29 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd

29 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd

29 MEI, 2013 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Thelathini na Saba – Tarehe 29 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Zungu Azzan) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 29 MEI, 2013 MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Kuhusu Utekelezajiwa Majukumu ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. PAULINE P. GEKUL (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA KAZI NA AJIRA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Kazi na Ajira Kuhusu Makadiro ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MASWALI NA MAJIBU Na. 295 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Kuhamia Chamwino MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE aiuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeendelea kufanya kazi zake Dodoma Mjini tokea kuundwa kwake karibu miaka kumi iliyopita. (a) Je, Serikali itatoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhamia Chamwino yaliyoko Makao Makuu ya Wilaya hiyo? (b) Je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu malipo ya uhamisho kwa watumishi wa Halmashauri hiyo watakaohamia Chamwino? 2 29 MEI, 2013 NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hezekiah Ndahani Chibulunje, Mbunge wa Chilonwa, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo. (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Chamwino bado unaendelea. Hadi sasa Serikali imepeleka shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo na kwa mwaka 2013/2014 zimetengwa milioni 500. Sambamba na ujenzi wa ofisi, Serikali imeidhinisha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba sita (6) za watumishi ambapo nyumba tatu ziko katika hatua ya umaliziaji. Aidha, Serikali imepima viwanja 3500 kule Chamwino ili pamoja na shughuli nyingine ziweze kutumika kujenga nyumba za watumishi. Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama za ujenzi wa nyumba za watumishi ni kubwa, Serikali peke yake haiwezi kukidhi gharama za ujenzi kwa Halmashauri zote zinazoanzishwa. Tunatoa wito kwa taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na mashirika binafsi kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za watumishi. Aidha, Serikali inaziagiza Halmashauri zote ambazo hawajahamia kwenye Makao Makuu yake wahamie mara moja. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uhamisho wa watumishi, mwajiri anapaswa kuzingatia taratibu zote za uhamisho wa watumishi kwa mujibu wa Kanuni L8 na L33 za Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009. Halmashauri ya Wilaya ya chamwino inashauriwa kutenga katika bajeti yake fedha za uhamisho kwa ajili ya watumishi wake. 3 29 MEI, 2013 MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili. Kwanza, swali langu lipo very specific, ninataka maekelezo kutoka Serikalini kwa watumishi kuhamia Chamwino. Maelezo ya Mheshimiwa Waziri juu ya hatua mbalimbali za ujenzi wa Makao Makuu yanaashiria kuwapa mwanya watumishi hao waendelee kusubiri mpaka majengo yaishe. Sasa bado nashikilia kwamba Serikali itamke ni lini watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino watahamia kwenye Makao Makuu ya Wilaya ukiachilia mbali ujenzi huu unaoendelea kwa sababu pale zipo nyumba za kutosha na isitoshe DC yuko kule kutoka Wilaya hii ianzishwe? Pili, kwa sababu azma ya kupata Wilaya mpya ni kuwasogezea wananchi huduma za utawala, sasa kwa kubakia muda mrefu baada ya kutangazwa Wilaya mpya watumishi hawajahamia bado, haioni kwamba inakinzana na azma rasmi ya kupata Makao Makuu ya Wilaya? NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hezekiah Ndahani Chibulunje, Mbunge wa Chilonwa, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi Chamwino nimekwenda na Makao Makuu ya Wilaya anayoyoyazungumzia nimefika na Mheshimiwa Chibulunje anafahamu kwamba tumefika katika yale maeneo. Maelekezo ni kwamba Halmashauri zote mpya na Wilaya zote mpya ambazo zimeanzishwa watumishi wake wanatakiwa wawe katika Makao Makuu ya Wilaya yaani pale ambapo huduma zinatolewa. Sasa lakini kitakuwa ni kichekesho kama unajua kabisa kwa mfano hapa tumeanzisha karibu 16 yaani Wilaya mpya nyingi tu, hivi tunavyozungumza ukienda katika Makao Makuu ni pori, tulichofanya pale ni kwamba tumekodisha tu maeneo 4 29 MEI, 2013 