February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 1

COUNTY ASSEMBLY OF

THE HANSARD

Tuesday, 18th February, 2014

The Assembly met at the County Chambers, Malindi Town, at 2.30 p.m.

[The Deputy Speaker (Hon. Mwambire) in the Chair]

PRAYERS

COMMUNICATION FROM THE CHAIR

HOUSE BUSINESS

The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Liason Committee members will have some communication on Thursday afternoon. We shall have an address from the Governor and before that time we are supposed to be at the Assembly at exactly 10 a.m. for a Kamkunji and later on go for lunch with the Governor before the afternoon session. All members of different committees who might have tasks on that day; all the work of the committees on Thursday has been suspended for that event, and again on Friday we have received an invitation that at 2 p.m. we are going to have a meeting with the Governor at Kilifi Bay. Again, all deliberations which are supposed to be undertaken by all the committees stand to be suspended for that function. We are aware that the committee on Transport and Public Works will be travelling for benchmarking outside the Country. We expect them to attend the Friday meeting with the Governor at Kilifi Bay but they should be prepared because thereafter they will required to spend the night in so that they can catch their flight. I think they understand well if I put it that way. Please observe those issues. Again after the adjournment we are going to have about 10 minutes ‘Kamkunji’ so members will remain to deliberate on a few issues leaving. Mr. Clerk, messages? The Deputy Clerk (Mr. Silas): No messages Mr. Speaker. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Papers? The Deputy Clerk (Mr. Silas): No papers. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Notices of Motion? The Deputy Clerk (Mr. Silas): There is no notice of Motion Mr. Speaker. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Statements? The Deputy Clerk (Mr. Silas): No statements. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Motion? The Deputy Clerk (Mr. Silas): There is a Motion by Hon. Stephen Bahati Mlanda. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Yes Hon. Stephen Bahati Mlanda.

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 2

MOTION

ERECTION OF BUMPS

Hon. Mlanda: Mr. Speaker Sir, I rise to move the following Motion:

AWARE THAT within the Kilifi Highways and Roads many accidents have happened, injuring and killing hundreds of people. Aware that part of these roads has some bumps erected such as Mombasa-Malindi road, Mombasa-Marikani, Mazeras-Kaloleni road. Noting that, along the roads, the bumps erected are very few and we have trading centers without bumps where accidents happen every month such as; Gede- Malindi road: Kizingo stage, Msabaha Trading Centre stage, Kwa Abudu Trading Centre, Kijiwe Tanga Trading Centre stage, Thalatha Meli Trading Centre and Kwa Chocha stage. If we come to the Malindi- Lamu road we need bumps at Gongoni stage, Marereni stage, Msumarini stage and Kanagoni stage. When we take the road from Kaloleni to Mazeras or Mazeras to Kaloleni, we need bumps at Mekingi, Bondora, Makini, Mukapuni, Shika Adabu and Mwanguta stages. We have the Kilifi road at Kwa Chokwe; we have the Kituoni stage, Kadenge Fujo, Malindi road. When you come to Mombasa- Nairobi Highway, we have Marikani District Hospital gate where we need a bump. And when we come to Marikani- Kaloleni road we need bumps at Brilliant, Kaloleni Matatu stage, and Kavinautu stage. Further aware, that the bumps are of paramount importance to reducing further accidents, this Assembly urges the County Executive member in charge of Roads, Transport and Public Works to make sure the bumps are built, signboards erected and coloured appropriately at the same areas to avoid further injuries and loss of the lives of our people within the Highways and Roads of . Mr. Speaker Sir, so many accidents have happened within these roads. It is just last month, Mr. Speaker; within Malindi-Watamu Road we witnessed a very ugly accident at around 8 o’clock in the evening. Mr. Speaker, to avoid such accidents, the committee of roads decided to bring this Motion to avoid further loss of lives of our people. Mr. Speaker, I now call upon Hon. Bakari to second this very important Motion. Thank you. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Yes, a seconder please. Hon. Bakari: Thank you Mr. Speaker. I stand to second. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Members, may I take this opportunity to propose the question that this County Assembly adopts the Motion as tabled by Hon. Stephen Bahati Mlanda. So if any member has any contributions; please make any contributions or amendments since this is the right time. Yes Hon. Hamza. Hon. Hamza: Thank you Mr. Speaker Sir. I wish to make amendments on this Motion. We have seen the roads which have been highlighted here but I should say they have been selectively noted and there are some very crucial roads that have been omitted.

