Constitution of Kenya Review Commission
CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, ALDAI CONSTITUENCY, HELD AT KOBUJOI DEV. TRAINING INSTITUTE Thursday, July 4, 2002 CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, ALDAI CONSTITUENCY, ON THURSDAY, JULY 4, 2002 AT KOBUJOI DEV. TRAINING INSTITUTE Present: Com. Charles Maranga - Chairing Com. Mosonik Arap Korir Com. Abida Ali-Aroni Secretariat in attendance: Hassan Mohammed - Programme Officer Anne Cherono - Assistant Programme Officer Susan Mutile - Verbatim Reporter Com. Charles Maranga: Ningetaka kumuita chairman wa 3Cs ili tuweze tukapata mwenye kutuongoza kwa maombi kwanza. Asante. District co-ordinator: Nitamuita Father Kiplang’at atufungulie kikao hiki na maombi. Karibu Father Kiplang’at Fr. Kiplang’at: Nitawaomba tusimame wote ili tuweze kuomba msaada wa Mungu. Kwa jina la Baba na la mwana na la Roho Mtakatifu Amina. Baba yetu uliye binguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike utakalo lifanyike duniani kama mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea usitutie katika kishawishini, lakini utuopoe maovuni. Mungu Baba, tunakushuru kwa zawadi ya maisha yetu, tunakushukuru kwa kutuweka Kenya, kama wananchi wa Kenya, tunakushukuru kwa nchi yetu ya Kenya, tunakushukuru kwa viongozi mbali mbali, unaoendelea kututeulia, tunakushukuru kwa zawadi ya siku ya leo ambayo wewe mwenyewe umeanzisha, tunakuomba ili 2 uwe nasi ili yale yote ambayo tutaweza kuchangiana pamoja yawe ya kutujenga na kujenga nchi yetu, kuleta amani upendo na umoja. Tunaomba wale wote watakaoongea uweze kuwapa Roho Mtakatifu, ili yote ambayo pamoja tutaongea yawe ya kutoka kwako na kutujenga kimwili na roho. Tunaomba baraka zako kwa Kristu Bwana Wetu Amina.
[Show full text]