Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Nne - Tarehe 6 Desemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, wote mtakuwa mmesikia taarifa ya msiba wa Kiongozi wetu wa Bara la Afrika na Kiongozi wa Nchi ya Afrika ya Kusini, ambaye ametutoka Duniani usiku wa kuamkia leo. Kwa heshima yake pamoja na kwamba nitaagiza Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa niaba yetu waandaye resolution tutaisoma kesho. Lakini kwa ajili ya leo ili tuweze kuanza kazi yetu vizuri naomba tusimame kwa dakika moja ili tumkumbuke kiongozi huyu. Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho yake Peponi. (Hapa Wabunge walisimama kwa dakika moja Kuombeleza Kifo cha Mzee Nelson Mandela) 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- SPIKA: Kamati ya Hesabu za Serikali watawasilisha kesho kwa kuwa hawakuarifiwa jana usiku wakati tulipokuwa tumeshatayarisha Order Paper. MHE. SELEMANI JUMANNE ZEDI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA): Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Kuhusu Utekelezaji wa Shughuli za Kamati hiyo kwa Mwaka 2013. MHE. ANDREW J. CHENGE - MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI: Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Utekelezaji wa Shughuli za Kamati hiyo kwa Mwaka 2013. MASWALI NA MAJIBU Na. 40 Vigezo vya Mji kuwa Makao Makuu ya Nchi MHE. HAROUB MOHAMMED SHAMIS aliuliza:- Nchi nyingi Duniani zina Makao Makuu ya Serikali katika miji mbalimbali:- Je, nini vigezo gani vitatumika kufanya Mji uwe na hadhi ya Makao Makuu ya Serikali? 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, ni kweli nchi nyingi Duniani ziliamua kuweka Makao Makuu ya Serikali katika Miji mbalimbali kwa kuitamka katika Katiba, Sheria au vinginevyo kwa kufuatia mazingira yafuatayo:- (a) Kuwa kitovu cha uchumi na biashara katika Nchi husika kama vile Bahdad ya Zamani, Bertlin, London, Constatinople, Athaens, Madrid, Moscow, Rome, Stockholm, Tokyo na Vienna; (b) Kuongoza katika nyanja za utamaduni, kiutawala, au kuwa mbele katika masuala ya Kitaaluma. fano Athens, Belgrade, Brussels, Cairo, London, Manila, Lisbon, Sofia na Vienna; (c) Uwamuzi wa Serikali kuweka Makao Makuu yake katika mji inaoona unafaa zaidi kwa madhumuni hayo kwa mfano Dodoma - Tanzania Canberra -Australia, Otawa – Canada, Abuja – Nigeria, Wellington- New Zealand, Washington DC - Marekani, Brasilia – Brazil na Islamabad- Pakistan; na (d) Kuwa vituo maalum vya dini mfano Rome, Jerusalem, Baghdad ya Zamani, Moscow, Belgrade na kadhalika. Mheshimiwa Spika, vigezo vinavyotumika kuufanya mji uwe na hadhi ya Makao Makuu ya Serikali ni pamoja na kuwepo kwa:- (i) Majengo ya kutosha kwa ajili ya ofisi za Serikali na Makazi ya watu; (ii) Huduma muhimu za kijamii za kutosha kama vile Shule, Vyuo na kadhalika; (iii) Huduma za maji ya kutosha; 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, SERA, URATIBU NA BUNGE] (iv) Mtandao wa uhakika wa kufikika kwa njia ya barabara, reli,uwanja wa ndege na kadhalika; (v) Huduma mbalimbali za kibiashara; (vi) Huduma ya umeme ya uhakika; (vii) Mazingira mazuri ya hali ya hewa nzuri; na (viii) Maamuzi yanayoambatana na hali halisi ya Nchi. MHE. HAROUB MOHAMMED SHAMIS: Mheshimiwa Spika, juzi siku ya Jumatano Mheshimiwa Waziri huyu huyu aliojibu sasahivi hapa akijibu swali la Dkt. Malole Mbunge wa Dodoma Mjini alisema kwamba Serikali inatarajia kutunga Sheria itakayofanya Mji wa Dodoma uwe Makao Makuu ya Serikali. Serikali inatarajia kwa maana hiyo kwamba Serikali imetanganza Mji wa Dodoma ni Makao Makuu wameufanya bila ya Sheria kuwepo, na hapa majibu yake ya leo anasema kwamba Mji Mkuu hutangazwa na Sheria ya Serikali ambayo ni Makao Makuu. Je ni kwanini Serikali imeanza kuufanya Mji wa Dodoma kuwa Makao Makuu kabla ya Sheria na Kuleta Mkanganyiko katika Nchi? Mheshimiwa Spika, vigezo alivyovitaja Mheshimwa Waziri katika majibu yake hapa kwamba Majengo ya kutosha kwa ajili ya ofisi ya Serikali na mengineyo hayapo Dodoma. Ya kufanya mji wa Dodoma uwe na hadhi yaku Makao Makuu ya Serikali inakuwaje Serikali ipange Dodoma kuwa Mji Mkuu wa Serikali bila kuwa na huduma hizi muhimu ambazo ni vigezo vilivyoweka na Serikali hiyo hiyo hatuoni hapa nikuyumbisha nchi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, si kweli kwamba uamuzi ya kuja Dodoma ulifanywa bila utaratibu nimesema tunatunga Sheria, lakini Mji huu ulikuja Kisheria vilevile kwasababu 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, SERA, URATIBU NA BUNGE] pamoja na mazungumzo mengi tangu mwaka 1961 uhuru ulipopatikana mazungumzo yalianza na katika miaka hiyo hiyo ya 1961 mazungumzo yalianza ndani ya Nchi na