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 3

I therefore like to add the following roads to be in incorporated in the list. We have the Mambrui stage, Mjanaheri, Misufini, Makaburini. We have Kaembeni, Magarini, Ngandu, Jeys and Beach. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Hamza please, guide us in a way that you inform us where we need to delete and add, so that we can go as per the Standing Orders. Hon. Hamza: These are roads found within Magarini road. We have only one road that I have included here which is found along Watamu road, which is Dongokundu Road. The rest are found within the Malindi- Magarini Highway. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Hamza, I think the memo requires that you meet either the Clerk or the Speaker before the sitting. Read from paragraph 1 and highlight the amendment that you have made as a proposal so that we can go as per paragraphs. Hon. Hamza: From paragraph 1 1 wanted to change the wording. There is a sentence on line 4; actually noting that along the roads the bumps erected are few and we have trading centers without bumps where accidents happen every month. I wish to move the amendment on that word ‘few’ and put ‘insufficient’ because it is the work of this house to ensure it worked to the sufficiency as to the number, thereby when we say ‘few bumps’ that means we need ‘as many as possible.’ We need to have many bumps and what I believe is that we want to have sufficient bumps not many bumps, so contrary to that I should say we should use the word ‘insufficient’ instead of ‘few.’ In addition, paragraph 2 we have Gede-Malindi road, we have Kizingo stage, Msamaha Trading Centre stage, Kwa Abudu Trading Centre, Kijiwetanga Trading Centre stage, Thalathameli Trading Centre and Kwa Chocha stage. We have the addition of Dongo Kundu stage. I suppose we are together. In Paragraph 4 we have the Kilifi Kwa Chokwe, we have the addition there, Kituoni, Kadenge Fujo, my road, and we have the addition of all the tarmac roads next to schools which should be marked with zebra-crossing. That is the additional or rather the amendment that I have made so far. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Any member to second the amendments? Yes Hon. Sadi. Hon. Sadi: I stand to support the amendment although I wanted to add something. The Deputy Speaker (Hon.Mwambire): Are you seconding the amendment or you are making another amendment? Hon.Lali: I want to add something.On paragraph 2, in Kilifi Kwa Chokwe, Kituoni, Kadenge fujo and NYB Road, it should start at Tusky’s junction, we should have a bump, there are so many accidents happening just after the Kilifi Bridge. The Deputy Speaker (Hon.Mwambire): Thank you. Honorable Members let us just go by the Standing Orders, where we have received some amendments which we have to second them, probably read through the amended question so that we can make contributions to adhere. Please allow me to do that. The Motion as amended reads: AWARE THAT within the Kilifi County Highways and Roads many accidents have happened, injuring and killing hundreds of people. AWARE THAT parts of these roads have some bumps ready erected such as: Mombasa –Malindi Road, Mombasa-Mariakani Road, Mazeras-Kaloleni Road the bumps erected are insufficient and we have trading centre’s without bumps where accidents happen every morning as such:

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 4

Gede-Malindi road, Kizingo Stage ,Msabaha Trading Centre stage,Kwa Abudu Trading Centre ,Kijiwe Tanga Trading Centre stage,Thalathameli Trading Centre and Kwa Chocha Trading Centre and the Motion has amended to add Dongokundu stage, Malindi –Lamu main Road, Gongoni, Marereni, Msumarini, Kanagoni. Kaloleni–Mazeras Road we have Mekingi, Bondora, Makini,Mukapuni, Shika Adabu, Mwanguta stages. In Kilifi we have Kwa Chokwe, Kituoni, Kadenge Fujo, NYB Road including all the tarmac roads next to schools should be marked with zebra crossing. Mombasa-Nairobi Highway; Mariakani District Hospital Stage. Mariakani-Kaloleni Road, Brilliant Hospital stage, Kaloleni Matatu stage, Kavina Utu stage. Further AWARE THAT the bumps are of paramount importance to reducing further accidents, this Assembly urges the Executive member in charge of Roads, Transport and Public Works to make sure the bumps are built, sign boards are erected and coloured appropriately at the said areas to avoid further injuries and loss of the lives of our people within the Highways and Roads of Kilifi County. Hon. Members allow me now to put the question that this assembly deliberate on the Motion as tabled by Hon.Bahati Mlanda and amended by Hon.Hamza.

