MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao Cha

MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao Cha

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Ishirini na Tatu – Tarehe 8 Julai, 2009 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:- Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. MUSSA A. ZUNGU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2008/2010 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2009/2010. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM - MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2009/2010. NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO Randama za makadirio ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa mwaka wa fedha 2009/2010. 1 MASWALI NA MAJIBU Na. 171 Kutangazwa kwa Miji Midogo MHE. DORAH H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa tarehe 17/09/2004 Miji midogo ipatato 90 ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 353 ambapo Mji wa Mererani ni miongoni mwa Miji iliyotangazwa ukiwa na wakazi wapatao 48,000. (a) Je, miongoni mwa Miji iliyotangazwa ni Miji mingapi imekwishaanza? (b) Je, ni Miji mingapi iliyopata ruzuku moja kwa moja ya kujiendesha toka Serikali Kuu? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dora Mushi, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka ya miji midogo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo kwenye Mamlaka ya Wilaya. Mamlaka hizi zinaanzishwa pale ambapo palikuwa na kijiji ambacho kimeanza kuendelezwa na kuwa na mazingira ya ki-mji. Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa amepewa madaraka ya kutangaza kijiji au vijiji vilivyofikia sifa zilizowekwa kuwa Mamlaka za Miji midogo. Mheshimiwa Naibu Spika, miongoni mwa Miji midogo 90 iliyotangazwa kupitia gazeti la Serikali Na. 353 la mwaka 1994 ni miji 41 iliyoanzishwa rasmi ikiwemo Mamlaka ya Mji mdogo wa Mererani. Mji huu ulizinduliwa rasmi tarehe 12 Agosti, 2008. Mamlaka hii ya Mji mdogo wa Mererani ina wajumbe 19, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu ambaye ameteuliwa na Baraza la Mamlaka ya Mji mdogo. Aidha, vijiji vilivyokuwa ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo vimefutwa na sasa kuna vitongoji. (b)Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna miji midogo iliyokwisha anzishwa ambayo imepokea ruzuku moja kwa moja ya kujiendesha kutoka Serikali Kuu. Mamlaka za Miji midogo, bado zinaendelea kupokea ruzuku zinazopitia kwenye Mamlaka za Wilaya zilizomo kwa kuzingatia Bajeti zilizojiwekea. Mamlaka ya Mji mdogo wa Mererani haukutengewa fedha yoyote kwa mwaka wa fedha 2008/2009 kwa sababu ilikuwa haijaanzishwa rasmi. Katika mwaka 2009/2010, 2 Mamlaka ya Mji Mdogo, wa Mererani imeandaa Bajeti yake ambayo imejumuishwa na ile ya Halmashauri ya Wilaya Simanjiro. MHE. DORAH H. MUSHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la pili. Pamoja na majibu mazuri ya Waziri naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa umbali wa kutoka Mji mdogo wa Mererani kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ni km 145; na kwa kuwa Mji huu wa Mererani una wakazi wapatao 48,000. Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kuwapa ruzuku moja kwa moja ili miji hii iweze kuwahudumia wananchi hawa? Swali la pili; kwa kuwa mji mdogo wa Mererani umepata neema ya kuwa miongoni mwa miji iliyotangazwa kama eneo maalum kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na kwa kuwa mji huu sasa unahitaji wawekezaji. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuhakikisha kwamba ina boresha miundombinu ya kuwavutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na barabara kwa kuweka lami, barabara inayo toka KIA kwenda Mererani? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la kupewa ruzuku moja kwa moja na Serikali; kwa mujibu wa Sheria mpaka sasa hivi Sheria yetu inasema kwamba miji yote midogo inapata ruzuku yao kupitia kwenye Halmashauri husika kwa sababu Sheria hiyo haijabadilika inabidi ruzuku hizo zipitie kwenye Halmashauri husika hadi hapo Sheria itakapobadilika. (Makofi) Nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli umbali kutoka Mererani mpaka Simanjiro ni mrefu sana na ndiyo maana tumeuanzisha huo mji mdogo wa Mererani ili uweze kupanuka na ili baadaye uweze kujitegemea kuwa mji kamili na wakati ukiwa mji kamili utakuwa unapewa ruzuku moja kwa moja. Kuhusu suala la wawekezaji nafahamu kabisa kwamba Mererani kuna uwekezaji na wawekezaji wengi wanavutika kwenda huko na miundombinu yake sio mizuri sana. Lakini Mheshimiwa Dorah kama anavyofahamu kwamba barabara kutoka KIA hadi Mererani inaboreshwa mwaka hadi mwaka ili iweze kupitika vizuri na barabara hiyo inapitika vizuri. Ombi lake naomba nishirikiane na wenzangu wa miundombinu kuona kwamba kama kuna uwezekano wa kuweka lami kutoka Mererani hadi KIA. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa vile mji wa Mbinga una hadhi hiyo ya kuwa mji mdogo na kwa kuwa tangu mwaka 2004 wamekuwa wakijaribu kuanzisha Mamlaka ya Mji mdogo na bado hawajafanikiwa. Je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari hata leo kuongea na Mkurugenzi 3 kubaini ni tatizo gani linalowapata watu wa Mbinga hadi sasa kushindwa ku-operate kama Mji mdogo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi kwamba mwaka 2004 tulitangaza Mamlaka za Miji midogo 90 lakini mpaka sasa hivi iliyoanzishwa ni Mamlaka za Miji midogo 41 tu. Hii ni kutokana na Halmashauri zenyewe kujipanga vizuri. Kama wameamua hata leo kwamba Mamlaka yetu iwe ina kuwepo, kwa sababu sisi upande wa Serikali tumeshatimizi wajibu wetu wa kutangaza ni wao katika Halmashauri husika kujipanga na kuamua kwamba sasa mji mdogo wetu tuuendeleze na procedure Wakurugenzi wanazifahamu Waheshimiwa baadhi ya Wabunge wanazifahamu na baadhi ya Mamlaka za Miji Midogo zimeanzishwa na sasa hivi zimekuwa zimefikia katika hadhi ya kuwa Mamlaka za Miji kamili. (Makofi) Na. 172 Kituo cha Afya Kikombo Kupewa Mgao wa Dawa na Vifaa MHE. EPHRAIM N. MADEJE aliuliza:- Kwa kuwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kikombo ulikamilishwa na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma zaidi ya miaka miwili iliyopita; na kwa kuwa utaratibu wa uanzishwaji wa kituo hicho ulikwishakamilika. (a) Je, kwa nini Serikali haijaanza kupeleka mgao wa dawa na vifaa ili kukiwezesha kituo hicho kutoa huduma zinazostahili kutolewa na Kituo cha Afya? (b) Je, Serikali iko tayari kuanza kupeleka dawa na vifaa hivyo haraka ili wananchi waanze kupata huduma hiyo muhimu? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ephraim Nehemia Madeje, Mbunge wa Dodoma Mjini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kukubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, ujenzi na taratibu zote za uanzishwaji wa Kituo cha Afya cha Kikombo ulikamilika katika mwaka wa fedha 2007/2008. Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma tayari imewasilisha maombi kwa Waziri Afya na Ustawi wa Jamii ili kituo hicho 4 kiingizwe kwenye orodha ya vituo vya afya na kuweza kupatiwa madawa kulingana na hadhi ya Kituo cha Afya. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na maombi ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia kwa Mfamasia Mkuu wa Wizara hiyo, Kituo cha Afya Kikombo kilianza kupokea madawa ya stahili ya Kituo cha Afya kuanzia robo ya nne ya mwaka wa fedha 2008/2009 yaani mwezi Aprili hadi Juni, 2009. Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imekuwa ikikitambua Kituo cha Afya Kikombo na kukinunulia dawa za ziada zinazohitajika ili kuwezesha wananchi kupata huduma zinazolingana na zile za Kituo cha Afya. Sambamba na jitihada hizo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imepeleka watumishi wenye hadhi ya Kituo cha Afya akiwemo Daktari Msaidizi mmoja, Afisa Muunguzi mmoja pamoja na vifaa vinavyotakiwa. MHE. EPHRAIM N. MADEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri ambayo kwa kweli yanaleta matumaini wananchi wa Kikombo kwamba sasa watapata huduma za afya kwa uhakika zaidi. Pamoja na hayo naomba niulize maswali mawili. Kwa kuwa majengo ya Kituo hiki cha afya yalikaa muda mrefu sana kabla hayajaanza kutumika. Baadhi yake haya majengo hivi sasa yana hali mbaya na hasa senyenge yake. Je, Serikali iko tayari kutoa fedha za ziada ili kuyakarabati majengo hayo? Je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari hivi sasa kuja awe mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa kituo hicho cha Afya ambacho tunatarajia kuufanya hivyo hivi karibuni? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi naomba ujibu kwa kifupi sana kwenda huko najua utakubali tu. (Kicheko) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA : Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli hicho kituo cha Afya baadhi ya majengo yamekaa kwa muda mrefu bila kutumika, kwa hiyo yameanza kuharibika. Nikubaliane naye kweli senyenge kwa kweli imeanza kuanguka. Niseme kwamba kwa kushirikiana na Manispaa ya Dodoma tutahakikisha kwamba tutakiboresha kile kituo cha Afya kwa sababu kinatoa huduma kwa watu wengi zaidi hata sisi Waheshimiwa Wabunge wakati mwingine tunaweza tukapata huduma katika sehemu hiyo. Kuhusu kuwa mgeni rasmi aliyepangiwa ratiba ni Mheshimiwa Waziri Mkuu bahati mbaya katika ratiba hiyo haikuweza kutimizwa. Sasa kama Mheshimiwa Waziri 5 Mkuu ataniruhusu nikawe mgeni rasmi badala yake kwa sababu ile aliiahirisha mimi niko tayari kuja na kukifungua kituo hicho rasmi.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    210 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us