NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Tisa – Tarehe 9 Februari, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Mwaka ya Upimaji wa Utekelezaji wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma kwa Mwaka 2016/2017 (Annual Performance Evaluation Report on Public Procurement Regulatory Authority for Financial Year 2016/ 2017). MHE. YAHAYA O. MASSARE (K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. GEORGE M. LUBELEJE (K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 108 Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapelaka fedha za kutosha kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga ambao umeanzishwa kwa nguvu za wananchi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Azza Hillal Hamad, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kupitia fedha za ruzuku kutoka Serikalini imekamilisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), nyumba moja ya mtumishi pamoja na jengo la kutolea huduma za ushauri nasaha ambalo liko katika hatua ya upauaji. Jumla ya shilingi milioni 365 zilitumika kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa mchanganuo ufuatao:- Ruzuku kutoka Serikali Kuu shilingi milioni 267; mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya shilingi milioni 86; nguvu 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) za wananchi shilingi milioni saba na mchango wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu shilingi milioni tano. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 zimetengwa shilingi milioni 110 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo ambapo kati ya hizo shilingi milioni 40 ni mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi milioni 70 ni ruzuku kutoka Serikali kuu. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2018/2019 zitatengwa shilingi milioni 110 kwa ajili ya kendeleza ujenzi wa hospitali hiyo ambapo shilingi milioni 50 ni mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi milioni 60 ni ruzuku kutoka Serikali Kuu. Serikali itaendeleza ujenzi wa hospitali hiyo kulingana na upatikanaji wa fedha ili wananchi waweze kupata huduma. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Azza Hillal, swali la nyongeza. MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa nikuliza swali hili toka nilivyoingia ndani ya ukumbi huu mwaka 2010. Ujenzi wa hospitali hii umeanza toka mwaka 2007 mpaka hivi tunavyoongea fedha inayoonekana hapo ndiyo ambayo imeshafika katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza, lakini wakati nauliza maswali yangu mawili ya nyongeza, nipongeze Serikali kwa hatua kubwa ambayo wameamua kuchukua katika uboreshaji wa vituo vya afya kikiwemo Kituo cha Afya cha Tinde. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, je, Serikali inawaahidi nini wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuhusu ukamilishwaji wa ujenzi huu kwa kuwa umekuwa ni wa muda mrefu? 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, je, Serikali imeweka mpango gani madhubuti ili kuhakikisha kwamba pindi ujenzi huu wa vituo vya afya unapokuwa umekamilika unaweza kupata wataalam wa kutosha katika majengo yetu ya upasuaji na huduma zingine zinazostahili? Nakushukuru. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri ya Rais TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika na mimi tangu nimemfahamu Mheshimiwa Azza amekuwa akipigania ujenzi wa hospitali, lakini kama hiyo haitoshi ni pamoja na kupigania Vituo vya Afya na Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Naomba kwa pekee nimpongeze kwa jitihada zake hizo na ndizo ambazo zimezaa upatikanaji wa vituo vya afya viwili, kwa maana ya Kituo cha Afya Tinde na Kituo cha Afya Samuye ambacho kimoja ni shilingi milioni 400 na kingine milioni 500. Mheshimiwa Naibu Spika, ukija upande wa maswali yake, anataka ahadi ya ukamilishaji wa hospitali hizo. Kama ambavyo nimekuwa nikijibu hapa, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba tunakamilisha ujenzi wa hospitali 64 katika Wilaya ambazo hazina Hospitali za Wilaya na hasa kwa wananchi wa wilaya yake ambao wameshaonesha moyo kwanza kwa kutenga eneo lakini pia ujenzi umeshaanza na ndio maana OPD imeweza kukamilika. Kwa kadri bajeti itakavyoruhusu hakika naomba nimuhakikishie tutatupia jicho letu kuhakikisha kwamba hospitali hiyo inakamilika. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ametaka kujua juu ya suala zima la hospitali inapokamilika na wataalam wawepo. Naomba nimuhakikishie, ni azma ya Serikali, si suala la kujenga majengo tu, tunataka tujenge majengo ambayo yatumike. Kwa hiyo, pale ambapo ujenzi unakamilika na wataalam watakuwa wamepatikana ili waweze kutoa huduma kwa wananchi waliokusudiwa. (Makofi) 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Desderius Mipata, swali la nyongeza. MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Vijiji vya Kasu, Milundikwa, Katani, Kisula pamoja na Malongwe, Kata ya Kandanse wameamua kujenga Kituo chao cha Afya Kasu na wadau mbalimbali wameonesha kuwachangia ikiwepo Mfuko wa Jimbo. Je, Serikali ipo tayari kuwaunga mkono juu ya juhudi zao hizo za kupata Kituo cha Afya? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ninafahamu Mheshimiwa Mipata na mwenzake Mheshimiwa Keissy katika Wilaya yao kule wamefanya kazi kubwa sana ya kuhamasisha ajenda ya afya na ndiyo maana nilipofika pale nimeona jiografia ya Wilaya ya Nkasi ina changamoto kubwa sana. Hii ndiyo maana katika kipaumbele chetu, kwa kuunga mkono wananchi wa Kasu, tumehakikisha kwamba katika kipindi cha hivi karibuni tutawezesha Kituo cha Afya cha Kasu na Wampembe kuhakikisha kwamba vile vituo vya afya viwili vya maeneo hayo viweze kupata huduma ya upasuaji kwa lengo kubwa kwamba population iliyopo kule na wengine kutoka nchi jirani muweze kuhakikisha mnawa- manage vizuri katika sekta ya afya. Kwa hiyo, hilo tumeliangalia na tunalipa kipaumbele. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa John Heche, swali la nyongeza. MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Tarime tumejitahidi na Mheshimiwa Kandege alikuwepo, tumejenga hospitali kubwa pale ya Wilaya ambayo iko Nyamwaga, tumejenga vituo vya afya karibia vine, kuanzia Nyandugu, Mriba na Sirari ambako ni kituo ambacho Waziri Mkuu alisema kiwe cha mfano nchi nzima. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa shida yetu ni watumishi, ni lini mnatuletea watumishi hasa kwenye Hospitali ya Nyamwaga ambayo tumeshanunua na vifaa ili ile hospitali ianze kuhudumia wananchi wa Tarime ambao wamefanya kazi kubwa pale kuijenga? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maneno kwamba wakifanya vizuri upande wa Upinzani hatuwapongezi, lakini kwa dhati kabisa naomba nipongeze kazi nzuri ambayo imefanywa na wananchi wa Tarime akiwepo na Mbunge Mheshimiwa Heche kwa sababu tumeenda tukatizama kwa macho na kuona ni kusadiki, mmefanya kazi nzuri. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Heche atakubaliana na mimi kwamba katika ziara aliyofanya Mheshimiwa Waziri Mkuu, aliahidi kwamba taratibu zikamilike mara moja ili Hospitali ya Nyamwaga ianze kufanya kazi na tena ni matarajio yetu kwamba muda sio mrefu itakuwa ni miongoni mwa Hospitali za Wilaya. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Josephine Genzabuke, swali la nyongeza. MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kakonko ni kati ya wilaya mpya na mpaka sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya. Eneo hilo la Kakonko limepakana na Mkoa wa Kagera na wananchi wengi wanakuja kutibiwa katika Kituo cha Afya cha Kakonko kwa kuwa hawana hospitali jirani yao. Serikali iliahidi kupeleka shilingi milioni 500, mpaka sasa shilingi milioni 500 hizo hazijapelekwa katika Wilaya ya Kakonko. Nilitaka kujua, je, ni lini Serikali itapeleka milioni 500 ili wananchi wa Kakonko waweze kupata huduma ya matibabu? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Kakonko ni sehemu yenye changamoto kubwa na Mheshimiwa Mbunge nakumbuka hata tulivyokuwa kule kipindi kile tumeona idadi
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages251 Page
-
File Size-