Wasifu Mfupi wa BIN Hasan (a.s.)

Mwandishi: MOHAMED RAZA DUNGERSI, Ph.D.

Mtarjuma: MUHAMMAD S. KANGU

Kimetolewa na : Bilal Muslim Mission of Tanzania S.L.P. 20033 Dar es Salaam - Tanzania Toleo la Kwanza: Sha‘ban 1434 / Juni 2013 Idadi: Nakala 1000

Fedha kwa ajili ya uchapishaji ilitafutwa na : BILAL COMREHENSIVE SCHOOL

Kimetolewa na : BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA S.L.P 20033 DAR ES SALAAM - TANZANIA YALIYOMO

Dibaji . . . 1

Utangulizi . . . 4 Sura 1: Imam Muhammad bin Hasan (a.s.) Al-Mahdi: Kuzaliwa Kwake na Maisha ya Utoto. . . . 6 Sura 2: Imam Mahdi (a.s.): Ghaibat Fupi na Ndefu (Ghaibat Al-Sughra na Ghaibat Al-Kubra) . . . 18 Sura 3: Filosfia ya Ghaibat . . . 31 Sura 4: Yako Wapi Makazi ya Imam Mahdi (a.s.) . . . 40 Sura 5: Majukumu na Wajibat za Wafuasi wa Imam (a.s.) Wakati wa Kipindi cha Ghaibat . . . 42 Sura 6: Kujitokeza Tena kwa Imam Mahdi (a.s.) . . . 48 Sura 7: Raj’at (Marejeo) . . . 56 Sura 8: Miujiza ya Imam Mahdi (a.s.) . . . 60 Sura 9: Semi za Imam Mahdi (a.s.) . . . 63

Maswali . . . 66 DIBAJI

Hivi ndivyo ilivyoanza.

Nilipokea barua kutoka kwa Mhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, Allama Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, akiniomba niandike masomo ya kufundisha kwa ajili ya Masomo ya Kimataifa kwa njia ya Posta juu ya Historia ya Uislamu ambayo Taasisi hii imekusudia kuyafanya. Kuwa muwazi zaidi, jukumu langu lilikuwa ni kuandika Vitengo (Units) tofauti 13, katika muundo wa vijitabu, vikiwa na maelezo mafupi ya wasifu wa maisha ya Hadhrat Fatima (s.a.) na Maimam Masoom 12. Madhumuni yalikuwa: Vijitabu hivi viwe rahisi kusomwa, vikikusudiwa kwa ajili ya Mashia/Waislamu wapya na vijana wa jumuiya ya Waislamu, wanaotafuta elimu kuhusu Maimam Masoom. Allama Rizvi kwa makhususi alisema kwamba vijitabu hivi havikukusudiwa kwa ajili ya wanachuoni bali wasomaji wa kawaida na kwa hivyo lazima viepuke mitego ya kiusomi.

Kwangu mimi, ina maana ya heshima ya pekee na utambuzi. Kwamba Allama Rizvi, mmoja wa waandishi na mwanachuo mashuhuri katika ulimwengu wa Shia, lazima ameniona mimi kuwa na uwezo wa kuelewa majukumu haya, ni kitu ambacho kamwe sijawahi kukiwazia katika ndoto zangu za kawaida! Sasa kwa vile fursa hii ilikuwepo pale, nilikubali changamoto hii kwa sababu mbili. Kwanza, hii itanipa mimi fursa adimu ya kufanyakazi chini ya usimamizi wa karibu wa Allama Rizvi, ambaye mwongozo wake utafungua maeneo makubwa ya ujuzi kwa ajili yangu katika nyanja muhimu za Historia ya Uislamu. Pili, nitakuwa ninafanya kazi ambayo inaweza kuwa sababu kwangu mimi kupata ‘SAWAB-E- JARI’ mara tu nitakapoondoka ulimwenuni hapa kwenda Akhera.

Nilikubali tume hii. Matokeo ya mara moja yalikuwa ni kitengo cha kwanza katika muundo wa kijitabu: IMAM (a.s.) kilichotoka mwaka wa 1992. Kijitabu hiki kilitoka baada ya

1 kupitiwa na kutathminiwa na Allama Rizvi mwenyewe. Kwa baraka za , kilipokelewa vizuri sana na jumuiya. Nilitiwa moyo na mwanachuoni mwinginc mashuhuri, Malim Ali Mohamed Jaffer wa Bilal Muslim Mission of Kenya. Alinisifia kwa kuweza kutoa kijitabu rahisi lakini chenye taarifa muhimu, ambacho kinafaa kwa wale wenye haja ya kupata ujuzi kuhusu Maimam kutoka Familia ya Mtume (s.a.w.w.). Aidha, Malim Ali Mohamed Jaffer alisisitiza kwamba lazima niendelee mbele na kutoa vijitabu kwa ajili ya Maimam 11 waliobakia. Na nilifanya hivyo, kitengo kwa kitengo, katika miaka iliyofuatia.

Nilipokuja kufikiria, niliona kwamba ukamilishaji wa mradi huu haikuwa safari nyepesi kwangu. Jukumu hili lilihusisha utafiti mkubwa na mpana, ukitumia muda mkubwa na nguvu. Hii ni kwa sababu kuandika kwa ajili ya maisha ya watu hawa mashuhuri kuna hitaji hadhari ya hali ya juu katika kutumia taarifa sahihi na uteuzi wa maneno yanayofaa. Ukiongeza juu ya hili, mradi huu ulikuwa katika mfumo wa hiyari na ulikuwa ufanywe wakati ambao nilikuwa na kazi ya kila siku kwa ajili ya kunipatia kipato cha kujikimu.Vipengele vyote hivi huelezea ni kwa nini imechukuwa muda mrefu kiasi hiki kwa mimi kukamilisha mradi huu; kitabu moja kwa wakati kuanzia 1992-2010. Kijitabu cha mwisho kutolewa kilikuwa juu ya maisha ya lmemu wetu wa 11 Hadhrat Hasan Askari (a.s.) na kilichapishwa katika mwaka wa 2001.

Baada ya kupita miaka mingi, kitabu cha mwisho juu ya maisha ya Imam Mahdi (a.s.), Allah amuweke salama na aharakishe kujitokeza kwake tena, sasa kiko mikononi mwako. Inasikitisha kwamba Allama Rizvi hayuko tena nasi leo kushuhudia ukamilishaji wa mradi huu. Malim Ali Mohamed Jaffer, pia ameondoka kwenye ulimwengu huu wa mpito kuelekea ulimwengu wa mwisho - Akhera. Allah awalipe wanachuoni hawa wawili maisha ya milele ya furaha kwajuuhdi zao kwa ajili ya Kumtumikia Yeye.

2 Nitakuwa sitendi haki kama sitashukuru juhudi za Al-Haj Fidahusein Hameer, mmoja wa wazee waasisi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania. Fidahusein bhai ameonesha kiwango kisicho na mafano cha subira na uvumilivu katika kushughulika na ukawiaji wangu kuhusu ukamilishaji wa mradi huu. Hakuna ambaye angeweza kuvumilia ucheleweshai huu kwa muda mrefu kiasi hiki na zamani sana angekwisha achana na mimi. Lakini sio Fidahusein bhai. Kukumbusha kwake kwa mara kwa mara lakini kwa upole kumeleta faida. Allah amlipe malipo mema na ampe maisha marefu yenye siha ili aendelee kuhudumia katika njia Yake.

Yote yamesemwa na kufanywa, nimefanya hadhari kubwa kuondoa makosa ya aina yoyote, kiukweli au vinginevyo, kutoka kwenye kazi hii. Hata hivyo, kama kuna kosa la aina yoyote ile, zito au jepesi, Naomba msamaha wa Allah.

Mohamed Raza Mohamed Husein Dungersi, Ph.D. New York, Marekanu 6 Juni 2010 22 Jamdiul-Thani 1431

NYONGEZA Kabla ya kuchapishwa kwa kijitabu hiki, Haji Fidahusein bhai Hameer alifariki dunia mwezi Februari 6 2011.

Faraja yangu pekee ni kwamba niliweza kumkabidhi muswada wa kijitabu hiki wakati wa uhai wake na aliondoka ulimwenguni hapa akijua kwamba kazi hii imekamilika. Allah aipumzishe roho ya Marhum katika ujirani wa Masoomeen wetu 14.

Februari 1, 2012 1 Rabiul Awwal 1433 New York, Marekani

3 IMAM MUHAMMAD BIN HASAN AL-MAHDI (A.S.)

UTANGULIZI “Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa.” (3:169)

Maimam wote wateule kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) (ambao kuhusu maisha yao tayari tumekwisha yajadili kwenye vijitabu vilivyotangulia) waliuliwa katika huduma ya njia ya Allah. Imam Ali (a.s.) aliuliwa wakati akiwa anasali swala ya alFajr katika msikiti wa Kufa. Kichwa cha Imam Husayn (a.s.) kilikatwa akiwa kwenye sajda katika uwanja wa mapambano wa . Maimam (a.s.) wengine tisa waliobakia wote waliuliwa kwa sumu, hivyo, maisha yao ya kimwili yaliishia katika njia isiyo ya kawaida. Kwa hiyo wote walikuwa mashahidi. Kwa mujibu wa aya ya Qur’an iliyonukuliwa mwanzoni, Maimam wote, katika hali ambayo sisi hatuitambui, wako hai na wanapokea riziki yao kutoka kwenye neema za Allah. Imam wa 12 na wa mwisho, Hadhrat Muhammad bin Hasan Askari (a.s.), anayejulikana kama Imam Mahdi, bado hajafariki kimwili. Yeye ni Imam wa zama - Al-Hujjah (Dhihirisho/Thibitisho), Al-Qaim (Mwazilishi) - hivi sasa kwa amri ya Allah, yuko katika “Ghaiba” (Ghaibu) na hafikiwi na waumini ingawa yeye anatambua hali ya kila mfuasi, kwa uwezo aliojaaliwa na Allah. Kwa amri ya Allah atajitokeza tena na kusimamisha utawala wa Allah katika ardhi hii kabla ya kuja kwa Qiyamat (Siku ya Hukumu).

Kwa Waislamu kwa ujumla, na hususan kwa Mashia, ni muhimu kwamba wote wanapata taarifa za msingi kuhusu Hadhrat Mahdi, Allah amlinde katika kipindi hiki cha Ghaibu, na aharakishe kujitokeza kwake tena. Hii ni kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye atakufa na hamjui Imam wake wa zama zake, anakufa kifo cha mjinga (JAHIL).” Wanachuoni

4 wanatafsri ‘ujinga’ kuwa na maana kutokuwa na ujuzi kuhusu mizizi na msingi ya Uislamu. Kwa maneno mengine, maana ya hadithi ni ‘yule anayekufa bila kupata taarifa ya msingi kuhusu Imam mteule wa zama zake, anakufa kifo cha asiye Mwislamu.’

Kwa mukhtasari, taarifa kuhusu Imam wetu wa zama, Hadhrat Mahdi (a.s.), zinaweza kuwekwa katika vigawanyo viwili: taarifa ya awali na ya pili. Taarifa ya awali hujumuisha ujuzi kuhusu hai- ba yake, kuwepo, matendo na kujitokeza kwa mara ya mwisho kwa Imam (a.s.). Kutokana na mwanga huu, tunahitaji kutambua majukumu yetu na wajibu wetu kwa Imam wakati yuko ghaibat yake. Kwa upande mwingine, taarifa ifuatiayo - ya pili inahusisha masuala kama makazi ya sasa ya Imam, alipo, dalili ambazo zitajitokeza kabla ya kujitokeza tena nk. Taarifa hii ni muhimu kuijua, lakini sio ya muhimu sana kama taarifa zilizopo chini ya kigawanyo cha awali.

Katika kitengo hiki, mkazo itakuwa juu ya vigawanyo vyote - cha awali na kifutacho - cha pili kuhusu ujuzi wa kumuelewa Imam wa 12, Hadhrat Mahdi, Allah amlinde katika kipindi hiki cha ghaibu, na aharakishe kujitokeza kwake tena. Msisitizo utakuwa pia juu ya jukumu la “Marjah” (wale ambao wako katika kipindi cha Ghaiba ya Imam (a.s.)).

5 SURA YA KWANZA IMAM MUHAMMAD BIN HASAN (A.S.) AL-MAHDI: KUZALIWA KWAKE NA MAISHA YA UTOTO

UTANGULIZI Dhana ya “Umahidi” (Umasihi), au ujio wa mkombozi katika siku za mwisho za kuwepo kwa uhai katika ardhi hii kama tuijuavyo, sio uzushi wa baadae uliobuniwa na Mashia waliposwagwa mpaka kufikia kiwango cha hofu ya kutisha katika sura ya ukandamizaji kutoka kwa maadui zao. Kwani Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia Waislamu katika mzunguko wake katika nyakati mbalimbali kuhusu kuja kwa Mahdi. Wanachuoni mashuhuri wa Sunni na Shia, wakati wote wamethibitisha hili katika vyanzo vyao maarufu. Kwa mfano, Shaykhul , Shaykh Suleiman bin Ibrahim Al-Qunduzi Al-Hanafi anaandika katika kitabu chake Yanabi ul Mawaddah kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anajadiliana na Myahudi akiitwa Naathaal, alimtangaza Ali bin Abi Talib (a.s.) kama mrithi wake, ambaye baadae atarithiwa na mwanawe Hasan (a.s.) na kisha Husayn (a.s.). Kisha Mtume (s.a.w.w.) alimuambia yule Myahudi kwamba mlolongo wa kurithi utaendelezwa kupitia Maimam tisa, wote wakiwa ni kizazi cha Imam Husayn (a.s.). Yule Myahudi akataka kujua majina ya watoto hawa tisa. Mtume (s.a.w.w.) akawataja kama ifuatavyo: “Baada ya Husayn atakuwa mwanawe Ali bin Husayn, baada yake mwanawe Muhammad bin Ali, baada yake Jafar bin Muhammad, kisha Musa bin Jafar, kisha Ali bin Musa, kisha Muhammad bin Ali, kisha Ali bin Muhammad, kisha Hasan bin Ali na baada yake ni mwanawe Muhammad bin Hasan Al-Mahdi.”

Tena Shaykh Suleiman anasimulia katika kitabu hicho hicho kwamba Sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) Jabir bin Samara alimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Uislamu utabakia maadamu warithi wangu 12 wanabakia, na wote watakuwa wanatokana na Kureish.” Bukhari, Muslim na Tirmidh wanasimulia hadithi kama hiyo hiyo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.).

6 Hata hivyo, baadhi ya wanachuoni wa Sunni, ingawa hawakatai ha- dithi hizi, wanasema kwamba Maimamu 12 waliotaja ni Makhal- ifa wanne wa kwanza na watawala nane kutokana na ukoo Banu Umayya. Hoja hii haina msingi kwa sababu zifuatazo: 1. Maimam wa Banu Umayya ni pamoja na Makhalifa Muawiya, Yazid na Marwan, ambao wote walikuwa wakandamizaji, madhalimu, na dhidi ya Uislamu. Hawawezi kuchukuliwa kama Waislamu, achilia mbali kuwa warithi wa Mtume (s.a.w.w.). 2. Makhalifa wa Bani Abbas walikuwa halikadhalika makatili, kama sio zaidi, wao pia hawawezi kuchukuliwa kama warithi wa Mtume (s.a.w.w.). 3. Kwa muda kidogo na kwa ajili ya hoja, hebu tuwakubali warithi 12 waliotajwa na Sunni; wa mwisho wao atakuwa Umar Ibn Abdul Aziz (kwa mujibu wa Mulla Ali Kari katika Sharhe Mishkat) au Walid Ibn Yazid (kwa mujibu wa Ibn Hajar katika Sharhe Bukhari). Hakuna nyororo ya mfulilizo. Swali linaloibuka ni baada ya kifo cha anayesemekana mrithi wa mwisho, nani atakuwa Imam wa zama? Ambaye atakuwa “Hujja” wa Allah katika ardhi ambaye bila huyo ulimwengu wote utakoma kuwepo?

Ni wafuasi wa Madhebu ya Jafary - Shia Ithna-Asheri tu, wanaoamini katika Maimam 12, wa mwisho wao akiwa ni Imam Mahdi (a.s.) ambaye bado yu hai. Kila mmoja wa Maimam hawa alikuwa ni kiigizo cha taqwa na watakatifu, wakikubaliwa kama hivyo na marafiki na maadui kwa pamoja. Kwa hiyo, ni madhehebu inayofuatwa tu na Mashia ndiyo yenye nyororo ya mfulilizo ya Maimam bila kuingiliwa au kukatika.

Kuna ma-Sunni wengine, ambao wanaamini katika dhana ya Umahdi, lakini wanahoji kwamba Mahdi aliyesemwa bado hajazaliwa. Uwelewa wetu ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba bila ya “Hujja” wa Allah ulimwengu hauwezi kubakia hata joti moja ya sekunde. Kwa hivyo, kama Mahdi bado hajazaliwa, basi

7 ni nani “Hujja” wa Allah katika ulimwengu? Ni fursa katika hatua hii kuangalia kwenye ambao kwamba Imam wa sasa wa zama alivyozaliwa. Inafaa kuzingatia hapa kwamba kuna wanachuoni maarufu wa Sunni ambao hawakiri tu kuzaliwa kwa Hadhrat Mahdi (a.s.), bali pia wanakubali kuwa alikuwa ni mtoto wa Imam Hasan Askari (a.s.). Wanachuoni hao ni pamoja na: Ubaidullah Amritsari (Sawanah Umry Hadhrat Ali), Ibn Khaldun (Tarikh Ibn Khaldun), na Abdul Rehman Jami (Sawai Dunnu Buwah).

KUZALIWA KWA IMAM MAHDI (A.S.) Makhalifa wa Banu Umayya na baadae Bani Abbas, walijua sana kuhusu hadithi ya Mtume (s.a.w.w.), yenye kusimulia kuja kwa Al-Mahdi, ambaye atakuwa Imam mteule wa 12 kutokana na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kupitia kwa bint yake Fatima (s.a.). Kwa dhahiri, wakati Imam wa 11 (a.s.) alipotambuliwa kuwa yuko hai, juhudi za kuzuiya kuzaliwa au kuishiliza kuwepo kwa Imam wa 12 zilizidishwa. Imam Hasan Askari (a.s.), Imam wa 11, aliwekwa kizuizini na kutengwa mbali na familia yake chini ya uangalizi mkali. Wakati Imam Hasan (a.s.) alipofichua mbinu ya mtawa wa Kikiristo, na yeye mwenyewe kupitia maelekezo ya maombi, alizuiya ukame katika Samarra, Khalifa Mo’tamid alimuacha akae na familia yake kwa muda. Ilikuwa ni wakati huo mimba ya Hadhrat Mahdi (a.s.) ilitungwa.

