7 MEI, 2020 BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 7 Mei, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Mchana) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa naomba tukae. Katibu. NDG. RAMADHANI ABDALLAH -KATIBU MEZANI HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Hotuba ya Bajeti ya Wizara na Randama ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. MHE. TIMOTHEO P. MNZAYA - (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. 1 7 MEI, 2020 SPIKA: Ahsante sana. Katibu ! NDG. RAMADHANI ABDALLAH -KATIBU MEZANI MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 222 Halmashauri Kutenga 10% kwa ajili ya Wanawake na Vijana MHE. GODFREY W. MGIMWA aliuliza:- Ilani ya Chama cha Mapinduzi inaeleza wazi juu ya kuwawezesha wananchi kiuchumi hasa kwenye suala la ujasiriamali:- Je, Serikali ipo tayari kutoa agizo la msisitizo kwa Halmashauri zote nchini kutenga fedha za asilimia 10 kwa wanawake na vijana bila kukosa kila mwaka kama inavyotakiwa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Godfrey William Mgimwa, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo;- Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290 kwa kuongeza Kifungu cha 37A(1) – (4) kinachoelekeza Halmashauri zote kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Aidha, ili kuimarisha usimamizi wa Sheria, Waziri mwenye dhamana ametunga Kanuni za usimamizi wa utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo zilizotangazwa kwenye Tangazo 2 7 MEI, 2020 la Serikali Na. 286 la tarehe 5 Aprili, 2019. Hivyo, suala la mikopo hiyo kwa sasa linasimamiwa kwa mujibu wa sheria tofauti na awali. Na. 223 Kituo cha Afya Kata ya Ulowa – Ushetu MHE. LUCY T. MAYENGA aliuliza:- Serikali ilitenga fedha kujenga Kituo cha Afya eneo la Nyalwelwe katika Kata ya Ulowa, Wilayani Ushetu:- Je, nini sababu ya kutopelekwa fedha hizo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lucy Thomas Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali imetumia jumla ya Shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu na Kituo cha Afya Ukene katika Halmashauri hiyo. Mpango wa Serikali ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya katika maeneo yaliyobaki kikiwemo Kituo cha Afya cha Ulowa kadri upatikanaji wa fedha utakavyoruhusu. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kawaida huwa inapokea vipaumbele vya vituo vya kupeleka fedha kutoka kwenye Halmashauri na Mikoa na sio sahihi kuwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI huwa inachagua maeneo ya kupeleka fedha. Kwa mwaka 2020/2021, tumetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha jumla ya maboma 555 ya Zahanati na Vituo vya Afya kwenye Halmashauri 184 na Halmashauri zote tayari zimewasilisha Vituo vyao vya kipaumbele. Kwa Halmashauri ya Ushetu wao wamewasilisha maboma ya Zahanati za Bugomba A, Makongoro na Nshimba. Sina 3 7 MEI, 2020 taarifa kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI iliwahi kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya kwenye Eneo la Nyalwelwe. Na. 224 Vijana Wanaohifadhi Kasa MHE. ANGELINA A. MALEMBEKA aliuliza:- Suala la ukusanyaji mapato ni la Muungano:- (a) Je, ni lini Serikali itaunga mkono juhudi za vijana wa Nungwi Mnarani Kaskazini Unguja ambao wanahifadhi Kasa? (b) Kwa kuwa wageni mbalimbali hutembelea eneo hilo na kulipa pesa kidogo: Je, Serikali haioni umuhimu wa kutoa ruzuku ili kuboresha shughuli hiyo na Serikali kujipatia mapato kwa kazi hiyo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Serikali inatambua juhudi na michango ya makundi mbalimbali yanayoshiriki katika kuchangia pato la Taifa ikiwemo kundi la vijana wa Nungwi Mnarani, Kaskazini Unguja ambao wanahifadhi Kasa. (b) Ofisi imepokea ushauri wa Mheshimiwa Angelina Adam Malembeka na kuahidi kulifanyia kazi kwa kuliwasilisha suala hili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ili iweze kuangalia uwezekano wa kutoa ruzuku na kushauri kuongezwa kiingilio kwa ajili ya kuboresha shughuli ya uhifadhi na hatimaye kuimarisha mapato. 