Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA

Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA

Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Kumi na Nne – Tarehe 1 Aprili, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 143 Wananchi Kuchangia Ujenzi wa Maabara Nchini MHE. PAULINE P. GEKUL (K.n.y. MHE. ROSE K. SUKUM) aliuliza:- Utoaji wa Elimu bora ni pamoja na kuwa na Maabara nzuri zenye vifaa vya kutosha na vilivyo bora; kutokana na ukweli huo, Mheshimiwa Rais alitoa agizo la ujenzi wa Maabara kwa kuhusisha michango ya Wananchi hali inayowanyanyasa sana Wananchi hivyo kuwa kero kubwa toka kwa Watendaji wa Vijiji na Kata kwa maagizo ya Mkurugenzi na Wakuu wa Wilaya:- Je, Serikali kupitia agizo la Mheshimiwa Rais imechangia kiasi gani kwa kila Wilaya kama kielelezo cha utekelezaji wa agizo hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rose Kamili Sukum, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ujenzi wa miundombinu ya shule nchini umekuwa unatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali, wananchi na wadau wa maendeleo. Wakati wa ujenzi wa shule nyingi za wananchi zijulikanazo kama Shule za Kata, baadhi ya miundombinu muhimu ikiwemo maabara haikukamilika. Kutokana na umuhimu wa maabara, Mheshimiwa Rais alitoa agizo ambalo kimsingi lilikuwa ni kukumbushia uzingatiaji wa kila shule kuwa na Maabara tatu. Kila Halmashauri ilipaswa kutekeleza kupitia vyanzo vya ndani na wananchi wamekuwa wakishirikishwa kupitia mikutano na vikao katika ngazi mbalimbali ili waone umuhimu wa kushiriki kwa hiari yao. Mheshimiwa Spika, maabara zilizokuwa zinahitajika kujengwa Kitaifa ni 10,389 ili kuwezesha shule zote kuwa na maabara tatu. Hadi kufikia Januari 2015, vyumba vya maabara 4,237 vilikuwa vimekamilika, ambapo Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari, maarufu kama MMES, imechangia jumla ya shilingi bilioni 17.9 na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang‟ imechangia shilingi milioni 273. Aidha, kwa mwaka wa Fedha 2010/2011, Serikali ilitoa shilingi bilioni tatu kwa Halmashauri zote kujenga maabara na Mkoa wa Manyara ulipata shilingi milioni 160 kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Wilaya ya Hanang‟. Wilaya ya Hanang‟ imepata shilingi milioni 80 zilizonufaisha Shule za Sekondari Mulbadaw na Chifu Gejaru. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Spika, ushirikishaji unawafanya wananchi wawe sehemu ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo, waweze kumiliki miradi husika na kuongeza kasi ya mafanikio. Kupitia Bunge lako Tukufu, napenda kuwapongeza sana wananchi wa Mkoa wa Manyara hususan Halmashauri ya Hanang‟ na wananchi wote nchini, kwa kuitikia wito wa Serikali kutekeleza shughuli hii muhimu ya ujenzi wa maabara. Wito kwa Wakurugenzi wote ni kuhakikisha kuwa, uhamasishwaji unafanyika bila kutumia nguvu. MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Niulize maswali mawili ya nyongeza. (i) Kwa kuwa agizo hili au mpango huu wa kujenga maabara ni mpango wa muda mrefu wa Serikali na Chama cha Mapinduzi waliahidi katika Ilani yao ya mwaka 2010; na kwa kuwa agizo hili la Rais lilitoka wakati mgumu katika Mkoa wa Manyara kwa sababu lilitakiwa litekelezwe mwezi Desemba na Januari, wakati Wananchi wako kwenye kilimo; na kwa kuwa Serikali imeshaahidi hapa kwenye Bunge kwamba, miezi hiyo hawatawasumbua Wananchi kwa sababu wanaingia kwenye msimu wa kupeleka watoto shule na msimu wa kilimo:- Ni kwa nini Serikali imepeleka agizo hili mpaka ngazi za Halmashauri, wananchi wanasumbuliwa wakati huu ambao hawana fedha na kwa nini wasisubiri msimu wa mavuno? (ii) Kwa kuwa michango hii ya wananchi haiko regulated katika Halmashauri, ni kijiji tu kinaamua au mtaa unaamua kiasi chochote. Mfano, Kijiji cha Dareda katika Wilaya ya Babati na Kijiji cha Dudie wana michango miwili tofauti; Dudie wanachangisha shilingi 40,000 mpaka shilingi 60,000 wakati Dareda siyo zaidi ya shilingi 10,000. Kwa nini Serikali sasa isitoe mwongozo kwenye Halmashauri zetu kuhusu michango ya wananchi katika miradi ya maendeleo badala ya kuwaacha wananchi wakionewa kwa muda mrefu na watendaji? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, kwa programu hii ya ujenzi wa maabara na Wilaya ya Hanang‟; kwanza, napenda nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Mbunge wa Hanang‟ kwa mchango mkubwa alioutoa kupitia mfuko wake wa Jimbo kwa ajili ya kuchangia vifaa vya ujenzi vya bati, saruji na nondo, ambazo zimesasidia sana kujenga maabara zetu kwa kiasi kikubwa. Nakushukuru sana Mheshimiwa Nagu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nataka nieleze kama ambavyo nimejibu kwenye jibu la msingi kwamba Mheshimiwa Rais alipotoa maelekezo, halikuwa agizo ambalo kila mmoja alitakiwa lazima akawasumbue wananchi. Yeye alikumbushia ujenzi wa Maabara kukamilika kwenye Shule zetu za Sekondari za Kata na kwa hiyo, kila Halmashauri ilitakiwa itafute mbinu mbalimbali na hasa kupitia vyanzo vyao vya ndani; hayo ndiyo malengo. Bado Halmashauri ilikuwa na uwezo wa kuwahamasisha wananchi na wadau wote wa elimu kuchangia Mpango huo na haukuwa wa lazima, ilikuwa ni hiari. Maeneo mengi kila Halmashauri ina utofauti wa michango hiyo kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kwa sababu kila Halmashauri ilikuwa inaenda kuomba ridhaa ya wananchi, wananchi wanajipangia kutokana na uwezo wao wa kuchangia na ndiyo sababu kumekuwa na utofauti huo. Kama kuna mahali kulitumika utaratibu tofauti, hilo siyo agizo la Mheshimiwa Rais na wala siyo msisitizo wa Serikali katika kukamilisha maabara hizo. Kwa hiyo, bado tunaagiza kama ambavyo nimeeleza kwamba wakurugenzi watakapoamua kuwaona Wananchi, kuwaomba kuchangia ujenzi wa maabara ili wakamilishe, hakuna haja ya kutumia nguvu. Wananchi wenyewe wataamua kuchangia na viwango watajipangia wenyewe, kitu cha msingi Mkurugenzi aweke utaratibu wa kuratibu jinsi ya kuupata mchango huo. Huo ndiyo utaratibu ambao tumeendelea kuutumia kwenye maeneo mengi. MHE. AMINA M. MWIDAU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Maabara ni muhimu sana na sote tunazihitaji, lakini ni kweli kabisa uchangishwaji wa Maabara hizi kuna manyanyaso ya haki ya juu sana kwenye maeneo yetu. Kwa kuwa Serikali inatambua hali za Wananchi wake mpaka kuna mradi huu wa TASAF wanapewa pesa Wananchi sasa hivi. Nataka kujua Serikali inazisaidiaje kaya maskini hasa ukiangalia kama kwetu Pangani kwa kweli watu ni maskini sana na wanachangishwa kwa kichwa. Je inazisaidiaje kaya ambazo hazina uwezo kuchangia maabara? Kwa nini zile pesa za TASAF zisiwekwe kwenye maabara? (Makofi) SPIKA: Wanasema if you think education is expensive try ignorance. (Kicheko) Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu! NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, bado nirudie na kusisitiza kwamba, uhamasishaji wa ujenzi wa Maabara ambao Mheshimiwa Rais alikumbushia Maabara hizo kukamilishwa kwa Halmashauri zetu, kama Halmashauri ilikuwa inakusanya michango kwa Wananchi, ilikuwa kwanza watoe elimu kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa michango hiyo kwa ajili ya kukamilisha Maabara hizo na Wananchi wenyewe waamue viwango kulingana na mapato yao kwenye maeneo yao ili pia jambo hilo liweze kukamilika. Mimi mwenyewe nimetembelea Bukoba, nimeona namba ambavyo Halmashauri ya Bukoba pale Manispaa, walivyokuwa wakifanya kazi ya kuhamasisha Wananchi kuchangia na Wananchi wenyewe walikuwa wanakuja kuchangia, wengine wanaleta mifuko 200 kwa hiari yao wengine ng‟ombe, wenyewe wanatamka kwa hiari yao. Kwa hiyo, msisitizo ulikuwa ni Wananchi kushirikishwa na wafanye maamuzi wao wenyewe namna bora kulingana na kipato chao wanachangia kwa kiasi gani. Bado Serikali imesimamia hilo na kama ambavyo nimeagiza kwenye jibu langu la msingi kwa Wakurugenzi wote nchini, kama wanahitaji mchango huo kutoka kwa Wananchi, kwanza, wakawaelimishe umuhimu. Pili, wawachie Wananchi wenyewe kufanya maamuzi ya kiwango gani cha kuchangia na wao Halmashauri waratibu tu utaratibu wa kuzipata zile fedha. Hayo ndiyo maelekezo ya Serikali na ndiyo tunachofanya. Sasa suala la fedha ya TASAF itumike; TASAF ni utaratibu tofauti na jambo hilo ni lazima tukae pia na Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo inashughulikia masuala ya TASAF na kupeleka migao kwenye Halmashauri. Mara nyingi Miradi yote ya TASAF inatokana na wananchi wenyewe kuamua. Mheshimiwa Spika, sasa kama fedha zimeshaenda awamu iko na wananchi wameamua kupeleka fedha hizo za TASAF kwenye maabara, huo uhuru umetolewa na maeneo mengi tumeona wakiamua kujenga madarasa, kujenga nyumba za walimu na tumeona mchango huo. Kwa hiyo, bado Serikali imeendelea kuhamasisha Wakurugenzi michango hiyo iwe ni ya hiari na wala siyo ya nguvu. (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU): Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru sana Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa majibu yake mazuri sana. Napenda nilieleze Bunge lako Tukufu kwamba, TASAF iliona sana umuhimu wa elimu katika kuondoa umaskini Tanzania na ndiyo maana Awamu ya Kwanza na ya Pili ilikuwa imejielekeza kwenye kutoa huduma ikiwemo elimu. Katika Awamu hii ya Tatu, TASAF inawawezesha kaya maskini kuondokana na umaskini kwa kupewa fedha kwa ajili ya lishe, kwa ajili ya watoto wao kwenda shule na kwa ajili ya watoto kupelekwa zahanati au akina mama wajawazito kwenda zahanati. Kwa hiyo, TASAF bado inaona umuhimu wa elimu, lakini haiwezi kuwa tu kwenye

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    158 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us