Shaykh Saduq anasimulia kwamba Imam Ali Naqi (a.s.) wakati fulani alimuita mfuasi wake, Bashir Ibn Sulaiman, na akampa jukumu la kwenda soko la watumwa mjini Bahgdad na amnunue mtumwa/kijakazi makhususi. Imam (a.s.) alitoa malezo kamili ya kijakazi huyo: Kati ya dalili ilikuwa kwamba atakuwa katika Hijabu kamili na atakuwa anapinga kuuzwa kwa wanunuzi wote. Bashir atampa barua ambayo alipewa na Imam. Atakaposoma barua hiyo, atamshinikiza mmiliki wa watumwa kukubali ofa hiyo kutoka Bashir. Ofa hiyo ilikuwa Dinari 120; atampata kijakazi huyo na kisha kumleta kwa Imam (a.s.).

8 Bashir anasimulia kwamba alikwenda Baghdad na akashuhudia mandhari hiyo kama vilevile ilivyotabiriwa na Imam Naqi (a.s.). Aliwasilisha barua ile kwa yule kijakazi, ambaye baada ya kuisoma barua ile aliibusu kwa heshima na yeye mwenyewe akajiingiza kuwa katika umiliki wa Bashir. Baadae Bashir alitambua kutoka kwake kwamba alikuwa anatokana na familia ya kifalme ya Mfalme wa kirumi. Alikuwa aolewe na binamu yake lakini ajali baada ya ajali zilitokea kabla ya ndoa yao kufanyika. Kwa ushauri wa watabiri, walisema ndoa yake lazima isimamishwe kwa wakati huo.

Wakati huohuo, aliota ndoto ambayo kwayo ndoa yake na Imam Hasan Askari (a.s.) ilifungwa rasmi na Mtukufu Mtume Isa (a.s.) (kwa vile alikuwa anatokana na kizazi cha Simon, Mfuasi mmojawapo wa Wafuasi 12 wa Mtume Isa) akiwa pamoja na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katika ndoto yake hiyo. Hadhrat Fatima, binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimsilimsha na kuwa Mwislamu. Kisha baadae, alipata ziara mbalimbali katika ndoto zake, kutoka kwa Imam Hasan Askari (a.s.). Wakati fulani Imam alimshauri kujigeuza na kujifanya kama mtumishi wa kawaida na kujiunga katika msafara wa jeshi la Wakiristo ambalo lilikuwa linakwenda kupigana na Waislamu. Katika mapambano hayo atachukuliwa kama mtumwa wa Waislamu na kuishia Baghdad. Imam (a.s.) kisha ‘atampata’ na ataungana na msafara wake.

Alifanya kama alivyoshauriwa na hivi ndivyo alivyofika kwa Bashir. Kisha Bashir akamleta kwa Imam Ali Naqi (a.s.), ambaye alimuozesha kwa Imam Hasan Askari (a.s.).

Mama yake Imam Mahdi (a.s.) anajulikana kwa majina kama haya: Nargis, Sausan, Ryhana na Malika.

Dada yake Imam Ali Naqi (a.s.), Hakima, alipewa jukumu la kumfundisha Uislamu, na akathibisha kuwa mwanafunzi mwenye utashi sana na mwenye uwezo. Ilikuwa ni katika muda

9 mfupi aliokaa na Imam Hasan Askari (a.s.) kwamba alipata ujauzito, uliopelekea kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.); mimba yake ilibakia bila kuonekena, kama ilivyokuwa kwa mama wa Mtume Musa (a.s.). Mimba hii iliwekwa kuwa siri hata kwa jamaa wa karibu wa familia, ikiwa ni pamoja na Hakima. Hakima alikuja kujua mimba ya Nargis wakati tu wa mkesha wa kuzaliwa kwa mtoto. Hakima, dada yake Imam Naqi (a.s.) anasimulia kwamba alimtembelea mpwawe, Imam Hasan Askari (a.s.) mara kwa mara, na kurudi nyumbani kwake wakati wa jioni. Katika mkesha wa mwezi 14 Shaban 255, wakati alipotaka kurudi nyumbani kwake, Imam Hasan Askari (a.s.) alimuomba abaki asiende, kwa vile anategemea kuzaliwa mtoto. Hakima alipatwa na mshangao: “Mtoto huyo mama yake ni nani?” aliuliza. “Mama yake ni Nargis” alijibu Imam. “Lakini hana dalili za ujauzito!” alisema Hakima. Imam Hasan Askari akasema: “Suala la Nargis ni kama la ujauzito wa mama yake Mtume Musa. Ili kumlinda Hujjah wake, Allah aliuweka siri ujauzito wa mama wa Mtume Musa. Kwa hali hiyo hiyo, Nargis amebeba mimba la Hujjah wa Allah bila ya kuonesha dalili, kwa ajili ya ulinzi wake.”

Hakima anasimulia kwamba alibakia. Baada ya usiku kuingia aliamka ili kusali swala za usiku zilizopendekezwa (Salatul Layl). Alimuamsha Nargis ambaye bado haoneshi dalili za ujauzito. Nargis alisali kisha akaenda kupumzika. Punde baada ya hapo alianza kupata uchungu wa kuzaa. Imam (a.s.) alimshauri kusoma aya za Qur’an - Suratul Qadr. Hakima anasema aliweza kusikia kisomo hicho hicho kutoka kwenye tumbo la Nargis! Ilikuwa hapo tena ukatokea mwanga ambao ulienea chumbani na Hakima hakuweza kuona kilichokuwa kinatokea. Wakati kuona kwake kuliporudi, Hakima alishuhudia mtoto tayari amekwisha zaliwa.

Kama ilivyokuwa kwa Maimam wote 11 wateule kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) waliotangulia, Hadhrat Mahdi (a.s.) pia alizaliwa safi ametakasika. Pia alizaliwa akiwa ametahiriwa. Katika mkono wake wa kulia kuna muhuiri wa Uimam unasomeka

10 hivi: “Haki imefika na batili imetoweka. Hakika batili ni yenye kutoweka.” (Qur’an 17:81).

Kama ilivyosimuliwa na Hakima, wakati Imam Mahdi (a.s.) alipozaliwa, alifanya sajda, akasoma Kalimah na kutaja majina ya Maimam 11 waliokuja kabla yake. Wakati alipofikia jina lake alimtaja Muumba wake Azza wa Jallah, alisema: “Ewe Muumba wangu! Tekeleza ahadi Yako kuhusiana na ulinzi wangu, Uongozi (Uimam) wangu na utawala (Ukhalifa) wangu. Nilipie kisasi kwa maadui zangu. Nipe mamlaka yaliyo wazi na kupitia kwangu mimi ujaze ulimwengu na uadilifu.” Hii ilikuwa Ijumaa, mwezi 15 Shaban 255 A.H./868AD.

Kisha mtoto aliletwa kwa baba yake. Wakati akiwa katika mikono ya baba yake, mtoto yule alimtolea baba yake salamu, akarudia kusoma Kalimah na majiana ya Maimam 12. Kisha alisoma aya ya Qur’an: “Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe ni viongozi na kuwafanya ni warithi.” (28:15) Kisha mtoto alipelekwa kwenye mikono ya mama yake, mwenye furaha.

Baada ya muda kidogo, ndege fulani weupe walijitokeza na kumchukuwa mtoto yule. Kiasili, mama yake alitokwa na machozi. Imam Hasan Askari (a.s.) akamfariji, akimuambia kwamba huo ulikuwa mpango wa Mungu ili kumlinda mtoto kutokana na maadui. Hata hivyo, alimuahidi kwamba mtoto atarudi na hatanyonya maziwa ya yeyote yule isipokuwa yakwake.

Hakima anathibitisha kwamba baada ya siku chache wakati alipomtembelea Imam Hasan Askari (a.s.) alimkuta mtoto yule pale, bali tu alikua kwa haraka sana. Imam tena akamuelezea kamba huyu alikuwa mtoto maalumu na kwa amri na rehema za Allah, mchakato wake wa kukua umekuwa wa haraka sana. Hakima anaendelea kusema kwamba wakati alipomuona mtoto punde kabla ya kuuawa shahidi kwa Imam Hasan Askari (a.s.)

11 amechanua kuwa kijana wa kupendeza. Kisha baba yake akamuambia kwamba yeye, baba mtu, hivi punde ataondoka katika ulimwengu huu, na kwamba kijana huyo, mwanawe, atakuwa Imam wa zama. Hakima anahitimisha kwamba kuanzia hapo alikuwa anamtembelea mara kwa mara, alimtembelea na kupata ufafanuzi juu ya masuala ambayo alihitaji kujifunza kwayo.

KUZALIWA KWA IMAM KULIWEKWA KUWA SIRI Kutokana na sababu zilizoelezwa mapema, kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.) kulifanywa kuwa siri isipokuwa kwa jamaa wachache wa familia na wafuasi. Mifano michache inatolewa hapa ili kuonesha vipi habari za kuzaliwa kwa Imam kulifanywa siri, bali wakati huohuo kukafichuliwa kwa watu wachache waaminifu, ili baadae isije kukawa na mkanganyiko kuhusu kuzaliwa kwake. • Hakima, bint wa Imam Taqi (a.s.), aliitwa ili awepo wakati wa kuzaliwa mtoto na baadae awe ni shahidi wa kuona.

• Wakati wa kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.), Imam Askari alimuamuru “Wakil” wake, Uthman Ibn Sayid, kugawa ratili l0,000 (ratili 1 ≈ gramu 406.25) za mkate na ratili 10,000 za nyama kwa ajili ya ‘aqiqah’ ya mtoto aliyezaliwa. Walionufaika na mgao huo walipata dokezo la habari kuhusu kuzaliwa kwa mtoto nyumbani kwa Imam Askari (a.s.). Matokeo yake, baadhi ya wafuasi walipokea habari hizo kwa kumtembelea na kumpongeza katika wakati huu wa furaha ya kuzaliwa mtoto. Hasan Ibn Husayn anasema kwamba alimtembelea Imam (a.s.) na kuonesha furaha zake kwa kuzaliwa kwa mtoto. Mgeni mwingine kama huyo alikuwa ni Abdullah Ibn Abbas Alawi.

• Daw bin Ali anamnukuu mtumishi wa kifurisi wa Imam Askari (a.s.) kuwa alishuhudia kuzaliwa kwa mtoto nyumbani kwa Imam Askari (a.s.).

• Muhammad bin Bilal bin Muhammad anadai kwamba Imam Askari (a.s.) alimjulisha kuhusu mrithi wake.

12 • Abu Hashim Al-Jafari, mfuasi wa karibu wa Imam Askari (a.s.), wakati fulani alimuuliza Imam Askari (a.s.): “Ewe bwana wangu! Je unaye mtoto?” Imam (a.s.) akajibu: “Ndiyo!” Abu Hashim aliendelea kuuliza: “Kama kitu chochote kikitokea kwako, ni wapi tutakapompata?” Imam akajibu: “Mtapata huko Madina”.

• Ahmad Ibn Ishaq, mfuasi wa karibu wa Imam Askari (a.s.), anasimulia kwamba alimsikia Imam (a.s.) akisema: “Shukurani zote anastahiki Allah ambaye hakuniondoa katika ulimwengu huu mpaka aliponionesha mrithi wangu; anaye fanana zaidi na Mtukufu Mtume wa Allah (swt) kwa sura na tabia.” Kusema kweli, kwa mujibu wa taarifa nyingine, Imam Askari aliandika barua kwenda kwa Ahmad Ibn Ishaq, akieleza kwamba: “Mtoto wa kiume amezaliwa nyumbani kwangu. Hata hivyo, taarifa hii inahitaji kuwekwa kuwa siri kabisa isipokuwa kwa wale ambao ni marafiki na wafuasi wangu wa karibu.”

• Muawiya Ibn Hakim, Muhammad Ibn Ayyub na Muhammad lbn Uthman wanaelezea kwamba Imam Askari aliwaita nyumbani kwake watu 40 miongoni mwa wafuasi wake na akawaonesha mtoto mchanga wa kiume aliyezaliwa hivi punde: Hadhrat Mahdi (a.s.).

Mifano mingi kama hii imehifadhiwa katika maandishi kiasi kwamba haiwezi yote kutajwa hapa. Itoshe tu kuzingatia kwamba wakati ambapo kuzaliwa kwa Hadhrat Mahdi (a.s.) kwa ujumla kuliwekwa kuwa siri, bado wakati huo huo baadhi ya marafiki na wafuasi wa karibu walipewa fursa ya kumuona mtoto huyo ili kwamba baadae waweze kusambaza habari hizi kwa ummah wote kwa ujumla.

Wakati ambapo wafuasi na marafiki wachache walijua kuhusu kuwepo kwa Imam Mahdi (a.s.), lakini mahali alipo paliwekwa siri hata kwao. Wakati alipokuwa na wazazi wake, Hadhrat Mahdi

13 (a.s.) alikuwa amefichwa pamoja na mama yake katika lelo (sehemu ya nyumba iliyo chini ya ardhi) - “Sardab”. Mhudumu alikuwepo ili kumleta kwa baba yake inapohitajika. Kwa mujibu wa Jassim Hussain, Imam Askari (a.s.) alimuondoa mwanawe nje ya Samarra. Anamnukuu zaidi Al-Masud kama chanzo chake na kueleza kwamba Imam Askari (a.s.) alimpeleka mwanawe akifuatana na Bibi yake Hadhrat Hadisa kwenda Madina na kuishi huko. Imam Mahdi alirudi Samarra muda tu kabla ya baba yake kuuliwa shahidi na akafanya yale yote ambayo Imam Masoom anatakiwa kufanya kwa Imam Masoom aliyemtangulia ambaye amefariki. Kuwepo kwa Hadhrat Mahdi (a.s.) kulikuwa wazi kabisa wakati alipomuambia ami yake, Jafar kutoa nafasi kwa ajili yake ili aongoze Swala ya maiti. Hili lilipelekea Khalifa kuzidisha kutafuta kwake ili ampate mtoto na kumuuwa. Lakini juhudi zake zote zilikuwa za bure.

MAMA YAKE IMAM MAHDI Ilitajwa mapema kwamba kwa mujibu wa Shaykh Saduq, alikuwa ni mjukuu wa Mfalme wa kirumi alikuja Samarra kama mtumwa/ kijakazi na hatimaye alinunuliwa na kuachwa huru na kuolewa na Imam Hasan Askari (a.s.). Jassim Hussain katika kitabu chake The Occultation of the Twelfth Imam (chapa ya 1982, uk. 68-69), anatia shaka kuhusu utaifa wake kama Mkiristo kutoka familia ya. Kifalme. Anamchukulia kama “mtumwa/kijakazi wa kawaida aliyelelewa katika nyumba ya Hakima, dada wa Imam wa kumi.” Jassim Hussain anatoa sahahu tatu kwa msimamo wake huo:

Sababu ya kwanza: Anasema: “Kulikuwa hakuna vita vikubwa kati ya Banu Abbas na Byzantine baada ya 242/856 na hakuna dal- ili katika vyanzo vyovyote kwamba Mfalme wa Byzantine alitoa maombi kwa Banu Abbas ili kumuacha huru mjukuu wake.”

Udhaifu wa Sababu hii: Syed Ameer Ali, katika kitabu chake A Short History of the Saracens, akijadili mkanganyiko wa kisiasa wa Khalifa Mu’taz

14 anasema: “Byzantine walichukua fursa ya matatizo ambayo yalikuwa yameukumba ukhalifa na kufanya njia mbalimbali za kuingia kwenye himaya ya Waislamu. Mara ya kwanza walibeba kila kitu mbele yao... Baadae walishindwa katika mfululizo wa mapambano.”

Kwa hiyo. kukataa kuja kwa Nargis nchini Iraq juu ya msingi kwamba hakukuwepo na vita vikubwa hakukidhi mahitaji ya historia. Aidha, habari tu ya kwamba hakuna kumbukumbu ya Mfalme kudai jamaa wa familia yake hakuondoi kuwepo kwake katika nyumba ya Imam (a.s.).

Sababu ya Pili: Sababu ya pili ambayo Jassim Hussain anaitoa iko juu ya habari kwamba vyanzo vikubwa ambavyo vinasimulia kuhusu utaifa wa Nargis vimeegemea juu ya simulizi ya Shaybani ambaye alikuwa “Mshabiki”' na kwa hiyo sio ya kutegemewa.

Udhaifu wa Sababu hii: Abu Muhammad al–Fadhl Ibn Shadhan in his Mukhtasaru Ithbati’r – Rajah chini ya hadithi namba 9, anamtaja Muhammad Ibn Abu Jabbar akisema kwamba alimuuliza Imam Askari (a.s.) kwamba ni nani atakaye kuwa mrithi wake. Imam alijibu: “Kwa hakika, Hujjah baada yangu ni mwanangu... ambaye ni Hujjah wa mwisho na Khalifa wa Allah.”

Muhammad aliuliza zaidi: “Atazaliwa na nani?” Imam (a.s.) akajibu: “Kutoka kwa bint wa Siza (Ceaser), mfalme wa Byzantine.”

Kwa nini Abu Muhammad al–Fadhl Ibn Shadhan ni chanzo cha kuaminika? • Alikuwa anaishi wakati ule ule alioshi Imam Hasan Askari (a.s.) na wakati wote alikuwa na mawasiliano naye. Asingeweza kusimulia kuhusu mama wa Imam wa 12 kama alivyofanya isipokuwa alikuwa na uhakika kuhusiana na hilo.

15 • Imam Hasan Askari (a.s.) ana maoni ya hali ya juu sana kuhusu yeye. Wakati fulani Fadhl alipeleka kitabu chake kwa Imam (a.s.) kwa ajili ya uthibitisho wake. Imam (a.s.) alimsifia Fadhl katika maneno haya: “Rehema ya Allah iwe juu ya al-Fadhl. Nawaonea wivu watu wa Khurasan kwa sababu ya al-Fadhl Ibn Shadhan.” Kusema kweli, alikuwa ni sahaba wa Imam Ridha (a.s.), Imam Jawad (a.s.), Imam Hadi (a.s.) na Imam Askari (a.s.). Na amenukuu hadithi nyingi kutoka kwao moja kwa moja.

Hoja kwamba chanzo kinachosimulia kwamba Hadhrat Nargis ni mjukuu wa Mfalme Byzantine hakiaminiki, haina dalili ya kutosha.

Aidha, akifafanua juu ya Muhammad Shaybani kama chanzo kisichoaminika, Sayyid Saeed Akhtar Rizvi anasema hivi: “Muhammad Shaybani ni ‘Majhul’, yaani, hakuna kinachojulikana kuhusu yeye (kwa kujitegemea) au kwa sifa zake. Kwa hali hiyo hatuwezi kusema kwamba ni mwaminifu au si mwaminifu.”

