Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 3 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA UCHUKUZI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA UCHUKUZI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Juu ya Wizara ya Uchukuzi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 358 Kuimarisha Huduma Kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mufindi MHE. MAHMOUD H. MGIMWA aliuliza:- Hospitali ya Wilaya ya Mufindi ipo karibu sana na Barabara Kuu na inahudumia watu wengi sana wakiwemo Wakazi wa Mufindi wanaotumia hiyo Barabara Kuu hasa yanapotokea matatizo ya ajali, hali ha kuwahudumia wanaokumbwa na ajali hizo huwa ngumu sana hospitalini hapo:- Je, Serikali haioni kuwa ni wakati mwafaka wa kuboresha na kuongeza huduma muhimu katika hospitali hiyo ili iweze kutoa huduma za uhakika kwa wanaokwenda kupata huduma kwenye hospitali hiyo; na je, ahadi hiyo itatekelezeka lini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mahmoud Hassan Mgimwa, Mbunge wa Mufindi Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuwa, Hospitali ya Wilaya ya Mufindi ipo karibu na Barabara Kuu na inahudumia wahanga wengi wa ajali kwenye maeneo hayo. Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekuwa ikiboresha huduma mbalimbali katika 1 Hospitali hiyo ili iweze kukidhi changamoto zinazojitokeza kwa kuhakikisha huduma zote muhimu katika hospitali zinakuwepo ikiwemo:- (i) Huduma katika chumba cha upasuaji kitakachotoa huduma saa 24; (ii) Huduma ya X-ray na Ultra Sound na kutoa huduma muda wote; (iii) Huduma ya maabara; (iv) Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) muda wowote; na (v) Huduma kwa Wagonjwa wa Ndani katika Wodi ambazo zinatoa huduma kuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 150. Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kutimiza azma hiyo, Halmashauri imeanza mchakato wa ujenzi wa wodi ya wazazi na kuongeza chumba cha upasuaji (Theatre), ambacho kitapunguza msongamano katika chumba kilichopo. Halmashauri imetenga shilingi milioni 242 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya akina mama katika kipindi hiki tulichonacho. Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri imeweka mpango wa kusomesha watumishi katika fani mbalimbali za afya ili kuongeza wataalam na kuimarisha huduma zinazotolewa. Mpango uliopo unawahusisha watumishi 11, ambao wapo masomoni wakisomea Shahada mbalimbali wakiwemo saba wa udaktari wa binadamu, watatu wakisomea shahada ya uuguzi na mmoja akisomea shahada ya kwanza ya dawa. Kati ya hao ni watumishi watano wanatarajiwa kuhitimu masomo yao mwaka 2011. MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri:- (i) Serikali ina mpango gani wa kupeleka Madaktari Bingwa katika Wilaya ya Mufindi? (ii) Kwa kuwa wodi ya akina mama inachukua wagonjwa wengi wa aina mbalimbali; Serikali ina mpango gani wa kuongeza jengo lingine kuwanusuru akina mama ambao wanakwenda na maradhi ya aina moja lakini wanapata maradhi ya maambukizi kwa sababu wodi hiyo inachukua wagonjwa wa aina zote? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mahmoud Hassan Mgimwa, Mbunge wa Mufindi Kaskazini, kama ifuatavyo:- Kwanza kabisa, anachozungumza hapa ili tuweze kuelewana vizuri, Mheshimiwa Mgimwa point anayotaka kuileta hapa inafanana na Tumbi Hospital ile ya Kibaha kwamba, kuna ajali nyingi sana zinatokea pale, kwa sababu ya matumizi ya barabara na watu wetu wanakwenda wakati mwingine wanazungumza na simu, mwingine amelewa pombe na nini, watu wamegongwa na wengine wamekufa. Anachokisema hapa ndicho kinachotokea kule Mufindi na Hospitali hii iko pale Mafinga. Kwa hiyo, tunakubali kabisa kama Serikali kwamba, matukio yameonesha kabisa kwamba, kwa kweli kumekuwa kuna ajali na Viongozi wa Serikali tumepiga simu kusema msaidie amepata ajali pale. Kwa hiyo, anachokisema hapa ni sahihi kabisa na sisi tunapenda kumpongeza kwa mawazo haya ambayo amekuwa nayo. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuhusu Madaktari, nimeeleza hapa kuwa, sasa hivi kuna Madaktari ambao wamekwenda masomoni, labda sana sana aulize kwamba; je, wakati hawa wanaendelea na masomo na huku Wananchi wanaendelea kuishi inakuwakuwaje? Hili ni jambo ambalo nitawasiliana na Wizara ya Afya, tutaangalia jinsi ambavyo tutawasaidia lakini kwa mpango wa muda mrefu ni hilo la Madaktari ambalo nimeelezea. La pili, hili la akina mama analolizungumza hapa; hivi tunavyozungumza, nimezungumzia habari ya wodi ya akina mama, wodi hii, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeweka pembeni shilingi milioni 242 na tender zimekwisha kufunguliwa. Ninaelewa anasema kwamba, sasa unajua wanalala mahali pamoja na nini, hilo tunategemea litawaondolea hilo tatizo na nimezungumza na Mkurugenzi Mtendaji asubuhi hii, nikijua kwamba ataniuliza swali hilo. Kwa hiyo, nina hakika na 2 ninachosema kwamba, akitaka aulize na tender zimeshafunguliwa na hela hizi zipo shilingi milioni 242. MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa hali ya Hospitali ya Mufindi Kaskazini haina tofauti sana na Hospitali ya Wilaya ya Mafia na ukizingatia Mafia ni Kisiwa hakuna njia yoyote ya haraka ya mgonjwa kukimbizwa kwenye hospitali nyingine. Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Mtaalamu wa Picha za X- ray na Madaktari Mabingwa kwa sababu vifaa vya X-ray viko pale lakini hakuna anayeweza kuvitumia? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaynab Vullu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, hii problem anayoisema hapa ni genuine, ni sahihi, hawa ni sawa sawa na wale wa kule Ukerewe wanakaa Mafia. Mimi nimekwenda Mafia sikuweza kwenda kwa gari, kwa sababu ni lazima uruke kwa ndege uende mpaka kule maana ni self contained na self contained ni lazima iwe na kila kitu humo ndani, ndicho anachokizungumza hapa. Sasa ndiyo usipowasaidia Watu wa Mafia watakufa pale. Kwa hiyo, nitakachofanya hapa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ni kuwasiliana na Waziri wetu wa Afya sasa hivi, kama hawana mtu wa X-ray sasa itakuwaje kule si itakuwa ni matatizo makubwa sana. Kwa hiyo, hili siyo jambo la kukaa tunajadili hapa ni jambo la kutekeleza, wala asiwe na wasiwasi. Na. 359 Mkataba wa Uundaji wa Boti Mpya MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Tarehe 13 Mei, 2010, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ilisaini Mkataba na M/S Sam Amzai Boat Builders Co. Ltd wa uundaji wa boti mpya kwa gharama ya shilingi 91, 360,000. Boti hiyo ilipaswa kuwa tayari imekamilika na kukabidhiwa tarehe 24 Agosti, 2010:- (a) Boti hiyo iko wapi na imekabidhiwa kwa nani? (b) Je, ni kwa kiasi gani masharti ya mkataba ya uundwaji boti hiyo yamesimamiwa na kukamilishwa ipasavyo? (c) Kama kuna kasoro zozote katika utekelezaji wa mkataba huo ni hatua gani zichukuliwe kwa wahusika? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlza, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:- Kama nimekosea namna ya kutamka jina lake, ninamwomba aniwie radhi. (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba iliingia Mkataba na Mzabuni, M/S Sam Amzai Boat Builders Co. Ltd wa uundaji wa boti mpya kwa gharama za Sh. 91,360,000. Gharama hii inajumuisha uundaji wa boti Sh. 85,360,000 na Sh. 6,000,000 kwa ajili ya usafirishaji wa boti hiyo kutoka Dar es Salaam inapoundwa hadi Muleba. Hadi kufikia leo boti hiyo haijakamilika hivyo haijakabidhiwa. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, makubaliano ya Mkataba yalikuwa kama ifuatavyo:- 3 (i) Mkataba ulianza tarehe 25 Mei, 2010 na Boti ilipaswa kukamilika tarehe 24 Agosti, 2010; (ii) Malipo yatalipwa kwa awamu nne; awamu ya kwanza Mzabuni atalipwa 50% ya uundaji wa boti; ya pili 40% baada ya kukamilisha uundaji; ya tatu 10% baada ya kukabidhi boti; na ya nne atalipwa fedha za usafirishaji kutoka Dar es Salaam hadi Muleba baada ya boti kukabidhiwa na kukaguliwa na mwajiri; na (iii) Iwapo Mzabuni atachelewa kukamilisha kazi, mwajiri atamkata asilimia 0.05 ya fedha za Mkataba kwa siku kwa kila siku ambazo hajakamilisha kuunda boti mpaka atakapokabidhi boti hiyo. Mheshimiwa Mwenyekiti, Mzabuni hakuzingatia masharti ya Mkataba wa kutengeneza boti kwa muda uliopangwa. Halmashauri kwa upande wake, imemweleza kwamba, masharti ya Mkataba huo yazingatiwe ikiwemo kutomlipa malipo ya awamu ya pili, tatu na nne. (c) Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na Mzabuni kutozingatia masharti ya Mkataba, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, tarehe 18 Machi, 2011 ilichukua hatua ya kumwandikia barua ikimtaka kuzingatia makubaliano yaliyoainishwa kwenye Mkataba huo na kama ilivyoeleza.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages102 Page
-
File Size-