Tarehe 28 Mei, 2016

Tarehe 28 Mei, 2016

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini na Moja – Tarehe 28 Mei, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA - KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha Mezani. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MHE. PETER A. P. LIJUAKALI - NAIBU MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: Hoja za Serikali, kwamba Bunge sasa likubali kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ..... WABUNGE FULANI: Kamati, Kamati, Kamati. 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, mtuwie radhi, sasa nimuite Mwenyekiti au mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo. Ni mimi kweli, Order Paper iko sahihi, namuita Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo, Maji na Uvuvi. Karibu Mheshimiwa Sanga. MHE. DEO K. SANGA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO, MAJI NA UVUVI): Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo, Maji na Uvuvi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka wa fedha 2015/2016 pamoja na Maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 MWENYEKITI: Mtoa hoja, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mheshimiwa Injinia Lwenge. (Makofi) WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mheshimiwa Dkt. Mary Michael Nagu, Mbunge wa Hanang, ambayo ilichambua Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, naomba sasa Bunge lako likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka 2016/2017. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa muda niliopewa ni mdogo na taarifa yangu ni ndefu, naomba kurasa zote 187 za hotuba yangu zinukuliwe kwenye Hansard. Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutumia fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliyofanyika mwezi Oktoba, 2015. Ushindi huo ni ishara na imani kubwa ya wananchi waliyonayo kwa Rais, Makamu wa Rais na Chama cha 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mapinduzi. Vilevile nakipongeza Chama cha Mapinduzi kwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kutumia fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kwa kuteuliwa kwake na Mheshimiwa Rais na baadaye kuthibitishwa na Bunge lako Tukufu kuwa Waziri Mkuu. Kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ishara tosha ya imani aliyonayo Mheshimiwa Rais, Waheshimiwa Wabunge na wananchi wa Tanzania kwa utumishi wake uliotukuka. Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi pamoja na viongozi wengine kwa ushindi walioupata katika uchaguzi uliyofanyika mwezi Machi, 2016. Ushindi huo ni ishara ya imani kubwa ya wananchi wa Zanzibar waliyonayo kwa Rais na Chama cha Mapinduzi. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile natoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Wizara inayomgusa kila mwananchi. Hakuna njia ya kurudisha imani hiyo kubwa isipokuwa kuahidi kuwatumikia wananchi wa Tanzania kwa uadilifu, haki na bila upendeleo wowote. Naahidi kufanya hivyo kwa kadri Mwenyenzi Mungu atakavyonijalia. Kwa ufupi nasema hapa kazi tu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe shukrani kwa wananchi wa Jimbo la Wanging‟ombe kwa imani yao walionipa kwa kunichagua kuwa Mbunge wao kwa kura nyingi za kishindo. Nawaahidi nitawatumikia wote kwa uaminifu, bidii na upendo. Naomba niwapongeze Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuwa wawakilishi wa wananchi kwenye Majimbo yao. Nakupongeza sana wewe binafsi Mheshimiwa Mwenyekiti, Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge. Mheshimwa Mwenyekiti, napenda kwa dhati kabisa kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa kwa Wizara yangu. Naishukuru Kamati hiyo pia kwa ushauri, maoni na maelekezo iliiyoyatoa wakati nilipowasilisha taarifa ya kazi zilizotekelezwa mwaka 2015/2016 na Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Wizara yangu kwa mwaka 2016/2017. Ushauri na maoni na mapendekezo ya Kamati yamezingatiwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu kwa hotuba yake aliyowasilisha hapa Bungeni ambayo inatoa dira ya utekelezaji wa kazi za 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Serikali. Hotuba hiyo imeonesha mwelekeo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kipindi cha mwaka 2016/2017. Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo, naomba nitoe pole kwa wananchi waliopoteza ndugu, marafiki na mali zao kutoka na matukio ya ajali na maafa mbalimbali yakiwepo mafuriko katika baadhi ya maeneo nchini. Namuomba Mwenyenzi Mungu awape nguvu na moyo wa uvumilivu waathirika wote na roho za marehemu wote zilazwe mahali pema peponi amina. Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sasa kuchukuka fursa hii kuwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yangu ambayo inatoa taarifa ya hali ya sekta ya maji na umwagiliaji nchini, utekelezaji wa bajeti hii ya mwaka wa fedha 2015/2016 na malengo ya sekta kwa mwaka 2016/2017. Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba yangu imezingatia sera na mikakati ya maendeleo ya Kitaifa na Kimataifa, Ilani ya Chama cha Mapinduzi, sheria na miongozo inayohusiana na sekta ya maji na umwagiliaji pamoja na mgawanyo wa kazi za kisekta. Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya sekta za maji na umwagiliaji nchini; Wizara inaendelea kutekeleza mpango na mikakati mbalimbali ya Serikali kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mujibu wa Sera ya Maji ya mwaka 2002 pamoja na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo kwa upande wa umwagiliaji kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Umwagiliaji ya mwaka 2010. Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji inahusisha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji, huduma na usambazaji wa maji vijijini na mijini na kuijengea uwezo sekta ya maji. Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo inahusisha uendelezaji wa miundombinu ya umwagiliaji. Hali halisi ya utekelezaji wa progamu hizo imefikia hatua mbalimbali kama ifuatavyo:- Mheshimwia Mwenyekiti, rasilimali za maji; nchi yetu ina kiwango kikubwa cha rasilimali za maji zilizopo juu na chini ya ardhi ambapo upatikanaji wake hutegemea mvua na aina ya miamba iliyopo. Hata hivyo, mtawanyiko wa rasilimali za maji hauko sawa katika maeneo yote ya nchi kutokana na hali ya kijiografia, kijiolojia na hali ya mabadiliko ya tabia nchi. Usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nchini unatekelezwa na Bodi za Maji za Mabonde. Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu za kitaifa za rasilimali za maji zilizopo zinaonesha kuwa kila mwananchi ana uwezo wa kupata mita za ujazo 1,952 kwa mwaka na ikilinganishwa na kiwango kinachokubalika cha kimataifa cha mita za ujazo1,700. Hata hivyo, inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2035 kiwango hicho kinaweza kupungua hadi mita za ujazo 883 kwa kila mwananchi endapo hatua madhubuti za utunzaji wa vyanzo vya maji hazitachukuliwa. Wizara kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo imechukua 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) hatua za kukabiliana na hali hiyo kwa kuhamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na uvunaji wa maji ya mvua ili nchi yetu isifikie kiwango hicho cha uhaba wa maji na kusababisha athari kubwa kwenye maendeleo ya nchi. Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ya maji vijijini; miradi ya maji vijijini inatekelezwa chini ya Programu Ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini. Idadi ya watu wanaopata huduma ya maji vijijini imeongezeka kutoka milioni 15.2 sawa na asilimia 40 ya wananchi waishio vijijini mwezi Julai, 2013 na kufikia watu milioni 21.9 sawa na asilimia 72 mwezi Machi, 2016. Hayo ni mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji vijijini. Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio hayo yamepatikana kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo, Serikali za Mitaa, wananchi, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa sekta ya maji. Lengo ni kufikia asilimia 85 ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wote waishio vijijini ifikapo mwaka 2020 kwa kuzingatia Sera ya Maji ya mwaka 2002 inayosisitiza kuwapatia wananchi hao maji safi na salama kwa umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao. Mheshimwa Mwenyekiti, huduma ya maji mijini hutolewa kupitia Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwenye Miji Mikuu ya Mikoa pamoja na Dar es Salaam, Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Maji ya Kitaifa. Uzalishaji wa maji kwa siku katika Miji Mikuu ya Mikoa umeongezeka kutoka lita milioni 385 mwezi Aprili, 2015 hadi lita milioni 470 mwezi Machi, 2016. Lengo la Serikali ni kuwapatia maji wananchi wote wanaoishi mijini na ikifika mwaka 2020 ifikie asilimia 95. Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya sekta ya umwagiliaji nchini; nchi yetu ina jumla ya hekta milioni 29 zinazofaa kwa umwagiliaji. Kati ya hizo, hekta milioni 2.3 zina uwezekano mkubwa wa kumwagiliwa, hekta milioni 4.8 zina uwezekano wa kati na hekta milioni 22.3 zina uwezekano mdogo. Hadi sasa eneo linalomwagiliwa ni hekta 461,326 sawa na asilimia 1.6 ya eneo lote linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na linachangia asilimia 24 ya mahitaji yote ya chakula nchini.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    214 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us