Tarehe 10 Februari, 2021
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Saba – Tarehe 10 Februari, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatazo iliwasilishwa mezani na: NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Mwaka ya Benki Kuu ya Tanzania kwa Mwaka 2019/2020 (The Annual Report of Bank of Tanzania for the year 2019/2020). Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha Mapitio ya Nusu Mwaka, 2020/2021 (Monitory Policy Statement: The Mid - Year Review 2020/2021). NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Rorya, sasa aulize swali lake. Na. 88 Daraja la Mto Mori – Rorya MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Mto Mori kwani mto huo umekuwa ukisomba watu na kusababisha vifo kwa wananchi wanaofuata huduma upande wa pili? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Mto Mori unakatisha katika barabara ya Kirogo-Nyamaguku yenye urefu wa kilomita 15, ikiunganisha Tarafa za Luo-imbo, Suba na Nyancha katika Wilaya ya Rorya.
[Show full text]