Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tano – Tarehe 15 Mei, 2014 (Kikao Kilianza Saa tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, leo ni siku ya Alhamisi, kwa hiyo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani hayupo hata ukikaa karibu hapo wewe siyo kiongozi. Kwa hiyo, nitaendelea na wengine kadiri walivyoleta, tunaanza na Mheshimiwa Eugen Mwaiposa. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na :- NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Hotuba ya Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. NYAMBARI C. NYANGWINE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. CYNTHIA H. NGOYE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumuzi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. RASHID ALI ABDALLAH – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Katiba na Sheria Kuhusu Makadirio, Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. KHATIB SAID HAJI (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kuhusu Makadirio, Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Waziri Mkuu kama nilivyoanza kusema, leo hatuna Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ambaye kwa mujibu wa Kanuni anatakiwa kuanza. Kwa hiyo, nitamwita Mheshimiwa Eugen Mwaiposa. MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru kabisa kupata nafasi hii ya kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Waziri Mkuu, mvua zilizonyesha nchini mwaka huu hasa kuanzia mwezi wa tatu zimeleta madhara makubwa sana katika baadhi ya Mikoa. Mfano mkoa wa Pwani, Dar es Salaam, Morogoro na kwingineko nchini. Kwanza niipongeze sana Serikali kwa kutumia TANROADS kwa jinsi ambavyo suala hili limeshughulikiwa hasa kuhakikisha kwamba wamerudisha mawasiliano kati ya Wilaya na Wilaya na Mikoa na Mikoa. Lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu madhara makubwa mengine yametokea kati ya kata na Kata na vijiji na vijiji ambayo mpaka sasa ninavyoongea kwa baadhi ya kata na Kata hakuna mawasiliano kabisa. Mfano mdogo tu katika jimbo la Ukonga hakuna mawasiliano kati ya Kata ya Gongo la Mboto na Ulongoni, Kata ya Kivule na Msongola, Kata ya Ukonga na Gongo la Mboto. Lakini hata Kata ya Kitunda na Magole. Swali langu Mheshimiwa Waziri Mkuu. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inasaidia sasa mawasiliano haya kurudi katika ngazi hizo ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za maendeleo? 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli anavyosema Mheshimiwa Eugen Mwaiposa tulipata madhara sehemu nyingi hapa nchini. Lakini Serikali imejitahidi sana kujaribu kurejesha hali ya kawaida na kuwezesha usafiri kuendelea kama kawaida. Lakini kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam, ni kweli kuna baadhi ya Kata ambazo tumepata hilo tatizo, lakini tulipokuwa tumepata nafasi ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa jambo la kwanza nililosisitiza ni kwamba lazima Manispaa zitambue kwamba barabara hizo ziko chini ya himaya zao na ni jukumu lao la kwanza kuhakikisha wanasimamia utengenezaji wa madaraja hayo na za sehemu zile ambazo zimekatika. Nikamwambia vile vile kwamba upande wa Serikali tutakapokuwa tumepata maombi ya ziada kwa maana ya kwamba uwezo wenu umeishia mahali fulani, basi na sisi tutaangalia tuone namna ya kusaidia ili kurejesha hiyo hali ya mawasiliano. (Makofi) MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba nimwulize swali moja tu la nyongeza. Kwa kuwa Manispaa zetu nchini nyingi ikiwepo Manispaa ya Wilaya ya Ilala uwezo wake wa kifedha ni mdogo na kwa kuanzia tu walikuwa wametenga shilingi bilioni 1.5 ambazo hazikuweza kusaidia. Lakini kwa kuwa Manispaa hiyo hiyo ilileta maombi ya Shilingi bilioni 4.5 ili kuweza kupatiwa fedha kutoka kwenye Mfuko wa maafa. Je, suala hilo sasa limefikia wapi? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, sina jibu la haraka haraka kwenye hilo eneo labda mpaka ni-check na Katibu Mkuu wangu ili tuweze kujua kama walifanikiwa kupata fedha kidogo au kiasi gani kwa ajili ya kurejesha mawasiliano ya barabara katika Jiji letu la Dar es Salaam. SPIKA: Niwaombe tena mnaouliza maswali naomba muwe very brief kusudi wote wafikiwe ama sivyo mtu akihutubia tu basi itakuwa muda hautoshi, Mheshimiwa Desderius John Mipata. MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 Mheshimiwa Rais alitoa ahadi nyingi kwa wananchi na zilichukuliwa kama ni mkataba wa kuchaguliwa kwake ili akishachaguliwa aweze kutekeleza mambo mbalimbali hayo aliyokwishaahidi. Mfano ninautoa ni katika jimbo langu la Nkasi, Mheshimiwa Rais aliweza kuwaahidi wananchi kutengeneza barabara tatu zinazounganisha kanda mbili tofauti muhimu sana, Ukanda wa Mwambao na ukanda wa Ufipa ya Juu. Barabara hizi Halmashauri katika kuhakikisha kwamba inatekeleza ahadi ya Rais, chini ya uwezo wake, ilipendekeza barabara hizi ziweze kupandishwa hadhi jambo ambalo halijawezekana. Lakini pia yalitumwa maombi maalum chini ya mfuko wa dharura yenye thamani ya shilingi bilioni tatu lakini tumepata milioni mia nane tu kwa barabara Kanakala, Kitosi na Wampembe. Barabara ya Minde na Namanyere haijapata kitu chochote na muda uliobaki haunihakikishii kwamba inawezekana ahadi hii ikatekelezwa. (Makofi) Je, Serikali bado inawaaminisha wananchi kwamba ahadi zote za Mheshimiwa Rais zitatekelezwa kabla ya muda wa kipindi chake kwisha? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, nia ni hiyo, dhamira ni hiyo, lakini kwa sehemu kubwa inategemea vilevile fedha ambayo inapatikana. Mliomba bilioni tatu mmepata milioni mia 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) nane ni kweli haijafikiwa kiwango kinachotakiwa, lakini hiyo haina maana kwamba ahadi hiyo haitatekelezwa. Hata kule kutoa hicho kiasi cha fedha ni kuonyesha dhamira kwamba bado nia iko pale pale. (Makofi) Kwa hiyo, kama tumeshindwa kwenye mwaka wa fedha ambao unaishia Juni mwaka huu, lazima tuangalie uwezekano wa mwaka huu ambao utaishia Juni mwaka kesho, (2015). Kwa hiyo mimi nadhani tuendelee tu kukumbushana na sisi tutajitahidi kujaribu kutoa msukumo zaidi ili barabara hizo ziendelee kuhudumiwa na bahati nzuri ni barabara ambazo nazijua nimetembea kule wakati wa ziara zangu. Kwa hiyo, tukishirikiana naamini tunaweza tukasaidia tukapunguza ile kero. MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri, nina swali moja la nyongeza. Pamoja na juhudi na ukweli alioueleza Mheshimiwa Waziri Mkuu juu ya azma ya Serikali kutekeleza ahadu za Mheshimiwa Rais. Lakini wapo watendaji ambao wanabeza juhudi za Waheshimiwa Wabunge, watendaji na viongozi wa Serikali wanaobeza juhudi ya Waheshimiwa Wabunge nikiwemo mimi katika kipindi nilichokaa hapa cha miaka mitatu na nusu. Barabara hizi nimezisemea sana, nimeandika barua Ofisini kwako, nimeweza kwenda Ofisi ya TAMISEMI kumwona Katibu Mkuu. Jitihada zote nilizozifanya ziliwezesha kupata kiasi kidogo tu cha fedha hizo, lakini wako viongozi na watendaji wa Serikali wanaobeza juhudi zangu. Je, Serikali ina kauli gani juu ya watendaji wanaobeza juhudi za viongozi waliochaguliwa na wananchi kama mimi. (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni dhahiri ni vigumu kwangu kulisemea kwa uhakika kwa sababu sina hakika ni viongozi gani wanaobeza au wanaoona kwamba hufanyi kazi yako vizuri. Lakini mimi nadhani kubwa wewe ni Mbunge, jukumu lako unalifahamu. Hayo mengine yanaweza yakasemwa lakini wewe tekeleza wajibu wako, watu wako wata-appreciate hao wengine wanaobeza ukipata nafasi basi ninong‟oneze tuone ni akina nani, wanabeza kwa misingi gani, tuweze vile vile kuwashughulikia. SPIKA: Shughuli nzito kabisa, Mheshimiwa Dkt. Antony Mbassa. MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami nipate kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali asubuhi ya leo. Mheshimiwa Waziri Mkuu katika Mkutano wa kumi na nne mwaka jana nilipata kusimama hapa na kuongea kero ya wananchi wanaoishi katika Kata ya Kaniha, kijiji cha Kaniha na Kijiji cha Mpago ambao walikuwa wanasumbuliwa kwamba wanaishi ndani ya hifadhi. Lakini nashukuru kwa maelekezo yako uliyoyatoa na timu ya wataalam uliyotuma iende kufanya kazi japo haijafika kule lakini walau wanapata unafuu japo leo tena katika vyombo vya habari imejitokeza watu wanabeza sisi tunawatetea wananchi inaonekana hakuna kazi tunayoifanya. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wananchi hawa pamoja na kilimo wanachoshughulika nacho lakini ni wafugaji wa nyuki. Mwaka jana wamesumbuka sana kupata kibali cha kwenda kurina asali yao. Hata mwaka huu dalili hizo zinajitokeza. Nini kauli yako Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhusu wananchi
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages181 Page
-
File Size-