Verbatim Report of Constituency
CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, SOTIK CONSTITUENCY, HELD AT NATIONAL CEREALS & PRODUCE DEPORT NDANAI ON Friday 12th July 2002 CONSTITUENCY PUBLIC HEARING SOTIK CONSTITUENCY HELD ON FRIDAY 12TH JULY 2002 AT NATIONAL CEREALS & PRODUCE DEPOT NDAWAI PRESENT 1. Com. Prof. A. I. Salim 2. Com. Wanjiku Kabira 3. Com. Abdizak Nunow SECRETARIAT IN ATTENDANCE 1. Collins Mukewa - Programme Officer 2. Robert Machatha - Assistant Programme officer 3. Vivian Muli - Verbatim Recorder 4. Joseph Koros - District Co-ordinator The meeting was called on order at 10.35 with Com. Nunow in the Chair. Com. Nunow: Nadhania hiki ni kikao cha tume, cha kurekebisha Katiba katika Sotik Constituency, na tungependa kuanza na kama kawaida katika vikao vyetu vyote huwa tunaanza kwa maombi. Tungepata mtu wa kujitokeza kutuongoza kwa maombi, someone to say the prayers for us. (not clear) endelea kujitokeza. Bwana Koros huko? Bwana Koros ambaye ni mwana kamati wa Constituency. Interjection: Ameenda kuita watu. 2 Com. Nunow: Okay, nani mwingine atatuangoza kwa maombi. Mheshimiwa Kimeto: Natuombe. Eeh mwenyezi Mungu, mwenye kuunda dunia na binguni, tunakuomba Mungu tutusaidishe kwa mambo yote tunayoyafikiria juu ya Katiba yetu, ili nchi yetu ipate kubadilika, kimawazo ku-uchumi, na yale yote mambo ya maendeleo. Mwenye enzi Mungu tunakuomba utusaidishe, utuongoze kwa kila njia, kwa kila namna. Uongoze wale ambao wanakuja kutoa maoni yao juu ya Katiba katika nchi hii, ili nchi ipate mafanikio mema katika siku za usoni. Mwenyenzi Mungu tunaomba kwa jina la Yesu Kristo muumba wetu, Amina. Com. Nunow: Asante sand Mheshima kwa maombi. Sasa ningependa majoa kwa moja niende nikiwajulisha wanatume wenzangu, na wafanyi kazi wa tume ambao wamekuja katika kikao hiki.
[Show full text]