(Question put and agreed to)

The Deputy Speaker (Hon.Mwambire): Hon. Members, now the Motion stands amended and we will make contributions as per the amended Motion. Any contributions, Hon.Mwingo? Hon.Mwingo:Mr.Speaker, before I contribute, I would like to make further amendment to the Motion. The Deputy Speaker (Hon.Mwambire): You are out of order Hon. Mwingo; amendments cannot be made on the floor. The procedure demands that you bring your amendments to either Clerk or the Speaker’s office two hours before the sitting because this Motion was introduced in this house sometimes back which means members had a copy of it and knew that this Motion was in place. Hon. Mwachenda. Hon.Mwachenda: Mheshimiwa Spika, mimi nasimama kuunga mkono hoja hii kwa sababu kusema kweli kwanza swala la bumps limesaidia mahali pakubwa sana katika hali ya kupunguza ajali za barabarani na vilevile zile sehemu zilizochorwa za wanafunzi kuweza kuvukia. Tumekuja kugundua kwamba ajali nyingi barabarani zatokea sababu ya utovu wa nidhamu ikiwapo madereva wengi huichukulia ya kwamba hao ufuko wao ni bora zaidi na iwapo atakuwa amevunja sheria kama kuendesha gari kwa kasi ataweza kumhonga ofisa wa polisi ili aweze kupita. Hata hivyo, Mheshimiwa Spika ni kweli kwamba wewe huwezi kuihonga ile nundu; nimerekebishwa na mwenzangu kwamba si ‘bumps’ Kiswahili ni ‘nundu.’ Kwa hivyo ni vigumu kwani wewe huwezi kuihonga ile nundu ambapo itakulazimu upunguze kasi ya gari lako ili uweze kuvuka ile nundu ambapo moja kwa moja utakuwa umeokoa maisha ya yule mtu ambaye pengine ulikuwa umgonge ama kuhatarisha hata maisha yako wewe binafsi. Kwa hivyo mimi nimesimama kuunga mkono hoja hii na nikizingatia ya kwamba kwa wadi yangu ile Jumamosi iliyopita nimezika mtu kwa sababu ya swala kama hili na hata jana

