NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _______ MAJADILIANO YA BUNGE _______ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Nne -Tarehe 5 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu! NDG. ATHUMANI HUSSEIN – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Maulid Said Mtulia, Mbunge wa Kinondoni, sasa aulize swali lake. Na 24 Idadi ya Watu Wenye Ulemavu Nchini MHE. MAULID S. MTULIA aliuliza:- Walemavu wana mahitaji maalum ukilinganisha na watu wasiokuwa na Ulemavu na idadi ya walemavu imekua ikiongezeka siku hadi siku kutokana na ajali za barabarani hasa zitokanazo na usafiri wa bodaboda:- (a) Je, Serikali inaweza kutoa orodha ya idadi ya watu wenye ulemavu nchini kwa kuzingatia makundi yao kwa asilimia? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (b) Je, Serikali ina mpango gani mahususi wa kuwajengea uwezo wa kujitegemea watu wenye ulemavu hasa Vijana, Watoto na Wanawake ili kuondoa utamaduni wa kuendesha maisha yao kwa kuombaomba? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maulid Said Mtulia, Mbunge wa Kinondoni lenye kipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, idadi ya Watu wenye Ulemavu kwa kuzingatia makundi yao na kwa asilimia ni kama ifuatavyo:- Watu wenye Ualbino ni 16,477 sawa na 0.04%; walemavu wasioona ni 848,530, sawa na 1.93%; walemavu ambao ni viziwi ni 425,322, swan a 0.97%; walemavu wa viungo ni 525,019, sawa na 1.19%; walemavu wa kumbukumbu ni 401,931, sawa na 0.91%; walemavu wa kujihudumia ni 324,725, sawa na 0.74%; na Ulemavu mwingine, yaani kwa ujumla wake ni 99,798, sawa na 0.23%. Kulinganisha na takwimu hizo jumla ya watu wenye ulemavu, kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 ni watu 2,641,802. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hivi sasa inakamilisha zoezi la uanzishwaji wa regista ambayo itasaidia kupata takwimu sahihi ya watu wenye ulemavu katika maeneo yote ya mijini na vijijini. Faida nyingine ya kuanzisha regista hizi zitatusaidia pia kutambua sababu za kuongezeka kwa ulemavu katika kila eneo na changamoto zinazowakabili. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha watu wote wenye ulemavu hasa vijana, watoto na wanawake hawaachwi nyuma kiuchumi, Serikali inaendelea kuwajengea uwezo kuhakikisha watoto wote ikiwa ni pamoja na wenye ulemavu wanapata elimu ya msingi na sekondari ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea. Pia inatoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa makundi ya vijana na wanawake wenye ulemavu kupitia vyuo vya watu wenye ulemavu na programu ya kukuza ujizi hapa nchini. Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawezeshwa kiuchumi, Serikali inatoa mkopo wa fedha ya asilimia mbili (2%) zinazotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri. Hata hivyo, mipango yote ya uwezeshaji kiuchumi nchini ni jumuishi ikiwajumuisha pia watu wenye ulemavu. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maulid Said Mtulia, swali la nyongeza. MHE. MAULID S. MTULIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii adhimu ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza, niipongeze Serikali kwa majibu mazuri ya kitakwimu na naamini kwa majibu haya na kuonesha kwamba tuna walemavu zaidi ya milioni mbili, itasaidia Serikali yetu kuja na mpango mkakati wa namna gani ya kuwasaidia. Nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa, hapo Dar es Salaam Mkuu wetu wa Mkoa alileta mpango kuleta vifaa vya kuwasaidia walemavu na walemavu wengi sana wakajitokeza, ikionesha kwamba kuna shida hiyo. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuhakikisha inawajengea uwezo walemavu, kwa maana wa viungo kuwaletea viungo ili wawe na uwezo wa kujitegemea wenyewe na wale wa kusikia wapate viungo vya kusikia ili waweze kujitegemea wenyewe na walemavu wengine? Pia, je, Serikali ina mpango gani wa kuwajengea uwezo ili kupunguza athali ya ulemavu kwa kutumia viungo bandia? 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili… NAIBU SPIKA: Mheshimiwa mbona umeuliza kwa nini mbili hapo, kuna swali lingine tena! Maswali ni mawili tu na umeshataja kwa nini mbili, kwa hiyo maana yake maswali yako mawili, maana nisije nikakosea kanuni hapa itakuwa balaa. Mheshimiwa Ikupa Stella Alex, majibu! NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maulid Said Mtulia, Mbunge wa Kinondoni kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeza Mheshimiwa Maulid Mtulia kwa jinsi ambavyo anafuatilia masuala ya watu wenye ulemavu. Pia naomba niweze kumjibu Mheshimiwa Mbunge, kwamba Serikali imekuwa na mipango mingi kwa upande wa uwezeshaji kwa watu wenye ulemavu, ikiwemo kuwapatia vifaa saidizi. Kwa sababu tunafahamu kwamba, mtu mwenye ulemavu, kulingana na aina yake ya ulemavu, asipowezeshwa kwa upande wa vifaa visaidizi, hawezi kujimudu. Kwa kuliangalia hilo, Serikali imekuwa ikitenga bajeti, lakini pia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, tumekuwa tukigawa vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu. Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, kwa kundi hili la watu wenye ulemavu, ili kuhakikisha kwamba wanaweza kufanya vizuri kama ambavyo nimeongea kwenye jibu langu la msingi, ni kwamba tumekuwa tukihakikisha kwamba tunawajengea uwezo kwa kuwawezesha katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kuhakikisha kwamba pia hata programmes ambazo tunakuwa tunaziandaa zinakuwa ni jumuishi kwa watu wenye ulemavu. Kwa hiyo, suala la vifaa kwa watu wenye ulemavu, tumekuwa tukilifanya kama Serikali. Tunaona hata katika shule zetu, tumekuwa tukitenga bajeti ambayo tunanunua vifaa visaidizi na kuvigawa kwenye shule zetu, lakini haviishii tu kwenye shule, tunavipeleka hata kwa watu ambao siyo wanafunzi. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, majibu ya nyongeza. NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ambayo ameyatoa Mheshimiwa Naibu Waziri, nataka niongezee kidogo katika majibu hayo. Kwanza Serikali imeondoa kodi katika baadhi ya vifaa saidizi kwa kutambua kwamba kuna kikundi ndani ya nchi yetu ambacho wanavihitaji vile vifaa na vinaweza vikawasaidia kuwa na maisha bora, kodi hizo katika baadhi ya vifaa zimeondolewa. Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nilikuwa nataka niwape taarifa tu Waheshimiwa Wabunge, kuanzia mwezi huu wa Aprili, Hospitali ya Mifupa MOI, wataanza zoezi la kufanya upimaji pamoja na kutoa vifaa, viungo bandia kwa baadhi ya wale walemavu ambao wanavihitaji. Kwa hiyo, naomba kupitia Waheshimiwa Wabunge kutoa taarifa kwa watu hawa ambao wanahitaji viungo bandia, basi kufika katika Hospitali ya Taifa, MOI kwa ajili ya kuweza kupata vifaa hivyo. Hata hivyo, katika masuala ya vifaa vya usikivu tumekuwa tunaendelea na kampeni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili vya kupandikiza vifaa vya usikivu, lakini vilevile kutoa vifaa saidizi kwa wale watoto ambao wanahitaji vifaa hivyo. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anthony Komu, swali la nyongeza. MHE. ANTHONY C. KOMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo moja la nyongeza. Kwa kutambua mahitaji makubwa ya walemavu wananchi wa Moshi Vijijini kwa kushirikiana na Padri Apolnarys Ngao ambaye anaishi Ujerumani na marafiki zake kule Ujerumani, tunajenga kituo kikubwa cha walemavu kule Parokia ya Mawela. Naomba kumuuliza Waziri kama atakuwa tayari kuja kuona hii jitihada, kuitambua na kuhamasisha michango zaidi ili kuweza kufanikishi hii nia njema? (Makofi) 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, unaomba kwenda huko kwa Mheshimiwa Anthony Komu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anthony Komu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa ameomba niweze kwenda kwenye hicho kituo ambacho kinaandaliwa sasa hivi, kwanza niwapongeze kwa hilo wazo jema kwa kundi hili la watu wenye walemavu. Mimi nikiwa kama Naibu Waziri mwenye dhamana hiyo, naomba niseme kwamba niko tayari. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Venance Mwamoto, Balozi wa Watu Wenye Ulemavu Nchini, swali. MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kazi nzuri ambazo zinafanywa na Serikali, kundi la watu wenye ulemavu limeongezeka na ni walemavu wa tofauti. Je, sasa Mheshimiwa Naibu Waziri atakubali kukutana na makundi hayo ili iwe rahisi kuwasaidia kwa sababu wana changamoto zinazotofautiana? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Venance Mwamoto, Mbunge wa Kilolo, Balozi wa Watu Wenye Ulemavu, lakini pia babu yangu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mwamoto, hajaanza leo kuhakikisha kwamba masuala ya watu wenye ulemavu yanakaa sawa, toka akiwa DC anafanya hivyo. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, nimefanya ziara nyingi hapa Tanzania kwenye mikoa mingi na katika zile ziara zangu, ni lazima nikutane na makundi ya watu wenye ulemavu. Kwa 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) hiyo,
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages180 Page
-
File Size-