Tarehe 6 Mei, 2016

Tarehe 6 Mei, 2016

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Nne - Tarehe 6 Mei, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MHE. VICKY P. KAMATA (K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA): Taarifa ya Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017. NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. JOSHUA CHAMWELA- KATIBU MEZANI: Maswali. 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 110 Utengenezaji wa Barabara ya Kutoka Njianne hadi Nandete kwa Kiwango cha Lami MHE. VEDASTO E. NGOMBALE aliuliza:- Moja ya matukio makubwa ya kihistoria katika nchi yetu ni vita ya Majimaji iliyopiganwa kati ya mwaka 1905 – 1907 kati ya Watanganyika na Wajerumani. Pamoja na kufahamu kwamba vita hivyo vilienea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, lakini vilianza katika Kijiji cha Nandete, Wilaya ya Kilwa; Serikali inaonesha jitihada mbalimbali ya kuienzi historia hiyo, ikiwa ni pamoja na kujenga mnara katika Kijiji hicho:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara ya kutoka Njianne hadi Nandete kwa kiwango cha lami ili kulifanya eneo hilo la kihistoria kufikiwa kwa urahisi na kuliongezea umaarufu kwa kutembelewa na watalii hususani wa kutoka Ujerumani jambo ambalo litaiongezea mapato Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na Taifa kwa ujumla. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vedasto Edgar Ngombale, Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa kujenga barabara ya lami kwenda eneo hili la kihistoria ni la msingi, lakini kwa sasa wakati Serikali inajenga barabara kuu zote nchini kwa kiwango cha lami hasa zikiunganisha Makao Makuu ya Mikoa yote. Hata hivyo, Serikali imekuwa ikitenga bajeti ya fedha kwa ajili ya matengenezo ili kuifanya ipitike wakati wote. Kupitia Wakala wa barabara Mkoa wa Lindi, katika mwaka wa fedha 2015/2016, zilitengwa shilingi milioni 58.8 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida kilomita 43 na matengenezo ya muda maalum kwa kiwango cha changarawe urefu wa kilomita sita, kwa jumla ya gharama ya shilingi milioni 192.3. Matengenezo ya barabara hii yameanza chini ya Mkandarasi Ungando Contractors Company wa Kibiti – Rufiji. Aidha, katika bajeti ya mwaka 2016/2017, barabara hii iko katika mpango wa kufanyiwa matengenezo. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kilomita 10 zinazohudumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, katika mwaka 2015/2016, zimetengwa shilingi milioni 70 ambazo zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya muda maalum kwa urefu wa kilomita nane. Katika mwaka wa fedha 2016/2017, zimetengwa shilingi milioni 967.6 ambazo zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara katika Wilaya ya Kilwa. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vesto Ngombale swali la nyongeza. MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa vita ya Majimaji au harakati za awali za kudai uhuru wa Tanganyika zilitokana na chokochoko na misingi imara ya kukataa kuonewa na kudai uhuru kulikofanywa na majemedari wetu wakati wa vita vya Majimaji. Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara hii ili kuwawezesha Watanzania kwenda katika eneo hilo wakajifunze namna gani nchi yetu ilivyojengwa katika misingi ya kudai haki? (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kwa kuwa barabara hii haipitiki kabisa Serikali ina mpango gani wa kuweka lami katika sehemu korofi kwa mfano mlima Ndundu, Mlima Ngoge pale Chumo, Mlima Kinywanyu na Mlima Karapina pale Kipatimu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi kwamba umuhimu wa barabara hii na Mheshimiwa Mbunge amesema kwamba sehemu hii ndiyo chemichemi za harakati ya ukombozi wa nchi yetu. Naomba nikiri kwamba, kuna maeneo mengi sana ya kijiografia ambayo wakati wa uhuru kama Tanzania tulipokuwa tunaenda katika mchakato walishiriki kwa kiwango kikubwa sana katika kufanikisha uhuru wa nchi yetu, nawapongeza sana ndugu zetu wa Kilwa katika hilo. Mheshimiwa Naibu Spika, nakiri wazi kwamba kwa sababu umuhimu wa barabara hii kama nilivyosema awali katika jibu langu, tukirejea tena marejeo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi, lengo lake kubwa ni kuhakikisha wananchi wanafikiwa wa maeneo mbalimbali. Mheshimiwa Ngombale tutafanya juhudi siyo hapo Kilwa tu, isipokuwa maeneo mbalimbali. Ndiyo maana Ofisi ya Rais, TAMISEMI ilikuwa ikifanya mikakati katika maeneo mbalimbali, tulianza hasa katika miji tumeenda katika halmashauri, lengo letu ni kwamba maeneo mbalimbali yaweze kufikika chini ya miradi yetu ambayo sasa hivi tuna mradi wa TSP Project ambayo inahusisha ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami katika maeneo mbalimbali. 