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 5 kwangu kumetokea ajali mbaya sana ya pikipiki kugongwa na lori na yote imetokana na kuendesha kwa kasi bila kufuata hizi sheria. Kwa hivyo naunga mkono kwa dhati hoja hii tuweze kukubaliana sote ili iweze kutimizwa. Asante. The Deputy Speaker (Hon. Mwambre):Hon. Mangi. Hon. Mangi: Thank you my Speaker. I stand to support this motion; in fact we should have passed this motion days ago. Bumps have really saved the lives of very many people not only in our County but in neighboring counties. I am not only supporting this motion but in fact it should be extended or rather the Executive member for Transport should direct his officers to identify other areas, which in future, require such bumps to be erected .We can borrow a leaf from our neighboring Country, Tanzania. When you travel to Tanzania, though we got it very rough because we are used to simpler things which normally finish our lives, bumps are very effective. It is high time now that we should urge our Government, not only County Government but National Government, to follow suit. I am really supporting this motion and I call upon my fellow Honorable Members to be supportive on the same. Thank you. The Deputy Speaker (Hon.Mwambire): Hon. Mbeyu. Hon. (Ms.) Mbeyu: Thank you Mr. Speaker Sir. I stand to give my views on this motion. My feeling… The Deputy Speaker (Hon.Mwambire): Hon.Mbeyu, when you stand, there are three words which are very important to us; one, you abstain, support or disagree or do not support, and then you proceed. Hon. (Ms.) Mbeyu: I support with the following recommendations. I think it is high time the mover of the motion finds out the distance between two bumps. Am seeing the distance here is not less than 100 metres; look at the bump between Kwa Chokwe and Kituoni. It is a distance which is less than 100 metres and you are putting a bump. Some of us are new drivers on the roads; we are buying new cars, we think we are going to break our cars and secondly; these bumps are too many on the roads such that we are inviting car-jackers because as you move one bump after the other, somebody will time you. So I think it is high time the mover or the committee involved finds out the distance between one bump and the other. Thank you. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Mupe. Hon. Mupe: Asante Sana Mheshimiwa Spika. Nimesimama kuunga hoja hii na kusema kwamba kwa hakika barabara zetu za kaunti zinataka haya matuta. Sababu mheshimiwa Spika ni kwamba tumeweza kugundua kwamba kuna ajali nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika na tumeweza kupoteza wananchi wetu. Mheshimiwa Spika ningeomba bunge liweze kuruhusu kamati ya Barabara, Usafiri na Ujenzi kuzuru kila wodi kuangalia ni njia gani ambazo zingeweza kuwekwa bumps na kutengenezwa ili maisha ya mwananchi wa Kilifi yaweze kupewa kipao mbele. Mheshimiwa Spika, nataka kusema nikiwa mwenyekiti wa kamati ya Barabara, Usafiri na Ujenzi. Katika bajeti ya mwaka huu, hatukuwa na pesa Bw. Spika; pesa zote ziliweza kuchukuliwa na KeRRA ( Rural Roads Authority) na KURA (Kenya Urban Roads Authority) na ndio maana unaona kwamba katika utendajikazi wetu ndani ya mwaka huu wa serikali, barabara zetu hazikuweza kuangaziwa vilivyo. Bwana Spika ningeomba kwa heshima na taadhima kwamba bunge hili liweze kupitisha bajeti ya kusimamia barabara. Sisi kama kamati ya barabara, Mheshimiwa Spika, tumeweka mikakati ya kwamba mwaka wa serikali katika bajeti tunataka kila eneo na wodi kuwe na milioni 10 hususan kusimamia barabara. Kwa hivyo waheshimiwa wajumbe wenzangu ninaomba wakati

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6 ule kamati ile ya barabara itakapokuwa imewasilisha bajeti ya mambo ya barabara tuweze kuipatia kipao mbele ili tuhakikishe katika kila barabara ambayo iko hapa ndani ya Kilifi hususan katika kila wodi imeshughulikiwa. Barabara zile tuweze kuzirekebisha na maswala ya bumps tuweze kuyaweka. Kwa hivyo Mheshimiwa Spika ningeomba kwa heshima na taadhima bunge hili liwezeshe kamati ya barabara kuenda mashinani na kuangalia ni barabara zipi ambazo zina shida kama hiyo ama ni sehemu gani ambazo Mheshimiwa Mlanda aliyeleta hoja hii ameweza kuziacha na sehemu zile zina ajali mara kwa mara. Kwa hivyo, nimesimama kuunga mkono. Asante Bwana Spika.

(Applause)

The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Thank you very much Hon. Mupe. Hon. Kiraga. Hon. Kiraga: Thank you Mr. Speaker. Probably before I continue Mr. Speaker I think we should get the right word for bump in Kiswahili because we are getting various interpretations. Mr. Speaker, I rise to support this Motion. It will be very prudent for the committee on Roads and Transport to go outside as the chairman has put it to verify which sections of our roads need bumps. If we come here and still pin point the different areas, then I believe everybody is going to do that for the road leading to his area of representation. Ii is better for the committee to verify because there are also laws and regulations guiding the placement of bumps. So it is only the committee with the relevant authorities or relevant government bodies who can direct us which areas need bumps. For sure, you cannot have a bump in less than 100 meters, that means if we are going to have such cases then driving vehicles will be very impossible on our roads. Otherwise, I highly support this Motion. Thank you very much. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Members before I give a chance to other members, allow me to give guidance in your contributions. Going by the motion, I think the Motion calls for the County Executive member in charge of Roads Transport and Public Works to implement what this Motion has indicated. We want to put bumps and erected sign boards and colour them appropriately at the said areas. If you go to Standing Order number 46, it gives us an eye opener that if somebody has something that needs to be added to this Motion after it has been passed or not passed, it should be after six months. Again the committee on Transport, Roads and Public Works can still continue benchmarking the roads within the county, not by passage of this Motion because they have a mandate to sit as a committee and to come up with a work plan on what they want to do. So after going round they will come up with a report which will justify that there are other bumps which are important. Some might not be important. So let the committee not be worried about moving around. Let us contribute based on what this Motion is about and the rest can be handled at the committee stage. I think everything is well articulated in the Standing Orders and so you need not to worry. Hon. (Ms.) Chiku, you can now make your contributions. Hon. (Ms.) Chiku: Thank you, Mr. Speaker Sir. I just wanted to give a comment about Kilifi-Malindi road in relation to Kwa Chokwe and Kituoni. As it has been said by the previous member, this stage Kituoni and Kwa Chokwe are at a distance of about 100 meters. I would also like to point out that in Kituoni there is a very sharp bend and it will be disastrous, Mr. Speaker Sir, to put a bump there. Instead of making the road safe now it is going to be a very dangerous

