Online Document)
NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 8 Julai, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali na tunaanza na ofisi ya Waziri, Mheshimiwa Kayombo, kwa niaba yake Mheshimiwa Rage. Na. 321 Ofisi kwa ajili ya Tarafa-Mbinga MHE. ISMAIL A. RAGE (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuliza:- Wilaya ya Mbinga ina tarafa sita lakini tarafa zote hazina ofisi rasmi zilizojengwa:- Je, ni lini Serikali itajenga ofisi kwa Makatibu Tarafa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence Cassian Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Ruvuma una jumla ya tarafa 24 yaani Tunduru wako saba, Mbinga wana tarafa sita, Nyasa wana tarafa tatu, Namtumbo wana tarafa tatu na Songea wana tarafa tano. Ni kweli tarafa za Wilaya ya Mbinga hazina ofisi rasmi zilizojengwa na Serikali. Ujenzi wa hizo ofisi unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa Mkoa wa Ruvuma umeweka kipaumbele katika ujenzi wa ofisi nne za tarafa katika Wilaya ya Nyasa na Tunduru. Tarafa hizo ni Luhuhu (Lituhi-Nyasa), Ruhekei (Mbamba bay-Nyasa), Mpepo (Tinga-Nyasa) na Nampungu (Nandembo-Tunduru). Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Mkoa ulitenga shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Tarafa ya Luhuhu (Lituhi), Ruhekei (Mbamba bay), Mpepo (Tingi) na Nampungu (Nandembo).
[Show full text]