IMAM MAHDI (A.S.) IMAM WA ZAMA HIZI NA KIONGOZI WA DUNIA Kimeandikwa na: Mulabbah Saleh Lulat ©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 – 9987 – 17 – 089 – 0 Kimeandikwa na: Mulabbah Saleh Lulat Kimehaririwa na: Alhaji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Mbaraka A. Tila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Decemba, 2014 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe:
[email protected] Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info “Yeyote anayekufa bila ya kumjua Imam wa zama zake basi amekufa kifo cha kijahiliyyah (zama za kijahiliyyah: zama kabla ya Uislamu).” Mtukufu Mtume (saww) Kwa jina Lako tukufu Kimeanza kila kitu Peke Yako twakusifu Wote watu Mola Wetu Uwezo na utukufu Ni Wako Mola wa watu Ewe Rasuli, Mkweli na Mwaminifu, Rehema kwa wote alamina, Rehema na amani za Mola zipo daima juu yako toka alipoumba nuru yako, Malaika wote wanakutakia rehema na amani, Na wote kaumu ni wajibu kukusalia, Nani kama wewe ewe mbora wa viumbe wa Mola? Huyu ni Al Mahdi nuru na fakhari ya kizazi chako, Kwa upanga wako, joho lako na kilemba chako atatokomeza wote ukafiri, Kila aina ya ukoma na udajali: ufalme, demokrasia, ukomunisti, ubepari, ulahidi, ushirikina, utaghuti, dini mseto,… vyote vitatoweka na kubaki Nuru ya Mwenyezi Mungu. Wanaokukejeli Abtaru1 na wakapambana na wewe, wote hawa batili wa- metoweka zahakani2 kama povu la baharini, Mola alikupa Kauthari, Aali Muhammadi, kizazi kilicho bora minal Awwa- lina wal Akhirina, Yawatosha utukufu kwamba asiyewasalia, yake sala ni batili, Sana umemtaja na kumbashiri huyu mtukufu wa kizazi chako, Katika kitabu hiki nimeyakusanya ya hamu ili Waislamu wayafahamu, Na pia wote kaumu, wenye akili huru na nyoyo zenye harara, Nataraji wako uombezi na radhi zako.