is to be published without full acknowledgement of the source. The thesis is to be used for private study or noncommercial research purposes only. Published by the University of Cape Town (UCT) in terms of the non-exclusive license granted to UCT by the author. i DECLARATION I, Victoria Melkisedeck Lihiru, hereby declare that the work on which this thesis is based is my original work (except where acknowledgments indicate otherwise) and that neither the whole work nor any part of it has been, is being, or is to be submitted for another degree in this or any other university. I authorise the university to reproduce for the purpose of research either the whole or any portion of the contents in any manner whatsoever.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA PILI Kikao Cha Nne – Tarehe 5 Februari, 2021 (Bunge
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Nne – Tarehe 5 Februari, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. ASIA MINJA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Almas Athuman Maige, Mbunge wa Tabora Kaskazini sasa aulize swali lake. Kwa niaba yake Mheshimiwa Innocent Bilakwate. Na. 42 Ujenzi wa Vituo vya Afya kwa Nguvu za Wananchi MHE. INNOCENT S. BILAKWATE (K.n.y. MHE. ALMAS A. MAIGE) aliuliza:- Wananchi wa Jimbo la Tabora Kaskazini wamejitolea kujenga Vituo vya Afya katika Kata za llolangulu, Mabama, Shitagena na Usagari katika Kijiji cha Migungumalo:- Je, Serikali ipo tayari kuanza kuchangia miradi hiyo? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Almas Athuman Maige, Mbunge wa Tabora Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua mchango mkubwa wa wananchi katika ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini. Hivyo, Serikali ina dhamira ya dhati ya kuchangia nguvu hizo za wananchi katika kukamilishaji vituo hivyo ili vianze kutoa huduma kwa wananchi. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa ukarabati na ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya nchini ikiwemo kukamilisha maboma ya majengo ya kutolea huduma za afya yaliyojengwa na wananchi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo ujenzi wake ulisimama kwa kukosa fedha.
    [Show full text]
  • Kenya and Tanzania Beyond 2015
    Jyrki Luukkanen, Peter Kuria, Mira Käkönen, Kamilla Karhunmaa, Joni Karjalainen, Rasna Warah, Colman Msoka and Kaisa Toroskainen KENYA AND TANZANIA BEYOND 2015: Exploring Domestic Debates and Envisioning Development Futures FINLAND FUTURES RESEARCH CENTRE Report to the Ministry for Foreign Affairs of Finland 1 This report has been carried out under the BEYOND 2015 project (Kenya and Tanzania Beyond 2015: Exploring domestic debates and envisioning development futures), a commissioned research funded by the Ministry of Foreign Affairs of Finland. All views presented in the text are those by the Research Cen- tre and its team, and do not represent the views of the Ministry. Contributors to this report (in alphabetical order): Kamilla Karhunmaa Joni Karjalainen Peter Kuria Mira Käkönen Jyrki Luukkanen Lotta Maijala Colman Msoka Noora Stenholm Kaisa Toroskainen Rasna Warah Research Leader: Jyrki Luukkanen, D.Tech, Research Director, Adjunct Professor Finland Futures Research Centre (Tampere office) Turku School of Economics, University of Turku Yliopistonkatu 58 D, 33100 Tampere, Finland E-mail: [email protected] Phone: +358 50 337 0710 Copyright © 2014 Writers & Finland Futures Research Centre, University of Turku FINLAND FUTURES RESEARCH CENTRE Turku School of Economics FI-20014 University of Turku Turku: Rehtorinpellonkatu 3, FI-20500 Turku Helsinki: Korkeavuorenkatu 25 A 2, FI-00130 Helsinki Tampere: Yliopistonkatu 58 D, FI-33100 Tampere Tel. +358 2 333 9530 utu.fi/ffrc [email protected], [email protected] 2 CONTENTS LIST OF
    [Show full text]