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 7 road where you have to negotiate a corner and then end up with a bump. Those are my observations Mr. Speaker. Thank you very much, Sir. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): We need to be guided; there are some words I want to hear from you as to whether you support, you don’t support or you abstain. Hon. (Ms.) Chiku: I do support the idea of keeping bumps on the Highway but the distance between Kituoni and Kwa chokwe is very short and since Kituoni has a very sharp bend then it is dangerous to negotiate a bend and then suddenly come to a bump, whereas we don’t have any bumps between Roka and Matsangoni. Those are my observations Sir. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. (Ms.) Elina. Hon. (Ms.) Elina: Asante Bw. Spika. Nataka kwanza kumuunga mkono Mheshimiwa aliyeleta hoja hii hapa bungeni. Hii ni kwa sababu hoja ni ya muhimu ndio unaona imejitokeza kila mtu anazungumzia. Mimi nitamuunga mkono yule Mheshimiwa aliyesema palipo na kilomita mia moja kuwekwe nundu kwa sababu ya zile hatari zilizoko. Kila mtu anajua pale Mida kumewekwa nundu mbili kwani nimetoka Kilifi na nimezipita hizo nundu. Nilipokuwa nimetoka Kilifi nimekuja nikakutana na kitu kama hicho pale kwa hivyo mimi ninaomba kabisa kamati inayohusika kwa kumuunga mkono yule aliyeleta hii hoja hapa ni yale machungu yanayoendelea; kupoteza watu katika Kilifi County. Sasa tuwapatie majukumu kupitia bunge hili kwa sababu vijiji vingi vimejengwa karibu na barabara. Utaona barabara iko katikati upande huu kuna nyumba na upande huu kuna nyumba; tunapoteza watu wengi sana kwa sababu hatukuwa na watu wa kuangalia mambo ya kesho. Walikuwa ni watu wa kurarua barabara mahali popote bila kuwa na mipangilio. Wakati huu, tunataka tuiweke Kilifi Kaunti kwa mipangilio. Kwa hiyo ni lazima kamati tuipatie majukumu ifanye ili hata wakati mwengine tutaambiwa tumesimamia hii Kilifi Kaunti tukijua tunaelekea ile mielekeo yake. Hili jambo tutalipoteza na ni jambo la maana sana; hivi ninavyokwambia hiyo gari imeanguka hapo ni ya madawa na kwa sababu ilikuwa ni ya madawa kumejaa askari wengi mpaka sote tukaanza kusimamishwa ili tusipite pale barabarani. Nataka nikwambie kwamba hali hii ya kupoteza watu iko kila mahali na tusipochunga hizi barabara zetu tutaendelea kupoteza watu wetu kwa sababu waliopewa kazi ya kukarabati barabara zetu ni wazembe kabisa. Barabara zetu ni mpya lakini ukiziangalia ni kama zina miaka zaidi ya karne moja. Ukishika hii njia ya Gongoni ambako mheshimiwa Kiraga anatoka unaweza kusikitika kabisa na ni mamilioni ya pesa yaliyojenga ile barabara. Kwa hiyo, kama sisi hatutaingilia kati tukatafuta mbinu za kuweka vizuizi vya magari ili yasiweze kuumiza watu wetu basi tutakuwa hatujawajibika kikazi kisawasawa. Mimi namuunga mkono aliyeleta hoja hii. Pia tuipatie jukumu ile kamati inayostahili iende kuzunguka kwa kaunti nzima kujua na kunakili ni mahali gani kwenye shule au kwenye hospitali ama barabara ambayo imekata familia na kuna trading centre. Tuwekewe hivi vizuizi vya magari kwa sababu bila hivyo tutapoteza vijana wengi barabarani na tutaendelea kumaliza watu wetu barabara. Mimi ningeomba bunge hili kama tutaweza kubaliana ni kwamba kamati husika izunguke iangalie barabara zilivyo na hizo trading centers zilivyo kama ni kitu gani tunaweza kuweka pale tusaidie watu wetu. Ni hayo Bw. Spika na nasema asante. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Mwayaa. Hon. Mwayaa: Asante sana Bw. Spika. Mimi kama mjumbe wa Kayafungo ninaunga mkono moja kwa moja uwekaji wa matuta katika barabara zetu za Kilifi Kaunti. Nasema hivyo kwa sababu kuna barabara moja ambayo ilinigusa sana nilipopitia katika wodi yangu; na hiyo ni Mariakani-Kaloleni hadi Mavueni. Katika barabara hii sijui kama wahandisi ambao walijenga walitumia uhandisi gani kwa sababu ukiangalia kutoka Mariakani ambapo walianza uhandisi

