1 Bunge La Tanzania
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Ishirini – Tarehe 4 Julai, 2005 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. ABDISALAAM ISSA KHATIBU): Taarifa ya Mwaka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwa Mwaka 2003/2004 (The Annual Report of the Institute of Finance Management for the Year 2003/2004) Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Mfuko wa Ukusanyaji Madeni Sugu ya Mashirika ya Umma kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 June, 2004 (The Annual Report and Accounts of the Loans and Advancers Realization Trust for the year ended 30th June, 2004) NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO : Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2005/2006. MHE. SOPHIA M. SIMBA – MWENYEKITI KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII: Maoni ya Kamati ya Maendeleo ya Jamii kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2005/2006. MHE. TEDDY L. KASELA – BANTU MSEMAJI WA UPINZANIA KWA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO: 1 Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2005/2006. MASWALI NA MAJIBU Na. 186 Taarifa Sahihi za Mtumishi Anayestaafu MHE. MWANNE I. MCHEMBA aliuliza:- Kwa kuwa, Mtumishi wa Serikali anapofikia umri wa kustaafu, taarifa za utumishi wake hutayarishwa na mwajiri wake na kuwasilishwa hazina kwa ajili ya kuandaa malipo ya pensheni na stahili nyingine zote na kwa kuwa, taarifa hizo huandaliwa kwa urahisi na mwajiri kwa wale Watumishi ambao taarifa zao zinaeleweka kama tarehe, mwezi na mwaka ambao mtumishi amezaliwa na taarifa za utumishi wake kwa ujumla:- (a) Kwa wale Watumishi ambao hawajui tarehe na miezi waliyozaliwa, pengine wanafahamu mwaka tu. Je, taarifa za Watumishi wa aina hiyo zinaandaliwa kwa kuzingatia kigezo gani? (b) Kabla ya kuandaliwa kwa taarifa za Watumishi hao je, wahusika wanapewa taarifa ya awali juu ya tarehe na mwezi wanaotakiwa kustaafu kabla taarifa zao hazijapelekwa hazina ili wajiandae. Kama wanapewa taarifa hizo zinatolewa miezi mingapi kabla ya kuzipeleka Hazina? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (UTUMISHI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Mwanne Mchemba, Mbunge wa Viti Maalum - Tabora, naomba kwanza kutoa maelezo mafupi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma, toleo la pili la mwaka 1994, mtumishi akiajiriwa kwa mara ya kwanza katika Utumishi wa Umma anapaswa kutoa taarifa zifuatazo:- Kwanza, Kanuni ya Namba D.18 inamwelekeza kupima afya yake ili kumwezesha mwajiri kutambua kama atafaa kwa kazi aliyoomba. Pili, Kanuni ya D.30 inamwelekeza kutoa taarifa kuhusu warithi wake kwa kujaza kadi maalum ya Next of Kin Card. Tatu, Kanuni ya D.31 inamwelekeza kutoa taarifa binafsi katika fomu maalum inayoitwa Personal Record Form ambapo pamoja na mambo mengine mtumishi 2 atatakiwa kujaza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa na kiwango cha Elimu yake kikamilifu. Mheshimiwa Spika, taarifa hizi ni za muhimu sana kwa kuwa zinamsaidia mwajiri na mtumishi mwenyewe katika masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwa ni pamoja na kutambua muda wa kustaafu kazi. Kwa hiyo, zinapaswa kujazwa kwa usahihi na umakini mkubwa. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Mchemba, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya F.47 ya Kanuni nilizozitaja hapo juu wakati wa kutambua muda wa kustaafu kazi wa mtumishi iwapo form ya taarifa binafsi itaonekana kuwa alijaza mwaka peke yake wa kuzaliwa bila tarehe wala mwezi mtumishi huyo atatambulika kuwa alizaliwa tarehe 1 Julai, ya mwaka ule alioutaja. Na ikiwa atakuwa alijaza mwezi na mwaka tu bila tarehe basi atatambulika kuwa alizaliwa tarehe 16 ya mwezi na mwaka ule alioutaja na taarifa zake zote za kiutumishi zitaandaliwa kwa kuzingatia tarehe hizo. (b) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za F.48 (a) na F.50 (b) ya Kanuni nilizozitaja hapo juu watumishi wanatakiwa kutoa taarifa kwa waajiri wao kwa maandishi miezi 6 kabla ya tarehe ya kustaafu. Aidha kwa Kanuni ya F.50 (e) inamwelekeza mwajiri vilevile kufuatilia kwa karibu na kumfahamisha mtumishi kuhusu tarehe ya kustaafu kwake na kuhakikisha kuwa mtumishi haendelei kufanya kazi baada ya kufikia umri wa kustaafu kisheria. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa kuzingatia Kanuni hizo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kwa barua yake yenye Kumb. Na. MUF/3/33/464/A/117 ya tarehe 27 Oktoba, 1997 iliwakumbusha waajiri wote na kuwataka wazingatie Kanuni hizo kikamilifu na wajibu wao wa kuwakumbusha watumishi. Na. 187 Upandishaji Vyeo Watumishi wa Serikali MHE. HAMIS J. NGULI (K.n.y. MHE. MGANA I. MSINDAI) aliuliza:- Je, Serikali imefikia wapi katika kupandisha vyeo Watumishi wa Serikali wakiwemo:- (a) Walimu wale wa zamani na hawa wapya ambao wanajikuta wamelundikana sehemu moja bila kujali waliotangulia kuajiriwa, elimu na kadhalika? 