Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Tatu – Tarehe 12 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 213 Ugumu wa Kutekeleza Kazi za Kiutawala Jimbo la Kwela MHE. IGNAS A. MALOCHA aliuliza:- Jimbo la Kwela, limegawanyika katika Makao Makuu Mawili yaliyojitenga Kijiografia, yaani eneo la ukanda wa juu (Mlimani) na eneo la ukanda wa chini (Bonde la Mto Rukwa) ambapo husababisha ugumu katika kuzitekeleza kazi za kiutawala za uwakilishi hasa ikizingatiwa pia kuwa miundombinu ya barabara ni duni sana:- (a) Je, Serikali haioni kuwa inafaa kuligawa eneo hilo kulingana na Jiografia ili kupata Jimbo jingine au Wilaya? (b) Je, ni kasoro gani zilizosababisha jimbo hilo kukosa sifa za kugawanywa kupata Majimbo mawili kulingana na Jiografia jinsi ilivyo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- 1 Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ignas Aloyce Malocha, Mbunge wa Kwela, kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Uchaguzi hugawanywa kwa kuzingatia Vigezo 13, kama ifuatavyo:- 1. Idadi ya watu; 2. Upatikanaji wa mawasiliano; 3. Hali ya kijiografia; 4. Mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu; 5. Hali ya kiuchumi ya Jimbo; 6. Ukubwa wa eneo la Jimbo husika; 7. Mipaka ya kiutawala; 8. Jimbo moja lisiwe ndani ya Wilaya/Halmashauri mbili; 9. Kata moja isiwe ndani ya Majimbo mawili; 10. Mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu; 11. Mazingira ya Muungano; 12. Uwezo wa Ukumbi wa Bunge; na 13. Idadi ya Viti Maalum vya Wanawake. Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kulingana na utaratibu uliopo, maombi ya kugawanya Jimbo ni lazima yajadiliwe na kupitishwa na Halmashauri husika na Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kabla ya kupelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. (b )Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichosababisha Jimbo la Kwela kukosa sifa za kugawanywa ni kutotimiza kigezo cha kwanza na cha msingi ambacho ni idadi ya watu. Jimbo la Kwela, lilitakiwa kuwa na wastatni wa idadi ya watu isiyopungua 237,130 ili liweze kufikiriwa katika ngazi ya Halmashauri. Kwa makisio ya Idadi ya watu ya mwaka 2009, Jimbo la Kwela lilikuwa na watu 140,356. Na ndio maana Halmashauri ya Wilaya, katika Kikao chake ambacho muhtasari wake ninao, muhtasari Na. 10/2 wa 2010 waliridhia kutokupeleka maombi tena Tume ya Uchaguzi baada ya kugundua kwamba kigezo hicho hawanacho tena. (Makofi) MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Ninalo swali moja dogo la nyongeza, pamoja na majibu na ufafanuzi mzuri wa Mheshimiwa Waziri, ninalo swali la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa swali la msingi lilitaja maombi ya vitu viwili, lilitaja Wilaya na Jimbo. Na kwa kuwa, katika ufafanuzi wake inaonekana Jimbo la Kwela, limekidhi vigezo karibu vyote, isipokuwa kigezo cha Idadi ya watu. 2 Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa kuwa hata kigezo cha idadi ya watu kwa mujibu wa ongezeko la watu kila mwaka 3.2% kwa takwimu za kiofisi nilizonazo inaonesha mpaka 2010 Jimbo la Kwela, lilikuwa na watu 200,287. Na kwa kuwa, Waziri ametaja takwimu nyingine, naomba baadaye aifuatilie takwimu. Lakini vile vile swali langu la nyongeza kwa kuwa mahitaji ya Wilaya katika ukanda huo ni ya muda mrefu toka utawala wa awamu ya kwanza. Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa kuwa eneo hilo... MWENYEKITI: Mheshimiwa nafikiri sasa ungeenda kwenye swali. MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa. Na kwa kuwa, eneo hilo ni duni sana katika huduma mbalimbali kama vile elimu, afya, maji na miundombinu mbalimbali na kusababisha watumishi wengi kutopenda kufanya kazi katika maeneo hayo. Je, Serikali haioni kuwa ni muhimu kwa sasa kusogeza utawala? Ili utatuzi wa matatizo hayo uweze kufanyika haraka? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Malocha, la nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, nakiri kwamba nitampa vielelezo nilivyonavyo. Lakini tu nitakupa muhtasari ambao umetoka kwenye Halmashauri yako hiyo hiyo, maana ndio walioniletea idadi ya watu na ndio waliokiri kwamba hatuendelei na maombi ya kuomba Jimbo, kwa sababu kigezo cha kwanza hatuna. Kwa hiyo, hicho kielelezo nitakupa kwa sababu kinatoka kwenye Halmashauri yako. Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la pili la kuomba Wilaya hapa, nimelisikia na mashahidi ni Waheshimiwa Wabunge waliopo hapa. Lakini ninakushauri tu kwamba hili nalo ni lazima lianze huku, haliwezi kuanzia hapa. Kwa hiyo, ninakushauri ulifikishe kwenye vikao vinavyohusika vya Kikanuni vya Halmashauri na baadaye vije katika utaratibu wa kawaida, Serikali italifikiria kulingana na vigezo vilivyowekwa. MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa bado maeneo mengi hapa nchini ni makubwa na inaonekena yataendelea kugawanywa. Lakini pia, ziko Halmashauri ambazo sasa hivi zina hadhi ya miji midogo na baadaye zitakapokuwa miji kamili, zitahitaji kuwa na Wabunge. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunajua uwezo wa Bunge hili au ukumbi huu ni kuwa na Wabunge karibu 360. Je, tutaendelea kugawanya haya maeneo lini na idadi hiyo itakapokuwa inazidi tutafanya nini wakati ukumbi wa Bunge bado una idadi ile ya Wabunge 360? 3 WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU,SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zambi la nyongeza, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli muundo wa Halmashauri na Miji ni changamoto kwa sababu, wakati mwingine sifa za kuwa Miji zinalazimisha kuwa Majimbo. Tumeliona kama Serikali na ni changamoto, hivi sasa tunalizungumza ili tuone hatulazimishwi na Sheria nyingine kuanzisha Majimbo kama zilivyo sheria za kuanzisha Halmashauri za miji. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mheshimiwa Zambi atakubaliana na mimi pengine, kazi inayoendelea mbele yetu ya marekebisho ya Katiba au ya kuandaa Katiba Mpya itatupa mwelekeo mpya wa namna Bunge letu linavyotakiwa kuwa kwa sababu haya ni mambo yote ambayo wananchi watazungumza. Pengine inaweza kuweka hata ukomo wa idadi ya Wabunge wa jumba hili, tusilazimike kujenga jengo jingine. Kwa hiyo, Mheshimiwa Zambi naomba tu avute subira kwa sababu ni mwaka huu tutapitisha ile Sheria na kazi itaanza. Acha tuone sasa baada ya miaka hiyo 50 tunasemaje juu ya mfumo na uendeshaji wa Bunge letu. Na. 214 Ukosefu Wa Ajira Kwa Maafisa Mipango MHE. FELISTER A. BURA K.n.y. PUDENCIANA W. KIKWEMBE aliuliza:- Serikali imekuwa ikitoa mafunzo ya Kada ya Afisa Mipango (Planning Officers) kupitia Chuo cha Mipango Dodoma na pia imekuwa ikitoa mafunzo katika Kada ya Uchumi katika vyuo vingine na kuwaajiri Wachumi hao kufanya kazi za Maafisa Mipango:- (a) Je, serikali haioni kuwa, kwa kufanya hivyo imeua kada ya Maafisa Mipango? (b) Je, Serikali, haioni kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuajiri Maafisa Mipango na kuwatenganisha kiutendaji na wachumi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS – MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pudenciana Wilfred Kikwembe, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuwa mwaka 2002 Serikali ilihuisha Miundombinu ya Maendeleo ya Utumishi ya Kada zilizokuwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji ambapo Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Wachumi na 4 ule wa Maafisa Mipango iliunganishwa kuwa Muundo mmoja wa Wachumi, ili kurahisisha mgawanyo wa majukumu baina ya watumishi wa Kada hizo na kuongeza upeo wa maendeleo yao. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua kuwa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilianzishwa ili kutoa mafunzo yanayolenga kutoa wataalam wa fani ya Mipango ya Maendeleo katika Ngazi za Mikoa, Wilaya, Vijiji, Kata na Tarafa, Wizara ya Fedha ambayo ndiyo Wizara mama ya Kada ya Wachumi, inaendelea na zoezi la kutathmini muundo wa Kada ya Maafisa Mipango wanaohitimu katika Chuo cha Maendeleo ya Mipango cha Dodoma ili kuainisha ujuzi ili kuhakikisha wote wanateuliwa kama Wachumi na hivyo kustathili huduma na marupurupu sawa wanapoajiriwa katika vyombo vya Serikali. MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Waziri, amesema kwamba Serikali inafanya tathmini kuhusu Kada hizi mbili, ya Maafisa Mipango na wale ambao wamesomea mambo ya uchumi. Je, tathmini hii itamalizika lini ili hao Maafisa mipango waweze kufanya kazi ambazo wamezisomea? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS – MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza napenda ku-declare interest kwamba na mimi pia nilikuwa Afisa Mipango. Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyonmgeza la Mheshimiwa Felister Bura, kama ifuatavyo. Tathmini yetu tunategemea mpaka mwezi wa 10 iwe imemalizika, ili mapendekezo yao yaingie katika Baraza la Majadiliano ya pamoja katika Utumishi wa Umma, litakalofanyika mwezi Novemba, 2011. Na. 215 Barabara Kuelekea Mvumi Hospitali MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE aliuliza:- Hospitali teule ya Mvumi ambayo pia ni ya Wilaya ya Chamwino iko umbali wa Kilometa 40 kutoka Dodoma Mjini na tangu mwaka 1936 kabla ya Uhuru, wananchi wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la usafiri. (a) Je, Serikali
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages248 Page
-
File Size-