Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Thealathini na Sita – Tarehe 29 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 328 Kupandisha Hadhi Kituo cha Afya Mlandizi MHE. ABUU H. JUMAA aliuliza:- Kituo cha Afya Mlandizi licha ya kuhudumia wananchi wa wilaya, vijiji na wilaya za jirani pia kimebeba jukumu kubwa zaidi ya uwezo wake la kuhudumia watu wanaopata ajali mbalimbali katika barabara kuu ya Morogoro. Na Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni zake za uchaguzi mkuu wa 2010 aliliona jukumu hilo na kuahidi kituo hicho kipandishwe hadhi na kuwa hospitali ili kiweze kuhudumia watu kulingana na ukubwa wa kazi waliyonayo. Je ahadi hiyo itatekelezwa lini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abuu Hamoud Jumaa, Mbunge wa Kibaha Vijijini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kituo cha afya cha Mlandizi kilichopo kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, kilianza kama Zahanati kwenye miaka ya 60. Kituo hiki kinatoa huduma za wananchi zaidi ya 71,088 wa wilaya ya Kibaha pamoja na wananchi wa maeneo ya jirani ya vijiji vya Halmashauri ya Mji wa Kibaha pamoja na Bagamoyo na kuhudumia wahanga wa ajali za barabara yaani barabara kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda Morogoro. Aidha, kituo hupokea wagonjwa wa rufaa kutoka zahanati 23 zilizoko wilayani. Kituo kina vitengo mbalimbali vya huduma kama vile vitengo vya wagonjwa wa nje yaani OPD, tiba afya ya uzazi na mtoto, maabara, kitengo cha macho, kinywa na meno, ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa maambukizi ya VVU, kifua kikuu na ukoma. Kituo kina watumishi wapatao 56 wa kada mbalimbali. Idadi hii inazidi mahitaji ya watumishi wa vituo vya afya ambayo ni 29. 1 Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia ahadi ya Mheshimiwa Rais ya tarehe 5 Oktoba, 2009 Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kupitia Kamati ya Huduma za Jamii ilijadili na kuamua kuwa kituo cha afya cha Mlandizi kipandishwe hadhi kuwa hospitali ya wilaya. Maombi ya kupandisha kituo hicho yamewasilishwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi. NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Abuu ameridhika, swali la nyongeza Mheshimiwa. MHE. ABUU H. JUMAA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri ambayo yamenipa matumaini makubwa lakini pia maswali ya nyongeza. Kwa kuwa kituo hiki kinafanya kazi na kutoa huduma nje ya malengo yake na ikiwa uwezo wake ni mdogo na kwa kuwa ahadi hii ya Mheshimiwa Rais na kwa kuwa Naibu Waziri anakiri kwamba maombi yetu tayari yalishakuwa katika Wizara yake. Je, ni lini sasa ahadi hii ya Mheshimiwa itatekelezwa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abuu Hamoud Jumaa, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Naibu Spika, anachosema Mheshimiwa Jumaa ni sahihi. Eneo hili tunalozungumzia hapa pamoja na kwamba liko karibu na Tumbi hospitali ambayo ndiyo inaangalia hao wahanga wa ajali mbalimbali. Lakini bado kituo hiki anachosema kimeshalemewa, ni kweli na hivi tunavyozungumza ukishapita tu pale kwenye kambale yaani unapita unatoka Dar es Salaam unakwenda wewe Morogoro, ukipita kwenye lile daraja kubwa pale ukienda pale ni Bagamoyo, lakini wale wote wanahudumiwa na kituo hiki hiki anachokizungumza. Ukitoka hapo ukienda kidogo Kibaha kule tayari umeshaingia tena kwenye eneo lingine ni nje ya hii. Na nimezungumza na Mkurugenzi Mtendaji hili jambo linalozungumzwa hapa ni kweli tusipowasaidia wenzetu kituo kile kimelemewa. Lakini issue hapa ni kwamba kituo hiki sasa kimekubalika kwamba kiwe hospitali ya Wilaya. Na in addition to that kuna maelekezo ya Mheshimiwa Rais yanayosema kwamba tujenge, wameomba maombi maalum ya shilingi 800. Nimefuatilia tumekwenda mpaka tumepanda kwa Mheshimiwa Mustafa Mkulo, tumekuta mpaka sasa hivi hawakupata kiasi chochote pale. Nimemwahidi mkurugenzi Mtendaji pamoja na TAMISEMI, kwamba tutafuatilia hizi hela na Serikali ipo hapa inasikia tukisema hivyo, ili tupate angalau hizo milioni 800 zikishapatikana tuweze kufanya kazi ambayo imeagizwa na Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha kwamba hospitali hii inakuwa hospitali ya wilaya badala ya kuwa ni kituo. Niombe nichukue nafasi kumshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyofuatilia jambo hili. Na. 330 Mashirika yanayosaidia Katika Janga la UKIMWI Nchini MHE. AMINA C. ANDREW (K.n.y. MHE. MARIAM R. KASEMBE) aliuliza:- Yapo Mashirika ya nje yanayosaidia kutoa msaada kwa nchi yetu kupambana na janga la UKIMWI:- (a) Je, Mashirika hayo ni mangapi na yapi na yanatoa msaada gani? (b) Je, hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini ikoje, sasa kitakwimu? NAIBU SPIKA: Tutalirudia tuendelee, Mheshimiwa majibu ya swali hilo, tutalirudia lile lingine kwa makosa tu bahati mbaya. 