MKUTANO WA NANE Kikao Cha Thelathini Na
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Nane – Tarehe 1 Agosti, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wake wa Saba Bunge lilipitishwa Miswada minne ya Sheria iitwayo: The Business Laws, (Miscellaneous Amendments) Bill, 2012. Halafu wa pili, The Tanzania Livestock Research Institute Bill, 2012, wa Tatu, The Social Security Laws (Amendemnts) Bill, 2012, wa nne The written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.2) Bill, 2012. Kwa taarifa hii napenda kuliarifu Bunge hili Tukufu kwamba, Miswada hiyo imekwishapata kibali cha Mheshimiwa Rais na kuwa Sheria za nchi zinazoitwa:- The Business Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2012, (No.3 of 2012); The Tanzania Livestock Research Institute Act, 2012, (No. 4 of 2012); The Social Security Laws (Amendemnt) Act, 2012 (No.5 of 2012), na wa nne The written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.2) Act, 2012 (No. 6 of 2012). Waheshimiwa Wabunge, hii ndiyo Miswada tuliyokuwa tumeipitisha na Mheshimiwa Rais ameweka mkono wake. Kwa hiyo, ni sheria za nchi. Tunaendelea, Katibu tuendelee. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI:- Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. PETER J. SERUKAMBA - MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU:- Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. PAULINE P. GEKUL (K.n.y. MHE. SAID A. ARFI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA UCHUKUZI):- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Uchukuzi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU Na. 300 Ujenzi wa Zahanati na Upatikanaji wa Watumishi MHE. PETER J. SERUKAMBA (K.n.y. MHE. DKT. HENRY D. SHEKIFU) aliuliza:- Mpango wa MAMM hususani ujenzi wa zanahati kila kijiji umeitikiwa vizuri na wananchi na kasi ni kubwa kuliko uwezo wa Serikali wa kupeleka watumishi na madawa:- (a) Je, Serikali inachukua hatua gani kurekebisha hali hiyo ili wananchi wasikate tamaa kujenga zahanati? (b) Je, ni lini Zahanati za Kwai na Milingano zilizopo Wilaya ya Lushoto na nyingine ambazo zipo tayari zitafunguliwa na kupelekewa watumishi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Henry Daffa Shekifu, Mbunge wa Lushoto, kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, nia ya Serikali ya kujenga Zahanati kila kijiji ni kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ambapo lengo ni kumfanya mgonjwa asitembee umbali zaidi ya kilometa 5 kufuata huduma hiyo kutoka pale alipo. Serikali inachukua jitihada mbalimbali ili kuhakikisha kwamba zahanati zinazojengwa zinapata watumishi wa kutosha. Mkakati mojawapo wa Serikali ni kuongeza udadhili wa wanafunzi wanaojiunga na vyuo katika fani za afya, kuwapanga madaktari wanaohitimu moja kwa moja katika vituo vya kazi na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto iliomba kibali cha kupata watumishi 45 wa kada za Afya ili kukidhi mahitaji ya zahanati zilizopo. Kati ya hao, watumishi ambao wamesharipoti ni 31 na watumishi 14 hawajaripoti. Watumishi hao watapangwa katika zahanati na vituo vya vya vilivyomo katika Halmashauri hiyo ili kuondoa upungufu uliopo. (b) Mheshimiwa Spika, zahanati ya Mlingano na Kwai kwa sasa zimeshaanza kutoa huduma za afya. Zahanati ya Mlingano kwa sasa ina watumishi 3 wanaoendeleza wakati zahanati ya Kwai inayomilikiwa na Shirika la Dini ina watumishi wapatao 11 ambao wanatoa huduma za afya kituoni hapo. Mheshimiwa Spika, Serikalil itaendelea na utaratibu wa kuwapanga watumishi wa kada za afya moja kwa moja katika vituo vya kazi kadri wanavyohitimu au kufuzu mafunzo yao kila mwaka ili kuondokana na upungufu uliopo. MHE. DKT. HENRY D. SHEKIFU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza. (a) Kwa kuwa tatizo hili la watumishi katika Idara ya Afya ni kubwa; na kwa kuwa Serikali imetangaza utaratibu wa kuanzisha hospitali za kata na kasi ya kuanzisha hospitali za vijiji imekuwa kubwa kuliko uwezekano wa kupata watumishi? Je, tuwambieni nini wananchi ambao wametoa nguvu zao zahanati zipo tayari, lakini hakuna watumishi? (b) Kwa kuwa, Wilaya ya Lushoto ni kati ya Wilaya ambazo zina watu wengi sana na idadi ya kupata watumishi imekuwa ni ndogo sana. Je, Serikali inatamka nini katika kuzipa umuhimu wa kwanza zile Wilaya ambazo kwa kweli zina watu wengi na kuna tatizo kubwa la watumishi? NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kirefu tulikuwa na upungufu