4 7 MEI, 2020 Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Malembeka kuwa, moja ya vipaumbele vya Serikali zetu mbili ni kuhakikisha inashajihisha makundi yote ambayo yanajitoa katika kuchangia pato la Taifa kwa namna moja au nyingine ikiwemo kundi la vijana. Na. 225 Wajawazito Wanaoenda Kliniki bila Wenza MHE. ZAINAB M. BAKAR aliuliza:- Kumekuwa na tabia ya baadhi ya zahanati kutotoa huduma kwa akinamama wajawazito wanapoenda kuanza kliniki bila ya wenza wao:- Je, Serikali haioni kwamba tabia hii inaendeleza vifo kwa wajawazito kwa kukosa huduma hiyo? WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zainab Mussa Bakar, Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kuimarisha Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto ikiwemo huduma kwa akinamama kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Aidha, Serikali imeendelea kutoa huduma kwa akinamama wakati wa ujauzito katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya, zikiwa ni pamoja na kupimwa wingi wa damu, shinikizo la damu, magonjwa mbalimbali kama Malaria, UKIMWI na Kaswende. Mheshimiwa Spika, lengo ni kutambua dalili za hatari au magonjwa wakati wa ujauzito na kuweza kuchukua hatua stahiki mapema ili kuzuia matatizo yatokanayo na 5 7 MEI, 2020 uzazi. Vilevile, Serikali inasisitiza wajawazito wote kuhudhuria kliniki mapema wakiwa na wenza wao ili kuweza kupata huduma hizi ndani ya muda muafaka. Mheshimiwa Spika, kulingana na Sera ya Afya ya mwaka 2007, huduma za afya ya uzazi hutolewa bure bila malipo na huduma hizi hutolewa muda wote katika vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, huduma hizi hutolewa kwa kila mjamzito bila kujali kama amekwenda na mwenza wake au hakwenda. Hata hivyo, Serikali inasisitiza kwamba ni vyema mjamzito akaambatana na mwenza wake ili wapate elimu ya afya kwa pamoja na ikibidi wapate baadhi ya vipimo kwa pamoja ili kuweza kuhakikisha afya bora ya mtoto aliyeko tumboni. Katika eneo hili la utoaji huduma kwa wanawake wakati wa ujauzito (Antenatal Care). Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefanikiwa kuongeza kiwango cha akinamama wajawazito 1,744,668 waliohudhuria kliniki wakati wa ujauzito, ambapo wajawazito 1,343,228 walitimiza mahudhurio manne au zaidi (ANC4+) sawa na asilimia 77 ikilinganishwa na asilimia 41 kwa mwaka 2015/2016 wakati Serikali ya Awamu ya Tano ikiingia madarakani. Hii ni kutokana na huduma nzuri zinazopatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo watoa huduma za afya wanawahudumia akinamama wajawazito bila kujali kama wameenda na wenza wao ama hawakwenda nao. Aidha, Serikali inaendelea kuwasisitiza wanaume juu ya umuhimu wa kuwasindikiza wenza wao pindi wanapohudhuria kliniki ya ujauzito. Na. 226 Mradi wa Maji wa Mabokweni Hadi Chongoleani MHE. MUSSA B. MBAROUK aliuliza:- Miongoni mwa Miradi ya Maji Vijijini ya Vijiji Kumi (10) kwa kila Halmashauri ni pamoja na Mradi wa Maji wa 6 7 MEI, 2020 Mabokweni, Kiruku, Mpirani, Bwagamoyo hadi Chongoleani; Mradi huu hautoi maji na wananchi wanaendelea kutaabika:- Je, tatizo ni nini? WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji Mabokweni uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Tanga ulisanifiwa kuhudumia vijiji/ mitaa mitano (5) ya Mleni, Kibafuta, Mpirani, Ndaoya na Chongoleani. Mradi huu ambao unagharimu kiasi cha Sh.2,412,977,490.00 utakapokamilika utawapatia huduma ya majisafi na salama wananchi wapatao 15,750. Mpaka sasa matenki mawili (water sump & storage tank) yamejengwa, ujenzi wa nyumba ya pampu na ufungaji wa pampu na umeme pamoja na ujenzi wa vituo 24 vya kuchotea maji umekamilika. Mheshimiwa Spika, hivi sasa, Serikali kupitia Wizara ya Maji imeukabidhi mradi huo kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiijini Tanga kwa kuzingatia Sheria ya Maji Na.5 ya mwaka 2019 kwa ajili ya kuukamilisha na hatimaye kusimamia uendeshaji ili wananchi wanufaike na mradi huo. Hadi sasa, wananchi wapatao 2,500 wa Vijiji vya Kibafuta na Kiruku wanapata huduma ya maji kufuatia kuunganisha maji katika vituo vitano vilivyopitiwa na mtandao. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unatekelezwa kwa kutumia Wataalam wa ndani (Force Account) ili kukamilisha mradi huo kwa wakati na kwa gharama nafuu. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2020. 7 7 MEI, 2020 Na. 227 Mradi wa Maji wa Igongwi MHE. EDWARD F. MWALONGO aliuliza:- Mradi wa Maji wa Igongwi unaotarajiwa kuhudumia Vijiji vya Kitulila, Luponde, Njomlole Uwemba, Ikisa na Madobole umechukua muda mrefu kukamilika:- Je, nini kauli ya Serikali kuhusu mradi huu muhimu kwa wananchi? WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edward Franz Mwalongo, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji Igongwi ni miongoni mwa miradi ya maji iliyoanza kutekelezwa katika Programu ya Sekta ya Maji kabla ya kukabidhiwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Njombe. Mradi huu unajumuisha Vijiji vya Kitulila, Luponde, Njomlole, Uwemba, Ikisa, Madobole, Luvuyo na Madope. Mradi wa Maji wa Igongwi ulipangwa kutekelezwa katika vipande vitano (Lot one hadi Lot five) na hadi sasa umefikia asilimia 63.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages220 Page
-
File Size-