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 8 wao hakuna hata tuta moja ambalo limewekwa kufikia saa hii na barabara imekamilika kutoka Mariakani mpaka Kaloleni. Tena inaanza tena kutoka Kaloleni kuja Mavueni ambako pia hakuna hata tuta moja. Kuna sehemu ambazo ni lazima ziwe zitaangaliwa ili kwamba ziweze kuwekwa hayo matuta kwani nikiangalia katika mswada huu mwisho pale imeandikwa Kavinautu stage ambako bado ni Mariakani. Ningeonelea iwekwe Kibao Kiche ambako kuna shule ya msingi na shule ya upili; pia kwa Makemba ambako ni karibu na Kaloleni. Hao wahandisi ambao wataendelea kutoka Kaloleni na kuenda mbele wawe wataangazia sehemu nyingine kama vile Chanagande na kuendelea. Asante Bw. Spika. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Kombo. Hon. Kombo: Asante Bw. Spika. Mimi naunga mkono mswada huu ambao umeletwa na ndugu yangu mheshimiwa Mlanda. Nikiwa nimekaa barabarani kwa miaka 25 kufikia leo nafikiri nimekuwa mjuzi barabara ingawa kwa mda huu wote nimeenda kwa neema ya mwenyezi Mungu bila ajali. Hata hivyo, naona mswada huu umekuja lakini unachangia padogo katika maswala ya usalama barabarani. Tukiangalia ‘bumps’ ambazo zimewekwa nyingi hazina rangi na hii imehatarisha maisha ya watumiaji wengi wa barabara kwani wengi kuenda na kupiga zile ‘bumps’ wakiwa wako kasi ya juu sana na kwa sababu hakuna ilani nyuma basi hupoteza mwelekeo na kufanya ajali hapo hapo. Kwa hivyo mimi ninasema ya kwamba mswada uko sawa lakini baada ya kuupitisha kamati ambayo inahusika iendelee kuangalia mambo mengine hasa kuhusu watumiaji wa barabara. Tunakuta ya kwamba watumiaji wa barabara wengi kwa wakati huu hawana vibali na hawajapitia shule kwa hivyo sheria nyingi za barabara hawazielewi. Kwa hivyo hiyo inakuwa changamoto kwa watumiaji wa barabara wengine ambapo utakuta vijana wetu wa boda boda na wa ‘tuk tuk’ anaku-overtake mahali ambapo hapaswi ku-overtake. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Kombo would you mind sticking to one language please so that we can understand you better; otherwise you will be out of order. Hon. Kombo: Samahani. Kwa hivyo tunakuta ya kwamba vijana wengi wanafanya makosa ambayo ni hatari kwao na hatari pia kwa watumiaji wengine wa barabara. Hii ni changamoto pia kwa waheshimiwa wote katika bunge hili kuwa turudipo majumbani tuangalie kuwa vijana hawa wa bodaboda na ‘tuk tuk’ tumeweza kutumia pesa ambazo tuko nazo tuweze kuwaingiza shule na kuwasaidia ili barabara zetu ziwe zitakuwa salama zaidi ya vile zilivyo. Vile vile tukiangalia watumiaji wa barabara wengine kama madereva wa malori tunakuta wao wanaendesha bila kujali wenye magari madogo ama hata wenye pikipiki. Kwa hivyo tunaomba serikali yetu ya Kaunti iweze kusukuma pia idara zile ambazo zinahusika na usalama wa barabara ili ziweze kutia ufunguo na kuhimiza usalama ili swala la usalama barabarani liwe litakuwa linatatuliwa. Kwa hayo nasema asante. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Nzaro. Hon. Nzaro: Thank you Mr. Speaker Sir. I rise to support the Motion with the following remarks. Mr. Speaker we have lost many lives on our roads simply because of over speeding. Since we want to reduce deaths on our roads then if we erect these bumps, in a way we would be helping our drivers to reduce their speed Mr. Speaker. Mr. Speaker I just want to say that I am not a road engineer but I think there are a lot of things happening on our roads which have to be addressed. Mr. Speaker I would also wish to indulge with the people concerned in making our roads so that the road engineers who we have in this County and the works officers who are building these roads be advised to give us the correct information on who is supposed to erect these bumps. Mr. Speaker with those few remarks, I beg to support.

