Constitution of Kenya Review Commission
CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, OTHAYA CONSTITUENCY, HELD AT OTHAYA CATHOLIC HALL ON 17TH APRIL, 2002 CONSTITUENCY PUBLIC HEARING, OTHAYA CONSTITUENCY, HELD AT OTHAYA CATHOLIC HALL ON 17TH MARCH, 2002 AT OTHAYA. Present:- 1. Com. Pastor. Zablon Ayonga 2. Mr. Patrick Lumumba Secretariat in Attendance 1. Charles Oyaya - Programme Officer 2. Daniel K’Onyango - Assistant Programme Officer 3. Susan Mutile - Verbatim Recorder 4. Christine Moraa - Sign Language Interpreter The meeting started at 9.00 a.m with Mr. Patrick Lumumba in chair. John Kibe: I am just calling the people, those ones who have come will tell you, okey, naomba mtusaidie ili tuanze kikao hiki na kabla hatujawajulisha, kwanza naomba Father Mbugwa aanze na Maombi, Father Mbugwa. Susan Mutile: And you should say your name. Father Mbugwa: Katika jina la Baba, la Mwana na Roho Mtakatifu, amina, mwenyezi mungu tunakushukuru kwa mkutano wa 2 leo, tunakuomba uwe nasi tunapojihandaa kwa mkutano ili tuwe na maneno ya kusema, Naomba haya katika njina la Baba, la Mwana na Roho mtakatifu, amina. Mr. Patrick Lumumba: Hiki ni kikao cha mbili kwa marekebisho ya Katiba kwa minajili ya kukusanya maoni ya wananchi, katika harakati za kurekebisha Katiba. Kabla hatujaanza kirasmi, nitawauliza wanachama wa kamati wa sehemu ya uwakilishi Bungeni wa Othaya ambao wako hapa wajijulishe kwa kikao hiki kabla hatujaanza mkutano. Kwa hivi bwana co-ordinator utatuelekeza na wote watajijulisha kabla hatujaanza. Asante. Johnson Mugo : Asante sana bwana Lumumba, nitawaita wanakamati tafadhali mfike hapa mbele, na kabla hawajafanya hivyo, mimi nataka kujijulisha, mimi ndiye Co-ordinator wa CKRC hapa Nyeri na jina langu ni Johnson Mugo, naona bwana Wambugu, mahali popote ako aje na Father Maina, na kitambo aje, ningependa Mrs Mwangi, ajijulishe, tafadhali.
[Show full text]