2 WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Reuben Kasembe, Mbunge wa Masasi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jumla ya Mashirika ya nje 16, ambayo yapo nchini kusaidia katika vita dhidi ya UKIMWI. Mashirika hayo ni Elizabeth Glacer Pediatric AIDS Foundation (EGPAF), International Centre for AIDS Program (ICAP), Department of Defence (DOD), yaani water reeds, Family Health International (FHI), Pharmacies International Foundation (PAI), Clinton Health Access Initiative (CHAI), Engenderhealth, JHPIEGO, MDH, AIDS Relief, Baylor Tanzania, AFRICARE, AMREF, PATHFINDER, MILDMAY na Supply Chain Management System (SCMS). Mashirika haya hutoa misaada ya fedha na kiufundi katika kutekeleza afua mbalimbali zinazolenga kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI yaani VVU, na kutoa huduma kwa wale ambao wanaishi na VVU. Baadhi ya afua zinazotekelezwa ni pamoja na uzuiaji wa maambukizi ya VVU, kutoka kwa mama kwenda mtoto (PMTCT), huduma na ushauri nasaha na upimaji VVU, kuelimisha jamii katika masuala mbalimbali ya UKIMWI, huduma za maabara, matibabu ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono, kusambaza kondomu na kutoa huduma ya tohara kwa wanaume. (b)Mheshimiwa Naibu Spika, ripoti ya taifa ya tafiti ya viashiria vya VVU na malaria ya mwaka 2008 yaani Tanzania HIV and Malaria indicator survey inaonyesha hali ya maambukizi ya VVU kwa ujumla ni asilinia 5.7. Hali ya maambukizi inatofautiana miongoni mwa watu katika makundi tofauti. Mathalani, maambukizi yako zaidi kwa wanawake asilimia 6.8 kuliko wanaume ambao ni asilimia 4.7, mijini ni asilimia 8.7 kuliko vijijini ni asilimia 4.7. Aidha, kijiografia, mkoa wa Iringa ndio wenye maambukizi ya juu ukiwa na asilimia 14.7. Mikoa iliyo na maambukizo ya chini ni mkoa wa Kigoma, Arusha, Kilimanjaro, Manyara ikiwa ni asilimia 2. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali pia hupata misaada ya kupambana na UKIMWI kutoka kwa Mashirika mengine ya nje, kama vile mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na UKIMWI, mfuko wa dunia wa kupambana na UKIMWI, kifua kikuu na malaria yaani Global Fund, mashirika ya umoja wa kimataifa, mashirika ya nchi mbalimbali kama vile Japan, nchi za Scandinavia, na Canada. Mashirika haya mara nyingi hutoa misaada ya fedha na wataalam katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kupambana na UKIMWI. MHE. AMINA ANDREW CLEMENT: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili ya nyongeza, kwa kuwa jimbo la Masasi wananchi wengi hujitoa wakaenda kupima UKIMWI wao wenyewe na halafu baadaye wakipatikana waathirika huwa wanatengeneza vikundi wakakaa pamoja ili kujikimu kiuchumi. Je, Serikali itawasaidia nini kupitia haya mashirika hivyo vikundi vya waathirika? Je, Serikali haiwezi kuwashawishi haya mashirika ili kuwajengea mazingira bora hawa watoto yatima walioachwa na waathirika wakaweza kuwalea? Ahsante sana. WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mbunge kama ifuatavyo:- La kwanza Serikali itawasaidia nini katika vikundi hivyo, Serikali kupitia mpango wa kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI yaani TACAIDS ina mikakati mbalimbali ikiwa mojawapo ni kusaidia vikundi hivi pamoja na kutoa elimu. Vile vile katika Halmashauri zetu tuna idara maalum ambayo inashughulikia kupitia Wizara ya Afya, ile idara ya Afya nao wanajishughulisha moja kwa moja na shughuli za kuweza kuwasaidia vikundi hivyo. Wito wangu Wabunge kwamba vikundi hivi kama vipo basi mvisaidie 3 kuwasilisha au kujitambulisha kwenye idara ya afya pale wilayani, wao wilayani watajua namna gani ya kuweza kuwasaidia hawa. Mheshimiwa Naibu Spika, la pili nimelipokea ombi au ushauri kwamba haya mashirika yaweze vilevile kuwashawishi na kuwashirikisha hivi vikundi ambavyo vinajitokeza. MHE. MARIAM S. MSABAHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kumwuliza Waziri swali la nyongeza, kwa kuwa elimu hii ya UKIMWI haitolewi vijijini na kwa kuwa hata kondomu hazifiki vijijini na imekuwa kondomu hizi hata vijana wanakuwa wanazifua kondomu na kubadilishana kondomu. Je atanihakikishiaje huduma hizi za UKIMWI zinafika vijijini? WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu, swali la nyongeza Mbunge Mariam Msabaha, swali lake kama ifuatavyo. Labda naomba nitoe maelekezo ya ziada kwamba labda nitofautiane kidogo na Mbunge Mariam Msabaha, kwamba