wa watumishi kwa asilimia kama 65 hivi kwenye mwaka 2005/2006. Lakini kwenye kipindi hicho hicho tumekuwa na ongezeko la Vituo vya Afya na kusudio zima tu la kuweza kufanya kila vituo vya afya viwepo na zahanati ziwepo katika maeneo yetu. Mheshimiwa Spika, sasa tumekuwa na changamoto ya kuziba mapengo ya vituo vipya ambavyo vimekuwa vikijengwa toka mwaka 2006/2007 mpaka sasa ambavyo vinazidi vituo 1,055, sasa hii ni nyongeza ya mapungufu ambayo tulikuwa nayo mwaka 2005/2006. Hivi sasa tuna upungufu wa karibu asilimia 50. Kwa tafsiri hiyo maana yake ni kwamba kumekuwa na juhudi ziada za kuongeza vyuo, kuongeza wanaodahiliwa na pia kuongeza ajira katika vituo vyetu. Lakini juhudi hizi hazikwenda sambamba na ongezeko la vituo vya Afya na Vituo vyetu vya Tiba ambavyo vinaongezeka kwa pamoja. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, juhudi zifanyike kama ilivyokuwa kwenye kipindi cha mwaka jana ambayo inaishia mwaka huu 2011/2012 tulipata ajira nafasi za kuajiri watu 9000 na ambao wameajiri mpaka sasa ni 7000. Kwa hiyo, katika tafsiri hii maana yake juhudi zipo zinafanyika na nimwombe Mheshimiwa Mbunge ashirikiane na Halmashauri kuonyesha mahitaji yake ili angalau kwenye kipindi cha mwaka huu tuweze kuziziba nafasi hizo ambazo zipo wazi. MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kuniona. Fedha za MMAM ni fedha za Serikali ambazo zimekuwa zikisaidia kuweza kuimarisha miundombinu na hasa ya Afya vijijini katika nchi nzima. Kwa kuwa katika baadhi ya Halmashauri fedha hizi zimeonekana kuweza kutumika vibaya kama taarifa za CAG ambapo zimekuwa zikibainisha na Wilaya ya Kasulu ni mojawapo ya maeneo ambayo fedha hizi zimeonekana kuweza kutumika vibaya; na kwa kuwa, nimeandika barua pengine kuweza kuiomba Serikali iweze kuchukua hatua hadi leo sijaona ni kitu gani ambacho kimefanyika. Mheshimiwa Naibu Waziri ninaamini kwamba kufanya ziara katika Wilaya ya Kasulu tunaweza tukatatua tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri upo tayari TAMISEMI, Mheshimiwa Aggrey Mwanri hufanye ziara katika Wilaya ya Kasulu na uweze kuona ni mambo gani mengine mabaya ambayo yamekuwa yakifanyika ili kuweza kuleta tija katika matumizi ya fedha za umma? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwanza, nikiri kwamba Mheshimiwa Mbunge amekuwa anaeleza haya matatizo, yapo matatizo mengi hayasemi hapa ambayo amekuwa ananieleza na ameonyesha hiyo. Juzi tumekwenda Kigoma pale tulizungumzia kuhusu matatizo ambayo yanajitokeza katika zahanati na katika hospitali zetu, na msimamo ambao umetolewa jana hapa Mheshimiwa Waziri alipokuwa anahitimisha hoja yale ndiyo msimamo ambao tunakwenda nao. Lakini hili la kwenda Kigoma ni wajibu wetu kufanya hivyo. Mheshimiwa Mbunge, nitakuwa tayari kufanya hivyo muda muafaka utakapofika kwa sababu tunayo ratiba kubwa ya kuzunguka nchi nzima, lakini tuta-consider hilo. Na. 301 Ruzuku kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari MHE. JOHN J. MNYIKA aliuliza:- Serikali hutoa ruzuku (Capitation Grants) kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari za Umma zikiwemo za Jimbo la Ubungo, japo utekelezaji wa sera hii unasuasua sana kwa kiwango kilichowekwa kutokana na mahitaji halisi ya wanafunzi. Viwango vinavyotengwa katika Bajeti ni chini ya vinavyotajwa kwenye Sera na fedha hazitolewi zote isipokuwa hutolewa kidogo kidogo na hazifiki kikamilifu mashuleni:- (a) Je, Serikali itahakikishiaje kuwa ruzuku iliyopangwa inafika kwa kiwango cha kutosha na kwa wakati? (b) Je, kwa nini Serikali isiwe na utaratibu wa kutangaza viwango vya ruzuku vilivyotengwa kwa kila mwanafunzi na kuhakikisha shule zinaweka wazi matumizi ya fedha hizo kwa wadau wote? (c) Je, Serikali itapitia lini viwango vya ruzuku vilivyowekwa katika Sera ili kuendana na mahitaji halisi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa John John Mnyika, Mbunge wa Ubungo lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, kila mwaka Serikali hutenga fedha za ruzuku ya uendeshaji kwa shule na shule za msingi na sekondari. Ruzuku hii hutolewa kila baada ya miezi mitatu (kila robo mwaka) kutegemeana na makusanyo ya Serikali kwa kipindi hicho. Pamoja na kuwepo changamoto katika kukusanya mapato ya ndani na nje, Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha fedha zinapelekwa kadri zinavyopatikana katika kila Halmashauri kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji wa shule zetu. (b) Mheshimiwa