au tumetafuta maeneo ili watu wakae kwa muda. Naelewa anachozungumza Mheshimiwa Chibulunje, kwa maana ya maelekezo ya Serikali, maelekezo ni kwamba Halmashauri zote na Watumishi wake wote wakae kwenye Makao Makuu ya Wilaya. Lakini katika uhalisia wake ukienda kule hakuna nyumba za watumishi, wako wengine ambao wamehamishimiwa katika maeneo ya Vijijini kama tunavyozungumza hapa, ndiyo maana nimezionyesha jitihada za Serikali kwamba zipo nyumba za Serikali zinazojengwa kule. Sasa najua kwamba anapozungumza pia habari ya posho, posho ya kuwahamisha hao watumishi kwenda kule ni shilingi milioni 750 ndiyo utakuwa umemaliza zoezi lote zima na ninajua watakwenda pale halafu kimyakimya watarudi tena utawakuta wamebana hapa Dodoma. Ni pamoja na Bahi ambao tumeshawelekeza kwamba waondoke waende Makao Makuu ya Bahi. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi ili nisichukue muda wako nataka niseme kwamba sisi tunajitahidi pamoja nao, hizi fedha wala hazikutengwa kwa hiyo, kwamba mimi nitamwambia njoo uchukue shilingi milioni 750 kachukue, hazipo, lakini tutakaa na yeye Mheshimiwa Chibulunje na wenzake tukae wote kwa pamoja tulitafakari jambo hili tuone tunapata wapi fedha hizi ili tuweze kuwahamisha hawa watumishi ili ugomvi uishe. (Makofi) Na. 296 Kujenga Mabweni kwa Ajili ya Wasichana MHE. JUMA A. NJWAYO (K.n.y. MHE. RIZIKI SAID LULIDA) aliuliza:- Mkoa wa Lindi ni wa mwisho kwa idadi ndogo ya mabweni ya wasichana hali inayopelekea kuongezeka kwa tatizo la mimba za utotoni. 5 29 MEI, 2013 Je, Serikali ina mikakati gani ya makusudi ya kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Riziki Said Lulida, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, SerikalI katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kila mwaka hutenga fedha za ujenzi na ukamilishaji wa mabweni na hosteli. Aidha, Serikal inatoa fedha za ruzuku ya maendeleo (LGDCG) kwa kila Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya shule kulingana na vipaumbele vya Halmashauri. Mwaka 2012/2013 Serikali kupitia Bajeti na mipango ya Halmashauri ilitenga zaidi ya shilingi bilioni 10.8 kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa hosteli mwaka 2013/2014 zimetengwa shilingi bilioni 5. Serikali mwaka huu kwa kushirikiana na Serikali ya Japan inajenga hosteli katika shule mbalimbali nchini. Katika shule za sekondari Nkowe, Ng’apa na Nachingwe ujenzi wa hosteli zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 288 unaendelea kwa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600. Mheshimwa Mwenyekiti, Mkoa wa Lindi unahitaji hosteli 280 ili kukidhi mahitaji kwa wanafunziwa shule za sekondari za Serikali. Kati ya mwaka 2005 hadi 2012 wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendeleo wamekamilisha ujenzi wa hosteli katika shule 20 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,514, hivi sasa wanafunzi wa kike 1,435 wanatumia hosteli hizo ikiwemo katika shule za sekondari Mnala, Nongogo, Nakiu, Chingongwe, Nangamo na Matekwe. 6 29 MEI, 2013 Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa mandeleo itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia nchini kila mwaka. Aidha, hatua hali zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wanaobainika kusitisha masomo kwa watoto wa kike. Natoa wito kwa jamii na wadau mbalimbali k ushirikiana kwa dhati katika jukumu la kumlea, kumlinda na kumsaidia mtoto wa kile popote alipo ili aweze kufikia malengo yaliyokusudiwa. MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ni dhahiri kwamba kuna mahitaji makubwa ya mabweni nchini na kwamba kwenye miji miji mikubwa kama Dar es Salaam watoto wetu wanapata adha kubwa sana asubuhi na jioni wanapokwenda shuleni kwa sababu daladala huwa zinawasumbua sana na tena wamewabandika majina ya kusoma. Kwa nini sasa Serikali isiwe na mkakati maalum wa kutafuta fedha ili kuhakikisha tunamaliza tatizo hili la mabweni katika nchi yetu yote? Pili, kumekuwa kunajitokeza tatizo la mimba hapa nchini linaloamuliwa rejareja kati ya wazazi na Walimu au waweka mimba na kadhalika, jambo ambalo linashusha sana idadi ya vijana wetu kuwa na elimu hapa nchini. Je, ni hatua gani za dhati zinachukuliwa na Serikali kutoa adhabu kali kwa wale wanaowasababishia watoto wetu wa kike mimba? NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    252 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us