Sababu ya Tatu: Jassim Hussain anahoji kwamba al-Kulayni, al-Numani na al-Saduq wanaelezea kwamba mama yake Hadhrat Mahdi alikuwa “kijakazi mweusi.”

Udhaifu wa Sababu hii: Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (katika jarida la Light Jz. 27 No. 3 Juni 1993 uk. 7-10) anajibu hoja hii na kuonesha makosa yake kwa mantiki na uwazi. Baadhi ya dondoo kutokana na majibu ya Sayyid Saeed Akhtar Rizvi zinatolewa hapa: “Namjua Bw. Jassim Hussain, ni Mwislamu mzuri. Lakini katika suala hili hakuilewa hadithi hiyo sawa sawa. Kumbuka kwamba kuwa tu Mwingereza hakumfanyi mtu kuwa amehitimu kuelewa kila kitabu juu ya filosofia, fizikia, kemia au hisabati za hali ya juu kwa sababu tu vimeandikwa kwa Kiingereza. Hali ni hiyo hiyo katika mafunzo ya Kiislamu pamoja na ....”

Kisha Sayyid Saeed Akhtar Rizvi aliichambua Hadith hiyo

16 iliyoko kwenye mjadala na akathibitisha kwamba bibi wa ki-Nubi aliyetajwa katika Hadith hii ni mke wa Imam al-Ridha (a.s.) na sio wa Imam Hasan Askari (a.s.). Sayyid Saeed Akhtar Rizvi anaendelea kuhoji: “Kwa kusimulia Hadith hii kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), Imam Ridha (a.s.) alitaka kuonesha kwa Ami yake kwamba Mtume alimuita Imam wa 12 (a.s.) kama mtoto wa msichana wa ki-Nubi, na kwamba ilikuwa isitokee kwa yeyote isipokuwa kupitia kwangu (Imam Ridha) kwa sababu Imam wa 8 alioa msichana wa ki-Nubi ambaye alimzaa Babu Mkubwa wa Imam wa 12, na hivyo, atakuwa mtoto wa mama wa ki-Nubi.”

Sayyid Saeed Akhtar Rizvi anahitimisha kwa kusema kwamba: “Alikuwa ni Imam ar-Ridha (a.s.) ambaye alipangiwa kuoa bibi wa ki-Nubi, na sio Imam Hasan Askari (a.s.).”

HITIMISHO Ili kumlinda na kumfanya atekeleze shughuli zake, kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.) kuliwekwa kuwa siri. Hata hivyo, taarifa kuhusu kuwepo kwake zilipelekwa kwa baadhi ya watu waaminifu katika jumuiya ili kwamba kutoka kwao jumuiya iweze kushawishika na kuthibitishiwa uwepo wa Imam wao, katika wakati ufaawo kufanya hivyo.

Kusema kweli, akiwa amerithi kutoka kwa baba yake, Imam Mahdi (a.s.) alibakia akiwa anapatikana na kufikiwa na wafuasi wake waaminifu kwa muda wa miaka 69, kabla hajaingia katika Ghaibu ya muda mrefu, kuanzia 329 AH na kuendelea hadi leo na (Ghaibat hiyo) itaendelea mpaka atakapo jitokeza tena.

17 SURA YA PILI IMAM MAHDI (A.S.) GHAIBAT FUPI NA NDEFU (GHAIBAT AL-SUGHRA NA GHAIBAT AL-KUBRA)

UTANGULIZI Wakati Imam Hasan Askari (a.s.) alipouliwa shahidi katika mwaka wa 260 AH, Imam Mahdi (a.s.) alikuwa na umri wa miaka 5. Hata hivyo, alichukuwa wadhifa wa Imam wa zama na kuendelea kufanya hivyo mpaka mwisho. Wakati ambapo Maimam 11 waliotangulia walikuwa wanafikiwa na watu wakati wote, maadamu walikuwa hawazuiwi na serikali za wakati wao, Imam wa 12 hafikiwi na watu kiasi hicho kwa sababu ambazo tayari tumezijadili. Kwa maana ya kufikiwa kwake, inafaa kutazamwa kutoka kwenye nukta mbili: 1. Kipindi cha Ghaibat fupi 2. Kipindi cha Ghaibat ndefu

GHAIBAT FUPI (AL-GHAIBAT AL-SUGHRA) (260 AH - 329 AH / 874 AD - 939 AD) Kwa kufariki kwa Imam wa 11 (a.s.), Makhalifa wa Bani Abbas walikuwa wanajishughulisha kuhusu Hujja (Imam) wa 12. Walikuwa wanafikiria kwamba kuna uwezekano wa aina mbili: • imam atakuwa amekwisha zaliwa; au • bado yuko tumboni mwa mama yake na karibuni atazaliwa.

Taarifa kwamba Jafar aliwasilisha habari kwa Khalifa kuhusiana na mtoto ambaye aliongoza ibada ya mazishi ya Imam Askari (a.s.), taarifa hiyo ilimshawishi Khalifa kwenye uwezekano wa kwanza. Hata hivyo, wakati juhudi zake za kumtafuta mtoto huyo ziliposhindwa, alichukuwa hatua mbili. Kwanza, aliuweka mtandao wake wa ujasusi haadhiri na akawaelekeza kumjulisha

18 wakati wowote watakapojua mahali alipo Imam kijana, ambaye baada ya hapo atakamatwa na mara moja kuuliwa. Pili, Khalifa alikuwa na mpango wa kuhakikisha kwamba kama mtoto hajazaliwa bado, basi wakati wa kuzaliwa kwake lazima achukuliwe na kuuliwa.

Wakati wa kipindi hiki. ilikuwa muhimu kwamba mahali alipo Imam (a.s.) pabakie kuwa ni siri kabisa. Hata hivyo, ili Imam abakie kuwa na mawasiliano na watu na kuwahudumia vilivyo, aliteuwa naibu wake - Uthman Ibn Said, ambaye ataongoza taasisi ya WIKALA, ambayo ilianzishwa mapema na Imam Sadiq (a.s.) na ambayo imekua na kuwa yenye nguvu sana chini ya usimamizi wa Maimam wengine baada ya Imam wa Sita. Hatua hii ya Ghaibu iliendelea kuanzia mwaka wa 260AH (874AD) mpaka 329AH (940AD), kwa kipindi cha miaka 69. Kipindi hiki hujulikana kama Ghaibat ndogo (al-Ghaibat al-Sughra). Wakati wa kipindi hiki Imam (a.s.) aliwateuwa SUFARA wanne (Safir-mmoja; au baiozi) au NAIB (Wawakilishi) mmoja baada ya mmoja. Walikuwa ni: 1. Uthman Ibn Said al-Umari 2. Muhammad Ibn Uthman Ibn Said al-Umari 3. Husayn Ibn Ruh al-Nawbakhti 4. Ali Ibn Muhammad al-Sammari

Yafuatayo ni maelezo mafupi ya maisha ya Manaib hawa wanne wa Imam (a.s.).

Uthman Ibn Said al-Umari : Safir wa Kwanza (260 AH - 280 AH) Wakati alipokuwa na umri wa miaka 11 tu, aliajiriwa kama mtumishi katika nyumba ya Imam Muhammad Taqi (a.s.). Alimhudumia Imam vizuri sana; kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kufanyakazi kama mlinzi wa getini; aliishia kuwa msaidizi mkubwa wa Imam (a.s.). Aliendelea kumhudumia Imam Naqi (a.s.) na Imam Hasan Askari (a.s.). Imam Naqi (a.s.) alimuwasilisha kwa wafuasi wake kama mtu mwenye heshima na akaeleza kwamba chochote

19 anachofanya ni kwa jina la Imam (a.s.), hufanywa kwa kufahamika na kwa idhini ya Imam (a.s.). Imam Hasan Askari (a.s.) naye pia alimuwasisha kwa wafuasi wake kwa sifa hiyohiyo

Wakati wa kifo cha Imam Askari (a.s.), Imam Mahdi (a.s.) alimteuwa kuwa mwakilishi wake. Akawa ni ni kiungo kikubwa kati ya Imam Mahdi (a.s.) na Jumuiya ya Shia, alichukuwa maswali yao na malipo (ya Zaka na Khums) kwenda kwa Imam (a.s.) na kurudisha majibu ya maswali yao kwao na maelekezo ya kila siku ya shughuli zao.

Mwenendo huu wa mawasiliano uliendelea kwa takriban miaka 20 wakati Uthman Ibn Said alipofariki mwaka wa 280AH.

Wakati Uthman Ibn Said alipofariki, Imam Mahdi (a.s.) aliandika barua ya maliwazo kwa mtoto wake, ambayo kwayo Imam (a.s.) alimteuwa mtoto huyo wa Uthman kuwa ‘Safir’ mwingine baada ya haba yake. Kiini cha barua hiyo yalikuwa: “Kwa Allah tumetoka, na kwake ni marejeo. Tumeridhishwa na utashi wa Allah. Ama kwa baba yako, aliishi maisha ya mafanikio na amepata kifo chake kwa heshima. Allah awe na huruma juu yake na ampe sehemu katika ujirani na wapenzi wake. Baba yako alikuwa siku zote anafanya kile ambacho kitampatia ukaribu na Allah na wateule wawakilishi Wake. Allah amuweke salama na afanye afaidi furaha ya milele.”

Abu Jafar Muhammad Ibn Uthman (280 AH – 305 AH) Siku zote alimsaidia baba yake kutekeleza majukumu mazito na hatari, kama muwakilishi wa Imam Mahdi (a.s.). Baada ya kifo cha baba yake, alihudumia kama mwakilishi mkuu wa Imam kwa muda wa miaka zaidi ya ishirini. Imam Hasan Askari (a.s.) pia alikuwa amempa heshima kubwa juu yake na aliwaelekeza wafuasi wake kuyachukulia maneno yake kama yale ya Imam mwenyewe. Imam Mahdi (a.s.) pia alimchukulia yeye kama mtu mwaminifu sana na alitaka wafuasi wake kuyachukulia maneno yake kama yale ya Imam (a.s.) mwenyewe.

20 Ili kuweza kuwa kiunganisho cha wafuasi na Imam wao, alijifanya muuza siagi na kwa kufanya hivyo aliugeuzia mbali mtandao wa ujasusi wa serikali.

Alikufa mwaka wa 305AH. Alitabiri siku na saa ya kifo chake na aliandaa kaburi lake mwenyewe. Alizikwa ndani ya nyumba yake mwenyewe mjini Baghdad.

Abul Qasim Husayn Ibn Ruh (305 AH – 326 AH) Alikuwa ‘Safir’ wa tatu. Alizaliwa Qum - Iran na alikuja Iraq akiwa kijana mdogo. Kisha alijiunga katika huduma ya Safir wa pili na akawa mmoja wa wasaidizi muhimu kwa Safir. Wakati Safir wa pili alipokuwa anakaribia kufariki, alimteuwa Husayn Ibn Ruh kama Safir mwingine, alifanya uteuzi huu kwa maelekezo ya Imam Mahdi (a.s.) mwenyewe. Aliendelea kusema: “Husayn lbn Ruh ni mtiifu, mwaminifu na wa kutegemewa. Katika mambo yenu mgeukie yeye na muamini. Ilikuwa ni wajibu wangu kuwasilisha ujumbe huu kwako na nimefanya hivyo.” lbn Ruh alikuwa mfanyakazi makini na alifanya juhudi katika njia ya Allah kwa uzuri sana. Wote marafiki na maadui walimheshimu na kuthibitisha uaminifu na uadilifu wake

Alikufa katika mwaka wa 326 AH.

Abul Hasan Ali Ibn Muhammad al- Sammari (326 AH – 329 AH) Wakati Husayn Ibn Ruh alipokaribia kufariki, alimteuwa Ali lbn Muhammad al-Sammari kama Safir mwingine. Mara hii tena, Husayn aliweka wazi kwamba chaguo hili sio lake bali ni la Imam (a.s.) mwenyewe. Alikuwa ni msadizi mwenye bidii wa Bin Ruh na anatokana na famila maarfu ya Shia. Kipindi chake kilikuwa kifupi.

Wiki moja kabla ya kifo chake, alipokea maelekzo ya maandishi kutoka kwa Imam Mahdi (a.s.), ambayo kiini yake yalikuwa: “Allah awalipe kheri ndugu zako katika msiba wako, kwani utakufa baada

21 ya siku sita. Hivyo jiandae mwenyewe lakini usiteuwe mtu yeyote kuchukuwa nafasi yako baada ya kifo chako. Kwani ghaibat ya pili sasa imeanza ... ”

Wakati wasaidizi wake walipomuuliza wamfuate nani baada ya kifo chake, alisema: “Suala hili liko kwa Allah na atalishughulikia.” Haya yalikuwa ni maneno yake ya mwisho. Alifariki tarehe 15 Shaban 329AH.

Kwa kufariki Safir wa nne, umekuwa ndio mwisho wa kipindi kifupi cha Ghaibat na mwanzo wa ghaibat ya Ndefu.

MATENDO YA SUFARA WANNE Matendo yao makubwa yalikuwa ni kutekeleza majukumu ambayo yalikuwa huko nyuma yakifanywa na Maimam. Hii ilikuwa ni kumuondolea Imam wa 12 (a.s.) mateso ambayo Maimam waliopita waliyapata mikononi mwa maadui zao.

Ili kukamilisha kazi ya kwanza, Sufara walilazimika kuwapa fikra maadui kwamba Imam wa 12 hayupo ili kuwapotezea malengo wasije kufanya madhara na kuhatarisha maisha ya Imam (a.s.), na kumuwezesha kuweka hai ujumbe wa kweli wa Uislamu. Kwa upande mwingine wanajukumu la kuwashawishi na kuwathibitishia wafuasi na marafiki kuhusu kuwepo kwa Imam (a.s.) bila ya kufichua mahali alipo.

Vilevile wana jukumu la kuwalinda Mashia kutokana na kugawanyika katika makundi tofauti kwa kukosa kuwasiliana na Imam wao anayeishi. Walifanya hivyo kwa kuwakumbusha Mashia Hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na za Maimau 11 waliopita, ambazo zilieleza hali ambayo Imam wao wa 12, Hadhrat Mahdi (a.s.) atakayokuwa nayo wakati atakapokuwa katika Ghaibat na kuwashauri ilivyo jinsi ya kuendcsha masuala yao ya kidini wakati wa kipindi hicho kigumu.

22 Vilevile Sufara walikusanya malipo (Khums nk.) kwa niaba ya Imam (a.s.) na kugawanya kwa mujibu wa matakwa na maelekezo ya Imam (a.s.).

Kwa hiyo, Sufara walikuwa ni kiungo imara kati ya Imam Mahdi (a.s.) na wafuasi wake. Kwa tabia yao isiyo na tuhuma na kupambwa na unyofu, uaminifu na uadilifu, Sufara waliweza kuwashawishi wafuasi wa Imam (a.s.) kwamba hakika walikuwa wanamuwakilisha Imam (a.s.) na walikuwa wanawasiliana naye moja kwa moja.

GHAIBAT NDEFU (GHAIBAT AL-KUBRA) Baada ya kipindi cha miaka kama 70 iliyokuwa chini ya uwakilishi wa Sufara wanne, kikaja kipindi cha Ghaibat Ndefu. Kulikuwa hakuna uteuzi zaidi uliofanywa na Imam (a.s.). Je, kwa hiyo, ina maana kwamba wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul Bayt waliachwa wenyewe bila ya mwongazaji? Hapana. Wakati wa kipindi cha Ghaibat Fupi, Sufara wamefanikiwa kuwafundisha wanajumuiya wa Shia kujiandaa wenyewe kwa ajili ya Ghaibat ndefu. Waliziweka kwao wazi zile hadith zote za Mtume (s.a.w.w.) na Maimam 11, ambao wameweka hukumu na taratibu ambazo wafuasi wao watazifuata wakati wa kipindi kirefu cha Ghaibat. Kwa mujibu wa Hadithi hizi, sasa wajibu utakuwa juu ya wanasheria (Fuqah) wa jumuiya kutenda kama waongozaji.

MWANASHERIA NI NANI (FAQIH) Hadithi zifutayo zitatuwezesha kumtambua mwanasheria ni nani:

Hadithi ya Kwanza: Umar Ibn Hanzala alimuuliza Imam Jafar Sadiq (a.s.) kumuelezea mwanasheria. Imam akasema: “Ni yule ambaye anasimulia hadithi zetu, yule ambaye ana elimu ya kile kilichoruhusiwa (Halal) na kilichokatazwa (Haram), yule ambaye ana ujuzi wa sheria na hukumu zetu.” Kisha Imam (a.s.) alimshauri Ibn Hanzala kumchukulia mwanasheria au wanasheria kama hao kama majaji

23 wa jumuiya, na kufuata hukumu zao. Kwani kukataa au kupuuza hukumu ya mwanasheria kama huyo, alisema Imam (a.s.), ni sawa na kumkataa Imam wa zama na kumkataa Imam wa zama ni sawa na kumkataa Allah. Na anayemkataa Allah si Mwislamu.

Hadithi ya Pili: Kwa mujibu wa Imam Hasan Askari (a.s.), mwanasheria mwenye sifa zifuatazo lazima afuatwe: • Lazima awe anajidhibiti mwenyewe • Lazima ailinde dini yake • Lazima aondokane na tamaa zake za uovu • Lazima awe mtii kwenye amri za Bwana wake

Hadithi ya Tatu: Ishaq Ibn Yakub alituma maswali kwa Imam wa 12 (a.s.) kupitia kwa Safir wa pili, akiuliza kuhusu utawala wakati wa kipindi kirefu cha Ghaibat. Imam (a.s.) alijibu hivi: “Ama kwa matukio yatakayotokea, geukeni kwa wasimuliaji wa Hadith zetu, kwa sababu wao ni uthibitisho wangu kwenu ambapo mimi ni uthibitisho wa Allah kwao.”

Wakati ambapo Hadthi hizi tatu zinatueleza kuhusu mwanasheria ni nani, Hadithi ya nne ambayo tutaiangalia, inafafanua jukumu la wanasheria, kama wawakilishi wa Imam (a.s.).

Hadithi ya Nne: Imam Ali Naqi (a.s.) alinukuliwa akisema: “Baada ya Ghaibat ya Qaim wenu, kundi la Maulamaa litawalingania watu kuamini Uimam wa Al-Qaim na kuilinda dini yake... Kama ambavyo nahodha anashikilia rada ya meli kwa uimara, Maulamaa watashikilia kwa imara kwenye nyoyo za Mashia walio dhaifu kiakili, kuwazuiya kutokana na kupotea. Maulamaa ni bora zaidi katika mtazamo wa Allah, Azza wa Jallah.”

