BJT 29 JANUARI 2019.Pmd
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kwanza – Tarehe 29 Januari, 2019 (Saa Tatu Asubuhi Bunge Lilianza) WIMBO WA TAIFA D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: KIAPO CHA UAMINIFU Mheshimiwa Mbunge afuataye aliapa:- Mhe. Abdallah Ally Mtolea SPIKA: Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba kutoa taarifa kwenu kwamba katika Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge, Bunge lilipitisha Muswada wa mmoja wa Sheria uliokuwa ukiitwa Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za za Kifedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance Bill, 2018). Kwa taarifa hii, napenda kuliarifu Bunge hili Tukufu kwamba tayari 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Muswada huo umepata kibali cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na kwa hiyo, imekuwa imekuwa ni sheria ya nchi inayoitwa Sheria ya Huduma Ndogo za Kifedha Na. 10 ya Mwaka 2018 (The Microfince Act No. 10 of 2018) Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI SPIKA: Hati za kuwasilishwa mezani Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU:- Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- Toleo Na. 44 la tarehe 02 Novemba, 2018; Toleo Na. 45 la tarehe 09 Novemba, 2018; Toleo Na. 46 la tarehe 16 Novemba, 2018; Toleo Na. 47 la tarehe 23 Novemba, 2018; Toleo Na. 48 la tarehe 30 Novemba, 2018; Toleo Na. 49 la tarehe 07 Desemba, 2018; Toleo Na. 50 la tarehe 14 Desemba, 2018; Toleo Na. 51 la tarehe 21 Desemba, 2018; Toleo Na. 52 la tarehe 28 Desemba, 2018; Toleo Na. 01 la tarehe 04 Januari, 2019; Toleo Na. 02 la tarehe 11 Januari, 2019; na Toleo Na. 03 la tarehe 18 Januari, 2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Jenista Mhagama. Tunakushukuru. Sasa nimwite Mwenyekiti wa Katiba na Sheria. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Bado ya Wizara. SPIKA: Aah bado, okay malizia Mheshimiwa. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Maelezo ya Waziri Mkuu kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018 [Political Parties (Amendments) Bill, 2018]. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Nchi kwa kuwasilisha huo Muswada mbele yetu. Nilichanganya kidogo mambo. Unajua leo asubuhi palikuwa bundi; bundi original, siyo…, hapo juu hapo. Kwa Dodoma, bundi wa mchana hana tatizo, ila wa usiku ndiyo shida. (Kicheko) Waheshimiwa tunaendelea. Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria tafadhali. Anakuja Mwenyekiti mwenyewe, Mheshimiwa Mchengerwa. Karibu. (Makofi) MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Maoni na ushauri wa kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018 (Political Parties (Amendments) Bill, 2018. SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria. Sasa nimwite Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Ofisi ya Waziri Mkuu. (Makofi) MHE. CATHERINE N. RUGE - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YA WAZI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kuhusu Muswada wa Sheria ya 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018 [The Political Parties (Amendments) Bill, 2018]. SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kama ilivyo kawaida, linaulizwa na Mheshimiwa Munira Mustapha Khatibu, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 1 Baadhi ya Kampuni Binafsi Kukandamiza Wafanyakazi MHE. KHADIJA NASSIR ALI (K.n.y. MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB) aliuliza:- Baadhi ya Kampuni binafsi zimekuwa zikiwafanyisha kazi Watumishi wao zaidi ya muda wa saa za kazi, kutowapa chakula na kuwalipa kima kidogo cha mshahara:- Je, Serikali ina kauli gani kuhusu suala hilo linalowakandamiza Wafanyakazi hao ambao wengi wao ni vijana? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Antony Peter Mavunde, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu Swali la Mheshimiwa Munira Mustapha Khatibu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, Serikali inasimamia ipasavyo mahusiano ya kikazi sehemu zote za kazi ikiwa ni pamoja na kampuni binafsi. Kupitia Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004, Serikali inasimamia viwango stahiki vya kazi ikiwa ni pamoja na masaa ya kazi, likizo mshahara na kazi staha kwa wafanyakazi wa sekta zote. Mheshimiwa Spika, ni wajibu wa Mwajiri kutii matakwa ya sheria kwa kumlipa mfanyakazi wake mshahara na maslahi stahiki. Hivyo, mwajiri anayekiuka matakwa ya sheria hii anastahili adhabu. Aidha, katika kuimarisha uwajibikaji upande wa waajiri, mwaka 2016, Bunge letu Tukufu lilifanya marekebisho katika Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya Mwaka 2004 na kuimarisha mfumo wa kaguzi za kazi mahali pa kazi kwa kuruhusu kutoa adhabu za papo kwa papo (compounding of offences) kwa waajiri wanaokiuka matakwa ya sheria, ikiwa ni pamoja na kutowalipa wafanyakazi malipo ya ziada kwa saa za ziada walizofanya kazi na kulipa mshahara chini ya kiwango cha chini cha mshahara. Mheshimiwa Spika, Ofisi yangu itaendelea kusimamia sheria na kuimarisha mahusiano kati ya waajiri na wafanyakazi na kufanya kaguzi za kazi sehemu za kazi ili waajiri watimize wajibu wao kwa kuzingatia matakwa ya sheria. SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Khadija Nassir. MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pia napenda kumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri. Nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, kwa vile bado malalamiko ya waajiriwa ni mengi sana nchini na bado utaratibu haujafafanua vizuri ni namna gani ambavyo waajiriwa hawa wanaweza kupata stahiki zao na usalama wao wakati 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wakiwa katika maeneo ya kazi, Serikali ina kauli gani juu ya hili? Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa vile bado ajira zetu za ndani hazina sheria ya moja kwa moja ambayo inawalinda waajiriwa, Serikali pia inasema nini juu hili? Mheshimiwa Spika, ahsante. SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Spika, katika swali la kwanza kuhusu malalamikio, Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiyafanyia kazi malalamiko na taarifa mbalimbali zinazowahusu wafanyakazi kwa kufanya kaguzi mbalimbali ambazo lengo la kaguzi hizi ni kutaka waajiri wote nchini wafuate utaratibu wa sheria unavyoelekeza kwa maana ya Sheria Na. 6 ya mwaka 2004 na Sheria Na. 7 ya mwaka 2004 ambazo zimetoa haki na wajibu kwa wafanyakazi pamoja na waajiri. Mheshimiwa Spika, ofisi yetu imeendelea kuchukua hatua kwa waajiri wote ambao wanakiuka sheria na mpaka ninavyozungumza hivi sasa, tayari tumeshawafikisha Mahakamani zaidi ya waajiri 19 katika kipindi cha mwaka 2017/2018 ambao wamekiuka utaratibu wa sheria. Ndiyo maana Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuepukana na malalamiko haya ya wafanyakazi. Mheshimiwa Spika, sehemu ya pili ya swali lake Mheshimiwa Mbunge alitaka kujua kuhusu sheria ya kuwalinda wafanyakazi. Kwa mujibu wa Sheria Na. 6 ya Mwaka 2004, imeainisha bayana haki za mfanyakazi na wajibu wa mwajiri. Sheria hii ndiyo inayotumika katika kuwalinda wafanyakazi. Ndiyo maana Bunge lako Tukufu mwaka 2016 lilifanya marekebisho ili kuongeza meno zaidi katika Idara ya Kazi katika kuwalinda wafanyakazi kwa kuhakikisha kwamba ikitokea mwajiri anakiuka taratibu za 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kisheria kuhusu mikataba na masaa ya kazi, Afisa Kazi akienda kumkagua atakuwa na uwezo wa kumtoza faini hapo hapo ambayo ni kiasi cha fedha, ambapo pia baadaye atakuwa na compliance order haya yote yaende kwa pamoja. Lengo ni kufanya sheria hiyo iwe na meno na wafanyakazi wetu waweze kulinda haki zao. Mheshimiwa Spika, ahsante. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na swali la Mheshimiwa Omari Abdallah Kigoda Mbunge wa Handeni, kwa Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Kigoda, tafadhali. Na. 2 Majengo ya Madarasa Yaliyotokana na Nguvu za Wananchi MHE. OMARI A. KIGODA aliuliza:- Je, ni lini Serikali kupitia Halmashauri itakamilisha majengo ya madarasa yaliyotokana na nguvu za wananchi? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Naibu Waziri, Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Omar Abdala Kigoda, Mbunge wa Handeni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua juhudi za wananchi na wadau wa maendeleo katika Sekta ya Elimu ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa miundombinu ya shule kama vile vyumba vya madarasa, madawati, matundu ya vyoo, nyumba za Walimu, mabwalo na maabara. 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Mji wa Handeni ina maboma