Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Nne – Tarehe 3 Julai, 2006 Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla ya kuendelea na mtiririko wa Orodha ya Shughuli za leo, ninayo matangazo yanayohusu wageni. Kwanza katika Ukumbi wa Public Gallery upande wa kushoto ni Madiwani na Viongozi wa Wilaya ya Dodoma, wageni wa Waheshimiwa William Kusila, Mheshimiwa John Malecela, Mheshimiwa Ezekiah Chibulunje na Mheshimiwa Mariam Mfaki. Karibuni sana Waheshimiwa Madiwani. Pia wapo wageni wa kutoka Jimbo la Nachingwea, ambao ni Madiwani 24 wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea wageni wa Mheshimiwa Mathias Chikawe, Mbunge na Naibu Waziri, wale pale mkono wa kulia. Waheshimiwa Wabunge, wanaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mama Joyce Mtauka, namtaja makusudi kwa sababu mama huyu hakupita kwa kubabaisha ni wale ambao ameshinda uchaguzi kwa kura nyingi kuwa Diwani. Pengine zuri zaidi amemshinda mwanaume. Hongera sana Mama Mtauka. (Makofi/Kicheko) Wapo pia wageni wa Mheshimiwa James Musalika, ambao ni walimu wa shule ya msingi na wapiga kura kutoka Jimbo la Nyang’wale wale pale. Karibuni sana. Tunaye pia mhubiri maarufu mwenye kituo cha ATN kule Dar es Salaam Mchungaji Fernandes, yule pale. Karibu sana Baba Mchungaji na ahsante kwa kazi yako njema ya kuongoza vijana katika njia iliyonyooka. (Makofi) HATI ZA ZILIZOWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Miundombinu kwa mwaka wa Fedha 2006/2007. 1 MHE. PAUL P. KIMITI – ((K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU): Maoni ya Kamati ya Miundombinu, kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makaridio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2006/2007. MHE. BAKARI SHAMIS FAKI – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI: Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2006/2007. MASWALI NA MAJIBU Na. 127 Kufufua na Kujenga Barabara MHE. MBARUK K. MWANDORO aliuliza:- Kwa kuwa barabara itokayo Mkinga kupitia Dima, Kinyatu, Gombero hadi Mjesani ni miundombinu muhimu unaounganisha Makao Makuu ya Wilaya ya mpya ya Mkinga na sehemu kubwa sana za Wilaya hiyo na kwa kuwa ubovu wa barabara hiyo umekuwa kero muda mrefu. Je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati muafaka kwa barabara hiyo kufufuliwa na kujengwa angalau kwa kiwango cha changarawe? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kassim Mwandoro, Mbunge wa Mkinga kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, barabara itokayo Mkinga kupitia Dima, Kinyatu, Gombero hadi Mjesani ina urefu wa km. 43.1. Barabara hii hupitia kwenye miinuko na sehemu kubwa ya maeneo haya ni pori. Mheshimiwa Slpika, ili kufufua na kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe, ni lazima pia kujenga Madaraja ya Msimbazi, Mkaka, Kombe na Ndoyo. 2 Tathmini iliyofanywa inaonyesha kwamba barabara hii mpaka ijengwe, inahitaji kiasi cha 863,815,000/= pamoja na na ujenzi wa madaraja. Hata hivyo kwa sasa Halmashauri haina fedha za kuyajenga madaraja hayo, Halmashauri kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara inaendelea kuzifanyia matengenezo barabara mbadala za Doda- Mazola, Stakishari – Mkinga na Mjesani – Mapatano ambazo hutumiwa na wananchi wa maeneo hayo kufikia Barabara Kuu ya Tanga – Horohoro na barabara ya Mkoa wa Tanga – Mabokweni – Mtoni Bombo ambazo huhudumiwa na Serikali Kuu. MHE. MBARUK K. MWANDORO: Mheshimiwa Spika, pamoja na jibu zuri la Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda ieleweke kwamba barabara hizi zilizozungumzwa na ni za mzunguko sana na hiyo ni barabara muhimu ambayo ni mojawapo natumaini Mheshimiwa Rais Mstaafu, alipozindua Wilaya hiyo aliagiza kwamba miundombinu itengenezwe kwa maana mapendekezo kama Serikali ichukue hatua hizo zinazostahili kujenga hiyo haraka iwezekanavyo. Ahsante sana. SPIKA: Hilo lilikuwa ni pendekezo tu siyo swali kwa hiyo, namwita Mheshimiwa Damas Nakei, kwa swali la pii. Na. 128 Ubora wa Miundombinu ya Barabara MHE. DAMAS P. NAKEI aliuliza:- Kwa kuwa katika kuondoa umaskini na hatimaye kuleta maendeleo vijijini, uwepo wa ubora wa miundombinu ya barabara ni kichocheo muhimu sana na kwa kuwa, barabara za Dareda - Bacho na ile ya Dareda kati – Dohom – Kiru Six kuelekea Magugu ni viungo muhimu katika usafiri na usafirishaji:- (a) Je, Serikali ina mpango gani kuhusu hizo barabara? (b) Kama Serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo, ni lini kazi ya ukarabati itaanza? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Damas Pascal Nakei, Mbunge wa Babati Vijijini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- 3 (a)Mheshimiwa Spika, Barabara ya Dareda hadi Bacho ni barabara ya kijiji inayoanzia Dareda Kati hadi Kitongoji cha Bacho kwenye Kituo cha Maonyesho ya Kilimo na Mifugo. Barabara za Dareda – Bacho na Dareda na Dareda Kati – Dohom – Kiiru Six kuelekea Magugu kwa ujumla ina urefu wa kilometa 3 na ipo chini ya Vitongoji vya Belmi na Bacho. Barabara nyingine ni ile ya Dareda Kati – Dohom hadi Kiru Six na kuunganisha barabara ya Wilaya ya Babati – Kiru – Err hadi Mbulu na kisha kuunganisha na barabara nyingine ya Wilaya ya Kiongozi hadi Kiru Six inayounga na Barabara Kuu ya Arusha – Babati. Barabara ya Dareda – Bicho na Dareda Kati – Dohom – Kiru Six inamilikiwa na Vitongoji vya Belimi na Bacho na barabara ya Dareda – Kati – Dohom hadi Kiru Six inamilikiwa na Vitongoji cha Hyasm na Vijiji vya Kiru Six na Kiru – Err. Wananchi wanaoishi katika maeneo yanakopita barabara hii wanashauriwa kuzifanyia matengenezo barabara hizi mara kwa mara ili ziweze kupitika. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu na barabara hizi kutokana na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kama vile mahindi, maharage, kawawa, vitunguu, mbaazi na alizeti. Vile vile barabara hizi zinaunganisha wananchi katika maeneo ya huduma za afya katika Kituo cha Dareda na Magugu na pia ni njia mbadala kwa magari yatokayo Arusha kwenda Dareda bila kupitia Babati Mjini. Gharama ya kuzifanyia ukarabati barabara hizo ambazo ni shilingi milioni 780. Gharama hizi ni kubwa kwa Halmashauri, hivyo taratibu zinafanywa ili barabara hizi ziweze kuingizwa katika barabara zinazohudumiwa na wakala wa barabara (TANROADS). MHE. DAMAS P. NAKEI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo kubwa ni kujenga barabara kwa changarawe: (a) Je, Serikali inaweza kujenga barabara hiyo kwa hatua (stage construction) kwa ikaanza na ujenzi kwa kuiweka katika hali ya kuwa barabara udongo ikawa gharama nafuu kuliko kusubiri upatikanaji hizo shilingi milioni 700? (b) Kwa kuwa barabara ya Dohom Kiru Six hadi Magugu kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, mwenyewe kwamba ni by pass nzuri, je Serikali inaweza ikakubaliana na mimi kwamba ingefaa kupandishwa hadhi na kuwa Barabara ya Mkoa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali ina mpango wa kuangalia barabara zote ambazo zinahudumiwa na Halmashauri katika nchi nzima, ili itambue hali halisi na kilomita ngapi ambazo zinahitajika kutengenezwa na Halmashauri katika Tanzania nzima. Zoezi hili likiisha tutaainisha barabara zile ambazo ni muhimu sana kwa kufuata kipaumbele. Nafikiri zoezi hili likiisha barabara zote za vijijini zitakuwa zinatengenezwa kufuatana na kipaumbele. Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, natambua kabisa kwamba barabara ya Dohom hadi Kiru Six kuelekea Magugu ni muhimu sana kwa sababu ni Magugu ni kama 4 Commercial Centre kwa ajili ya vijiji hivyo. Kwa hiyo, nafikiri tutaliangalia suala ili kuona kwamba tutatekeleza kwa kiasi gani. (Makofi) Na. 129 Gesi Asilia MHE. ABUBAKAR KHAMIS BAKARY aliuliza:- Kwa kuwa gesi asilia ni jambo la Muungano chini ya Ibara ya 4(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kwa kuwa kuna gesi inayopatikana Tanzania na imeshaanza kutumika:- (a) Je, ni asilimia ngapi ya mapato yanayopatikana hupewa Zanzibar? (b) Je, gesi hii itasaidiaje kutatua shida ya upungufu mkubwa wa umeme huko Tanzania Zanzibar? SPIKA: Kabla ya Mheshimiwa Naibu Waziri, hajajibu swali nimemuona Mheshimiwa Kabwe Zitto, amekaa Kiti cha Kiongozi wa Upinzani sijataarifiwa, inaelekea kwa mkao huo sasa yeye kwa asuhuhi hii yeye ndio Kiongozi wa Upinzani. Naomba tulitambue hilo na kumpongeza kwa nafasi hii. (Makofi) NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI alijibu:- Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Abubakar Khamis Bakary, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a)Uzalishaji wa gesi asilia ya Songosongo ulianza mwezi Julai mwaka 2004. kama nilivyojibu katika swali Na. 741 lililoulizwa na Mheshimiwa Hasanain Gulamabbasi Dewiji, Mbunge wa Kilwa Kusini, kwenye mkutano huu tarehe 21/6/2006. Mauzo ya gesi asilia katika kipindi cha miezi 23 iliyoishia mwezi Mei, 2006 yalikuwa Shilingi 29,969,713,199/=. (Makofi) Kati ya maduhuli yaliyokusanywa, jumla ya shilingi 11,663,702,459.25 zililipwa kwa Pan African Energy Tanzania Limited kufidia gharama za uzalishaji gesi, uwekezaji katika miundombinu na gawio lao kwa mujibu wa mkataba uliopo. Salio la jumla ya shilingi 18,306,010,739.75 zililipwa kwa Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) kulipa medani ya muda mrefu, gharama za uendeshaji, mrabaha wa gawio lao kwa mujibu wa mkataba uliopo. Kati ya kiasi kilicholipwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages127 Page
-
File Size-