Sia tu kwamba Maimam wameacha maelekezo imara na yaliyo wazi

24 ya jinsi ya wafuasi wao watakavyowachagua viongozi wao katika imani, bali pia wameonesha hili kwa vitendo wakati wa uhai wao.

MIFANO YA JINSI GANI MTUME (S.A.W.W.) NA MAIMAM (A.S.) WALIVYOOACHA VIELELEZO VYA KIVITENDO VYA KUFANYWA WAKATI GHAIBAT NDEFU ITAKAPOANZA Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Musab lbn Umayr kwenda Makka na Saad Ibn Maadh kwenda Madina kama wawakilishi wake ili kuwaongoza Waislamu wa kule.

Wakati Imam Ali (a.s.) alipokuwa madarakani, alimuelekeza gavana wake wa Makka, Qasim Ibn Abbas awepo mskitini asubuhi na jiioni na kuzungumzia masuala ya dini.

Imam Jafar Sadiq (a.s.) aliwafundisha kwa maelekezo wanafunzi wake waaminfu kama vile Muhammad Ibn Muslim na Abu Basir Asadi ili jamaa wa jumuiya waweze kurejea kwao kwa ajili ya mwongozo wa kidini. Vilevile alimhimiza Aban Ibn Taghlab kutoa hukumu juu ya masuala ya kisheria (fiqh).

Imam Ridha (a.s.) inafahamika kwamba aliwatuma baadhi ya wafuasi wake, ambao walihitaji mwongozo wa kidini, kwa wawakilishi wake kama vile Zakaria Ibn Adam na Yunus Ibn Abdul Rahman.

Kwa sababu ya juhudi hizi zilizofanywa na Mtume (s.a.w.w.) na Maimam (a.s.), hatimaye wakati Ghaibat kubwa ilipowafikia watu, jumuiya ilikuwa tayari kuipokea bila majereha yoyote makali.

FUQAHA (WANASHERIA) KAMA WAWAKILISHI WA IMAM MAHDI (A.S.) WAKATI WA GHAIBAT KUBWA Fuqaha walipanua shughuli zao na kuchukuwa nafasi ya uongozi ili kwamba waweze kuzuiya jumuiya ya Mashia kugawanyika vipande vipande kwa kukosekana uongozi imara. Mmoja wa fuqaha ambaye alikuja kukubalika kama mwongozaji wa jumuiya wakati

25 wa kuanza kwa Ghaibat kubwa alikuwa Shaykh Muhammad Ibn Muhmmad Ibn Noaman, mashuhuri kwa jina la Shaykh Mufid. Alikuwa mwanachuoni mkubwa na aliandika kwa mapana sana juu ya masuala ya dini. Vilevile alikuwa mwalimu mkubwa.

Miongoni mwa sifa zake ni: Imam Mahdi (a.s.) inafahamika kwamba alimuandikia barua katika matukio matatu tofauti; wakati alipofariki, Imam Mahdi (a.s.) aliandika beti akiomboleza kifo chake na hasara ambayo jumuiya imepata.

Katika hatua za mwanzo za Ghaibat Kubwa, wanasheria walijiona wao kama wasimuliaji tu wa kawaida wa Hadith. Lakini kwa sababu ya urefu wa Ghabat, walichukwajukumu la MUJTAHIDEEN. Wakati ambapo SUFARA walifanya kazi kama ‘wajumbe’ tu wa kawaida kuchukuwa masuala ya dini na kuyapeleka kwa Imam (a.s.) na kurudisha majibu kwa waliouliza. Hili Iikawa haliwezekani wakati wa kipindi kirefu cha Ghaibat; kwa hiyo, ikawa ni wajibu juu ya wanasheria wenyewe kujibu maswali hayo. Mchakato wa IJTIHAD ukawa umeanza. Inaweza kutamkwa kwa usalama kabisa kwamba Shaykh Mufid alikuwa Faqih wa kwanza kutekeleza Ijtihad, na kutoa hukumu za kisheria (FATAWA). llichukuwa muda kwa jumuiya ya Shia kujirekebisha yenyewe ili kuongozwa na Faqih, mmoja baada ya mwingine. Mtindo huo unaendelea mpaka leo.

DHANA YA IJTIHAD NA MARJAEAT Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.), aliongoza ummah wa Waislamu na kuwasaidia kutatua matatizo yao katika kuelewa na kuzingatia sheria za Mwenyezi Mungu. Baada ya Mtume (s.a.w.w.) jukumu hili la kuongoza ummah lilibebwa na Maimam wateule wa Mwenyezi Mungu. Wakati wa kipindi kifupi cha Ghaibat, ummah wa Waislamu ulipata mwongozo wake kutoka kwa SUFARA, walioteuliwa na Imam (a.s.) na kuwaongozwa yeye mwenyewe. Kwa

26 kuja kwa Ghaibat Kubwa, jukumu la mwongozo limechukuliwa na Faqih, ambao sana hujulikana kama MUJTAHIDEEN (Umoja: MUJTAHID).

MUJTAHID NI NANI? Mujtahid ni yule ambaye ni mtaalamu katika sheria (fiqh) za Kiislamu; pia huitwa Faqih. Kupitia mchakato wa IJTIHAD anaweza kutoa hukumu (Fatawa) kwa kutegemea juu ya Qur’an na Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

IJTIHAD kilugha maana yake kufanya juhudi. Kwa maneno mwingine, mwanasheria ambaye anazo sifa zote muhimu na ambaye anafanyajuhudi kutafuta ufumbuzi juu ya masuala ya dini, ni Mujtahid.

Katika muktada wa sheria za Kiislamu, IJTIHAD imefungwa pamoja na elimu na ujuzi wa sayansi za kidini na mada zinazohusiana nazo kama vile lugha ya Kiarabu, nahau, sintaksi (tawi la isimu/kisarufi), mantiki, sharh, hadith, usool, fiqh, nk.

Mtu wa kawaida ambaye sio Mujtahid yeye mwenyewe anafanya ‘TAQLID’ ya Mujtahid. Yule ambaye anategemea juu ya Taqlid ya Mujtahid anaitwa MUQALLID.

Hata hivyo, lazima ikumbukwe kwamba Taqlid hutekelezwa tu katika masuala ya ‘Furu’ (matawi) ya Uislamu na sio katika ‘Usool’ (mizizi).

Katika kitabu chake cha Taudhihul Masael Ayatullah al-Udhma, Sayyid Ali Husseini Sistani anafafanua juu ya suala hili kwa maneno haya: “Ni lazima kwa Mwislamu kuamini katika Misingi ya Imani kwa ujuzi na uelewa wake mwenyewe, na hawezi kumfuata yeyote katika masuala haya.....”

Kumbuka: Taqlid ni katika “masuala ya sheria za kidini tu”.

27 SIFA ZA MUJTAHID Kwa maneno ya Ayatullah Sistani, Mujtahid lazima awe: • Mwanaume • Shia Ithna-Asheri • Mtu mzima • Mwenye akili timam • Aliyezaliwa kihalali • Anayeishi (yaani, awe yuko hai) • Mwadilifu

Kisha akaongeza mahitaji mengine: “Mujtahid ambaye anafuatwa lazima awe A’alam (MSOMI KULIKO WOTE) ambaye ana uwezo zaidi wa kuelewa sheria za kidini kuliko Mujtahid yeyote wa wakati w a ke .”

Dhana ya A’alam sio mpya. Ilikuwepo tangu kuanza kwa Ghaibat Kubwa. Ayatullah Sayyid Muhsin Al-Hakim anataja katika kitabu chake Mustamsak Juz. I, kwamba Sayyid Murtadha Alamal Huda (355-438AH) anaelezea katika kitabu chake Az Zareeh kwamba dhana ya Taqlid ya Mujtahid A’alam imekubaliwa na wote pamoja na jumuiya ya Shia.

Inawezekana (na kusema kweli, hilo lipo kwa sasa) kuwepo na zaidi ya A’alam mmoja. Kwa hiyo, mtu ana uhuru wa kuwa Muqalid wa A’alam yeyote kama huyo. Vipi mtu wa kawaida ataweza kufanya uamuzi kama huo? Kuna njia tatu ambazo mtu wa kawaida anaweza kujua ni nani A’lam wa kufuatwa: 1. Kwa ujuzi wake mwenyewe, kama yeye mwenyewe ni mwanachuoni. 2. Kwa ushuhuda wa watu wawili waadilifu wenye ujuzi ambao watamtaja A’alam huyo. 3. Wakati idadi ya watu wasomi ambao ni mahodari katika kumtambua A’alam -Ahlul Khibra - watakapotoa ushuhuda.

HITIMISHO Ummah wa Waislamu hupokea mwongozo moja kwa moja katika

28 mambo yao kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kisha kwa Maimam (a.s.) mpaka katika zama za Imam wa 11, Hadhrat Hasan Askari (a.s.). Hata hivyo, wakati wote, waongozaji hawa wateule waliwajulisha wafuasi wao zama zijazo wakati wafuasi hawatakuwa na njia ya kumfikia Imam wao. Hivyo, Maimam waliweka mikakati (mbinu) za kufuatwa na wafuasi, ambao watakuja kuishi katika zama hizi wakati Imam atakuwa anaishi katika Ghaibat.

Kutokana na mafundisho haya, hatimaye wakati Ghaibat ilipowafikia juu yao, wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul Bayt hawakuachwa katika shimo. Wanasheria, wenye haiba kama ya Shaykh Al-Mufid, walichukuwa hatamu za uongozi na kuanza kutekeleza katika njia ambayo Mtume (s.a.w.w.) na Maimam wateule wa Mwenyezi Mungu walitaka wao wafanye. Lazima izingatiwe kwamba ingawa Mujtahid ni mtu mchamungu sana na mwenye kumuwakilisha Imam, yeye sio Masoom. Hufikia kutoa hukumu baada ya utafiti wa muda mrefu na makini. Kama ikitokea kwamba hukumu fulani haiafikiani na amri ya Allah, Mujtahid hataadhibiwa Siku ya Hukumu. Vilevile Muqalid hatawajibika kwa kosa lake la unyofu wa kibinadamu.

Katika zama za sasa, Mujtahid e Taqlid wawili mashuri zaidi ni: Ayatullah Sayyid Ali al-Husaini Sistani (anayeishi Najaf, Iraq) na Ayatullah Sayyid Ali Husseini Khamenei (anayeishi Tehran, Iran).1 Allah awaweke Marjaa hawa na wengine wote katika hifadhi Yake na Aharakishe kujitokeza tena kwa Hadhrat Hujjat Ibnul Hasan (a.s.).

1 Neno la mwenye tovuti: Mamujtahid maarufu wengine ni Ayatullah Shaykh Bashir Hussain al-Najafi, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeed al-Hakeem na Ayatullah Shaykh Muhammad Ishaq al-Fayadh (wote wanaoishi Najaf, Iraq; Hawa watatu, pamoja na Ayatullah Sistani, wanajulikana kama Nne wakubwa; hawa nne ni Ayatullah wakuu wa zama zetu wanaopatikana katika jiji takatifu la Najaf, Iraq); Ayatullah Sayyid Muhammad Taqi al-Modarresi (anayeishi Kerbala, Iraq), Ayatullah al-Shaykh Wahid Khurasani (anayeishi Qum, Iran) na Ayatullah Sayyid Sadiq Hussaini Shirazi (wanaoishi Qum, Iran).

29 Itakuwa ni makosa kufikiri kwamba Imam Mahdi (a.s.) mwenyewe hahusishwi kabisa. Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (katika Your Questions Answered V. I. Q. 45) anaelezea jukumu la Hadhrat Mahdi (a.s.) katika maneno haya: “Imam wetu wa Zama bado anawaongoza wanachuoni, lakini wakati tu suala au swali ni katika hali ambayo halikutolewa ufumbuzi wa wazi huko nyuma. Kama Imam aliyepita au Aalim tayari ameweka mwanga kwenye suala hilo, Imam wa zama anabakia kimya. Lakini kama suala ni jipya na Aalim hana uwezo wa kulitatua yeye mwenyewe, Imam kwa kawaida wakati wote huwaongoza Ulamaa katika hali hiyo. Ningeweza kukupa mifano mingi ambayo mimi mwenyewe naitambua, lakini siko huru kuisimulia.”

30 SURA YA TATU FILOSFIA YA GHAIBAT

UTANGULIZI Allah Azza wa Jallah, Mwenye kustahiki shukurani zote, kamwe hajawaacha viumbe wake bila mwongozaji. Kwa ujumla alituma waongazaji 124,000 kama Wajumbe Wake kwenye jumuiya tofauti na zama tofauti. Mjumbe wa mwisho alikuwa ni Hadhrat Muhammad Mustafa (s.a.w.w.). Baada ya Mtume (s.a.w.w.) walikuja Maimam kutoka kwenye kizazi chake, kila mmoja wao, licha ya vikwazo walivyowekewa na maadui zao, walikuwa waongozaji dhahiri na mnara wa mwanga kwa ajili ya ummah. Mpango huu uliendelea mpaka alipouliwa kishahidi Imam Hasan Askari (a.s.) katika mwaka wa 260AH, wakati mwanzo wa GHAIBAT ulipokuja na kuweka kivuli chake juu ya maisha ya waumini.

Hii lazima itakuwa imekuja kama changamoto kubwa kwa jumuiya ya Shia; kwa kutambua kwamba sasa watajifunza kuishi bila ya kuwa na njia ya moja kwa moja ya kumfikia Imam wa zama yao. Lazima watakuwa wametazama nyuma kimazoea katika siku zile wakati ambapo baba na babu zao walikuwa na fursa ya kuwasiliana moja kwa moja na Maimam wao wateule wa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, walikuwa na faraja kwamba Imam mwenyewe ameteuwa ‘Naibu’ wake ambaye atakuwa kiungo kati ya waumini na Imam wao. Vilevile, huu ulikuwa ni wakati ambapo Imam (a.s.) atawasiliana moja kwa moja na wafuasi kwa barua, njia ya kubadilishana ikiwa ni manaibu - SUFARA.

Ni vigumu mno hata kwa mawazo mapana yasiyo na mpangilio kuweza kutambua mtanziko wa waumini wakati mpango huu wa mawasiliano kupitia ‘manaibu’ na wenyewe pia ukafikia mwisho kwa kuanza kwa Ghaibat Kubwa - GHAIBA AL-KUBRA. Kuanzia hapo na kuendelea, kutakuwa hakuna uteuzi wa moja kwa moja wa manaibu utakaofanywa na Imam (a.s.) mwenyewe. “Wazee” wa jumuiya watakuwa na jukumu hili la kuchagua Faqih ili

31 kuwaongoza. Faqih kama huyo katika haiba ya Shaykh Mufid, lazima ajitokeze ili kuelezea hekima na filosofia kuhusiana na mpangilio huo.

Katika sura hii, tutaangalia kwa ufupi baadhi ya masuala yanaoleta changamoto ambayo hupita kwenye akili za waumini kuhusiana na Ghaibat ya Imam wetu wa 12. Hadhrat Hujjat Ibnul Hasan, Allah umuweke salama na kuharakisha kujitokeza kwake tena.

MASUALA MAKUBWA YAHUSIANAYO NA GHAIBAT KUBWA Mumini, ambaye ana ujuzi wa historia ya Kiislamu na akawa amesoma kuhusu siku hizo za “maziwa na asali” wakati wahenga zake walikuwa wakiwafikia kwa uhuru Maimam wateule wa Mwenyezi Mungu, na kuuliza maswali ambayo yanaweza kupangiliwa kama ifuatavyo: • Kwa nini tunanyimwa njia ya kumfikia Imam wetu?

• Je, inaingia akilini kwamba Imam mteule wa Mungu abakie katika Ghaibat, wakati anatakiwa kuuhudumia Ummah wa Mtume (s.a.w.w.)?

• Imam wa sasa, Hadhrat Mahdi (a.s.) alizaliwa mwaka wa 255AH. Leo tuko katika mwaka wa 1431. Hiyo hufanya maisha ya Imam kuwa umri wa miaka 1176. Aidha, ataishi mpaka Siku ya Qiyama. Je, inawezekana kwamba mwandamu aishi umri mrefu kama huo?

KWA NINI TUNANYIMWA NJIA YA KUMFIKIA IMAM WETU (A.S.) Swali la kwanza na muhimu zaidi, hebu natuiweke nukta moja wazi na hiyo ni kutokuwepo kimwili kwa Imam (a.s.) haimaanishi kwamba hafikiwi. Kusema kweli, katika barua yake kwa Shaykh Mufid, Imam wetu wa 12 (a.s.) alielezea kwamba anayo habari juu ya sisi wote, ingawa tunaweza kuwa hatulitambui

32 hilo. Anatuhakikishia taa ya mwongozo na msaada wake, na kwa kuanisha anaelezea kwamba wote tungeangamia mikononi mwa maadui zetu kama isingekuwa msaada wake. Amini usiamini, kila tendo, zuri na baya, linalofanywa na mfuasi linaripotiwa kwake kupitia mawakala wa kiungu. Anafurahi kuona matendo mazuri ya mfuasi na anahuzunika juu ya matendo mabaya ya mfuasi.

Kwa nyongeza, kama mumini ana shida, anaweza kuomba msaada wa Imam. Kwa idhini ya Allah, Imam (a.s.) ama husaidia bila kuonekana au husaidia moja kwa moja na kwa kuonekena. Mifano mingi imesimuliwa wakati Imam (a.s.) alipojitokeza ana kwa ana kwa ajili ya kuwasaidia waumini. Ukosefu wa nafasi unatuzuiya kusimulia mifano kama hiyo ambayo vinginevyo ingechukuwa nafasi yote ya kijitabu hiki. Njia na namna mbalimbali za kumuita Imam (a.s.) zimeelezewa katika vitabu vya “Du’a” na “Amal” ambapo kwayo msomaji anayetaka anaweza kuvirejelea. Ama kwa sisi, tutaangalia katika sababu mbalimbali ziwezekanazo za kwa nini Allah amechagua mpango huu kwa ajili yetu.

SABABU ZA KUHUSIANA NA GHAIBAT Jambo hili la Ghaibat la Imam wa 12 (a.s.) ni mpango wa kiungu; kwamba Allah amechagua njia hii ya kuendeleza mwongozo Wake inaweza isieleweke kikamilifu kwetu sisi wanadamu. Kwani katika hekima Yake isiyo na ukomo, Angeweza kusanifu mpango wowote ule mwingine lakini kwamba Aliamua kuwa na mpango huu makhususi mahala pake, ni siri Yake, anaijua Yeye Mwenyewe na wateule Wake - Maimam. Ili kulielewa jambo hili, tunahitaji kutafuta msaada wa Mtume (s.a.w.w.) na Maimam (a.s.) kutoka kizazi cha Mtume (s.a.w.w.).

