Constitution of Kenya Review Commission (Ckrc)
CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, NYERI TOWN CONSTITUENCY HELD AT NYERI TOWN HALL ON April 19, 2002 CONSTITUENCY PUBLIC HEARING , NYERI CONSTITUENCY, HELD AT NYERI TOWN HALL ON 19TH APRIL, 2002 Present: 1. Mr. Keriako Tobiko - Commissioner 2 2. Ibrahim Lethome - Commissioner 3. Com. Bishop Njoroge - Commissioner Secretariat Staff in Attendance: 1. Stephen Wanjohi - Programme Officer 2. Dan Juma - Asst. Programme Officer 3. Josephine Ndung’u - Verbatim Recorder 4. Leah Omondi - Sign Language Interpreter Prayer: Our Heavenly Father in the name of Jesus Chirst , we come here before you Lord, to deliberate things on our new Constitution. God we want to ask you to be with us. Send us the Holy Spirit Lord which will enable us to say the right things and guide us in everything we might say. God help us and guide us, be with us from now upto the end. Lord we ask this in Jesus name, Amen. Stephen Wanjohi: Ningependa ku-introduce staff wachache tumekuja na wao kutoka Nairobi, mimi naitwa Stephen Wanjohi, programme Officer. Huyu mama anaitwa Josephine Ndungu, ata-tape ile mambo yote munasema, atapeleka kwa Commission. Tuko na mama anaitwa Leah Omondi, simama wakuone. Leah Omondi ni sign language interpreter na tuko na repotuer anaitwa Dan Juma ni kijana wa university, School of Law ndiye anachukua minutes hapa. Com. Keriako Tobiko: Hamjamboni, kwa jina naitwa Keriako Tobiko, mimi ni Commissioner wa tume hii ya kurekebisha Katiba. Com. Ibrahim Lethome: Hamjambo, asalamu alaikum, jina langu ni Commissioner Ibrahim Lethome. Asanteni Com. Bishop Njoroge: Hamjamboni, jina langu ni Commissioner Bishop Bernand Njoroge, na mimi nitakuwa chairman wa kikao hiki, na ninafurahi kwasababu ya kuja kwenu, na ninatumai ni kwa sababu hii ambayo tumepatiwa kama wakenya tuweze kutoa maoni, tutaitumia kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe, na kwa inchi yetu.
[Show full text]