5 JUNI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Arobaini na Tatu - Tarehe 5 Juni, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Ifuatayo Iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA M. SALUM): Randama ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 5 JUNI, 2013 MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa tunaanza maswali Ofisi ya Waziri Mkuu. Na. 343 Miradi ya Miundombinu ya Kiuchumi Chini ya PPP MHE. RASHID ALI ABDALLAH (K.n.y. MHE. HAMAD RASHID MOHAMED) aliuliza:- (a) Je, ni miradi mingapi ya miundombinu ya kiuchumi chini ya PPP imeainishwa hadi mwaka 2012? (b) Je, baada ya Kanuni za PPP kuwa tayari utekelezaji wake umefikia wapi na ni Wawekezaji wangapi waliojitokeza kwa ajili ya miradi hiyo? (c) Je, kiasi gani (fedha na hisa) cha kushiriki katika miradi hiyo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi, lenye sehemu (a) (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwaka 2012 jumla ya miradi 9 ya miundombinu inayoweza kutekelezwa kwa ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi imeainishwa kama ifutavyo:- 2 5 JUNI, 2013 Mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze (Road toll); Mradi wa ujenzi wa barabara la Arusha-Moshi (Road toll); Ujenzi wa Bandari ya Mbegani- Bagamoyo; Ujenzi wa Bandari ya Mwambani Tanga; Ujenzi wa Bandari ya Nchi kavu Kisarawe (Kisarawe Cargo Freight Station); Upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Mtwara; Uboreshwaji wa Bandari ya Kilwa; Upanuzi wa Bandari ya Kasanga pamoja na Upanuzi na Uboreshaji wa Bandari ya Kigoma. (b) Baada ya Kanuni za PPP kukamilika, Serikali imechukua hatua za kuanzisha Kitengo cha Uratibu chini ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) na Kitengo cha Fedha chini ya Wizara ya Fedha. Aidha, Maafisa Dawati (Desk Officer) wameshateuliwa kwenye Wizara na baadhi ya Taasisi za Serikali ikiwemo kuwapatia mafunzo maalum ya kuwajengea uelewa Maafisa Dawati 60 kutoka Mamlaka za Serikali na Sekta binafsi ili waweze kuratibu ubainishaji wa miradi hiyo. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya PPP, Wawekezaji wanatarajiwa kupatikana baada ya Mamlaka husika za Serikali kuwa zimekamilisha upembuzi yakinifu wa miradi na kuitangaza kwa lengo la kupata wawekezaji watakaoingia ubia na Serikali. Mchakato wa upembuzi yakinifu unaendelea katika maeneo mbalimbali kabla ya kuitangaza miradi itakayohusika. (c) Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maelezo yangu ya ufafanuzi katika sehemu (b) ya swali hili, fedha na hisa katika miradi inayotarajiwa kuwekezwa kwa utaratibu huo wa PPP bado hazijaainishwa. MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yak mazuri, pamoja na majibu hayo, nitakuwa na swali moja tu la nyongeza. Miradi iliyoainishwa, ni miradi tisa, tena mikubwa sana, Mheshimwa Waziri, hauoni kuna haja ya kuweka kipaumbele miradi michache ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati. 3 5 JUNI, 2013 WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:- Miradi iliyoainishwa ni tisa, ni michace, hapana siyo michache, miradi hii, umesema ni mingi, lakini mimi naona ni michache, kwa sababu tunatarajia kila Sekta na kila Wizara iainishe miradi ambayo inaweza kufaa kwa utaratibu huu wa PPP. Kwa sababu hii miradi yote hatutegemei kwamba itachukuliwa au itajengwa na Kampuni moja, sisi tunatangaza, na watu wa mataifa yote, ni tenda ya Kimataifa, mtu yeyote Duniani anaweza kuja kuchagua mradi mmoja aka- invest kwa mradi ambao anaona unafaa kuingia PPP kati yake na Serikali kwa aina yoyote ya Sekta. Kwa hiyo, ingawa wewe nafikiri ni mingi, lakini mimi nafikiri ni michache, na sisis Serikali bado tunaendelea kuainisha miradi mingine na ndiyo maana tumewaelimisha wale vijana katika kila Sekta ili wajue namna ya kuainisha, ni aina gani ya miradi ambayo inaweza kuingiwa kwa ubia kati ya Sekta binafsi na Sekta ya umma. MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na mafanikio kadhaa katika Public Private Partnership, kuna changamoto ambazo zimejitokeza ukimemo urasimu, ikiwemo kutokuwa na uwazi katika mipangilio yote ya PPP na vilevile kutokuaminiana kati ya wawekezaji na Serikali. (Makofi) Je, Serikali inatoa kauli gani sasa ili tufikie sasa muwafaka wa kuweza kuwaelimisha watanzania na hatimaye kuwa na mafanikio katika miradi ya PPP? SPIKA: Mheshimiwa wa Nchi naomba ujibu kwa kifupi. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Leticia Nyerere kama ifuatavyo:- 4 5 JUNI, 2013 Urasimu, ndiyo, lakini kutokuelewana, hakupo, kwa sababu miradi hii hatujaanza kutekeleza, na kama unavyojua kwamba Sera yake imepitishwa mwaka 2009, halafu tukatunga Sheria ya mwaka 2010, na Kanuzi zake tumetayarisha 2011, na kwa mujibu wa Sheria tunatakiwa kuanzisha units mbili za kusimamia mambo hayo, moja itakuwa TIC na nyingine Wizara ya Fedha. Sasa kwenye upande wa urasimu na sisi tumeona kwamba jambo hili ili liende haraka lazima liwe na one stop center, liwe na unit moja badala ya kuwa na units ambazo zinasimamiwa na Wizara mbili tofauti. Kwa hiyo, marekebisho haya yanafanywa, tutaleta ndani ya Bunge ili tuwe na unit moja ya kusimamia badala ya units mbili, lakini mpaka sasa hayo unayoyasema ume- experience, hatuja- experience bado sisi, ya kwamba kuna kutokuelewana, au mpalaganyiko wowote, hapana. Tunaendelea vizuri, sasa hivi kama nilivyosema tunaainisha miradi ya kutosha ili tuweze kuifanyia upembuzi yakinifu, tuitangaze, tupate watu ambao wanaweza kuwa na nia ya kuwekeza pamoja na Serikali.(Makofi) SPIKA: Naona tuendelee na swali linalofuata, muda. Na. 344 Upatikanaji wa Maji Katika Mji wa Muheza MHE. HERBERT J. MNTANGI Aliuliza:- (a) Je, Serikali itasaidia lini jitihada za kuipatia Halmashauri fedha kuelekea kutekeleza miradi ya maji ya visima na kuboresha vyanzo vya maji? (b) Je, ahadi ya kuupatia Mji wa Muheza maji kutoka chanzo cha Mto Zingi itatekelezwa lini? 5 5 JUNI, 2013 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Herbert J. Mntangi lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Mji wa Muheza unafikia asilimia 56.3 ya mahitaji yote ya wakazi wa eneo hilo. Ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji maji katika Mji wa Muheza, Serikali katika mwaka wa fedha 2011/2012 ilitenga shilingi milioni 302.6 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji katika vijiji vya Ubembe, Kwembosi, na Kisiwani. Aidha, katika mwaka huo, Halmashauri iliidhinishiwa maombi maalum ya shilingi milioni 100.0 ambazo zinatumika kwa ajili ya kuendeleza kisima kilichopo eneo la Polisi Mang’enya. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, kiasi cha shilingi milioni 232.9 zilitengwa na hadi sasa zimetolewa shilingi 170.6 sawa na asilimia 73.3 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji katika kijiji cha Kibanda. Aidha, katika bajeti ya mwaka 2213/14, Serikali imeidhinisha jumla ya shilingi milioni 116.4 na zinatarajia kujenga mradi wa maji ya bomba kutoka katika kisima chenye uwezo wa kuzalisha lita 26,000 kilichoko katika kijiji cha Kigongomawe. Serikali itaemdelea kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kadri fedha zitakavyokuwa zinapatikana. (b) Mheshimiwa Spika, ili kutatua taizo la maji katika Mji wa Muheza, Serikali inapanga kutumia chanzo cha Mto Ziggi ambacho ni cha uhakika. Tayari upembuzi yakinifu umefanyika kupitia Kampuni ya Ushauri ya Misri (Arab Consulting Engineers). 6 5 JUNI, 2013 Baada ya usanifu, gharama zinazohitajika ili kutekeleza mradi huo ni shilingi bilioni 13.4. Andiko la mradi huu limewasilishwa katika Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa ajili ya kufanyiwa kazi ili kupata fedha zitakazowezesha utekelezaji wa mradi wa maji kwa kutumia chanzo cha Mto Ziggi. MHE. HERBERT J. MNTANGI: Mheshimiwa Spika, naombakumshuru sana Mheshimwia Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya swali langu, hata hivyo nina mawili ya nyongeza. Moja, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji alifika Muheza katika kisima hicho cha Polisi Mang’enya, na akaona teknolijia mpya ambayo tumetumia ya kutumia sola kuweza kuwasilisha maji katika maeneo mengi ndani ya Mji wa Muheza. Sasa tumegundua maji katika maeneo mengine makubwa manne, ndani ya Mji wa Muheza, pale Genge na Michungwani, lakini hatua fedha za kuweza kununua teknolojia hiyo mpya. Je, Wizara itatusaidia kuwasiliana na Wizara ya Fedha ili waweze kuleta fedha kwa haraka tuweze kufanikiwa kupata kujenga miundombinu hiyo? (Makofi) Mheshimiwa Spika, la pili, wapo Wamarekani wamefika Muheza kutusaidia katika kutafuta maji, na wamekuja na mashine mpya nzuri ya kisasa ya kiuweza kutafuta na kuchimba na wamefanikiwa katika visima hivyo ambavyo nimevitaja vinne, na wako tayari kutuuzia mashine mashine hiyo kwa shilingi milioni 200 tu, lakini hatuna fedha. Je, Wizara inawez akutusaidia ili tusipoteze nafasi hii ya kuweza kupata mashine hiyo? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages280 Page
-
File Size-