3 (b) Je, ni kitu gani kilisababisha msongamano huo na Serikali imechukua hatua gani kuondokana na hali hiyo isije kurudia tena? (c) Kwa kuwa, Serikali imebadilisha utaratibu wake wakuwapandisha vyeo Watumishi wake kwa kuingia mkataba kati ya Mwajiri na Mwajiriwa na wakati huo huo vitendea kazi bado ni duni na haba mpango wenyewe haueleweki kama vile walimu kukosa vitabu na vifaa vingine vya kufundishia. Je, utaratibu huo utafanikiwa kwa kutumia vigezo gani? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (UTUMISHI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mgana Msindai, Mbunge wa Iramba Mashariki, lenye sehemu (a), (b) na ( c) kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, katika kuboresha Utumishi wa Umma Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya zoezi la tathmini ya kazi ambapo miundo ya Utumishi ilipunguzwa kutoka 260 hadi 163 zoezi hilo lilifanyika kwa kuunganisha kada zinazofanana kimajukumu na kielimu, matokeo yake ikiwa ni kupunguza ngazi zilizopo katika miundo ya Utumishi ili zilingane na ngazi mpya za mishahara zoezi hili ambalo lilikamilika mwaka 2003 limesaidia sana kuboresha mfumo wa mishahara katika Utumishi wa Umma kwa kupunguza ngazi za kupanda hivyo watumishi kuchukua muda mfupi kupanda kama atakuwa na sifa stahili na bidii kazini. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa zoezi hili na tathmini ya kazi yamejitokeza matatizo hususan ya mlundikano wa Watumishi wa muundo tofauti katika kazi. Sababu ya msingi ikiwa ni watumishi waliocheleweshwa kupandishwa vyeo kujikuta wamekuwa ngazi moja na wale walioajiriwa nyuma. Serikali inatambua kuwepo kwa tatizo hili na imechukua hatua kwa kuwaagiza waajiri mbalimbali kukamilisha zoezi la kuwapandisha vyeo watumishi kabla ya kuanza utekelezaji wa zoezi hili la tathmini ya kazi. Pamoja na hatua hiyo, Serikali imetoa Waraka Na. C/CB/178/123/01/17 wa tarehe 10/3/2005 kwenda kwa waajiri wote kuwataka wawasilishe katika Ofisi yangu taarifa kuhusu Watumishi wote waliolundikana katika cheo kimoja kwa madhumuni ya kuelewa ukubwa wa tatizo na kisha kuchukua hatua nyingine za lazima. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kifungu Na. 6 (1) (a) na (b) mamlaka kuhusu ajira, upandishwaji vyeo na uthibitishwaji kazini kwa Watumishi, yamepelekwa kwa waajiri. Aidha, ni kweli pia kwamba, upandishwaji vyeo utazingatia matokeo ya kazi na kwamba, mwajiri na mtumishi watawekeana mkataba wa kazi ambao upimaji wake utafanyika kwa uwazi. Mheshimiwa Spika, ni kweli vilevile kwamba mkataba huu wa kazi unatamka mtumishi na mwajiriwa kuzingatia suala la vitendea kazi vitakazohitajika katika kufikia makubaliano hayo. Ninapenda kuwaondoa hofu watumishi kuwa kukosekana kwa 4 vitendea kazi hakutegemewi kuathiri utendaji kazi kwa watumishi kwani atakuwa na nafasi ya kueleza sababu zilizomfanya asitekeleze malengo yake ikiwa ni pamoja na suala la vitendea kazi. Mtumishi hawezi kuadhibiwa kutokana na mwajiri kushindwa kumpatia vitendea kazi. MHE. HAMIS J. NGULI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Nashukuru pia kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Lakini je, kwa kuwa wapo watumishi wengine ambao wamesimama kwa muda mrefu kupandishwa vyeo na sasa hivi wako karibu hata kustaafu. Na kwa kuwa Mheshimiwa Waziri anasema mpaka taarifa zipelekwe kwake ili aweze kutathimini ni ukubwa kiasi gani ambao watumishi hao wapo. Je, atawahi kiasi gani kuweza kuwapandisha hao watumishi vyeo ambao wengine tayari sasa hivi wamekaribia kustaafu? Mheshimiwa Spika, kwa kuwa utaratibu huu wa kuwapandisha watumishi vyeo kulingana na kazi wanazozifanya bado mpya ni kiasi gani elimu imetolewa kwa ajili ya kuelimisha kwanza waajiri pamoja na watumishi wenyewe hasa vijijini? Ahsante. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (UTUMISHI): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali miwili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nguli kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kati ya wale ambao wameathirika na utekelezaji wa tathmini ya kazi ni pamoja na wale ambao karibu wanastaafu na kwa mujibu wa barua tuliotuma au waraka tuliotuma tumewaomba waajiri wahakikishe wanazifikisha taarifa hizo mapema na Ofisi yangu itahakikisha kwamba inachukua hatua ya kuwakumbusha ili walete taarifa. Lakini