MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita

MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Sita – Tarehe 27 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo ni Kikao cha 36. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CATHERINE V. MAGIGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI) Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu utekelezaji na Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. TUNZA I. MALAPO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA MADINI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza Malapo, tunakushukuru. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Azza Hilal, Mbunge wa Viti Maalum - Shinyanga. Na. 297 Hitaji la Mabweni Shule za Sekondari-Shinyanga MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga Mabweni katika shule za sekondari zilizoanzishwa Kitarafa ili kuwasaidia watoto wa kike waweze kupata elimu iliyo bora Mkoani Shinyanga? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Selemani Saidi Jafo, tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Azza Hilal Hamad, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa shule za sekondari kuwa na mabweni ili kuboresha elimu. Kwa sasa mpango wa Serikali ni kuziboresha shule za sekondari zilizopo ambapo kipaumbele ni katika ujenzi wa miundombinu muhimu wa vyumba vya madarasa, vyoo mabweni na maabara ili kuboresha mazingira ya kufundishi na kujifunzia. Ukarabati wa shule hizo unahusisha miundombinu ya mabweni hasa kwa watoto wa kike ili kuweza kupata elimu iliyo bora. Hadi sasa, shule za sekondari 1241 zimejengewa mabweni kati ya shule za sekondari 3634 zinazotumia ruzuku ya Serikali Kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri na mchango wa jamii. Serikali itaendelea kujenga mabweni na kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kadiri bajeti itakavyoruhusu. SPIKA: Mheshimiwa Azza Hillal swali la nyongeza tafadhali. MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza maswali ya nyongeza. Awali ya yote niipongeze sana Serikali kwa kazi kubwa ambayo inaifanya katika kuhakikisha inaboresha miundombinu katika shule zetu. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza:- Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; Je, Serikali iko tayari sasa kuhakikisha inajenga mabweni katika shule zetu zilizoanzishwa kimkakati zaidi katika shule ya sekondari Samuye, Kizumbi, Isagenhe na Ukenyenge zilizopo katika 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mkoa wa Shinyanga kwa sababu Wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali mrefu na hivyo kukumbana na vishawishi vingi barabarani na kupelekea kupanga mitaani? Mheshimiwa Spika, swali la pili; Je, Serikali hamuoni sasa ni wakati muafaka wa kuweza kufikiria kutokuwapangia shule zilizoko mbali wanafunzi hawa kwa kuwa kila Kata sasa hivi ina shule? Mheshimiwa Spika, nakushukuru. SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Jafo. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kwanza nikiri, Mheshimiwa Azza takribani wiki mbili au tatu zilizopita alikuwa akinijulisha suala zima la changamoto ya miundombinu ya elimu katika Mkoa ule wa Shinyanga na nilimuhakikishia kwamba Serikali tutafanya kila liwezekanalo, lile linalowezekana tutaenda kulifanyia kazi alichanganye pamoja na ajenda hiyo ya elimu pamoja na ajenda ya afya. Mheshimiwa Spika, hata hivyo naomba niseme kwamba Serikali tutaangalia kila kinachowezekana katika maeneo uliyoyaainisha lile litakalowezekana kwa sasa tutaweza kulifanya. Lakini ni azma ya Serikali kuhakikisha tunapambana miundombinu inaimarika kama tulivyofanya pale sekondari ya Tinde ambapo Mbunge tumeenda wote pamoja pale kwa ajili ya kuona eneo gani lazima tufanye hilo. Mheshimiwa Spika, suala la kutowapangia mbali kwa vile kila Kata sasa ina shule, jambo hili ndiyo kielelezo chetu ni kwamba kama katika Kata hasa zile zetu ambapo kama kuna vijana wamefaulu katika eneo lile ni vyema sasa watoto wakapangiwa kwa karibu zaidi kuepusha usumbufu huo mabao Mheshimiwa Mbunge ulizungumza. Kwa hiyo, 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tumelichukua Serikali na tutalitolea maelekezo katika maeneo mbalimbali. SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Waziri kivuli wa Elimu. MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, pamoja na