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 9

The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Chitibwi. Hon. (Dr.) Chitibwi: Thank you Mr. Speaker Sir. I rise to support the Motion with some few remarks to make. I think we have got a lot of road bumps but the unfortunate thing is that we only had paint without very nice reflecrors on these roads; after some time the paint faded away and in the end, as one of Hon. member who was on the floor was speaking about, instead of stopping the accidents it will be increasing the accidents. Some time back when I was driving along this road I drove on a bump in the night and there were no reflectors. The bump had been painted but after some time I think the paint faded away. So I think it will be best for the roads Executive members to find well designed areas and a way of putting the reflectors so that in the night drivers can be safe on the roads instead of only keeping the pedestrians safe and abandoning the drivers. So for these few remarks and to add on this issue of reflectors, I support the Motion. Thank you. The Deputy Speaker (Hon.Mwambire): Hon.Mwingo. Hon.Mwingo:Asante sana Bw. Spika. Mimi vile vile nasimama kuunga mkono hoja hii kwa sababu maisha ya watu wetu yamepotea na sababu hasa ni kukosa haya matuta. Tumepoteza sana watu wengi tukiangazia pia vile vile eneo la Mtepeni hasa mahali kama Mtwapa. Kama tunavyojua ni kwamba kampuni nyingi ziko kule; kuna kampuni ile ya EPZ ambayo sote tunaijua. Pia kuna mahali kama pale kanisani Bamba na vilevile kuna Kikambala Trading centre na kuna Msumarini na pia kuna Vipingo. Hizo ni sehemu ambazo zimepoteza watu wengi sana. Kwa hivyo mimi naunga mkono mswada huu na ni matumaini yangu kwamba katika sehemu zote ambazo zimetajwa hapa, na hata zile zingine ambazo waheshimiwa mmezitaja kamati husika itanakili na mzitie maanani ili wakati wa kutengeneza ziwe nazo pia zitaangaliwa. Naunga mkono maradufu hoja hii. Asante Bw. Spika. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Matsaki. Hon Matsaki: Asante sana Bw. Spika. Mimi nataka tu nizungumze kwa uchache. Kwanza naunga mkono hoja hii na sababu ambazo nataka nizungumzie. Mimi nimeona barabara ambazo zimetajwa haswa kutoka kwa wadi yangu. Sisi sote tunajuwa tuko na mtambo pale na malori makubwa mengi wakati wakibeba yale makaa yao huwa wako kasi sana. Kwa hivyo basi yale matuta pale Makini na Bondora ni sawa kabisa kwa sababu kuna visa vingi hutokea pale; mara nyingine hata yale magari hukosea njia kwa sababu ya kasi zao na kujaribu kuingia upande wa mabanda ya biashara. Kwa hivyo mimi nimesimama kuunga hoja hii kwa dhati zaidi. Asanteni. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Pascal. Hon. Pascal: Asante sana mheshimiwa Spika. Mimi vile vile nasimama kuunga mkono hoja hii kwa sababu kama tunavyojua nchini Kenya tuko na tabia ya kutofuata sheria; madereva wengi wamekuwa wakiendesha magari yao kwa kasi na kutofuata sheria na wamekuwa wakisababisha ajali sana. Kwa hivyo ninasimama kuunga mkono hoja hii isipokuwa tunaona ya kwamba katika hoja hii zile sehemu ambazo zimeangaziwa ni zile za barabara kuu lakini tunazo barabara ambazo zinafanyiwa kazi sana na watu wengi pia wanapoteza maisha. Kwa hivyo tujaribu kuangalia hata zile barabara ambazo sio za lami tuzihakikishie kwamba tunaziwekea haya matuta kama wenzangu walivyosema. Jambo muhimu ambalo ningesisitizia ni kwamba haya matuta tukiyaweka inatakikana tuweke zile alama ambazo zinatuonyesha ya kwamba labda mahali fulani na baada ya kilomita fulani kuna tuta. Hii ni kwa sababu tunaweka hayo matuta lakini ni kama tunazidisha ajali kwa sababu mtu ataenda mbio na akifika pale kwa vile hakuna ishara anaenda kugonga yale matuta na kusababisha ajali nyingine. Kwa hivyo ninaunga mkono ili tuweze kuona tunatafuta zile

