
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 24 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Azzan Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae. Katibu! NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2017/2018. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. STANSLAUS H. NYONGO – (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA): Taarifa ya Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MHE. CECILIA D. PARESSO – (K.n.y. MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MHE. CECILIA D. PARESSO - (K.n.y. MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MHE. JOSEPH K. MHAGAMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA NA SHERIA): Taarifa ya Kamati ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano kwa mwaka 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MWENYEKITI: Katibu. 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 85 Utaratibu wa kuwasimamisha kazi Watumishi wa Umma MHE. MCH.PETER S. MSIGWA (K.n.y. MHE. RUTH H. MOLLEL) Aliuliza:- Nchi yetu inaendeshwa kwa kuzingatia Katiba, Sheria na Kanuni katika kuajiri na kuwasimamisha kazi watumishi wa umma. Kuna baadhi ya watumishi wa umma wamesimamishwa kazi na Mheshimiwa Rais, RC na hata DC bila kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni zake. Je, Serikali inasemaje kuhusu hili? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA Alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ruth Mollel, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua za nidhamu katika utumishi wa umma hutekelezwa kwa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali. Kwa mujibu wa Ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Rais ndiye mwenye mamlaka ya mwisho kuhusu usimamizi na uendeshaji wa utumishi wa umma, ikiwemo kuanzisha, kufuta Ofisi na kuchukua hatua za nidhamu. Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara hiyo ya 36(2) imempa Rais uwezo wa kukasimu madaraka yake kwa mamlaka mbalimbali ndani ya utumishi wa umma. Hata hivyo kukasimu madaraka hakuwezi kutafsiriwa kwamba Rais hana mamlaka hayo tena kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 36(4) ya Katiba na Kifungu cha 21(4) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298. Mheshimiwa Mwenyekiti, pale maelekezo ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wa umma yanapotolewa na Viongozi wa Serikali, Mamlaka za Nidhamu za watumishi husika ndizo zenye dhamana ya kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa. MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nakubaliana naye kwamba kwa mujibu wa Sheria na Katiba yetu, Rais ndiye mwenye mamlaka ya mwisho na ndiye Mwajiri Mkuu. Swali la msingi limeulizwa kwamba kumekuwa na practice ya kuanzia Rais mwenyewe na ma-DC na RCs kutumbua au kuwasimamisha watu kwa njia ya mnada, kupigia kura atumbuliwe au asitumbuliwe, kwa hiyo, swali la msingi linaulizwa hapa, ni kwa nini Serikali isifuate utaratibu na kanuni na sheria ambazo sisi wenyewe tumeziweka? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, hawa ma-RC na ma-DC ni kada ya kisiasa kama sisi Wabunge tulivyo, hawana weledi na ndiyo maana Baba wa Taifa alisema tuliweka sheria ngumu sana ili mtu asizuke tu na kufukuza watu ovyo ovyo. Kwa kumuenzi Baba wa Taifa ambaye alithamini sana kada ya watendaji wa umma; je, Serikali itatoa tamko sasa kwamba ma-RC na ma-DC wasikurupuke tu kuwafukuzisha watu bila kufuata taratibu na kanuni za nchi? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kuhusiana na kwa nini Serikali 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) isifuate utaratibu, napenda kuendelea kusisitiza kwamba Serikali inafuata uratatibu na kwamba kwa wateule ambao wameteuliwa na Mheshimiwa Rais, hatua zao za kinidhamu huchukuliwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa mujibu wa kifungu cha 4(3)(d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema katika Ibara ya 36(4), Mheshimiwa Rais pamoja na kukasimu bado anayo mamlaka ya mwisho na hakatazwi kutumia mamlaka yake. Kwa watumishi wengine wa umma, kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Mamlaka za Nidhamu zimepewa mamlaka yao ya mwisho kabisa ya kuweza kuchukua hatua kwa watumishi wengine ambao sio wateule wa Rais. Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuendelea kusisitiza kwamba jambo la msingi katika mamlaka za kinidhamu zinapochukua hatua, wanatakiwa wazingatie hatua tatu zifuatazo:- Kwanza kabisa waweze kutoa hati ya nashtaka; pili, watoe fursa ya kujitetea kwa yule mtuhumiwa au mtumishi; na mwisho, tatu, uchunguzi wa kina uweze kufanyika ili kuthibitisha tuhuma hizo. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napenda kusema, utaratibu mzima wa kina na mwongozo umefafanuliwa katika kanuni ya 46 na 47 za Kanuni za Utumishi wa Umma. Endapo kuna mtumishi wa umma anaona hajaridhika na hatua za kinidhamu zilizochukuliwa, anayo fursa kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Utumishi wa Umma kuweza kukata rufaa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la pili kwamba Serikali inatoa tamko gani katika hatua ambazo zimechukuliwa na ma-RC na ma-DC? Naendelea kusisitiza kwamba kifungu cha 6(1)(b) na kifungu cha 4(3)(d) kimeelekeza Mamlaka za Nidhamu ni zipi? Ndicho ambacho Serikali imekuwa ikifuata. (Makofi) 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Silinde, ajiandae Mheshimiwa Chatanda. MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwenye majibu ya Mheshiwa Waziri amesema, endapo mtumishi hajaridhika na hatua za kinidhamu alizochukuliwa, akate rufaa. Sasa endapo mtumishi huyo ametumbuliwa na Mheshimiwa Rais na hajaridhika na hayo matokeo, wapi achukue hatua za kuja kukata rufaa? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza Mheshimiwa Silinde ameuliza swali zuri sana; na kama atakuwa amefuatilia hata katika hotuba yangu ya bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi), ziko kesi mbalimbali ambazo hata Ofisi ya Rais (Utumishi) pia tunashitakiwa. Wako ambao wanafungua kupinga maamuzi ya Mheshimiwa Rais, wako ambao wanafungua kesi kupinga maamuzi ya Katibu Mkuu Kiongozi, lakini pia katika Tume yetu ya Utumishi wa Umma ambayo ni mamlaka yenye Mamlaka ya Urekebu wamepokea kesi mbalimbali. Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, katika mwaka huu wa fedha tu peke yake, zaidi ya watumishi wa umma 76 wameweza kukata rufaa katika Tume ya Utumishi wa Umma na endapo hawataridhika, bado tunacho Kitengo cha Rufaa chini ya Mheshimiwa Rais pia (Public Service Appeals) wanaweza pia wakakata rufaa nyingine. Kwa hiyo, namhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge kwamba taratibu zipo na zinafuatwa na ziko wazi kabisa na wako ambao hata wanajikuta walikata rufaa dhidi ya Mheshimiwa Rais na wakaja kushinda endapo kama kuna taratibu inaonekana hazikufuatwa. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Chatanda. MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana… 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Utumishi kwa majibu mazuri sana. Nilitaka kuongezea, kuna moja ambalo limewataja Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuchukua hatua za kuwasimamisha au kuwafukuza kazi watumishi wa umma. Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kifungu cha (5) cha Sheria ya Tawala za Mikoa, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ndio wawakilishi wa Serikali Kuu kwenye maeneo yao. Ukisoma pia kifungu cha 87 cha Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, kinawataja hawa na kwa ajili ya usahihi wa nukuu, napenda nisome kwa sababu wakati mwingine tunauliza swali lile lile kila siku. Bahati mbaya imeandikwa kwa Kiingereza, inasema hivi; “In relation to the exercise of the powers and performance of the functions of the Local Government Authorities confered by this Act, the role of the Regional Commissioner and the District Commissioner shall be to investigate the legality when questioned of the actions and decisions of the Local Government Authorities within their areas of jurisdiction and to inform the Minister to take such other appropriate action as may be required.” (Makofi) MBUNGE FULANI: Yes! WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukisoma kifungu hiki unaona kabisa kwamba wao kuchukua hatua zozote zile, ziwe za kiutumishi ni sahihi, isipokuwa utaratibu aliouzungumza Mheshimiwa Waziri wa Utumishi ndiyo unaotakiwa. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa anaposema wewe hufai, umefanya makosa haya, akasema publicly, siyo ndiyo kafanya tendo hilo la kumsimamisha au kumuadhibu yule mtumishi, anachofanya pale, baada ya tamko lile, sasa Mamlaka ya Nidhamu ya mtumishi husika ndiyo inachukua hatua.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages359 Page
-
File Size-