Shaykh Saduq katika kitabu chake Kamal-ud din na Shaykh Kulaini katika Al-Kafi wanamnukuu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Maimam ni warithi wangu na wako 12 kwa idadi na wa mbele zaidi miongoni mwao ni Ali ambapo wa mwisho ni Mahdi, Abul Qasim Muhammad bin Hasan Al-Askari. Yeye ni mrithi na naibu wangu

33 wa 12. Ni wa 12 mwenye mamlaka ya Allah juu ya watu. Ghaibat yake itakuwa ndefu na itakuwa ni mtihani na majaribio juu ya watu wa zama hiyo.”

Kwa mujibu wa hadthi hii, kwa mchakato wa Ghaibat hii, imani ya mumini imefanyiwa mtihani. Wale ambao watathibitisha thamani yao italipwa kwa wingi na Muumba, kwa mujibu wa hadithi ifuatayo kutoka kwa Imam Ali (a.s.): “Jueni kwamba yeyote yule miongoni mwa Mashia ambaye yuko imara katika imani, kamwe hakengeuki kutoka njia ya Uislamu, wala hapotoki na kuingia kwenye makosa na moyo wake hubakia vilevile wakati wa kutokuwepo kwa Imam, atakuwa karibu na mimi na kupata daraja sawa na langu katika Siku ya Ufufuo.” (Amal Al- Wara cha Shaykh Tabrasi).

Hakika, Maimam wote kutoka kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) wamewatahadharisha waumini vipindi hivi vya majaribio na mateso, na walielekeza kuhusika kwao kwa wale ambao wataishi katika kipindi cha Ghaibat. Hata hivyo, wameahidi kwamba waumini wa kweli wataishi katika kipindi hiki cha majaribio kwa mafanikio na kwa hiyo watalipwa kwa wingi kwa kuwa na imani imara kama hiyo. Kwa hiyo lazima tujione wenyewe kama wenye bahati kwa kupewa fursa hii adimu ya kuthibitisha utii wetu kwa Mtume (s.a.w.w.) na mwakilishi wake wa mwisho katika ardhi hii, na kisha kulipwa kama inavyostahiki. Hii inathibitishwa na hadithi ya Imam Musa Kadhim (a.s.) iliyonukuliwa katika Asbat Ul Huda cha Sheikh Hur Aamili; akifafanua juu ya hali ya Mashia wanaoishi katika zama za Ghaibat Kubwa, Imam (a.s.) alisema: “Mnasemaje kuhusu wale Mashia ambao watabakia wamefungamana na sisi wakati wa kipindi cha Ghaibat? Watabakia imara katika urafiki wetu na kuwachukia maadui zetu. Wanatokana nasi kama ambavyo nasi twatokana nao. Wanaridhika na uongozi wetu na sisi tumeridhishwa nao kama wafuasi wetu. Bahati iliyoje waliyokuwa nayo! Kwa Jina la Allah, katika Pepo watakuwa katika ujirani wetu.”

34 Allah angeweza kuchagua njia nyingine ya kumlinda Imam (a.s.). Kwa nini achague njia hii makhususi? Kama utafikiri kwa undani juu ya suala hili, utaona kwamba, kusema kweli, kwa njia ya Ughaibu, Imam (a.s.) na wafuasi wa Imam (a.s.) wanalindwa zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Utafiti makini wa kipindi cha Maimam 11 wa mwanzo itaonyesha ukweli kwamba ukandamizaji dhidi Maimam na wafuasi wao ilikuwa kila mahali kama ilivyokuwa makali na makubwa. Ukubwa wa ukandamizaji ilikuwa kwa sababu Imam wa zama alikuwa anaonekana na vilevile wale ambao husishwa na yeye pia walikuwa wanatambulika kwa urahisi na kuadhibiwa. Wakati Imam akiwa haonekani, maadui zake wanakuwa kidogo kwa sababu kwa mtazamo wao wanaona Imam hayupo. Wafuasi wa Imam walikuwa hawachukuliwa kama tishio halisi. Kwa hiyo, hatari ambayo wafuasi wataopata ni mdogo. Ingawa itaonekana kama suala la kejeli, lakini ni kweli kwamba ujumbe wa Allah imepata nguvu na ufanisi zaidi katika kipindi cha muda Ghaibat Ndefu kuliko kabla. Vile vile, kina na kiwango cha ukali wa ukandamizaji wa kimataifa dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bayt ni kiasi kidogo sasa kuliko katika siku hizo wakati Maimam walikuwa wanaonekana na kufikiwa na wote.

Kinga ambayo Imam Mahdi (a.s.) anafaidi kupitia Ghaibat ni kwamba, yeye yuko huru kutokana na mateso na unyanyasaji ambao Maimam wengine walikuwa wanapata kwa sababu walikuwa wanaonekana. Anaendelea kuhudumia katika njia ya Allah bila kuingiliwa.

Pia kuna nukta nyingine ya kiutendaji kwenye dhana ya Ghaibat ya Imam Mahdi (a.s.). Katika kufikisha ujumbe wa Allah kwa jamii ya wanadamu, kwa upana mkubwa, Allah ametumia njia ambazo zinaendana kabisa na njia za wanadamu. Kwa hiyo, utaona kwamba Mtume (s.a.w.w.) na Maimam (a.s.) ingawa wamejaaliwa kuwa na ilmu isiyo ya kawaida kwa mwanadamu na uwezo, bado waliishi kama wanadamu wa kawaida na kutumia uwezo wao wa kimiujiza wakati inapokuwa lazima kabisa na kwa idhini ya Allah.

35 Kufariki kwa Imam wa 11 (a.s.) kulionesha mabadiliko katika mpangilio wa kiungu wa kufikisha na kulinda ujumbe wa Allah. Imam wa 12 alikuwa mwakilishi mteule wa Allah katika ulimwengu. Kutokana na hali hiyo, alifanywa asiishi njia ya maisha ya kawaida na kifo, kinyume na kuishi. Ili Imam (a.s.) awe imara na asioneshe hali za kawaida za kibinadamu kama vile mchakato wa kuzeeka, ungechukuliwa usio wa kawaida, ukichukulia ukweli kwamba Mitume wote (pamoja na tofauti kidogo) na Maimam kumi na moja kabla yake wamepitia mchakato huu. Aidha, kama Imam (a.s.) angekuwa katika udhibiti kamili, hayo yangekuwa ni mabadiliko kamili ya utaratibu: ikimaanisha kuwepo kwa kipindi “Qiyamat Sughra” au “Raj’at”. Kipindi hiki bado kitakuja wakati Allah akipenda kuwa hivyo. Katika kipindi cha mpito, tunayo Ghaibat Ndefu.

Kwa hiyo, Ghaibat Ndefu, inawapa changamoto wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul Bayt ili kuthibitisha utii wao kwenye ujumbe wa Allah, ulioletwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.), na kuwekwa hai na Maimam wateule (a.s.) wa kiungu. Kwa ufupi ni fursa waliyopewa wafuasi, ili kufanyakazi ndani ya muundo uliosanifiwa na kufafanuliwa na wateule wawakilishi wa Allah, na kufanya hivyo katika kuafikiana na mwenendo wa njia za ulimwengu, uliokaliwa na wanadamu.

JE, INAWEZEKANA IMAM MTEULE WAKIUNGU KUHUDUMIA KATIKA NJIA YA ALLAH AKIWA KATIKA GHAIBAT? Kwa sababu Imam Mahdi (a.s.) haonekani machoni mwa watu, hakumfanyi yeye awe hana uwezo katika njia yoyote. Allah Azza wa Jallah, haonekani na kamwe hataonekena machoni mwa watu. Bado ni kufuru kufikiri kwamba Hana uwezo. Hewa ambayo tunavuta haiwezi kuonekena, lakini bado kuwepo kwake siku zote tunakuhisi. Kwa hoja hiyo hiyo, Imam Mahdi (a.s.) anahudumia njia ya Allah kwa kiwango cha juu kabisa ingawa hili hatuwezi kuliona kwa macho. Kumbuka: Ghaibat ya Imam (a.s.) sio kamilifu wala thabiti; sio ya kudumu wala ya zamani za kale.

36 Ulikuwepo wakati alikuwa anafikiwa na familia yake, marafiki zake wa karibu na wafuasi wake. Kisha, wakati wa Ghaibat Fupi, alikuwa anafikiwa kupitia manaibu wateule wake. Sasa, pamoja na tofauti ndogo, hafikiwi na mtu. Utakuja wakati kipindi cha “Raj’at” wakati atakapo kuwa anaonekana kabisa na akiwa katika udhibiti kamili wa matukio ya ulimwengu huu.

Aidha, wakati wa nyakati za dharura, alifanya mwenyewe aonekane. Mifano mingi imetajwa wakati Imam (a.s.) alipojitokeza kuwaokoa wale ambao walihitaji msaada wake, kwa mahitaji binafsi au kwa ajili ya njia ya ujumbc wa Allah.

Ukweli huu unathibitishwa na barua ya Imam Mahdi (a.s.) ambayo aliituma kwa Shaykh Mufid; dondoo ya barua hiyo inatoiewa hapa chini: “Tunayo habari ya mazingira yako na hakuna habari zako zozote zinazofichwa kwetu. Sio hatujali kukuangalia wewe wala kukusahau wewe, Kwa sababu kama ingelikuwa sio hivyo, mateso yangemiminika juu yako na maadui zako wangekuangamiza. Hivyo, muogope Allah na umtii Yeye, Utukufu uwe juu ya Enzi Yake.”

JE, INAWEZEKANA MTU KUISHI UMRI MREFU KAMA HUO? Ni ukweli kwamba Allah ameweka sheria kadhaa zenye kuendesha mambo ya ulimwengu na sheria hizo zimebakia bila kubadilika. Lakini je, ina maana kwamba Allah hana uwezo wa kubadilsha hizi zinazoitwa “sheria za maumbile” wakati akipenda kufanya hivyo? Kusema kweli, sheria hizi hubadilishwa mara kwa mara chini ya hali mbili: 1. Wakati Allah akipenda ujumbe ufike kwamba Yeye ni Mwenye Kudura na anaweza kubadilisha sheria ambazo amezitengeneza, na kwamba hafungwi au kuwa na mipaka katika muundo au maumbile yoyote.

2. Wakati Mjumbe wake mteule anapopewa changamoto kuthibitisha kwamba yeye ni Mjumbe wa Allah; basi mteule Mjumbe wa Allah anajaaliwa uwezo wa kimiujiza ambao

37 unapita mipaka iliyowekwa na “sheria za kimaumbile”.

Suala hili la umri mrefu wa Imam Mahdi (a.s.) ni mfano wa dhahiri wa hali hizi mbili. Hata hivyo, yeye sio mfano pekee. Kuna mifano mingi ya wanadamu ambao walipewa umri mrefu usio wa kawaida. Kwanza na ya mbele zaidi, kuna watu wanne ambao ni wakubwa kwa umri kuliko Imam Mahdi (a.s.) na ambao bado wanaishi hadi leo; hao ni: 1. Hadhrat Khidhr (a.s.). 2. Hadhrat Isa (a.s.). 3. Hadhrat Ilyas (a.s.). 4. Hadhrat Idris (a.s.).

Waislamu wote wanaamini kwamba watu hawa wanne wako hai na imara. Ama kwa Nabii Isa (a.s.) anasubiri kudhihiri tena kwa Imam Mahdi (a.s.) ili naye apate kurudi na aungane naye.

Waislamu wote pia wanaamini kwamba Azazil au Shaitan amekuwa hai tangu zama za kale na ataishi mpaka wakati wa kujitokeza tena kwa Imam Mahdi (a.s.).

Juu zaidi ya mifano hii, mifano zaidi michache inatolewa hapa ya wale watu ambao kwamba Allah aliwaruzuku maisha marefu. Hawa ni: • Mtume Nuh (a.s.) - miaka 2500. • Mtume Suleiman (a.s.) - miaka 700. • Mtume Hud (a.s.) - miaka 464. • Mtume Adam (a.s.) - miaka 900. • Mtume Sheeth (a.s.) - miaka 900.

Baadhi ya makafiri na washirikina walipata maisha marefu: • Iblis - tangu zama za kale. • Anak, bint wa Mtume Adam - miaka 3000. • Shaddad - miaka 900. • Dajjal - zaidi ya miaka 1400.

38 Kwa hiyo, hufuatia kwamba, umri mrefu wa Imam Mahdi (a.s.) sio jambo geni wala la pembeni. Kwa utashi wa Allah anafaidi umri mrefu. Na kwa utashi wa Allah, kwa sasa haonekani machoni mwa watu na chini ya Ghaibat. Anasubiri siku ile ambayo Allah atamuamuru kujitokeza tena na kusimamisha utawala wa Allah juu ya ulimwengu. Hiyo ndio siku ambayo lazima wote tutamani kuwa hai, ili kumkaribisha Imam (a.s.).

HITIMISHO Uamuzi wa Mungu kwamba lazima kuwe na Maimam 12 tu, baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), umefanya hiyo kuwa ni lazima kufanywe mahitaji maalumu kwa ajili ya Imam wa 12 (a.s.) ili aweze kuishi na kutekeleza majukumu yake bila ya vikwazo. Sifa kubwa za mahitaji hayo ni: 1. Imam (a.s.) haonekani mchoni mwa watu. Kwa kawaida hafikiwi na mtu. Sehemu alipo hapajulikani. Ataendelea kuishi katika hali hii mpaka Allah atakapomuamuru kujitokeza tena.

2. Imam Mahdi (a.s.) amewekwa huru kutokana na mchakato wa kuzeeka; wakati wowote alipojitokeza, alifanya hivyo kama kijana wa kiume aliyeko kwenye miaka ya 40. Hatimaye wakati atakapojitokeza kutoka kwenye Ghaibat yake Ndefu, atakuwa katika umri ambao watu walimuona wakati wa kipindi cha Ghaibat: Kijana wa kiume wa miaka 40.

3. Anabakiwa kutoonekana machoni na kwa kawaida hafikiwi na wafuasi wake. Hata hivyo, kwa Rehema za Mungu, anajulishwa kikamilifu mambo yote ya ulimwengu. Pia anajulishwa kuhusu ustawi wa Ummah. Huwasaidia wale wenye shida bila ya wao kujua hilo. Wakati wa dharura wakati wafuasi wake wanapomuita kwa ajili ya msaada huwajibu bila kukawia.

4. Kwa sababu haonekani machoni na sehemu alipo haijulikani, anatekeleza majukumu yake bila vikwazo ambavyo kwavyo Maimam 11 waliotangulia walilazimika kuendesha shughuli zao.

39 SURA YA NNE YAKO WAPI MAKAZI YA IMAM MAHDI (A.S.)

UTANGULIZI Mahali alipo Imam Mahdi (a.s.) ni siri ya Allah peke Yake. Hakuna anayeweza kusema kwa uhakika wowote, kuhusu kuwepo kwa Imam kwa wakati wowote. Hata hivyo, kutegemeana na ujuzi binafsi wa watu fulani wanaotegemewa, ambao wakati mmoja au mwingine, walipata bahati ya kukutana na Imam (a.s.), inawezekana kufanya kazi kidogo ya kiintelejia kuhusu mzunguko wa Imam (a.s.).

Sehemu ambazo Imam Mahdi (a.s.) amewahi kuonekena: • Ndani ya Masjid-ul-Haram kwenye Ka’aba - Makka • Ndani ya Masjid-Sahla - Iraq • Ndani ya Masjid Jamkaran - Iran

MASJID-UL-HARAM Inaaminiwa kwa nguvu sana kwamba Imam Mahdi (a.s.) anatekeleza ibada ya Hijja kila mwaka na kuchanganyikana na waumini, bila kujulikana. Watu mbalimbali wamepata bahati ya kukutana na Imam (a.s.) wakati wa msimu wa Hijja.

MASJID-SAHLA Imependekezwa kwamba wale ambao wanakusudia kuwa katika hadhara ya Imam (a.s.) watembelee Msikiti huu siku ya mkesha wa Jumanne. Kuna watu mbalimbali waaminifu ambao wamedai kumuona Imam (a.s.) Msikitini humo siku ya Jumanne jioni. Pia inaelezwa kwamba kama mtu atatembelea Msikiti huu Jumanne 40 usiku mfululizo bila kukata, atapata fursa ya kumuona Imam (a.s.) ana kwa ana.

MASJID-JAMKARAN Msikiti huu upo km. 6 mashariki ya mji mtakatifu wa Qum. Msikiti huu ulijengwa kwa amri ya Imam Hujja mwenyewe

40 kupitia kwa mumini mchamungu akiitwa Shaykh Hasan bin Muthil katika mwaka wa 373AH. Vilevile Imam (a.s.) amependekeza kwa waumini kutembelea Msikiti huu na kusali sala zao humo, kwani rakaa mbili ndani ya Msikiti huu hulipwa kama vile Swala hizo zimeswaliwa katika eneo la Kaaba - Nyumba ya Allah.

Mbali na sehemu hizo, kuna taarifa kuhusu makazi ya siri ya Imam yanayoitwa “Jazira al-Khazra” (Visiwa vya kijani) ambavyo vimetembelewa na baadhi ya watu kwa bahati tu. Maelezo kuhusu visiwa hivi yameelezwa katika vitabu mbalimbali lakini hapa hatutayarudia kutokana na ufinyu wa kijtabu hiki.

41 SURA YA TANO MAJUKUMU NA WAJIBAT ZA WAFUASI WA IMAM (A.S.) WAKATI WA KIPINDI CHA GHAIBAT

Ingawa Imam wetu (a.s.) yuko kwenye Ghaibat, siku zote yuko pamoja nasi. Anamjua kila mmoja wetu na ni mwenye kujihusisha kwa kina kuhusu ustawi wetu. Lau ingekuwa si kwa ajili yake na kinga anayotoa kwetu pamoja na idhini ya Allah, tungekwisha angamia zamani. Ukizingatia hili akilini, inakuwa wajibu juu yetu kujifunza wajibat wetu wenyewe kuelekea kwake. Katika sura hii, kwa ufupi tutaangalia wajibat chache zinazotegemewa kutoka kwa muumini wa kweli wa Imam Mahdi (a.s.).