kupendekeza Mji wa Makao Makuu uhame Dar es Salaam, wakati ule ilipendekezwa iwe katika miji ya Dodoma, Iringa , Arusha na Tabora. Lakini Bunge hili katika kikao chake cha mwezi Februari,1966, kwa Muswada Binafsi ya Mbunge wa Musoma, Mheshimiwa Joseph Nyerere. Alileta Muswada Binafsi hapa na Bunge likaunga mkono kwamba Makao Makuu sasa yahame kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma. Baada ya hapo na mfumo uliokuwepo vikao mbalimbali vya chama na Serikali viliendelea vikaazimia lakini hiyo haikutosha Serikali ilitayarisha General Notice Namba 230 ambayo ilitangazwa tarehe 12 Oktoba, 1973 ambayo ndiyo ilianzisha na ku-establish Dodoma kuwa Makao Makuu. Kwa hiyo labda tu tofauti Mheshimiwa Mbunge hajui kati ya hii General Notice inaweza kufanya kazi kama Sheria na Sheria, lakini Dodoma ipo Kisheria na sababu ni nyingi sana wale watu wa zamani kama sisi tunajua tumeshiriki wote katika kufanya maamuzi ya Dodoma kuwa Makao Makuu. Lakini la pili, Mheshimiwa Mbunge kinachoanza kwanza ni wazo na uwamuzi, hamwezi kuwanza kujenga kutenga Bajeti na nchi hizo mkaanza kujenga, kutenga Bajeji kukusanya mapesa kujenga majengo kabla hamjafanya uwamuzi. Kwa hiyo, sisi tumeanza kwa utaratibu tumeanza kufanya uwamuzi kwamba Makao Makuu yetu ni Dodoma, halafu ndiyo tunaanza maandalizi. Sehemu zote wanafanya hivyo kwanza unaanza uwamuzi maana kwanza hamuwezi kufanya kujenga, kujenga infrastructure majengo bila kufanya uwamuzi wa makusudi kwamba tunajenga kwa ajili ya nini. Kwa hiyo sisi tunakwenda vizuri tumefanya uwamuzi inachukua muda mrefu hatukusema lazima iwe leo lakini baadaye tutakuja kukaa wote. (Makofi) 5 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Na. 41 Upungufu wa Watendaji wa Vijiji Nchini MHE. FATMA A. MIKIDADI (K.n.y. MHE. SAIDI MOHAMED MTANDA) aliuliza:- Maeneo mengi ya vijiji nchini yamekuwa na upungufu mkubwa wa watendaji wa vijiji hali inayochelewesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo. (a) Je, ni Vijiji vingapi vya Jimbo la Mchinga havina Watendaji wa Vijiji? (b) Je, ni kwa kiwango gani ukosefu wa watendaji hao umechangia kuzorotesha Maendeleo ya Wananchi? (c) Je, ni lini Watendaji wa Vijiji wataajiriwa na kupangwa kwenye vijiji husika? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Mchinga, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mchinga lina vijiji 46 katika ya vijiji hivyo vijiji 37 vina Watendaji wa vijiji na 9 havina Watendaji wa vijiji wakuajiriwa na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi. Vijiji ambavyo havina Watendaji nafasi hizo zinakaimiwa na Watendaji ambao hupangiwa kukaimu nafasi hizo na Mkurugenzi wa Halmashauri ili shughuli za maendeleo ziweze kuendelea katika vijiji hivyo. Mheshimiwa Spika, inapotokea kijiji hakina kabisa mtedaji ni dhahiri kuwa shughuli za maendeleo zitazorota kutokana na pengo hilo. Aidha, kama nilivyoeleza katika 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA] sehemu (a) hapo juu Serikali imekuwa na utaratibu wa kuwakaimisha Watendaji wa vijiji jirani kufanya kazi katika vijiji ambavyo havina watendaji ili kuziba pengo wakati jitihada za Serikali zinafanyika kupata Watendaji wenye sifa. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/ 2013, Serikali Kuu ilirejesha katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa nafasi 10 za Watumishi wenye kada za chini ili watumishi hao wakiwemo Maafisa Watendaji wa Vijiji wajiriwe na Halmashauri wenyewe baada ya kupata kibali cha kuajiri kutoka Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma. Katika mwaka 2012/2013 Halmashauri iliomba kibali cha kuajiri Watendaji wa vijiji 10 na mwaka 2013/2014 Halmashauri iliomba kuajiri watendaji watatu (3) kupitia barua yenye Kumbukumbu Namba LDW/W.20/21/20 ya tarehe 3 Desemba, 2012. Tunaomba rai Mheshimiwa Mbunge aendelee kuvuta subira wakati kibali cha kuajiri na mamlaka husika kitakapotolewa. MHE. FATUMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Pamoja na hayo nina maswali mawili ya kuuliza. Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kumekuwa na utataka mkubwa wa kuajili watendaji kwa sababu ya vigezo vinavyotumika kwamba vijijini huwezi kumpata mtendaji ambaye amesoma sana hivi ndiyo maana tukakosa kuajili au kuwapata Watendaji. Kwa hiyo swali langu ni kwamba je, Serikali itaangalia upya vigezo vya kuajiri watendaji wa vijijini? Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Serikali itatupatia nafasi zilizobaki ambazo hazijajazwa katika Jimbo la Mchinga? Kwa sababu Uchaguzi Mkuu unakuja, Katiba mpya inataka ifanyiwe kazi, kama hakuna
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages224 Page
-
File Size-