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. February 18, 2014 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 10 sehemu za mashule na makanisa ambazo mara nyingi zinatumiwa na wananchi ili tuziweke hayo matuta ndipo tupunguze hizi ajali. Asante sana mheshimiwa Spika. The Deputy Speaker (Hon. Mwambire): Hon. Members if you allow me I will give a chance to the mover of the Motion to respond to the member’s contribution. Okay, Hon. Chokwe Kaunda then to the mover of the Motion to respond. Hon. Kaunda: Asante sana mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi. Nasimama kuunga mkono hoja hii. Pongezi sana kwa mheshimiwa Mlanda kwa kuleta hoja hii katika bunge. Sitaki niongee sana isipokuwa mheshimiwa Spika ningeomba kwamba kamati inayohusika na Barabara, Usafiri na Ujenzi izingatie mambo muhimu kwani naamini kuwa sio kasi tu barabarani ama ukosefu wa matuta unaoleta ajali katika barabara zetu. Naamini kuwa kuna mambo mengi yanavyoendelea. Kwa mfano, kitaifa tunaona kwamba kuna kile kidumbwasha cha kuweza kupuliza ili ujue kama umelewa ama hujalewa. Nafikiri vitu kama vile vingeweza kusisitizwa sana mahali hapa ili kuweza kukabili hii hali ya ajali nyingi katika barabara. Kuna mambo kama hayo ya vile ving’arisho barabarani na mambo mengi yanayohusika. Kwa hivyo naomba kwamba kamati inapoenda kukaa iyazingatie mambo haya yote. Vile vile kuna mambo ya mikanda ndani ya gari. Yale pia ni mambo muhimu sana. Sina zaidi isipokuwa ninasimama kuunga mkono. Asante kwa nafasi hii mheshimiwa Spika. The Deputy speaker (Hon. Mwambire): Hon. Steven Bahati Mlanda. Hon. Mlanda: Mr. Speaker Sir, I stand to sincerely thank all members of this Assembly who have contributed a lot and also not forgetting my chairman for Transport and Roads who have decided that the committee goes round Kilifi County to see those areas that need these bumps, sign posts and also zebra crossing. Mr. Chairman I will make sure that it will be done according to our contributions. I thank you Mr. Speaker. The Deputy speaker (Hon. Mwambire): Hon. Members allow me now to put the question that this County Assembly adopts the Motion as tabled and amended by Hon. Steven Mlanda and amended by Hon. Hamza. (Question that the amendment be made put and agreed to)

ADJOURNMENT

The Deputy speaker (Hon. Mwambire): There being no bills to be transacted in this house I now call this house to adjourn until tomorrow at 9.30 a.m. for the morning sitting. Thank you. The house rose at 3:30 p.m

Disclaimer: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.