Ya kwanza na muhimu zaidi, kwa sababu ni Imam wa zama na mwakilishi wa Allah anayeishi, lazima tumkumbuke wakati wote. Njia nzuri ya kumkumbuka kufanya kuwa ni tabia yetu kusoma na kutafakari juu ya maombi (Du’a) zinazofokasi juu yake kama Imam mteule wa kiungu kutoka kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) na ambaye anamwakilisha Mtume (s.a.w.w.) katika ulimwengu. Baadhi ya Du’a zinatakiwa kusomwa kila siku, nyingine, kama vile “Du’a Nudba” husomwa katika nyakati maalumu. Kwa mfano inapendekezwa kusoma “Du’a Nudba” siku za Ijumaa, siku za Idd-ul-Fitr, Idd-ul- Adha na Idd-ul-Ghadir. Kisha kuna mbalimbali ambazo hutakiwa kusomwa. Halikadhalika, kila siku katika matukio maalumu.

Pili, kwa vile Imam wetu anajali sana kuhusu usalama wetu, hatuna budi, kuomba kwa ajili ya usalama wake. Ingawa tu wenye dhambi sana na tusiostahiki, hivyo hivyo, wakati tunapomuombea, huonesha tofauti kubwa kwake, kwa maana kwamba anajisikia mwenye furaha kwamba wafuasi wake wanamkumbuka akilini mwao.

42 Tatu, lazima tukumbuke kwamba yeye ni mawla (mwenye kutawala mambo yetu), aliyeteuliwa kama hivyo na Allah, na kwamba utii kwake unapita utiifu wote ambao tungetakiwa kufanya kila siku katika maisha yetu. Lazima tumhakikishie kwamba katika uchambuzi wa mwisho ni yeye na yeye peke yake, ndiye mtawala wa mambo yetu.

Kuthibitisha kwamba tunamaanisha kile tunachosema, jukumu letu lifuatalo ni kutengeneza muundo wa maisha yetu katika matendo yale ambayo humpendeza yeye, na kujiepusha na matendo yale yote ambayo humchukiza. Kumbuka: Imam anajulishwa kikamilifu kuhusu matendo yetu; yale mazuri humpa furaha na yale mabaya humhuzunisha.

Moja ya jukumu kubwa la Imam Mahdi (a.s.) ni kuweka ujumbe wa Uislamu hai na kuenea mingoni mwa wanadamu. Kwa hiyo, jukumu letu ni kutekeleza kazi hii katika jina la Imam Mahdi (a.s.). Kuna shughuli nyingi ambazo tunaweza kuzifanya katika kukuza na uendelezaji wa njia ya Allah. Shughuli hizo hujumuisha: kujenga shule, uchapaji wa vitabu na kuwekeza katika rasilimali watu ambazo zaweza kutumika kama njia ya kulingania ujumbe wa Uislamu.

Tena, kama ishara ya ukarimu kwa Imam wetu anayeishi, lazima tutumie chochote tunachowcza katika jina lake. Kwa mfano tunaweza kutoa sadaka kwa jina lake.

Mwisho lakini si kwa umuhimu, lazima tukumbuke wakati wote kwamba yuko hai na ni mlinzi wetu, aliyeteuliwa kufanya hivyo na Allah. Kwa hiyo, tunatakiwa kuvuta subira na kuomba kwa Allah kuharakisha kujitokeza tena kwa Imam (a.s.).

Wakati wa kipindi hiki, wafuasi wa Imam (a.s.) wanapita katika mifululizo ya majaribio na mateso. Imam (a.s.) anayaelezea katika ile du’a mashuhuri ambayo husomwa katika mwezi wa Ramadhani:

43 ‘Du’a Iftitah’. Hivi ndivyo du’a inavyoeleza: Ewe Allah tunalalamika Kwako: Kwa kutokuwepo kwa Mtume wetu (s.a.w.w.), Na Ghaibat ya kiongozi wetu, Na wingi wa maadui zetu, Uchache wa idadi yetu, Ukali wa majaribio yetu, Na ushindi wa wakati dhidi yetu.

Kwa matokeo ya changamoto zilizotajwa hapo juu, wafuasi wa Imam (a.s.) wanaweza kupambana na matatizo makubwa manne: Utengano miongoni mwao, mashaka kuhusiana na kuwepo kwa Imam, kukata tamaa na kupoteza imani. Maimam ambao wamekuja kabla ya Imam Mahdi (a.s.) walionya kuhusu matatizo haya. Kwa mfano, Imam Muhammad Baqir (a.s.) ananukuliwa akisema kwamba: “Mtajaribiwa katika uimara wa imani yenu. Inaweza kuwatokeni bila ya ninyi wenyewe kujua, kama wanja wakati unawekwa kwenye macho hufanya kuwepo kwake na hutoweka bila ya kuwa na fahamu. Kwa njia hiyo hiyo, baadhi watakuwa na imani wakati wa asubuhi lakini huipoteza wakati wa jioni, bila ya kulijua hilo.”

Imam wetu wa Sita Hadhrat Jafar Sadiq (a.s.), alimuambia Abu Basir, mmoja wa sahaba zake kwamba, wakati wa kipindi cha Ghaibat Kubwa, theluthi mbili za wafuasi wa Imam Mahdi (a.s.) wataipa dini mgongo kutokana na mashaka na kukata tamaa.

Hatimaye, wale wafuasi wa Imam (a.s.) ambao watabakia imara katika imani yao wataonekana wanyonge. Katika maneno ya Imam ya Ali (a.s.), wafuasi kama hao wataonekana duni na wasio na thamani, kama mdudu. Migawanyiko miongoni mwa wafuasi itatokea. Watasemana wenyewe kwa wenyewe na kuitana waongo. Hatimaye, wachache tu watabaki imara juu ya imani zao.

44 HATUA ZA KUJIKINGA KWA WAFUASI WA IMAM (A.S.) ZAHITAJIKA KUCHUKULIWA Ya kwanza na muhimu zaidi, tunahitaji kumkumbuka Imam (a.s.) wakati wote na kuomba kwa ajili ya usalama wake na kujitokeza tena kwa haraka kutoka kwenye Ghaibat. Du’a maalumu na Sala kwa madhumuni haya zaweza kupatikana katika vitabu vya maombi kama vile Mafatihul Jinan cha Shaykh Abbas Qumi.

Pili, lazima tukubali kwa usahihi kabisa ukweli kwamba sio tu kwamba Imam Mahdi (a.s.) yuko hai, bali pia yuko imara kwa idhini ya Allah ya kuwasaidia wale ambao wanahitaji msaada wake. Hata hivyo, mtu lazima awe na imani kamili katika uwezo wa Allah usio na mipaka na uwezo wa Imam, na kumuita kwa imani kamili. Bila ya shaka yoyote msaada utakuja, hayo ameyasema Mtume (s.a.w.w.): “Hata kama kisu kiko shingoni mwako na ukamuita Imam wako wa Zama, atakuja kukusaidia.”

BAADHI YA NJIA ZA KUMUITA IMAM KWA AJILI YA MSAADA • Soma pamoja na kuelewa du’a ambazo zimeandikwa na kuhifadhiwa na kupendekezwa maalumu kwa ajili ya kumuita Imam (a.s.) kwa msaada wa haraka.

• Tuma ombi lako - ARIDHA - kwake ukieleza matatizo yako na kuomba ufumbuzi wake. Kwa kawaida, hili hufanywa siku ya mwezi 15 Shaban, siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.). Hata hivyo, hili linaweza kufanyika wakati wowote. Aridha hiyo inatumwa kupitia kwa mmoja kati ya yoyote wa Sufara wa Imam (kwa kawaida huwa kupitia kwa Husayn Ibn Ruh) na huwekwa kwenye kisima au kijito kinachotiririsha maji au inazikwa.

• Mtaje Imam (a.s.) kupitia Ziyarat maalumu zilizopendekezwa kwa ajili ya kuomba msaada wa Imam (a.s.). Moja ya Ziyarat

45 hizo husomwa siku za Ijumaa. Ziyarat nyingine inaitwa Ziyarat ya ‘Ale Yasin’.

• Kuna Swala ya “Istaghasa”, huswaliwa wakati mtu ana haja ya msaada wa haraka. Namna ya kuswali swala hii, tazama katika Mafatihul Jinan.

• Baada ya kumsaidia mtu aitwaye Said Hashim Ibn Hasan Mu- sawi Rishti, Imam (a.s.) alimshauri kwamba iwapo atalazimika kuhitaji msaada wa Imam siku zijazo, lazima afanye vitu vitatu: Baada ya Swala za usiku (Salat Layl), soma Ziyarat , na Ziyarat Jamia Kabira.

MALIPO KWA WALE AMBAO WANABAKIA KATIKA NJIA ILIYONYOOKA LICHA YA MAJARIBIO NA MATESO Kuna malipo mengi kwa wale ambao wana imani kamili katika kuwepo kwa Imam Mahdi (a.s.) na ambao wamengojea kwa subira kujitokeza kwake lakini wamefariki. Baadhi ya faida hizi ni: • Mtume (s.a.w.w.) aliwajulisha masahaba zake kwamba malipo kwa ajili ya tendo jema la wafuasi wake wakati wa siku za mwisho itakuwa mara ishirini kuliko tendo kama hilo likifanywa na sahaba zake. Hii ni kwa sababu ya uzito wa majaribio na mateso ambayo wafuasi wa baadae watakumbana nayo.

• Imam Ali (a.s.) ananukuliwa akiscma kwamba wale ambao walikuwa tayari na kungojea (kujitokeza tena kwa Imam) watalipwa na Allah hadhi ya mashahidi wanaogaragara kwenye damu zao.

• Hadithi kutoka kwa Imam Jafar Sadiq (a.s.) inaelezea kwamba mtu anayekufa wakati akiwa anangojea kwa ajili ya Imam kujitokeza kwenye Ghaibat yake, atalipwa kama mtu ambaye haswa ameungana na Imam wakati wa kujitokeza kwake.

46 • Bado kuna hadithi nyingine kutoka kwa Imam Jafar Sadiq (a.s.) inayosema kwamba wale ambao watavuta subira kwa majaribio na mateso na kuwa imara katika imani ya Imam wao, watapata malipo yafuatayo: • Dhambi zao zitasamehewa, • Matendo yao yatapewa daraja kama matendo ya ibada, • Kwasababu yao Adhabu ya Kiungu itaepushwa.

HITIMISHO Sasa kwa vile tunatambua hatari iliyo mbele yetu kwa kutokuwepo kwa Imam wa zama yetu na pia njia za kujiepusha tusiangukie kwenye hatari hizo, tunahitaji kuishi maisha yaliyo jaa tahadhari. Kamwe wakati wowote tusimruhusu Shaitan apandikize mbegu zake za mashaka katika akili zetu kuhusiana na Imam wetu. Kwani mashaka kama hayo huzalisha kutoridhika, kukata tamaa na hatimae kupoteza imani. Mazingatio yetu lazima yawe ni kubakia imara katika matendo ya ibada na kuishi maisha ya uchamungu na ufahamu wa Allah, kama ilivyoelezwa kwetu na Mtume (s.a.w.w.) na Maimam (a.s.). Kuziweka akili zetu wakati wote zikiwa zimejaa ukumbusho wa Imam wetu, dondoo ifuatayo kutoka kwenye Ziyarat ya Ijumaa na iwe ni wimbo wetu wa kila siku: “Mimi ni mgeni wako kwa siku ya leo, natafuta hifadhi na sadaka kwa vile unatokana na familia ya wale ambao ni wema na wakarimu katika kutoa hifadhi na makazi.”

47 SURA YA SITA KUJITOKEZA TENA KWA IMAM MAHDI (A.S.)

UTANGULIZI Imam Mahdi (a.s.) ana hamu kubwa ya kutoka kwenye Ghaibat. Inasemakana yuko tayari wakati wote kujitokeza lakini lazima apate amri kutoka kwa Allah kufanya hivyo. Kutokana na hadithi mbalimbali zilizotujia kutoka kwa Maimam wateule (a.s.) wa kiungu, tumekuja kufahamu kwamba hata Imam Mahdi (a.s.) mwenyewe hajui ni lini haswa ataamriwa kutoka kwenye Ghaibat. Hadithi zifuatazo zinaunga mkono habari hii: Abu Hamza Thimali anamnukuu Imam Jafar Sadiq (a.s.) akisema kwamba Mtume (s.a.w.w.), alipoulizwa na Salman Farsi kwamba kujitokeza kwa Imam Madhi (a.s.) kutakuwa lini, alijibu: “Hakuna ajuaye hilo mbali na Allah....”

Hata hivyo, kabla hajajitokeza, kutakuwa na dalili fulani ambazo zitawawezesha wafuasi kujiandaa wenyewe kwa ajili ya tukio hili kubwa. Hadthi mbalimbali zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na Maimam (a.s.), zinazoelezea dalili mbalimbali ambazo zitajitokeza mapema kabla ya mwisho wa Ghaibat Kubwa, zinaweza kupangwa katika makundi yafuatayo: a. Dalili za jumla b. Dalili makhususi

Kumbuka: Dalili hizi huchukuliwa kama “Mutasharihat”: Tunaamini kwamba zitatokea lakini maana ya kweli na tafsiri yake anaijua Allah Peke Yake tu.

DALILI ZA JUMLA Hadithi ya Kwanza: Mtume (s.a.w.w.) ananukuliwa akisema kuwaambia sahaba zake kwamba katika siku za mwisho dalili zifuatazo zitaonekena: • Mali itaabudiwa; watu wataheshimiwa kwa sababu ya utajiri wao.

48 • Imani itakuwa katika jina tu; Uislamu utakuwa wa mdomo tu. • Qur’an itasomwa katika matukio maalumu na maelekezo yake hayatafuatwa. • Misikiti itajaa watu wenye kuabudu lakini nyoyo zao zitakuwa zimejaa uadui na kuhusudiana wenyewe kwa wenyewe. • Wengi wa wanachuoni wa dini watakuwa walafi na wayakinifu.

Hadithi ya Pili: Imam Ali (a.s.) katika khutba yake katika msikiti wa Kufa alitangaza: “Mimi ni baba wa Mahdi.” Wakati alipoulizwa ni lini Mahdi atajitokeza tena, alionesha matukio ambayo baadhi ni: • Sheria za Mungu zitakuwa zimefichwa; Sheria za dini hazitawekwa wazi kwa ajili ya hofu. • Wanawake wachamungu, wapole na wenye heshima watadhalilishwa, kunyanyasa na kukandamizwa. • Uzushi (Bid’a) utaingizwa katika dini. • Iraq itakuwa imetawaliwa (na wavamizi), utakuwepo ukandamizaji wa kutisha, na kutakuwepo na umwangaji wa damu.

Hadithi ya Tatu: Imau Jafar Sadiq (a.s.) aliwaambia masahaba zake kwamba katika siku za mwisho wa ulimwengu, dalili zifuatazo zitajitokeza: • Watu wachamungu watakufa kwa wingi wakati ambapo watakuwepo madhalimu na wakandamizaji. • Qur’an itatafsiriwa kwa mujibu wa matakwa na haja za watu. • Ukafiri na batili vitapata nguvu. • Matendo yaliyoharamishwa na maovu yatafanywa kwa wazi na hakuna atakayepinga hilo. • Ushoga na usagaji utakuwa jambo la kawaida. • Sifa bandia zitaonekena kila mahali.

49 • Vijana hawatakuwa na heshima kwa wazee. • Utajiri utatumika katika shughuli za uovu ili kupata utukufu na hakuna mtu atakayejitokeza kulikomesha hili. • Wachamungu na watu wema watadharauliwa na kupuuzwa. • Unywaji pombe utafanywa hadharani na maovu ya aina hii yatawafurahisha watu. • Kuwaita watu katika fadhila itakuwa ngumu, ambapo itakuwa ni rahisi kufanya vitendo vya uovu na dhambi. • Wanawake watajikusanya na kufanya mikutano. • Matajiri ingawa hawana dini wataheshimiwa kwa sababu ya utajiri wao; watu wema watadharauliwa (kwa sababu ya kukosa kwao utajiri). • Riba itatozwa; uzinifu utakuwa shughuli yenye sifa. • Watu watatenda kwa mujibu wa matakwa na haja zao ingawa hili ni kinyume na mafundisho ya Qur’an na hadithi za Mtume (s.a.w.w.). • Michango ya wahisani na zawadi haitatolewa katika njia iliyoelekezwa na Allah bali kwa njia za kuleta utukufu na umaarufu. • Wanawake watawatawala wanaume. • Watu hawatakuwa na ghera ya kusikiliza Qur’an, hadithi au mijadala ya kidini bali ari ya kushiriki katika mazungumzo ya kipuuzi. • Watu watakuwa na mali lakini hawatataka kutekeleza amri za kidini zilizoamrishwa juu ya wajibat wa kifedha. • Wakati wakiambiwa kuhusu hukumu za kidini, watu watasema: “Hili haliingii akilini mwangu.” • Kutokuwatii wazazi itakuwa ni jambo la kawaida, watoto watawafedhehesha wazazi wao na kuleta tuhuma za uwongo dhidi yao; watakuwa wanasubiri kwa hamu kufa kwa wazazi wao na kushcherekea juu ya vifo vya wazazi wao. • Siku ambayo itapita bila kufanya uovu itachukuliwa kama siku iliyotumiwa vibaya.

50 • Sadaka na msaada utatolewa kwa misingi ya mapendekezo ya watu (wanaotoa sadaka au msaada huo ). • Watu watakuwa wayakinifu sana, watavutiwa na fahari ya ulimwengu huu, starehe na utajiri.

Kisha Imam (a.s.) akawaonya wafuasi wake kwamba wakati dalili kama hizo zikijitokeza, watu wa zama hizo lazima waombe kujikinga kwa Allah kutokana na adhabu yake ambayo itakuwa katika muundo wa majanga na vifo vya ghafla.

DALILI MAKHSUSI Imam Ali (a.s.) alisema kwamba kabla tu ya kujitokeza tena kwa Imam Mahdi (a.s.) dalili tisa makhususi zitaonekana: 1. Dajjal atajitokeza. 2. Sauti kubwa itasikika kutoka angani. 3. Sufiani atajitokeza na kuanzisha vita vikali. 4. Jeshi la Sufiani litamezwa katika eneo la wazi katika ardhi kati ya Makka na Madina. 5. Sayyid mchamungu atauawa mjini Makka. 6. Sayyid kutokana na kizazi cha Imam Hasan (a.s.) atajitokeza na jeshi lake mwenyewe. 7. Sura ya binadamu itajitokeza angani mkabala na jua. 8. Kutakuwa na kukamatwa kwa jua katika mwezi wa Ramadhani 15 na kukamatwa kwa mwezi katika siku ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani. 9. Katika matukio matatu tofauti, sauti kubwa zitasikika kutoka angani katika mwezi wa Ramadhani.

