Tarehe 9 Aprili, 2021

Tarehe 9 Aprili, 2021

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Sita – Tarehe 9 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Taarifa za Matoleo y a gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo: - 1. Toleo Na. 06 la tarehe 05 Februari, 2021; 2. Toleo Na. 07 la tarehe 12 Februari, 2021; 3. Toleo Na. 08 la tarehe 19 Februari, 2021; 4. Toleo Na. 09 la tarehe 26 Februari, 2021; 5. Toleo Na. 10 la tarehe 05 Machi, 2021; 6. Toleo Na. 11 la tarehe 12 Machi, 2021; 7. Toleo Na. 12 la tarehe 19 Machi, 2021; na 8. Toleo Na. 13 la tarehe 26 Machi, 2021. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge maswali tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini sasa aulize swali lake. Na. 38 Upungufu wa Walimu Shule za Msingi na Sekondari Maeneo ya Vijijini MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, Serikali inachukua hatua gani kumaliza tatizo la upungufu wa Walimu nchini, hasa shule zilizopo maeneo ya vijijini? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa David Ernest Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deodatus Phillip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo: - Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari, kuanzia Disemba 2015 hadi Septemba 2020, Serikali imeajiri walimu 10,666 wa shule za msingi na walimu 7,515 wa shule za sekondari na kuwapanga kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa. Aidha, kuanzia mwezi Desemba 2015 hadi 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Septemba 2020, Halmashauri ya Mji Njombe imeajiri walimu 21 wa shule za msingi na walimu 111 wa shule za sekondari. Vilevile Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaajiri walimu wapya 6,000 wa shule za msingi na sekondari ifikapo Juni 2021 ili kujaza nafasi zilizoachwa na walimu waliofariki ama kustaafu kazi. Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kupitia ofisi za wakuu wa mikoa imekuwa ikifanya uhamisho wa ndani kwa kuwahamisha walimu waliozidi hasa kwenye maeneo ya mijini na kuwapanga kwenye shule zenye uhaba mkubwa wa walimu ambazo nyingi zipo maeneo ya vijijini. Serikali itaendelea kuajiri na kuwapanga walimu kwenye shule za msingi na sekondari hasa zenye mahitaji makubwa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Deodatus Mwanyika, swali la nyongeza. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya swali la msingi lakini niulize swali la kwanza. Kwanza tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, mama yetu Samia Suluhu Hassan, kwa maamuzi aliyoyatoa siku ya Jumatatu ya kuruhusu kuajiriwa kwa walimu 6,000 kwa haraka, tunamshukuru sana. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni ukweli kwamba walimu 6,000 wanaokwenda kuajiriwa bado wanakwenda kufanya replacement; mahitaji ya walimu katika shule bado ni makubwa sana. Maamuzi ya Serikali ya kutoa elimu bure kwa nia njema yamefanya kuwe na uhaba mkubwa sana wa walimu katika maeneo hasa ya vijijini. Kwa hiyo, pamoja na mipango ambayo imeelezewa lakini bado kuna tatizo kubwa na ninapenda kujua, je, Serikali inaweza 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) bado ikatoa commitment kwamba itaajiri walimu wa kutosha? Kwasababu hii namba iliyotajwa hapa bado haitoshi. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; naelewa kuna vigezo ambavyo vinatumika kwenye ugawaji wa walimu kwenye maeneo mbalimbali. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa yale maeneo ambayo ni miji ambayo iko ndani ya halmashauri vigezo ambavyo vinatumika kwa kweli havina uhalisia kwasababu maeneo hayo unakuta yanaangaliwa sana kwasababu yana miji lakini vilevile yana maeneo mengi sana yenye shule nyingi sana ambayo wananchi wamejitoa wakajenga shule ambazo zipo katika maeneo ya vijijini. Wanapoangalia vigezo vya reallocation unakuta kwamba hawaangalii hivyo. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali; je, Wizara itakuwa tayari kupitia upya vigezo vya ku-allocate walimu ili maeneo ya halmashauri za miji ambayo yana maeneo makubwa ya zaidi ya kilometa 25 yaweze kupata walimu ili elimu yetu iwe na tija? Ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikiri wazi kabisa kwamba alichozungumza Mheshimiwa Mbunge ya uhaba wa walimu nchini pamoja na replacement ya walimu 6,000 ambayo tunakwenda kuifanya hivi karibuni bado upo. Na Serikali imeji-commit hapa katika statement yangu ya awali kwamba tutaendelea kuajiri kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Na mpango huo upo na ni endelevu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge ondoa wasiwasi kwenye hilo kwa sababu Serikali iko makini, na Serikali ya Rais wa Sita, mama Samia Hassan Suluhu, imejipanga kuhakikisha tunaondoa kabisa tatizo hilo. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, amezungumzia kuhusu Wizara kama tutakuwa tayari kupitia vigezo vya 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ugawaji wa walimu upya. Nikubali kabisa hilo tumelipokea, moja, ni kama ushauri, lakini pili, tutaendelea kulizingatia kuhakikisha kabisa ugawanyaji wa walimu wote nchini unafuata usawa na haki katika maeneo yote. Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masache Kasaka, swali la nyongeza. MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Tatizo ambalo linaikumba Njombe Mjini la uhaba wa walimu, ndilo tatizo hilohilo ambalo linaikumba Wilaya ya Chunya kwa uhaba wa walimu. Ajira mara ya mwisho iliyopita Wilaya ya Chunya tulipata takribani walimu 26 tu ambao ni idadi ndogo ukilinganisha na ukubwa wa Wilaya ya Chunya. Je, Serikali inatuhakikishia vipi kwamba kwenye awamu hii ya ajira itakayokuja tutapata walimu wa kutosha, hasa maeneo ya vijijini, ili kuweza kukidhi mahitaji ya watu wa Wilaya ya Chunya? Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, moja, nikubaliane na yeye kwamba kweli hata Chunya nakufahamu vizuri. Eneo ni kubwa na kuna idadi ndogo sana ya walimu. Lakini kwa sababu ameleta hapa ombi na sisi kama Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI tumelipokea hilo ombi na katika mgawanyo wa walimu 6,000 tutalizingatia hilo. Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, taratibu zile za Bunge la Bajeti zimeshaanza, kwa hiyo, ntakuwa nakata mtu yeyote anayeuliza swali kwa kuchangia. Maswali yawe mafupi muda wetu wa maswali ni mfupi. Kwa hiyo, ukipewa fursa uliza swali, usianze kutoa mchango mrefu, ikiwa ni pamoja na wale wenye maswali yao ya msingi, uliza swali ulilojiandaa nalo. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, swali la nyongeza. MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kumekuwa na tatizo kubwa la walimu katika nchi nzima, na kuna walimu ambao wanajitolea kufanya kazi za kufundisha katika maeneo mbalimbali nchini, zinapojitokeza ajira walimu hawa hawapewi nafasi; je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha walimu wanaojitolea wanapewa kipaumbele pale nafasi zinapotoka? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya vigezo ambavyo sasa hivi Serikali imekuwa ikitumia katika kuajiri walimu ni pamoja na kuzingatia walimu wote ambao wamejitolea kwa muda mrefu katika shule wanazofundisha. Kwa hiyo, hata katika hizi nafasi 6,000 ambazo tunakwenda kuzijaza zitazingatia vigezo hivyo. Na tumetoa maelekezo kwa maafisa elimu wote ngazi za wilaya kuleta taarifa za walimu wote wanaojitolea katika shule zao ili tuweze kuwazingatia katika ajira mpya. Ahsante sana. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rose Tweve, swali la nyongeza. MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Mheshimiwa Naibu Waziri katika majibu yako ya msingi ameonesha kabisa changamoto ya walimu pamoja na kuajiri hawa waliopo bado changamoto itakuwepo, hasa kwenye walimu wetu wa sayansi. Na technology inakua, hasa matumizi yetu ya simu. Sasa kama Serikali, mna mkakati gani wa kuhakikisha sasa tuna-link, hasa zile shle zilizopo vijijini tukatumia hii mitandao ili wakawa na access ya wale walimu wanaofundisha wenzao mjini wapate elimu sawa na kule vijijini? Nakushukuru sana. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kwamba kwenye masuala haya ya TEHAMA bado kuna changamoto kubwa sana hususan vijijini, na hata kwenye mitandao ya simu sisi wote ni mashuhuda kabisa kwamba networking

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    185 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us