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili litakuwa katika mpango wetu, mkakati mpana wa kuhakikisha Halmashauri nyingi zinafikiwa na haya ni mambo ambayo tunayafikiria, ndiyo maana hata ukiangalia bajeti yetu ya mwaka huu tuna bajeti takribani ya bilioni 43 kwa ajili ya kuondoa vikwazo, lakini bilioni zaidi ya 200 kwa ajili ya kuhakikisha Halmashauri ziweze kufikiwa vizuri. Kwa hiyo, ni mambo ambayo Serikali yetu inayaangalia na ndani ya miaka mitano tuna imani tutafanya mambo makubwa sana. Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lile la kuhusu sasa vile vipande korofi ikiwezekana viwekewe lami na najua Halmashauri ya Kilwa jinsi gani jiografia yake ilivyo na wakati mwingine malori yanashindwa kupanda. Tutawaelekeza wenzetu wa TANROAD ambao tunashirikiana nao kwa karibu zaidi na barabara takribani kilomita 48 zinahudumiwa na TANROAD, tutahakikisha Serikali inayapa kipaumbele yale maeneo korofi ambayo mvua ikinyesha barabara hazipitiki kwa kuyafikiria kwa jicho la karibu zaidi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Gekul MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Pamoja na mikakati ya Serikali kujenga barabara za lami, lakini kuna ahadi ya Mheshimiwa Rais ambayo aliitoa katika maeneo yetu wakati anaomba kura, ya ujenzi wa barabara za lami. Katika Bunge hili tuliomba tupatiwe time frame kwamba ni muda gani hizi ahadi zinatekelezwa. Nataka kufahamu ni lini Mheshimiwa Waziri atatuletea ratiba ya ujenzi wa barabara hizo za lami kwa ahadi ya Rais ili tufuatilie kwa karibu ikiwemo Jimbo langu la Babati Mjini kilomita ishirini za lami? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI jibu fupi tafadhali! NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ni lini, kifupi time frame ya ujenzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, imeainishwa ndani ya miaka mitano 2015- 2020. Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha ndani ya kipindi hiki zile ahadi ambazo tumeahidi kwa kadri ilani yetu ilivyojielekeza, tutajitahidi kwa kadri iwezekanavyo, ili mwisho wa siku tuone kwamba ilani yetu imetekelezwa kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maendeleo ya kutosha na siyo Babati peke yake, isipokuwa kwa Tanzania nzima kwa mujibu wa Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Na. 111 Kurekebisha Mishahara ya Walimu Waliopandishwa Vyeo MHE. DOTO M. BITEKO aliuliza:- Je, kwa nini Serikali inachukua muda mrefu sana kurekebisha mishahara ya Walimu baada ya kupandishwa vyeo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko, Mbunge wa Bukombe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba miaka ya nyuma kulikuwepo na ucheleweshaji wa kurekebisha mishahara kwa kuwa mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara wa wakati huo ulimtaka kila Mwajiri kuwasilisha marekebisho ya Watumishi wake Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzia mwaka 2012 Mfumo huu wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara uliimarishwa kutoka Toleo la 7 kwenda Toleo la 9 la Lawson ambapo mwajiri alisogezewa huduma ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kiutumishi yanayotokea katika ofisi yake bila ya kulazimika kusafiri kwenda Dar es Salaam. Utaratibu huu umekuwa na manufaa ambapo kwa sasa mabadiliko mbalimbali ya kiutumishi yanafanywa na mwajiri kwa kuzingatia mzunguko wa malipo ya mishahara kwa kila mwezi. Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na utaratibu huu mzuri, mazingira machache yanayoweza kuchelewesha marekebisho ya mishahara kufanyika kwa wakati, kutokana na kuingizwa kwa taarifa za watumishi kwenye mfumo baada ya orodha ya malipo ya mishahara katika mwezi husika kufungwa, au waajiri kufanya mabadiliko bila ya kuweka taarifa muhimu hususan viambatisho kama vile barua za kupandishwa

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    267 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us