Baadhi ya dalili hizi zimeelezwa kwa urefu, nyingine hazikuelezwa katika maelezo makubwa; maana yake anaijua Allah Peke Yake.

KUJITOKEZA KWA DAJJAL Dajjal atajitokeza siku ya 18 baada ya kujitokeza kwa Imam Mahdi (a.s.). Alizaliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.), ambaye inaaminika alimtembelea pamoja na masahaba zake. Amefung-

51 wa jela lakini atatoka kwenye kifungo chake na kuuliwa na Imam Mahdi (a.s.). Kuna mgongano wa hadithi kuhusiana na sehemu ambako atajitokeza. Baadhi ya hadithi zinasema kwamba atojitokeza kutoka India; nyingine zinasema atajitokeza kutokea Palestina, bado nyinge zinasema atajitokeza kutokea Isphahan (Iran).

Dajjal atakuwa na jeshi lenye nguvu, jeshi hilo litajumuisha Wayahudi 70,000. Atajitokeza wakati ulimwengu utakuwa umepigwa na ukame kwa muda wa mika mitatu mfululizo. Atadai kuwa yeye ni Mungu. Atawaahidi chakula na Pepo wale watakaoungana naye. Kwa upande mwingine wale watakaomkataa watatishiwa Moto wa Jahannam.

Juu na zaidi ya hayo, atakuwa na uwezo wa kutoa taswira ya Pepo na Jahannam. Vilevile atakuwa anacheza muziki. Wale ambao wanapenda muziki watavutiwa naye.

Huu utakuwa wakati mgumu sana kwa waummi. Watalazimika kujilinda wenyewe na vishawishi ambavyo kwamba Dajjal atawapa kwa kubadilishana na kiapo chao cha utii na imani. Watu wengi wenye imani dhaifu wataangukia katika mawindo ya mbinu za Dajjal.

Kisha Imam ataelekea kwenda kumaliza hatari inayokuja kutoka kwa Dajjal. Baada ya mapambano makali, Imam (a.s.) atamuuwa Dajjal. Kipindi cha kujitokeza kwa Dajjal na maangamizi yake kutadumu kwa muda wa siku arubaini.

KUJITOKEZA KWA SUFIYANI NA TANGAZO LAKE Sufiyani ni mtu mwenye sura mbaya na duni aliyejaa chuki kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w.), kizazi chake na wafuasi wake. Atajitokeza kutoka Palestina katika mwezi wa Rajab. Atatawala kwa muda wa miezi nane tu, lakini hizo zitakuwa siku ngumu sana. Ataitawala Syria, Misr na Kaskazini-Magharibi ya dola za Afrika za Algeria,

52 Tunisia na Morocco. Vilevile ataivamia Jordan na kuiunganisha na Himaya yake. Makao Makuu yake yatakuwa Damascus.

Jeshi lake litakuwa na makafiri 70,000 ambao watawatisha sana Waislamu popote watakapokwenda. Watashambulia Iraq na kuharibu kuta zinazozunguka Msikiti wa Kufa. Kisha wataiteka Madina na kusababisha vurugu katika jiji hilo. Mwisho wa utawala wa kidhalimu utafika wakati atakapoamua kuendelea kuelekea Makka kuivunjia heshima Nyumba ya Allah.

Akiwa njiani kuelekea Makka, jeshi la Sufiyani litakutana na adhabu ya kiungu. Ardhi ambayo watakuwa wanatembea juu yake itawameza wote, isipokuwa watu wawili wataachwa ili waje wausimulie ulimwengu uliobakia kilichomtokea Sufiyani na Jeshi lake.

Hadithi nyingine kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) inaelezea matukio kumi ambayo hatimaye yatapelekea kwenye Siku ya Hukumu. Matukio hayo machache ni: 1. Moshi: Moshi utayazunguka mazingira ya ulimwengu. Utasababisha mchochoto kama mafua. Athari ya jumla itakuwa watu watajihisi kama vile wako kwenye nyumba ya moto. Hali hii itaendelea kwa muda wa siku arubaini. Hili litakuwa ni onyo kwa watu ili kuweka matendo yao pamoja. Baadhi watafanya hivyo, lakini walio wengi hawatafanya hivyo.

2. Dajjal: Kama ilivyoelezwa kabla, atakuwa kiumbe mwenye nguvu sana ambaye atashawishi watu kumkubali yeye kama mungu na kujiunga na majeshi yake. Mtume Isa (a.s.) na Imam Mahdi (a.s.) watapigana naye, watamshinda na mwishowe watamuuwa. Baadhi ya wanachuoni wana rai kwamba Dajjal atakuwa ni mfumo wa serikali kubwa wakati huo na itabadilishwa kwa kipindi cha utawala wa Imam Mahdi (a.s.).

3. Dabatul Ardh: Kilugha hii ina maana ya “Mtembeaji wa

53 Ardhi”. Huyu atakuwa ni mtu ambaye atatenganisha waumini kutoka kwa makafiri. Atanyanyua kichwa chake na watu watamuona. Kwa mujibu wa baadhi ya hadthi, mtu huyu atakuwa Imam Ali (a.s.).

4. Kuchomza jua kutokea magharibi: Baadhi ya wanachuo- ni wanatoa tafsiri ya maana ya maneno halisi ya hadithi hii, wengine wanatoa maelezo ya kisitiari.

Maelezo ya maneno halisi: Kwa mchakato wa kisayansi uitwao “Precision of the equinoxes”, Ncha ya kasikazini itachukuwa nafasi ya ncha ya kusini na ncha ya kusini itachukuwa nafasi ya ncha ya kasikazini. Kwa mabadiliko haya, jua litachomoza kutokea magharibi.

Maelezo ya kisitiari: Huelezea kujitokeza tena kwa Imam Mahdi (a.s.). Imam Ali (a.s.) anasema: “Yeye ni jua ambalo litachomoza kutokea linakozamia (magharibi)”.

5. Ujio wa Nabii Isa (a.s.): Atatokeza upande wa mashariki wa Damascus. Ataswali nyuma ya Imam Mahdi (a.s.). Pamoja na Imam Mahdi (a.s.) atamuuwa Dajjal na kuvunja msalaba.

6. Kujitokeza kwa Juji wa Maujuji: Kwa uwezekano zaidi, watakuwa ni binadamu kutokana na kabila na taifa makhususi. Watautawala ulimwengu. Watakuwa na udhibiti kamili wa njia za angani. Watakuwa na uwezo wa kutupa ‘mishale’ angani na kuirudisha tena. Baadhi ya wanachuoni wamechukulia ‘mishale’ kumaanisha ndege (makombora) zinazorushwa anga za juu. Watakuwa na majivuno. Hatimaye ‘minyoo’ itawauwa wote. Tena, baadhi ya wanachuoni wameichukulia ‘minyoo’ kwa kumaanisha mlipuko wa virusi.

7, 8, 9. Mimomonyoko mitatu ya ardhi: Mmoja utatokea Mashariki na mmoja Magharibi na mmoja utatokea katika rasi ya Arabia.

54 10. Kutokea kwa moto: Utaanzia Yeman na kuwafukuza watu wakutane katika sehemu moja, Mahshar.

HITIMISHO Hakuna shaka kwamba punde au baadae, Imam Mahdi (a.s.) atakuja kutoka kwenye Ghaibat yake na kusimamisha Ufalme wa Allah juu ya ardhi, katika misingi ya haki na usawa. Hata hivyo, lini hili litatokea, hakuna ajuaye isipokuwa Allah. Vivyo hivyo, tumepewa maelekezo fulani ya lini hili tutegemee hili kutokea. Tumeelezwa baadhi ya dalili ambazo wakati zikuwa dhahiri, lazima tujitayarishe kumpokea Imam (a.s.).

Kweli, baadhi yetu hatutaishi muda huo mrefu kuweza kushuhudia tukio hili kubwa. Hata hivyo, imeelezwa katika hadithi kwamba wale ambao kwa kweli na kwa unyofu wanataka kuwa na Imam Mahdi (a.s.) wakati akija kutoka kwenye Ghaibat yake, lakini wakafa na matakwa yao haya, watafufuliwa kutoka kwenye makaburi yao wakati Imam (a.s.) atakapojitokeza tena. Je, unataka kuwa mmoja wa watu kama hao?

(Ndio hakika! ! - Mtarujuma)

55 SURA YA SABA RAJ’AT (MAREJEO)

UTANGULIZI Dhana ya Raj’at ni moja ya imani kwa kawaida zinazokubaliwa za itikadi za Shia Ithna-Asheri. Kuikataa dhana hii humuweka mtu miongoni mwa wale ambao hawaikubali kwa ukamilifu Madhehebu ya Ahlul Bayt. Dhana hii imetajwa kwa mukhtasari kwa maneno mazito katika Qur’an na kuungwa mkono na hadithi mbalimbali kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na warithi wake - Maimam (a.s.). Kwa hiyo, ni muhimu sana kuelewa kile ambacho kinahusu dhana hii ya Raj’at, na kutambua dalili zake katika mwanga wa Qur’an na baadhi ya hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na Maimam (a.s.).

RAJ’AT NI NINI Raj’at ni neno la Kiarabu ambalo lina maana ya Kurudi (au marejeo). Hata hivyo, katika muktadha wa itikadi ya Shia Ithna-Asheri, in- aonesha kwenye kipindi kile, baada ya kujitokeza tena kwa Hadhrat Mahdi (a.s.), wakati ambapo baadhi ya watu ambao wamekwisha fariki watarudishiwa uhai wao; kutakuwa na ufufuo mdogo. Ufu- fuo kamili kwa watu wote waliokufa utatokea Siku ya Qiyama. Kwa hiyo, kwa mukhtasari kuna aina mbili za ufufuo zilizotajwa katika Qur’an: Raj'at au ufufuo mdogo wa uchaguzi wa baadhi ya watu waliofariki; na Qiyama au ufufuo kamili wa watu wote. Rai hii im- eelezwa kwenye Qur’an. Tafakari aya zinazofuata:

Sura 27:83: “Na siku tutakapowakusanya watu kutoka kila umma, kundi katika wanaokadhibisha ishara zetu. Nao watagawanywa mafungu mafungu.”

Linganisha aya hii na ambayo inasema “Kundi” “Kutoka kila ummah” na hii aya ifuatayo ya 47 sura ya 18 ambayo inasema: “Na siku tutakayoipitisha milima na utaiona ardhi iwazi; Tutawafufua wala hatutamuacha yeyote katika wao.”

56 Sura ya 27 aya ya 83 inataja tu ufufuo mdogo (Kundi tu ndilo litakalo kusanywa); hiyo ni Raj’at.

Sura ya 18 aya 47 inataja ufufuo wote kwa ujumla (Tutawafufua wala hatutamuacha yeyote katika wao).

NI NANI WATAKAORUDI KUTOKA KWENYE UMAUTI WAO WAKATI WA KIPINDI CHA RAJ’AT? Baada ya Imam Mahdi (a.s.) kuja kutoka kwenye Ghaibat yake, baadhi ya watu wachamungu sana na baadhi ya watu waovu sana, ambao tayari wamekwisha kufa, Allah atawafufua. Sababu kubwa ya ufufuo huu ni kuwafanya watu wema waone na kufaidi kutokana na ufalme wa kweli wa Mungu na kwa watu waovu ili wapate kuadhibiwa kwa ajili ya matendo yao maovu ambayo waliyafanya dhidi ya watu wema. Kwa kuunga mkono ukweli huu, zingatia hadithi ifuatayo kutoka kwa Fadhl Ibn Shadhan in his Mukhtasaru Ithbati’r – Rajah (Hadith Na. 7). Hadithi hii inasema kwamba katika Siku ya Ashura, Imam Husayn (a.s.) aliwajulisha wasaidizi wake ni kina nani watauliwa kishahidi siku ifuatayo: “...Shrehekeni (kwa habari nzuri za) Pepo. Wallahi tutaipata, baada ya kile ambacho kitatupata, muda mrefu kwa kadiri Allah atakavyotaka; Allah atatufua sisi na ninyi wakati Qaim wetu atakapojitokeza. Atalipiza kisasi kutoka kwa wakandamizaji na utawaona (watakuwa) wamevaa minyororo na pingu (wakiwa katika) aina mbalimbali za kuadabishwa na adhabu...”

Hivyo kwa mujibu wa hadithi hii, wahanga wote wa Karbala watafufuliwa na vivyo hivyo wale ambao walishiriki katika kuwakandamiza katika siku ile ya Ashura, pamoja na Yazid, Ubaidullah Ibn Ziyad, Umar Ibn Saad na Shimr Ibn Dhiljaushan. Mashahidi watapata fursa ya kutaka kulipiza kisasi chao kutoka kwa wale ambao waliwakandamiza au kuwauwa.

Wakati wa Raj’at, Mtume (s.a.w.w.), Imam Ali (a.s.) na Maimam wengine kumi watarudi. Pamoja nao watakuwepo wafuasi wao

57 ambao kwa ukweli walitamani na kutaka kuwa na Imam Mahdi (a.s.) lakini walikufa kabla ya Imam (a.s.) hajajitokeza kutoka kwenye Ghaibat.

Utakuwa ni wakati huu kwamba Nabii Isa (a.s.) atashuka chini kutoka Mbinguni kumsaidia Imam Mahdi (a.s.) kumshinda Shaitan na wafuasi wake.

UFALME WA ALLAH KATIKA ARDHI WAKATI WA RAJ’AT Imam Mahdi (a.s.) atamuuwa Shaitan na wale wote ambao walimsaidia, na atasimamisha Ufalme wa Allah juu ya ardhi. Kwa maneno hayo Abu Said Khudri, sahaba mashuhuri wa Mtume (s.a.w.w.), ananukuu hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Watu watakusanyika kumzunguka Mahdi kama nyuki wa Sali wanavyomzunguka malikia wao. Mahdi ataujaza ulimwengu na usawa na haki kama ambavyo utakavyo kuwa umejazwa na ukandamizaji. Watu watabadilika kuwa wema na kurudi kwenye sifa zao za asili ... ”

Imam Mahdi (a.s.) atatawala kwa muda usiojulikana. Mwishowe, atauliwa kishahidi. Baada yake Maimam wote, kila mmoja kwa wakati wake atatawala kwa muda anaoujua Allah peke Yake.

Wakati wa kipindi hiki, kutakuwa na hali kamili ya amani, ustawi na utulivu. Simba na ngamia, duma na ng’ombe na mbuzi, wataishi kwa upendo kati yao wenyewe kwa wenyewe.

MWISHO WA RAJ’AT Dhana ya Raj’at iko wazi; hata hivyo, maelezo yake hayajulikani kwa ukamilifu. Lakini hii sio kinga. Kuna maelezo mengi yanayohusiana na maisha na kifo ambayo Allah ameyafanya siri kwetu.

Yote yametajwa na kufanywa, hatimaye pia Raj’at itafikia mwisho. Kila kiumbe cha Allah kitafikia mwisho: watakoma

58 kuwepo. Kipindi hiki cha ‘kutokuwepo’ kitadumu kwa muda unaojulikana kwa Allah tu. Aya zifuatazo za Qur’an zinaelezea kwa ufupi lakini kwa uwazi mwisho wa Raj’at na kuanza kwa Qiyama: “Na siku tutakayoipitisha milima, na utaiona ardhi iwazi. tutawafufua wala hatutamuacha yeyote katika wao.” (18:47)

HITIMISHO Dhana ya Raj’at ni sehemu muhimu sana ya imani ya Shia Ithna- asheri. Ina mizizi yake katika Qur’an na hadithi nyingi kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na warithi wake wateule wa kiungu, Maimam (a.s.). Kuikata ni sawa na kukataa sehemu muhimu ya Madhehebu ya Ahlul Bayt. Raj’at wakati mwingune hutajwa kama ‘Qiyamat Sughra’ au Siku ndogo ya Ufufuo. Qur’an Sura ya 40 aya ya 11 inaweka kwenye tafakari hatua mbalimbali za kuwepo mwanadamu katika maneno haya: “Watasema: Mola wetu! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili! Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka?”

Vifo viwili maana yake ni: • Kifo baada ya maisha haya ya ulimwengu. • Kifo baada ya Raj’at.

Na matukio miwili ya uhai ni: • Maisha wakati wa Raj’at. • Maisha kwenye Qiyama.

59 SURA YA NANE MIUJIZA YA IMAM MAHDI (A.S.)

UTANGULIZI Ni kipi kinachoweza kuwa muujiza zaidi kuliko ukweli kwamba Imam (a.s.) yuko hai leo; akiwa amezaliwa mwaka wa 255 A.H, na ataishi mpaka wakati wa Raj’at. Zaidi na juu ya hayo, yuko huru kutokana na kuzeeka kimwili. Aidha, hazuiwi kwa ukomo wa nafasi, wala mwendo na siku zote ana habari ya ustawi wa Ummah. Kuwepo haswa kwa ulimwengu huu hutegemea kuwepo kwake na anashughulikia mahitaji na mwito wa waummi.

BAADHI YA MIUJIZA YAKE 1. Kipindi alipokuwa tumboni mwa mama yake, hakuonesha dalili zozote za ujauzito. Hili lilithibitishwa na shangazi wa Imam Hasan Askari (a.s.), Hakima Khatun. Alikuja kujua ujauzito wa Nargis (Mamake Imam Mahdi) masaa machache kabla ya kujifungua mtoto.

2. Tofauti na mtoto wa kawaida wa mwanadamu, maisha ya utoto ya Imam Mahdi (a.s.) yalikuwa sio ya kawaida. Siku ya pili ya kuzaliwa kwake, mtumishi wa nyumbani akiitwa Nasiim, alipiga chafya karibu na susu ambamo Imam mtoto alikuwa amelala. Kwa mshangao mkubwa wa yule mtumishi, Imam (a.s.) alizungumza kwa Kiarabu kilicho wazi: “Allah awe na huruma juu yako” na kisha akaongeza: “Yeyote yule anayepiga chafya, anahakikishiwa maisha yake takriban kwa muda wa siku tatu.”

3. Siku arubaini baada ya kuzaliwa Imam Mahdi (a.s.), Hakima Khatun alimtembelea Imam Hasan Askari (a.s.). Alishangazwa kumuona mtoto Imam Mahdi (a.s.) amekua kwa haraka sana kiasi kwamba anaonekana kama mwenye miaka miwili.

4. Akiwa Imam wa zama anayeishi, Hadhrat Mahdi (a.s.) ni mwendelezo wa chanzo cha mwongozo kwa yeyote yule

60 anayemuita kwa ajili ya msaada kama inavyooneshwa na vielelezo vichache ambavyo vinatolewa hapa chini: • Muhammad bin Yusuf al-Shasti anasimulia kwamba alikuwa na tezi lisilo pona kwenye mgongo wake. Madaktari wa zama hizo walikata tamaa juu yake. Aliandika barua ya msaada kwa Imam Mahdi (a.s.) akiomba msaada wake. Imam (a.s.) alimjibu pamoja na maombi (du’a). Muhammad alipona kabisa, kwa mshangao wa madaktari ambao walisema: “Siha inaweza tu kurudishwa moja kwa moja na Allah.”