juhudi za Serikali kuhakikisha kwamba wanajenga mabweni, utakubaliana nami kwamba baadhi ya mabweni hayo yamekuwa yakiungua mara kwa mara na hivi karibuni shule ya Ashira mabweni yake mawili ya wasichana yameungua. Je, Serikali mna utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba kunakuwa na ulinzi katika shule hizo ili hii rasilimali kubwa ambayo imeshatumika ya fedha kujenga mabweni hayo iweze kulindwa? Mheshimiwa Spika, ahsante. SPIKA: Pole sana kwa sekondari ya Ashira. Majibu Mheshimiwa Waziri wa Nchi, tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Dada yangu Susan. Mheshimiwa Spika, ni kweli na niwape pole Wananchi wote wa Tanzania kwa sababu watoto wale, juzi nilikuwepo Ashira ile shule wkeli imeungua lakini ukija kuangalia taarifa ya awali inaonyesha kwamba ni hujuma tu kwa sababu yale mabweni mawili hayaungani na siyo kwamba kulikuwa na short ya umeme. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni kweli inawezekana maeneo mengine kuna hujuma na nawaomba niwaeleze Serikali juzi nilisha-deploy timu yangu ya Mainjinia iko pale tokea jana inafanyakazi na leo hii haraka iwezekanavyo ndani ya wiki mbili, tatu tuanze ukarabati wa yale majengo kwa sababu siyo muda mrefu vijana wa form five wengine tutawaingiza katika maeneo yale. Kwa hiyo, tutafanya 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ukarabati wa shule ile yote kwa ujumla wake kuhakikisha inarudi Ashira katika hali yake ya kawaida. Mheshimiwa Spika, lakini hata hivyo ni maelekezo yetu sasa kipaumbele suala zima la walinzi na hasa kuangalia usalama wa shule zetu nini kifanyike kwa sababu tunatumia fedha nyingi sana, haiwezekani watu wenye nia mbaya wakahujumu juhudi hii kubwa ya Serikali na Wananchi wake kwa ujumla. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa sababu ya muda, naomba tuendelee na Viwanda na Biashara swali la Mheshimiwa Maria Ndila Kangoye. Mheshimiwa Maria Na. 298 Sekta Binafsi Kuanzisha Viwanda Vikubwa na vya Kati MHE. MARIA N. KANGOYE aliuliza:- Serikali iliahidi kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda vikubwa na vya kati na kuweka utaratibu wa kuvilinda dhidi ya viwanda vya nje. (a) Je, Serikali imefikia wapi katika zma hii ambayo ni mwelekeo wa kufikia uchumi wa kati na utoaji ajira hasa kwa vijana? (b) Je, Serikali imeweka mkakati upi ili kuweza kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha kupunguza gharama za uwekezaji na uendeshaji wa viwanda? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Eng. Stella Martin Manyanya, tafadhali. NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maria Ndila 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Kangoye Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, jukumu la Serikali kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda vikubwa na vya kati ni la msingi na endelevu. Serikali imeendelea kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika viwanda kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania yaani TIC na mamlaka ya kuendeleza maeneo huru ya uzalishaji kwa ajili ya kuuza nje yaani EPZA. Uhamasishaji huo unaambatana na kutoa vivutio mbalimbali ikiwemo misamaha ya kodi katika mitambo na mshine zinazotumika kwneye uzalishaji. Aidha, Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) limekuwa likihamasisha na kusaidia uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati ambavyo ni msingi wa maendeleo ya viwanda vikubwa kupitia mafunzo na uwezeshaji wa kiufundi na mitaji. Mheshimiwa Spika, pamoja na niliyoeleza katika swali namba 4404 lililojibiwa tarehe 07 Mei, 2019, ili kulinda viwanda vya ndani dhidi ya ushidani usio wa haki, Serikali kupitia Tume ya Ushindani (FCC) na Shirika la viwango Tanzania yaani TBS na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vimekuwa vikidhibiti uingizaji wa bidhaa hafifu, bandia na zinazoingia kwa njia zisizo rasmi bila kulipiwa kodi. Vilevile Serikali imekuwa ikitoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya bidhaa za ndani na kutozwa zaidi baadhi ya bidhaa zinazoingizwa kutoka nje. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa mazingira bora ya biashara na uwekezaji ni kichocheo muhimu kwa maendeleo ya viwanda Nchini. Kwa kuzingatia

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    271 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us