MKUTANO WA NNE Kikao Cha Ishirini Na N
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nane – Tarehe 19 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne. S. Makinda ) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa fedha 2011/2012. MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII - MHE. MARGARET S. SITTA: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka 2010/2011 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI – MHE.CHRISTOWAJA G. MTINDA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Juu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 258 Gharama ya Kituo cha Afya cha Kharumwa MHE. HUSSEIN NASSOR AMAR aliuliza:- 1 Kituo cha afya cha Kharumwa kinazidiwa uwezo kutokana na kupokea wagonjwa wengi kutoka Jimbo la Nyang’hwale na Wilaya za jirani. Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ziara za kampeni Jimboni humo, aliahidi kukipandisha hadhi kituo hicho kuwa hospitali za Wilaya ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa:- Je, gharama za upanuzi huo zitakuwemo kwenye Bajeti hii ya mwaka 2010/2011? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kituo cha afya cha Kharumwa kinatumika kama Hospitali ya Wilaya mpya ya Nyang’hwale. Mpango wa Serikali ni kukiboresha kituo hicho ili kiweze kutoa huduma bora kwa wananchi wa eneo hilo. Katika mwaka 2010/2011 Halmashauri ilitumia shilingi 9.8 wa ajili ya kujenga tanuru la kuchomea taka hatarishi (Incinarator). Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya mwaka 2011/2012 Halmashauri imewasilisha maombi maalum Wizara ya Fedha na Uchumi ya shilingi milioni 700 kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha Afya cha Kharumwa. Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika Bajeti ya mwaka 2011/2012 imetenga shilingi milioni 42.4 kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM) kwa ajili ya kuboresha Wodi za wagonjwa na kupanua chumba cha upasuaji wa kituo hicho. Aidha, shilingi milioni 30 zimetengwa katika Bajeti ya Halmashauri kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Mheshimiwa Spika, mpango wa muda mrefu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ni kujenga Hospitali ya Wilaya katika Wilaya mpya ya Nyang’hwale itakayoanzishwa. Eneo la ujenzi wa hospitali hiyo limetengwa katika eneo lililopo Kharumwa kutokana na kituo cha afya Kharumwa kuwa na eneo dogo. MHE. HUSSEIN AMAR NASSOR: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, pia naipongeza Serikali kwa kukipandisha kituo cha afya na kuwa hospitali ya Wilaya, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa sababu msongamano wa wagonjwa katika kituo hicho cha afya ni mkubwa na mpango huu wa kukiboresha kituo hicho ni wa muda mrefu kidogo. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuweza kuwapeleka Madaktari, Wauguzi na kupeleka madawa kwa haraka ili kuweza kupunguza msongamano huo? (b) Je, Waziri utakuwa tayari kufanya ziara katika Jimbo la Nyang’hwale katika Kata ya Nyang’hwale ili kuweza kukiangalia kituo cha afya kilichopo ambacho kina 2 majengo mazuri kilichotelekezwa na kuweza kuangalia matatizo mbalimbali yaliyopo katika zahanati za Jimbo hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, hiki anachosema Mbunge kwamba kuna msongamano, ni kweli, na mimi mwenyewe nimefika katika Wilaya hii mpya inayozungumzwa hapa. Population yao ni laki nne na wana vituo viwili tu vya afya ambavyo vinafanya kazi. Kituo cha afya kwa wastani kinakuwa na watu kama elfu 50 sasa you can imagine kama wapo watu laki nne, hilo ni tatizo. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, anachosema hapa Mbunge kwamba kituo hiki ambacho Rais aliahidi kwamba kitapanuliwa, kitapanuliwa kama tulivyoeleza kwenye mpango huu unaozungumzwa hapa, na pembeni ya hospitali hapo kuna eneo ambalo tumelipata ambalo ndilo litakalotumika kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunapanua ile hospitali ya Wilaya ambayo tumeizungumzia hapa. Mheshimiwa Spika, ningependa kutahadharisha tu kwamba wapo wananchi ambao wanajiingiza katika lile eneo na wanataka kuchukua lile eneo, nimemwelekeza Mkurugenzi Mtendaji ahakikishe kwamba anapata Hati Miliki. Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Madaktari na Madawa sisi hatuna tatizo kwa sababu tutazungumza na wenzetu wa Wizara ya Afya. Kuna kitu kinachoitwa intergrated logistic system ambacho kinatusaidia kujua kiasi cha dawa kinachohitajika katika eneo na wakati huo huo kujua Madakatri wanaohitajika katika lile eneo. Mheshimiwa Spika, naomba Mbunge tuwasiliane naye ili tuweze kumsaidia kwa sababu nimefika katika eneo lile na kitu anachosema ni kweli. Mimi naomba nimpongeze hapa kwa kazi nzuri anayoifanya. Mbunge huyu tangu amekuja hapa ameshauliza maswali mengi sana yanayohusu maendeleo ya Mkoa huu mpya, kwa hiyo nampongeza sana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kuhusu hiki kituo anachozungumza cha kutelekezwa hapa, wanaojenga hospitali ni Halmashauri, wanaojenga vituo vya afya ni Halmashauri, wanaojenga zahanati ni Halmashauri wala siyo Wizara ya Afya na ndiyo maana tunajibu maswali haya. Kama kuna kituo ambacho kimetelekezwa hapa maelekezo yangu ni kwamba wakutane na waseme kwamba kituo hiki tunataka kukinyanyua, kifanye kazi ili kiweze kuwasaidia kuwaendeleza wananchi kiafya. (Makofi) MHE. SAID MOHAMED MTANDA:Mheshimiwa Spika nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, kituo cha afya cha Kitomanga ni miongoni mwa vituo ambavyo Rais aliahidi kukipandisha hadhi na kuwa hospitali ya Wilaya, na kwa kuwa tayari Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini imetenga fedha shilingi milini 40 kwa ajili za wodi za wagonjwa katika eneo hili. 3 Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kukifanya kituo hicho kuwa hospitali kamili ya Wilaya kwa kukamilisha kazi zilizobaki? SPIKA: Swali ni jipya kabisa, lakini kwa sababu Waziri anazunguka sana basi ajibu swali hilo. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, hili eneo analolizungumzia nimefika, anazungumzia eneo linaloitwa Bamvua, hawa wana matatizo. Mbunge ameomba niende katika Wilaya yake, mimi ninamwahidi kwamba nitakwenda kule na nitazungumza na Waziri Mkuchika akiniruhusu nitakwenda kuangalia kituo hicho ili nione. Mheshimiwa Spika, nampongeza pia Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya, huyu anashughulika na mambo ya maji anahangaika na watu wake pale. Mimi napenda kuwaambia wananchi wa Mchinga wamefanya kazi nzuri ya kumleta mtu wa namna hii mwenye uzoefu mkubwa amefanya kazi katika Chama. Kwa hiyo tutamsaidia kuona jinsi tutakavyosaidia katika hospitali hii anayoizungumzia hapa. (Makofi) Na. 259 Hospitali ya Rufaa ya Musoma MHE. VINCENT J. NYERERE aliuliza:- Wananchi wa Musoma na Mara walichanga na kujenga hospitali katika eneo la Kwangwa:- Je, ni lini Serikali itaendeleza ujenzi na kumaliza Hospitali hiyo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vincent Joseph Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, nia ya Serikali ya kuendeleza ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara ya Kwangwa bado ipo. Hatua mbalimbali za wananchi ili kuchangia ujenzi huo zilianza mwaka 1985. Hata hivyo, pamoja na michango ya wananchi iliyochangwa wakati ule iliyofikia kiasi cha shilingi 47,408,158 zilitosha kufikisha ujenzi wa hospitali hiyo hapo ilipofikia. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na hospitali ya Rufaa katika Mkoa wa Mara, uongozi wa Mkoa wa Mara katika Bajeti ya mwaka 2011/2012 umewasilisha maombi maalum ya shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo hadi kiwango ambacho kitawezesha kutumika. 4 MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Waziri, ningependa kujua kwakuwa Bajeti tayari imeshapita ni kiasi gani sasa kinatolewa kwa ajili ya hospitali hii? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI):Mheshimiwa Spika, hospitali hii inayozungumziwa hapa ni hospitali ambayo Waziri wa Afya ameizungumzia kwa muda mrefu sana na majibu alieza hapa kwamba ni kazi gani ambazo zinafanyika pale. Moja ya vitu ambavyo Waziri wa Afya amelizungumzia ni jinsi ya kuangalia namna ya kuendeleza utaratibu ule ule uliotumika kwa maana ya kuchangisha wananchi, kuhakikisha kwamba hela hizi zinapatikana kwa ajili ya kuweza kumalizia kazi zinazofanyika pale. Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuwapongeza sana wananchi wa Mkoa wa Mara kwa kazi yao nzuri iliyofanyika pale na kwa mchango wao mkubwa ambao waliufanya pale ndiyo maana tumetafuta hiki kiasi kilichotamkwa hapa. Mheshimiwa Spika, mimi nimemwita RAS amekuja ofisini jana, nikamwuliza swali hili ambalo Mbunge analiuliza. Je, Serikali imetenga kiasi gani kwa ajili suala hili kwa sababu walipeleka maombi maalum, mpaka sasa hivi hatujapata majibu kutoka Hazina kwa sababu maombi maalum siyo maombi yanayokuja