• Hasan bin Fadhl alikuwa na maswali matatu ambayo alitaka Imam (a.s.) ayajibu. Aliandika barua kwa Imam (a.s.), akiweka maswali mawili, bila kutaja swali la tatu, akifikiri kwamba si sahihi kuuliza swali hilo. Imam (a.s.) alimuandikia akitoa majibu ya maswali mawili, na hali kadhalika jibu kwa swali la tatu, ingawa halikutajwa kwake katika barua ya maswali.

• Allama Hilli alikuwa mmoja wa wanchuoni mashuhuri wa zama zake, akiishi Hilla. Mama mjamzito alifariki. Ndugu zake waliomba hukumu; kama wanaruhusiwa kumtoa mtoto kutoka tumbo la mama. Hukumu ya Allama ilikuwa kwamba maiti ya mama izikwe pamoja na mtoto tumboni mwake. Miaka kadhaa Baada ya tukio hili, mwanaume mmoja akiwa na mtoto alimtembelea Allama. Katika kuuliza, Allama alijulishwa kwamba mtoto anayeulizwa alikuwa ni yule ambaye mama yake alifariki na Allama kwanza alitoa hukumu kwamba mwanamke azikwe pamoja na mtoto lakini kisha akabadilisha hukumu yake na mtoto alitolewa kutoka kwa mama aliyefariki. Allama alipatwa na mshituko aliposikia hili. Hakubadilisha hukumu yake. Alikuwa na imani kwamba Imam Mahdi (a.s.) alikuja kumsaidia. Allama aliamua kutotoa hukumu yoyote kuanzia wakati ule na

61 kuendelea. Hata hivyo, alipokea barua kutoka kwa Imam (a.s.) ikimuamuru kuendelea na kazi yake na kwamba ikijitokeza haja wakati wowote, Imam mwenyewe atamsaidia, kama alivyofanya katika suala hili husika.

• Allama Sheikh Hur Aameli ni mwanachuoni mkubwa wa Shia na mkusanyaji wa kazi kubwa (ya kimaandishi) juu ya fiqh iitwayoWasail Ush-Shia. Anasimulia kwamba wakati alipokuwa kijana, aliugua na hali yake ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba kulikuwa hakuna matumaini ya kupona. Ndugu zake wamemkatia tamaa na kusalimu amri kwenye kifo. Kisha yeye aliota ndoto ambayo kwayo aliwaona Maimam Masoomin. Anakumbuka kwamba alimsalimu Imam Jafar Sadiq (a.s.) na kisha alikwenda kwa Imam Mahdi (a.s.). Alimlilia Imam (a.s.) huku akimuomba Imam (a.s.) amuombee ili apate kupona kutokana na maradhi haya yasiyotibika. Imam (a.s.) akamhakikishia kwamba atapona. Kisha Imam akampa kikombe kilichojaa maji. Alikunywa maji yale. Alipoamka usingizini alikuwa amepona kabisa.

Miujiza mingi zaidi kama hii ilitokea lakini ufinyu wa kijitabu hiki hauruhusu kutaja miujiza zaidi.

62 SURA YA TISA SEMI ZA IMAM MAHDI (A.S.)

UTANGULIZI Tofauti na Maimam wengine kutoka Ahlul Bayt ambao walikuwa wanafikiwa na wafuasi wao licha ya vikwazo, Imam Mahdi (a.s.), kwa sababu ambazo tayari zimekwisha elezewa, aliishi maisha yake zaidi katika Ghaibat. Kwa sababu kukutana moja kwa moja na Imam (a.s.) kumekuwa kidogo, maneno na ushauri kutoka kwake yamekuwa na ukomo katika idadi lakini sio kwa mapana. Ushauri mwingi wa Imam huyu ulikuja kupitia ‘Sufara’ wake au kupitia barua zake akijibu masuala yaliyoletwa kwake na wafuasi. Kwa nyongeza ya hilo, Du’a na Ziyarat ambazo Imam (a.s.) amependekeza kwa wafuasi wake pia zina sehemu muhimu za ushauri.

Ufuatao ni ushauri kadhaa uliotolewa kutoka kwenye vyanzo hivi: 1. Viumbe wa Allah hawakuumbwa bure wala hakuwafanya viumbe wawepo bila madhumuni yoyote.

2. Allah alimnyanyua Mtume (s.a.w.w.) katika Utume kama rehema kwa ulimwengu na kupitia kwake akakamilisha neema Zake, mfululizo wa Mitume, na akamtuma kama mwongozaji kwa wanadamu.

3. Nyoyo zetu ni mapokezi ya Utashi wa Mungu. Chochote Allah anachotaka, sisi (Ahlul Bayt) hupenda hicho hicho.

4. Waongo ni wale wanaoweka muda kuhusiana na kutoka kwenye Ghaibat kwa Imam Mahdi (a.s.).

5. Hakika, Mimi (Imam Mahdi) ni chanzo cha usalama kwa ajili ya watu wa ardhi hii.

6. Mtu yeyote anayekula (kwa ulafi) sehemu yoyote ya malipo yetu

63 (kama Khums), hakika, inakuwa sawa kwake kama anayekula moto na ataishia kwenye moto wa Jahannam.

7. Kila mmoja miongoni mwenu lazima ashikamane na matendo yale ambayo yanakukurubisheni karibu na upendo wetu na kukuweka mbali kutokana na yasiyotupendeza na kutukasirisha.

8. Fungeni milango kwa maswali yale ambayo hayana faida kwenu.

9. Mimi ni Mahdi (Masihi). Mimi ni Qaim (wa zama). Mimi ni yule ambaye nitaujaza ulimwengu na uadilifu kama ambavyo utakuwa umejaa dhuluma. Kamwe ulimwengu haupo bila ya Hujja (Ushahidi) wa Allah.

10. Hakuna kinachomchochota Shaitwan kama Swala, hivyo chungeni Swala ili kumchochota Shaitwan.

11. Hakika, tuna ujuzi kamili wa hali zenu na hakuna kitu chochote ambacho kinafichwa kwetu kuhusiana na ninyi.

12. Hakika sisi ni wasikivu wa kuwaangalia ninyi wala hatuwapuuzi katika kuwakumbukeni ninyi.

Katika muundo wa maombi (Du’a), Imam Mahdi (a.s.) anawashauri wafuasi wake kufanya yafuatayo: 1. Wanachuoni: kuchunga uchamungu na kuwaonya wengine. 2. Wanafunzi: wafanye juhudi na wawe makini katika kupata elimu. 3. Wajifuanzao: kusikiliza na kukubali kile ambacho wanashauriwa. 4. Waislamu wote: • Wawaangalie wagonjwa na kuwafariji. • Wawakumbuke maiti kwa upendo na huruma. • Watendeeni wakubwa na wazee kwa huruma, kuwathamini na kwa utulivu.

64 5. Vijana: kujifunza kuelekea kwenye wema na toba. 6. Wanawake: kuchunga adabu na haya. 7. Masikini: kuwa wavumilivu na kutoshrka. 8. Matajiri: kuwa wanycnyekcvu na watoaji.

HITIMISHO Allah (swt), atupe sisi wote hekima ari ili kuyaweka katika matendo mafundisho haya ya Imam wetu. Kama tukifanya hivyo, tutapata manufaa ya ulimwengu huu na Akhera. Kwani Imam (a.s.) imetuahidi kuhusu faida hizi kwa maneno haya: “Na kama wafuasi wetu, (Allah awafanye wafanikiwe katika kumtii Yeye), wangekuwa wameungana pamoja na nyoyo zao katika kutekeleza ahadi ambazo ziko juu yao, kusingekuwa na kukawia kwa ajili yao neema ya kukutana na sisi, furaha yao ingeharakishwa kwa kushuhudia ujio wetu pamoja na uelewa kamili.”

65 MASWALI

SURA YA KWANZA 1. Eleza kwa ufupi jinsi utakavyo tetea ukweli kwamba dhana ya u-Mahidi (umasihi) inakubaliwa na Waislamu walio wengi. 2. Kwa nini hoja ya kwamba Imam Mahdi (a.s.) bado hajazaliwa ni dhaifu? 3. Kwa nini kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.) kuliwekwa kuwa siri? 4. Toa mifano mitatu ambayo inazunguka kuzaliwa kimuujiza kwa Imam Mahdi (a.s.). 5. Ni vipi Imam Hasan Askari (a.s.) alivyopeleka ujumbe kwa wafuasi wake wachache kuhusiana na kuzaliwa kwa mtoto wake, Imam Mahdi (a.s.)? 6. Kila neno katika safu (A) hapo chini lina mfanano wake katika safu (B). Fananisha kila neno, (i) mpaka (x) kutoka safu (A) na mfanano wake katika safu (B).

Safu A Safu B 1. Uthman Ibn Sayid i. Bint wa Imam wa tisa 2. Ahmad Ibn Ishaq ii. Mama yake Imam Mahdi (a.s.) 3. Hadhrat Hadisa iii. Swala za usiku zilizopendekezwa 4. Bibi wa ki-Nubi iv. Wakil wa Imam Hasan Askari (a.s.) 5. Salatul Layl (swala za v. Rafiki wa karibu wa Imam Hasan usiku) Askari (a.s.) 6. Fadl Ibn Shadhan vi. Mama yake Imam Hasan Askari (a.s.) 7. Sausan vii. Mji ambako Imam Mahdi (a.s) alizaliwa 8. 329 AH viii. Mke wa Imam Ridha (a.s.) 9. Hakima ix. Kuanza kwa Ghaibat kubwa 10. Samarah x. Msimuliaji wa Hadithi

66 SURA YA PILI 1. Onesha kwa herufi (U) kwa maelezo yaliyotolewa hapo chini ambayo ni uwongo, na kwa herufi (K) kwa maelezo ambayo ni sahihi. Kwa kila maelezo ya uwongo, eleza kwa nini ni uwongo. i. Imam Hasan Askari (a.s.) aliuliwa shahidi katika mwaka wa 260 AH punde tu baada ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.). ii. Imam Mahdi (a.s.) hafikiwi na watu kama ilivyokuwa kwa Maimam wengine 11 kabla yake. iii. Kwa wakati huu tulionao tunaishi katika kipindi kiinachoitwa “Ghaibat Sughira” iv. Imam Mahdi (a.s.) aliwasiliana na watu kupitia “Sufara” wake wakati wa “Ghaibat Sughira” v. Kifo cha ‘Safir’ wa mwisho wa Imam Mahdi (a.s.) kilisadifu na kuanza kwa “Ghaibat Kubra”.

2. Elezea kwa ufupi sifa za ‘Sufara’ wa Imam Mahdi (a.s.)

3. Eleza kwa nini kazi za ‘Safir’ zilikuwa zimejaa hatari.

4. Kwa maswali (I) mpaka (V) hapo chini kuna chaguo nne zilizotolewa. Chagua moja ambayo ni sahihi zaidi: I. Kifo cha ‘Safir’ wa 4 kinamaanisha: a. Kutakuwa hakuna mwongozo zaidi kutoka kwa Imam (a.s.) b. Kutakuwa na ukomo wa mwongozo kutoka kwa Imam (a.s.) c. Jumuiya ya Shia itaachwa peke yake d. Mwisho wa Ghaibat Ndogo na mwanzo wa Ghaibat Kubwa.

II. Kumkataa Faqh ni kosa kubwa kwa sababu: a. Analinda dini. b. Ni mtiifu kwa amri za maula wake. c. Kumkataa yeye ni sawa na kumkataa Imam (a.s.) na Allah (swt) d. Hakuna lolote hapo juu.

67 III. Zakaria Ibn Adam na Yunus Ibn Abdul Rahaman wanatajwa kama mifano ya jinsi gani Imam aliteuwa mafaqih wanaolingana: a. Walikuwa wafuasi wa Imam Ridha (a.s.) b. Walikuwa mafaqih wa zama zao c. Hakuna lolote hapo juu.

IV. Mujtahidin ni tofauti na Sufara kwa vile: a. Mujtahidin wamekuja baada ya Sufara b. Mujtahidin ni wengi kuliko Sufara amabo walikuwa wanne tu c. Kazi zao zinatofautiana. d. Yote hapo juu.

V. “Muqalid” ni: a. Mtu anaye fanya juhudi b. Faqh c. Mujtahid d. Hakuna lolote hapo juu

5. Eleza unaelewa nini kwa haya yafuatayo: a) Ijtihad b) Mujtahid c) Taqlid d) Muqalid e) Alam

6. Kamilisha maelezo yafuatayo kwa kujaza nafasi zilizo wazi: i) Faqih lazima awe a) ______b) ______c) ______d) ______

ii) Imam Jafar (a.s.) aliwafundisha wanafunzi wake waaminifu

68 ili waweza kufanya ______.

iii) Fuqah walichukuwa nafasi za uongozi kwa sababu ______.

iv) ______alikuwa mtu wa kwanza katika kipindi cha ______kutowa Fatwa

v) Kwa mujibu wa Ayatullah Sistani, Mujtahid mbali ya kuwa mwanaume na Shia Ithna-Asheri, lazima awe: a) ______b) ______c) ______d) ______e) ______

SURA YA TATU 1. a) Ni matatizo gani yaliyokuwa yanaikabili jumuiya Shia mwan- zoni mwa Ghaibat Kubra? b) Tatizo hili limetatuliwa vipi?

2. Katika maelezo yafuatayo hapo chini (A) mpaka (E) chagua moja ambayo ni sahihi zaidi: A) Baada ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.): i) Jumuiya ya Shia iliachwa bila mwongozaji kwa sababu alikuwa Mtume wa Mwisho. ii) Jumuiya ya Shia iliachwa ichague yenyewe kutafuta kiongozi wao wenyewe iii) Mwongozo ulikuja kutoka kwa warithi wa Mtume, Maimam iv) Mwongozo ulikuja kupitia Ijtihad.

B) Kwa kuuliwa kishahidi kwa Imam Hasan Askari (a.s.): i) Mwongozo wa moja kwa moja ulifikia mwisho. ii) Jumuiya ya Shia iliachwa bila mwongozo

69 iii) Jumuiya ya Shia iligeukia kwa Fuqaha kwa ajili ya mwongozo iv) Yote hapo juu

C) Katika barua ambayo aliituma Imam Mahdi (a.s.) kwenda kwa Shaykh Mufid, Imam alisema: i) Jumuiya ya Shia ni walengwa wa maadui zao ii) Alikuwa anafahamu mahitaji ya jumuiya iii) Atakuja kuwasaidi wakati wowote watakapo mhitaji iv) Yote hapo juu

D) Wakati akiitwa kwa ajili ya msaada: i) Imam wakati wote husaidia kwa kupitia njia ya mzunguko ii) Imam husaidia moja kwa moja, pamoja na idhini ya Allah. iii) Imam kamwe hasaidii moja kwa moja iv) Imam hujitokeza kwa ajili ya kutoa msaada moja kwa moja au kwa njia ya kuzunguka.

E) Fursa moja ambayo Imam Mahdi (a.s.) alipata chini ya hifadhi ya Ghaibat ni: i) Yuko huru kutokana na mateso na unyanyasaji kutoka kwa maadui zake ii) Anaishi maisha ya utulivu iii) Hasumbuliwi na watu, pamoja na wafuasi wake iv) Wajibu wake una ukomo.

3. a) Ni tatizo gani kubwa ambalo liliikabilijumuiya ya Shia wakati wa kipindi cha Ghaibat Kubwa? b) Ni malipo gani yatakuwa kwa ajili yao?

4. Eleza vipi Ghaibat Kubwa inavyo mnufaisha Imam (a.s.) na jumnuiya ya Shia.

5. Toa mifano kuelezea kwamba: “Umri rilrefu wa Imam Mahdi (a.s.) sio jambo geni wala sio kitu cha kipekee”.

70 SURA YA NNE NA YA TANO 1. Ni shemu gani ambako Imam Mahdi (a.s.) inasimuliwa kwamba alionekana ana kwa ana?

2. Kwa ufupi elezea, huku ukitoa mifano miwili au mitatu makhususi, jinsi ya kumkumbuka Imam Mahdi wakati wote.

3. Ni nini wajibu wa wafuasi wa Imam Mahdi (a.s.) wakati wa zama za Ghaibat Kubra?

4. (a) Ni matatizo gani makubwa ambayo wafuasi wa Imam Mahdi (a.s.) lazima wawe na hadhari nayo wakati wa Ghaibat Kubra'? (b) Matatizo haya yatashughulikiwa vipi?

5. (a) Ni manufaa gani ambayo wanaweza kuyapata wafuasi wa Imam Mahdi (a.s.) katika mchakato wa kungojea kujitokeza kwake tena? (b) Ni mahitaji gani yanahitajika kwa ajili ya kupokea manufaa haya?

SURA YA SITA Maelezo yote hapo chini sio ya kweli. Eleza kwa nini sio ya kweli? 1. Mbali na Imam Mahdi (a.s.) mwenyewe, hakuna mtu mwingine anaye elewa ni lini atatoka kwenye Ghaibat.

2. Dalili zote zilizotajwa katika hadithi kuhusiana na wakati kabla Imam hajajitokeza kutoka kwenye Ghaibat, zitajitokeza hivi punde au baadae.

3. Kujitokeza kwa Dajjal ni mfano wa “ujuzi wa sekondari”

4. Wakati moshi ukijotekeza, milango yote ya toba itafungwa.

5. Dalili zote za kujitokeza kwa Imam Mahdi (a.s.) lazima zichukuliwe neno kwa neno.

71 SURA YA SABA 1. Eleza tofauti kati ya Raj’at na Qiyamat.

2. Eleza kwa ufupi nani atafufuliwa wakati wa Raj’at na kwa sababu gani.

3. Kwa nini Raj’at inatajwa kama “Mbingu katika Ardhi”?

4. Kwa nini ni muhimu kupata ujuzi kuhusu Raj’at?

SURA YA NANE NA YA TISA 1. Ni kwa njia zipi ushauri kutoka kwa Imam Mahdi (a.s.) hutofautiana na zile za Maimam wengine waliokuja kabla yake?

2. Chagua shauri (uashauri) Mbili zozote kutoka kwa Imam uliofikishwa kawa maombi (du’a) na eleza ni jinsi gani utaufanyia kazi.

72 Kimetolewa na: Bilal Muslim Mission of Tanzania S.L.P 20033 Dar es Salaam – Tanzania