Online Document)

Online Document)

Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 31 Machi, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAJI: Taarifa ya Nane ya Mwaka ya EWURA kwa mwaka 2014 (The 8th EWURA Annual Report for the year 2014). MASWALI NA MAJIBU Na. 130 Hitaji la Maji MHE. RIZIKI S. LULIDA aliuliza:- Vijiji vya Mvuleni, Mloo, Mnang‟ole, Kilolambwani na Minambwe vina shida kubwa ya maji na wananchi wanapata shida kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Riziki Said Lulida, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua ukubwa wa tatizo la maji na adha inayowakabili wananchi wa vijiji vya Mvuleni, Mlolo, Mnang‟ole, Kilolambwani na Minambwe. Halmshauri ya Wilaya ya Lindi ikishirikiana na Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini tayari imefanya utafiti wa maji chini ya ardhi katika vijiji vya Mvuleni na Kilolambwani. Hata hivyo, sampuli za maji zilizochukuliwa kutoka kijiji cha Kilolambwani zilionyesha kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kwani yana chumvi nyingi. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri imepanga kufanya utafiti mwingine katika chanzo kingine cha maji katika kijiji cha Kilolambwani. Vijiji vya Mvuleni na Kilolambwani ni miongoni mwa vijiji 10 vilivyopo katika Mpango wa Utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Bajeti iliyotengwa katika Halmashauri kwa ajili ya miradi ya maji kwa mwaka 2015/2016 ni shilingi milioni 565.6 ambapo kati ya hizo shilingi milioni 357.5 zitatumika kwa ajili ya miradi ya vijiji vya Mvuleni, Mlolo, Kilolambwani na Minambwe. Mheshimiwa Naibu Spika, katika kijiji cha Mnang‟ole utafiti wa maji chini ya ardhi umefanyika. Ujenzi wa mradi wa maji umepangwa kutekelezwa katika bajeti ya mwaka 2015/2016 ambapo zimetengwa shilingi milioni 27.5 kupitia fedha za ruzuku ya maendeleo (CDG). Mheshimiwa Naibu Spika, Minambwe ni kitongoji katika kijiji cha Kilangala „A‟ ambapo kuna mradi wa maji uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA). Halmashauri ikishirikiana na jamii imekuwa ikiufanyia ukarabati ili kuongeza huduma ya maji katika maeneo ya kijiji. Mpaka sasa kupitia Mpango wa Matokeo ya Haraka (quick wins), Halmashauri imekwishanunua jenereta kwa ajili ya mradi huu. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, nakushukuru. MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nitoe shukrani za dhati kwa Waziri mwenye dhamana ya Maji wakati nilipompelekea tatizo hili alinipatia maafisa kutoka Bonde la Mto Ruvuma, Ndugu Msengi na Ndugu Amadeus tukaenda katika maeneo hayo na kuona matatizo yalipofikia. Hayo maeneo ni mapito ya wanyama na wananchi wanatembea kwa kilomita nyingi zaidi ya 20 kutafuta maji usiku na hivyo kuwa ni kero kubwa. Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, kwa vile imeshindikana na hali inaonekana ni tete kutokana usemi wako kuwa maji ni mabaya hayafai kwa matumizi ya binadamu. Je, Serikali ina mpango gani wa kuvuna maji ya mvua ili wananchi wapate maji? Wananchi wa kule wanasema wanataka maji kwa sababu imeshakuwa kero, akina mama wanakwenda kujifungua hospitalini na hawana maji. Kwa nini wasitumie njia ya kuvuna maji ya mvua ili kupunguza kero? Hilo la kwanza. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, tukishirikiana mimi na Mama Jane Goodall alipeleka fedha kwa ajili ya kuchimba kisima katika kijiji cha Mnyangara na alipeleka kila kitu lakini mpaka leo wananchi hawajapata huduma hiyo kwani kumetokea upungufu mkubwa. Je, Serikali itakuwa tayari kutumia fedha angalau shilingi milioni 10 ili kumaliza tatizo hilo ili na wale wananchi wa Mnyangara waweze kusaidiwa? Ahsante! NAIBU SPIKA: Majibu ya swali hilo, Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Amos Makalla. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo kwa kiasi kikubwa yametosheleza katika swali lile la msingi. Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nimhakikishie kwamba wiki mbili zilizopita nimefanya ziara katika Mkoa wa Lindi na nilikuwa katika Jimbo la Mchinga ambapo vijiji hivi anavyovitaja nimepata taarifa zake. Nilikuwa na Mbunge, Mheshimiwa Mtanda lakini nimshukuru kwa kazi kubwa hiyo aliyoifanya lakini nataka nimhakikishie tu kwamba vijiji alivyovitaja ikiwemo Kilolambwani ambako yalipatikana maji yaliyokuwa na chumvi, walipima tena na huu mradi umewekwa katika WSDP, Awamu ya II. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ushauri alioutoa wa kuvuna maji ya mvua, ni mzuri. Naomba Waheshimiwa Wabunge muendelee kuhamasisha huko tunakoishi katika Majimbo yetu kwani itatusaidia katika maeneo ambayo ni vigumu zaidi kupata maji ardhini au sehemu nyingine zozote zile. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Kijiji cha Mnyangara, hili tumelipokea, tutakaa na Mheshimiwa Lulida na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo pia na wataalam ili tuone ni namna gani tunaweza tukalikabili tatizo hili pamoja na jitihada kubwa ambazo zimeshafanywa na huyo mfadhili ambaye umemtaja. Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. NAIBU SPIKA: Tunaendelea, Mheshimiwa Waziri wa Maji, Profesa Maghembe, majibu ya nyongeza! WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa. Niendelee kuwashukuru Naibu Mawaziri kwa majibu mazuri sana waliyotoa. Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitaongezea kidogo kwenye jibu la swali la nyongeza la pili lililotolewa na Mheshimiwa Amos Makalla. Mheshimiwa Lulida ameuliza kama Serikali iko tayari kutoa shilingi milioni 10 ili kumaliza hilo tatizo dogo ambalo lipo katika Kijiji alichokitaja. Napenda nimhakikishie kwamba Serikali itatoa fedha hizo ili kutatua tatizo hilo. (Makofi) NAIBU SPIKA: Nakushukuru sana. Tunaendelea na swali linalofuata la Mheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola. Na. 131 Tatizo la Maji Safi na Salama Kata za Igowole na Nyololo MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Kata ya Igowole na Nyololo zinakabiliwa na tatizo la maji safi na salama:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua tatizo la maji katika Kata hizi za Igowole na Nyololo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola Mbunge wa Mufindi Kusini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua ukubwa wa tatizo na hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Jimbo la Mufindi Kusini zikiwemo Kata za Igowole na Nyololo. Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imekuwa ikitenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa. Katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi iliidhinishiwa shilingi 940,998,278/= kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa miradi katika vijiji kumi. Fedha zilizopokelewa hadi sasa ni shilingi 292,258,930/=. Mheshimiwa Naibu Spika, ili kutatua tatizo la maji katika Kata ya Nyololo, Serikali inatekeleza mradi wa maji wa mtiririko katika kijiji cha Maduma ambapo katika bajeti ya mwaka 2013/2014 zilitengwa shilingi 74,434,248/= kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) fedha zote zimeshapokelewa. Mradi huu unategemewa kukamilika Mei, 2015. Mradi mwingine ambao unatekelezwa na Serikali katika Kata ya Nyololo ni mradi wa pamoja unaojumuisha vijiji vitatu (3) vya Nyololo, Shuleni, Njojo na Lwing‟ulo. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Kata ya Igowole, Serikali imepanga kutekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Sawala, Mtwango, Lufuna, Kibao, Luhunga na Igoda katika mwaka 2015/2016. Jumla ya shilingi 949,827,800/= zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji hivyo. Serikali itaendelea kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kadri upatikanaji wa rasilimali fedha utakavyoruhusu. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kigola, swali la nyongeza. MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi ya maji katika kijiji cha Ikiliminzoo ambapo niliomba shilingi 750,000,000/= na Serikali ilishaleta na mradi ule umekamilika na namuomba Waziri wa Maji atembelee na kufungua mradi ule mkubwa sana. Kwa hiyo, sasa hivi Ikiliminzoo wanaendelea kupata maji. Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile huu mradi wa Maduma, naishukuru Serikali kwa kutusikiliza sisi Wabunge tukiomba msaada na mmeshafanya kazi nzuri na kweli fedha zilishakwenda mradi unafanyiwa kazi. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niulize maswali madogo mawili. Swali la kwanza, nimeuliza kuhusu Kata ya Mtwango na Igowole ni tofauti. Kwanza, namshukuru kwamba Kata ya Sawala tatizo la maji litatatuliwa na sasa hivi kuna shilingi 200,000,000/= niliambiwa zimeshatayarishwa. Nimeuliza kuhusu Kata ya Mtwango Mjini hakuna maji kabisa. Mimi Mbunge nimechimba kisima kirefu ambacho kimegharimu karibu shilingi 17,000,000/=. Je, Serikali inaweza ikaniongezea hata shilingi 50,000,000/= ili niweze kufunga motor kwa ajili ya kupeleka maji kwenye tenki la maji? Kwa sababu pale mjini hakuna maji kabisa, wananchi wananunua ndoo moja ya maji kwa shilingi 50/=. Je, Serikali inaweza ikanisaidia na mimi niongezee pale ili wananchi wa Kata ya Igowole waweze kupata maji? Mheshimiwa Naibu Spika,

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    141 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us