Tarehe 8 Novemba, 2018

Tarehe 8 Novemba, 2018

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Tatu – Tarehe 8 Novemba, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Tatu na leo ni Kikao cha Tatu. Katibu. NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu karibu. (Makofi) Namwita Mheshimiwa Lucia Michael Mlowe, Mbunge wa Viti Maalum, uliza swali lako. MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tatizo kubwa sana la kukosa soko la mahindi hasa kwa mikoa ile inayolima mahindi kwa wingi. Je, Serikali inatoa tamko gani kwa wananchi hawa ambao mpaka sasa hivi wamekata tamaa kabisa ya kulima mahindi? (Makofi) 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Swali langu la pili, naomba kujua... SPIKA: Swali moja tu. MHE. LUCIA M. MLOWE: Aah, aHsante Mheshimiwa Spika. SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wakulima wa mahindi. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lucia, Mbunge, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, upo ukweli kwamba wakulima wetu wa zao hili la mahindi, zao ambalo linalimwa sehemu kubwa sana nchini kama zao la chakula na pia kama zao la biashara, tumekuwa na upungufu wa masoko yake. Awali unatambua kwamba tumeshajadili sana hapa ndani ya Bunge tutumie mfumo gani wa kuuza zao hili ambapo pia huku ndani inaonekana tunajitosheleza kwa chakula, lakini pia nyakati kadhaa kumekuwa na maeneo ambayo yamekosa chakula na kwa hiyo, tunatumia zao hilo hilo kwa ajili ya chakula. Mheshimiwa Spika, Waziri wa Kilimo alitoa maelekezo na tamko kwamba tunaruhusu wakulima kuuza na kutafuta masoko ya nje, lakini tunaruhusu pia nchi jirani ambazo zina upungufu wa chakula kuja nchini kununua chakula. Jambo muhimu ambalo tunataka kwenye eneo hili na tunalisimamia, pamoja na kutoa ruhusa hiyo, nchi lazima itambue tunatoa mahindi kiasi gani? Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Kilimo ameweka utaratibu kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya walioko kwenye maeneo ambako mahindi haya yanatoka ili yule ambaye amepata soko nje au kama kuna mkulima amepata mnunuzi kutoka nje, basi kuwe na utaratibu wa kutoa taarifa au kuripoti kwa Mkuu wa Wilaya mwenyeji, tuwe na takwimu ya kiasi gani cha chakula kimetoka nje. Kama kimeuzwa, tuwe na taarifa za bei za upande huo ili tujiridhishe 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kwenye taarifa zetu kwamba zao hili kwa mwaka huu wa kilimo tumeingiza dola kiasi fulani cha fedha ndani ya Serikali. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, muhimu zaidi ni kwamba kibali cha kuuza nje kipo na kibali cha kuruhusu mataifa ya nje kuja ndani kipo. Wizara inaendelea kufuatilia pia mahitaji ya chakula cha ndani ili tusije tukatoa chakula chote Taifa likabaki halina chakula tukaanza kuhangaika baada ya kuwa tumetoa chakula nje. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, maeneo yote yanayolima mahindi, kwanza, Serikali kupitia Kitengo chetu cha NFRA kilitoa fedha siyo nyingi, lakini tulienda kununua katika maeneo mbalimbali na bado wakulima wana mahindi mengi. Kwa ruhusa hii, sasa mataifa ya nje na sisi tunaweza kwenda kuuza nje na utaratibu huo unaendelea kusimamiwa na Wizara ya Kilimo kupitia Kitengo chake cha NFRA. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Mlowe, swali la nyongeza. MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi tena niweze kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Spika, kutokana na tatizo hili lililojitokeza la ukosefu wa soko la mahindi na kusababisha wananchi wauze kwa bei ya chini sana na kukosa pesa za kuweza kununulia pembejeo, je, Serikali sasa iko tayari kushusha bei ya pembejeo kwa wananchi hawa? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri Mkuu tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba tena nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Lucia, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, suala la gharama ndogo au upatikanaji kwa bei ndogo ya pembejeo limefanyiwa kazi vizuri sana na Wizara. Nasema hili kwa sababu awali mbolea 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tulikuwa tunaagiza randomly, kila mmoja anaagiza na kuleta nchini na kwa hiyo kila mmoja alikuwa anaweza kuuza kwa bei ya juu sana, lakini Wizara imekuja na mkakati mzuri wa kuagiza kwa pamoja. Tumetafuta mzabuni mmoja awe analeta mbolea yote nchini, yeye awe ndiyo anasambaza kwa wenzake kwa udhibiti wa bei ambao umewekwa na Wizara. Mheshimiwa Spika, sasa hivi tunapata mbolea karibu asilimia 40 ya bei ya awali ambayo ni ndogo ukilinganisha na zamani. Bado tuna mjadala wa namna bora ya kufikisha pembejeo kwa mkulima, ikiwemo na mbolea kule kijijini ili aipate kwa urahisi lakini kwa bei ile ile ambayo sisi Serikali tunasema ni muhimu mfuko wa mbolea wa aina hii upatikane kwa kiasi hiki. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Wizara imeendelea kuratibu kupatikana kwa mbolea kwa bei nafuu lakini kwa wakati ambapo pia wao wameshaamua na sasa wanasimamia kupeleka mbolea kwenye maeneo kulingana na msimu angalau mwezi mmoja, miwili kabla ya msimu haujaanza. Kwa hiyo, tunaendelea kuratibu vizuri kumwezesha mkulima aweze kupata pembejeo ikiwemo mbolea kwa bei rahisi, kwa wakati na pia katika mazingira ambayo siyo magumu sana kwa sababu wafanyabiashara wako tayari na wameanza kuleta pembejeo pia. Mheshimiwa Spika, mpaka leo hii kwa kumbukumbu zangu kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Kilimo, tumeshaleta pembejeo kwa maana mbolea zaidi tani 260 ambazo zinakaribia asilimia 60 ya mahitaji ya nchi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge na wakulima wote wa mahindi na wakulima wa mazao karibu yote nchini, Wizara inaendelea kuratibu vizuri upatikanaji wa pembejeo wa kila zao ili wakulima waweze kufanya kazi yao ya kilimo katika mazingira rahisi. Ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Emanuel Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kabla ya swali langu, naomba nitoe pongezi kwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi inavyoshughulikia mambo mbalimbali na hasa hivi karibuni lile janga la kuzama kwa MV... SPIKA: Mheshimiwa Mwakasaka, maswali kwa Waziri Mkuu ni moja kwa moja swali ili tuweze kuokoa muda. MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri Mkuu swali langu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tatizo kubwa la malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi au niseme watumishi kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya likizo zao. Sijui Serikali imejipangaje kutatua tatizo hili la muda mrefu? (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anazungumzia matatizo makubwa ya malimbikizo ya watumishi na ulipaji wake. Ni kweli kwamba Serikali imejikita katika kuratibu maslahi ya watumishi wetu ikiwemo kupanda madaraja, masuala ya mishahara na pia hata malimbikizo ikiwa ni sehemu ya madeni ya watumishi. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Fedha ilitenga fedha kwa ajili ya kulipa malimbikizo haya ambayo yanatokana na kupanda kwa madaraja, lakini pia madeni mengine ya utumishi kwenye sekta hiyo kama alivyosema ya likizo na kumbukumbu zangu zinaonesha na juzi nilikuwa Lushoto nilizungumza na wafanyakazi, niliwapa takwimu kwamba kuanzia mwezi wa Julai mpaka Septemba, 2018 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Serikali ilishalipa madeni mbalimbali yakiwemo malimbikizo ya watumishi ya shilingi bilioni 184.9. Hiyo ikiwa ni awamu ya tatu ya malipo mbalimbali yaliyoanza toka mwaka 2017. Kwa hiyo, lazima hapo sasa watumishi waone kwamba Serikali inaendelea kulipa malimbikizo mbalimbali ya watumishi. (Makofi) Mheshimiwa Spika, pia suala la likizo ni sehemu ya malipo ambayo TAMISEMI inaratibu vizuri kwa kupokea taarifa ya idadi ya watumishi kwa Idara kutoka kila Halmashauri nchini kwa wanaokwenda likizo miezi mitatu/minne kabla. Serikali kutokana na fedha ambayo imetenga, inapeleka fedha kwenye Halmashauri hiyo, kwa hiyo, ni juu ya Afisa Utumishi na Mkuu wa Idara kuratibu watumishi wangapi wanakwenda likizo. Mheshimiwa Spika, Idara nyingine hazina shida, shida tunayo sana katika sekta ya elimu na sekta ya afya ambazo zina watumishi wengi. Kwa hiyo, Wakuu wa Idara na Maafisa Utumishi wetu ndani ya Halmashauri na Wizara wamepewa maelekezo maalum ya kuratibu likizo zao vizuri ili kila mmoja aweze kulipwa nauli ya kwenda kwake. Mheshimiwa Spika, kwenye likizo uratibu huo unaendelea. Mkakati wa Serikali ni kwamba kama likizo inaanza tarehe 1, basi tunataka tarehe 30 mtumishi apate hundi yake na malipo ya nauli kwenda nyumbani kwake ili tarehe 1 aanze likizo yake. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali imejipanga vizuri, kwanza, tumedhibiti kuzalisha madeni, lakini pili, yale machache yaliyopo, yote tunayalipa. Kwa utaratibu huu, yale ya mwanzo yote ndiyo hayo ambayo nimesema tumelipa shilingi bilioni 184.9 ili kuweza kukamilisha kulipa madeni yote ya watumishi. Zoezi hili linakuja baada ya kuwa tumekamilisha utafiti au uthamini kwa maana ya uhakiki wa madeni mbalimbali. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunayo takwimu ya madeni na tunaendelea kuwalipa. Watumishi nchini 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) waendelee kuiamini Serikalini yao, waendelee kuamini utaratibu tunaotumia ili kutuwezesha Serikali kulipa madeni kwa wale wote wenye stahiki zao. (Makofi) SPIKA: Ahsante

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    197 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us