Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Nane – Tarehe 5 Septemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Hiki ni Kikao cha nane cha Mkutano wetu wa kumi na mbili. Nawakaribisheni nyote, Katibu. MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nina orodha ya Wabunge 15 kama ambavyo nimekuwa nikisisitiza ni vizuri yeyote atakayepata nafasi kuuliza swali aulize kwa kifupi iwezekanavyo, kama kuna la nyongeza vile vile kwa kifupi iwezekanavyo ili kuwapa nafasi Wabunge wengine wenye nia ya kuuliza maswali. Kama ilivyo ada tunaanza na Mheshimiwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni endapo ana swali. 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru kunipa nafasi ya kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali. Mheshimiwa Waziri Mkuu nchi yetu sasa iko katika kipindi kigumu ambapo Taifa linashiriki mchakato wa kuipata Katiba mpya ya Taifa letu. Ni dhahiri kwamba mchakato wa kuipata Katiba mpya unahitaji ustahimilivu, ushirikiano, uwazi, ukweli, dhamira njema na kipekee sisi ambao ni Wabunge ndani ya Bunge hili tunatambua na tunastahili kutambua kwamba wako wadau wengi sana nje ya Bunge hili ambao nao ni wadau kama sisi katika mustakabali mzima wa Katiba. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa matukio ambayo yalitokea juana ndani ya Bunge lako, panaonekana kuwepo ufa mkubwa ambao unaweza ukafanya dhamira njema ya kuiandika upya Katiba ya Taifa letu ikapata ufa mkubwa katika hatua hii ya kutunga na kurekebisha Sheria hii. Mheshimiwa Waziri Mkuu Mkuu, wewe kama kiongozi wa Serikali Bungeni, ambayo Serikali yako ndiyo imeleta Muswada ulioleta sintomfahamu iliyotokea jana. Unatoa kauli gani kwa Watanzania kuhusiana na sintomfahamu hii? (Makofi) NAIBU SPIKA: Naomba utulivu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge hili ndiyo limepewa mamlaka ya kutunga Sheria. Serikali 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) inacholeta ni mapendekezo. Yanaweza kuwa ni mapendekezo yanayohusu Sheria, yanaweza kuwa ni mapendekezo yanayohusu Marekebisho ya Sheria. Mapendekezo hayo ndiyo maana yanapita kwenye hatua mbalimbali. Kuna hatua ya ushirikishwaji wa wananchi kwa kupitia Public Hearing lakini kubwa tunapokuja hapa matarajio ya wananchi ni kwamba Wabunge tuliyomo humo ndani tutaujadili Muswada huo kikamilifu na maeneo yote ambayo yanadhaniwa yanaweza yasiwe na tija au neema kwa nchi yetu ni jukumu letu sisi Wabunge kujadili kwa uwazi, kwa uaminifu, kiukweli na kazi kubwa ya Serikali katika mjadala ule ni kuona mahali gani inawezekana kweli tulipitiwa. Hili tunalikubali, sehemu gani tunadhani Waheshimiwa Wabunge hapa tunadhani bado msimamo wa Serikali ni sahihi. Lakini hatimaye tunafikia maamuzi ya pamoja yanayoonyesha nini hasa kinatakiwa kuwemo katika Sheria hiyo. (Makofi) Niseme tu Mheshimiwa Mbowe, kilichotokea jana mimi nasema it is very unfortunate situation, very unfortunate. Nimejiuliza sana kumetokea nini hasa. Mambo gani ambayo yasingeweza kujadiliwa ndani ya Bunge hili na tukafikia muafaka. Suluhu ikaonekana badala ya Wabunge kutoka nje. Mimi nimepata taabu nalo sana. Sasa kama kwa kufanya hivyo ndiyo kuwakilisha watu kikamilifu mimi nafikiri hapana. (Makofi) Kwa hiyo, niombe sana tutumie fursa hii ya kuwa Wabunge ndani ya Bunge kikamilifu. Hakuna Sheria 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) hapa itakayotungwa ambayo haitakuwa imejadiliwa kwa kiasi cha kuweza kuridhiana. Mara ngapi tumekubali baadhi ya mawazo kutoka kwa Wabunge, mara nyingi tu. Kwa hiyo mimi sikuona kwamba ilikuwa kuna jambo kubwa sana pale la kutufanya mpaka Wabunge wote mtoke. Kwa hiyo, mimi ushauri wangu kwa kweli tujaribu kuzingatia taratibu za Bunge na kwa kweli tujadili kikamilifu kwa maslahi ya Watanzania. (Makofi) NAIBU SPIKA: Swali fupi la nyongeza Mheshimiwa Kiongozi wa Upinzani. MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili jambo la Katiba, naomba niweke wazi siyo jepesi kama Waheshimiwa Wabunge wenzangu wanaopiga makofi wanavyotaka kuliona. Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni kweli kwamba yako matukio ya kibabe, ya kejeli, ya matusi, ya dharau, ambayo yana-delay process nzima ya kutafuta muafaka katika jambo hili. (Makofi) Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na rai uliyotoa, sisi tunaamini kwamba yako maeneo mengi yasiyo na tija ambayo yanafanya msingi wa Sheria au wa Muswada wa marekebisho ulioletwa jana uwe kwamba hauna tija kwa mchakato huu hauna tija kwa Taifa na sisi tunaamini kwamba kwa sababu kuna lengo jema na kwa sababu unasema kuna dhamira njema upande wa Serikali ni muafaka kwako na Serikali 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) yako kuuondoa Muswada huu mkaurejesha katika maeneo yanayohusika. (Makofi) NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tumsikilize Mheshimiwa anapouliza swali ili tuwe na ufuatiliaji wa pamoja. Huyu ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni mpeni heshima yake asikike anauliza swali gani kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Kiongozi wa Upinzani endelea. MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Waziri Mkuu narudia, maadamu umedai kwamba kuna dhamira njema kutoka upande wa Serikali na Chama kinachoongoza nchi. Ni ushauri rasmi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwamba Muswada huu kama ulivyoletwa jana una maeneo makubwa ambayo utaweka ufa mkubwa kwenye Taifa hili kuliko mnavyofikiria. Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunakushauri Mheshimiwa Waziri Mkuu, tumia Mamlaka yako ondoeni Muswada huu ukafanyiwe kazi za msingi mapema kabla, kafanyeni Political Management kwenye process hii kisha muulete Muswada ambao una muafaka wa pande mbili za Muungano kisha tutakwenda pamoja. Unatoa kauli gani kuhusu kuondoa Muswada huu? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu majibu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mbowe anasema Muswada una mambo mengi ambayo anafikiri si kwa maslahi ya nchi. Hivi kweli Mheshimiwa Mbowe 5 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) unangoja mpaka kweli Muswada unafika ndani ya Bunge ndipo unakuja na hoja ya namna hiyo wakati tulikuwa na fursa kubwa kwenye Kamati ndiyo, ndiyo utaratibu ndiyo. (Makofi) Tulikuwa na fursa kwenye Public Hearing, kwenye Kamati yenyewe ya Bunge ndiyo, ni utaratibu tu. Ni utaratibu. Lakini mimi nasema katika mambo ambayo nimeelezwa jana kwamba ndiyo yaliyojiri na kusababisha mkatoka nje, hakuna mtu ambaye ataona umuhimu wa kuondoa Muswada huu hata kidogo. Kwa sababu ni vitu ambavyo ndani ya Bunge hili hili vinazungumzika na vinaweza kubadilishwa kulingana na mamlaka mliyopewa. (Makofi) MHE. JAMES F. MBATIA: Nashukuru sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kutokana na Montevideo Convention ya tarehe 26 Desemba, 1933 imeleza tabia kuu nne za dola ikiwekwa upande wa ardhi, watu, utawala pamoja na ushirikiano wa mambo ya nje. Mfumo wetu wa kiutawala au wa dola ni mgumu is a complex state uki-compare na wenzetu ambao wana simple state. Tendo la kuunda dola ni tendo la kisiasa ambapo mfano Mwalimu Nyerere na Karume mwaka 1964 tarehe 22 Aprili, 1964 walisaini Mkataba wa Muungano. Mfano mwingine Mwaka 2009 Maalimu Seif na Rais wa Zanzibar wakati huo Mheshimiwa Amani Karume walizungumza kisiasa kwanza, tendo la kisiasa, Sheria ikafuata baadaye. 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Waziri Mkuu swali. Hatuoni kwamba ni busara majadiliano ya kisiasa yakafanyika kwanza na kwa uwazi kwa kushirikiana zaidi badala ya kuanza kwa Sheria zaidi tukaji-engage zaidi kwenye masuala ya kisiasa ya mazungumzo ambapo yatatusaidia, dhana halisi ya kuunda dola, dhana halisi ya kuunda Katiba ambayo ni tendo la kisiasa na Sheria inafuata baadaye? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu majibu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, sina tatizo na ushauri wa Mheshimiwa James Mbatia, hata kidogo. Ni jema tu, tatizo tu ni kwamba kwa sababu nimeshindwa kuelewa ushauri huu unaunganishwa na nini hasa. Kwa sababu kama unazungumza Sheria hii ambayo tumeleta mabadiliko, mapendekezo ya marekebisho fulani fulani, kulikuwepo na mashauriano makubwa ndani ya Vyama kwanza, lakini hata baina ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. (Makofi) Ndiyo maana hata huu Muswada mwingine wa pili tumeuondoa kwa dhana hiyo hiyo, tulikutana kwenye ngazi za Viongozi wa Vyama, kura ya maoni hiyo. Baadaye tukaja na mapendekezo. Tulipokwenda kuona wenzetu wa Zanzibar wakasema tunahitaji muda zaidi wa mashauriano. Tumekubali na tuliondoa Muswada ili wapate muda zaidi wa kushauriana. Kwa hiyo, unalolisema ni la msingi na lazima liendelee kujengewa misingi imara zaidi katika hatua zake zote. Sasa pengine kwa hilo uliloshauri kama kuna 7 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) namna ambayo unalitazama kwa maana ya suala lenyewe kwa upana wake kwamba pengine mambo mengine yote yawe suspended yaahirishwe kwanza, kwanza tuzungumze kwa ujumla jumla hivi ni jambo jema tu mimi sioni kama lina tatizo hata kidogo. Tutategemea sasa tunataka kuzungumza katika mfumo gani na kwa kujaribu kuzingatia mambo gani halafu tunaweza tukatoka pale tukaelewana tukaona sasa tunakwenda namna gani. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbatia, swali fupi la nyongeza. MHE. JAMES F. MBATIA: Nashukuru Mheshimiwa Naibu Spika. Labda nifafanue kwamba kusudio langu ni kwamba ukiona kura ya maoni iliyofanyika Zanzibar tarehe 31 Julai, 2010 siku ya Jumamosi, ambapo asilimia 66.4 ya Wazanzibar waliamua kufanya kurejea au Toleo la 10 au mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar na kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Zanzibar ni sehemu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kiasi kikubwa Katiba
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages263 Page
-
File Size-