Majadiliano Ya Bunge

Majadiliano Ya Bunge

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Ishirini na Nane – Tarehe 12 Julai, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA): Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka 2010/2011. Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa Mwaka 2008/2009 [The Annual Report of Tanzania Education Authrority for the Year 2008/2009]. MHE. OMARI SHABANI KWAANGW’ - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 pamoja na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011. MHE. NURU AWADH BAFADHIL K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: 1 Taarifa ya mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2008/2009 [The Annual Report and Audited Accounts of the Local Authorities Pensions Fund (LAPF) for the Year 2008/2009]. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE): Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MASWALI NA MAJIBU Na. 201 Migogoro Katika Shule Za Sekondari za Kata – Mwibara MHE. DR. RAPHAEL M. CHEGENI (K.n.y. MHE. CHARLES M. KAJEGE) aliuliza:- Kwa kuwa, mojawapo ya vyanzo vya migogoro katika Shule za Sekondari za Kata katika Jimbo la Mwibara ni Bodi za Shule hizo:- (a) Je, Serikali inatambua hilo? (b) Je, ni sifa/vigezo gani vinatumika kuwachagua Wajumbe wa Bodi hizo? (c) Je, Serikali imefanya juhudi gani za kumaliza hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla sijajibu swali la Mheshimiwa Kajege, ninakuomba kwa unyenyekevu mkubwa uniruhusu kwa niaba ya wananchi wa Jimbo langu la Siha, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye Mkutano Mkuu umempitisha kwa kishindo na ninataka nimthibitishie kwamba wananchi wa Siha wapo na yeye na wataendelea kumpa ushirikiano. Kwa kipekee, pia nimpongeze Mheshimiwa Makamu wa Rais Dr. Shein, kwa kupitishwa na Halmashauri ya Kuu ya Taifa kuwa mgombea wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar pamoja na Dr. Bilal kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya hayo yote nakushukuru sana kwa kunipa ruksa hiyo. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Charles Muguta Kajege Mbunge wa Mwibara, lenye sehemu (a), (b) na (c) naomba kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mwibara lina Shule za Sekondari za Kata 8 na shule moja ni ya binafsi. Shule hizo ni hizi zifuatazo; Bulamba, Chitengule, Chisorya, 2 Kwiramba, Muranda, Mwigundu, Nansimo na Nyeruma. Shule zote 8 katika Kata ya Jimbo la Mwibara zina Bodi ambazo zimeundwa kisheria kwa kuzingatia sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 kama ilivyorekebishwa na sheria namba 10 ya mwaka 1995. Kwa kuzingatia sheria hiyo, Bodi za shule zimepewa majukumu ya kusimamia uongozi na uendeshaji wa mipango yote ya maendeleo ya shule, kusimamia nidhamu kwa walimu na wanafunzi na kusimamia matumizi ya fedha za shule. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo sasa napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa kulikuwa na migogoro katika shule mbili za Sekondari za Kata katika Jimbo la Mwibara, ambayo ni migogoro katika shule za Sekondari za Nyeruma na Muranda. Mgogoro wa shule za Sekondari Nyeruma ulikuwa ni kati ya Bodi ya Shule na Mkuu wa Shule. Chanzo cha Mgogoro huu ni Mkuu wa Shule kutoshirikisha Bodi ya Shule katika uendeleshaji wa shule, kutothamini michango yao ya mawazo na kutokusoma mapato na matumizi ya michango kutoka kwa wazazi. Mgogoro wa shule ya Sekondari ya Muranda ulikuwa kati ya uongozi wa shule na baadhi ya viongozi wa Kata ya Namhula, baada ya kutokea mgomo wa wanafunzi tarehe 19 mpaka terehe 20 Februari, 2009 uliosababishwa na mwanafunzi mmoja kuja na silaha (panga) shuleni na kutishia kuwajeruhi walimu wa shule hiyo, kinyume na taratibu za shule, hasa baada ya shule kuwafukuza wanafunzi 14 waliobainika kuchochea mgomo wa wanafunzi wa tarehe 19 mpaka tarehe 20 Februari, 2009. (b) Mheshimiwa Spika, sifa au vigezo vinavyohitajika katika kuteua wajumbe wa Bodi za shule ni hizi zifuatazo:- (i) Mjumbe wa Bodi ya Shule asiwe kwenye Bodi za shule zaidi ya tatu. (ii) Mjumbe asitoke nje ya mkoa. (iii) Mjumbe asiwe na majukumu mengi ya kitaifa. (iv) Wajumbe wanaopendekezwa watoke kwenye maeneo mbali mbali kama Taasisi za Kidini na Jumuiya zisizo za Serikali. (v) Wadau wa Elimu wanaoendelea na kazi zao Serikalini. Mfano, Wakaguzi wa Shule, Walimu, Maafisa elimu, walimu waliostaafu, wanaruhusiwa pia. (c) Mheshimiwa Spika, juhudi zilizochukuliwa katika kutatua mgogoro wa Shule ya Sekondari Nyeruma, ni uongozi wa Halmashauri ya Wilaya kwenda shuleni Nyeruma, kukutana na wajumbe wa Bodi ya Shule, Walimu, Wazazi na kusikiliza pande zote. Mapendekezo yaliyofikiwa ni kumhamisha Mkuu wa Shule, kupisha Ukaguzi wa vitabu vya fedha katika shule hiyo. Aidha, hatua zilizochukuliwa kutatua mgogoro wa shule ya Sekondari Muranda, ni kuwafukuza wanafunzi baada ya kukiuka taratibu za 3 shule, kurejesha hali ya utulivu shuleni, kuagiza uongozi wa shule kuitisha Kikao cha Bodi ya shule na kumhamisha Mkuu wa Shule na kupeleka Mkuu wa Shule mwingine. MHE. DR. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, Mheshimiwa Naibu Waziri, ameelezea sifa na vigezo vya hawa wajumbe wa Bodi wa Shule za Sekondari. Kwa kuwa, matatizo yaliyojitokeza Mwibara, yanafanana na shule nyingi za sekondari hapa nchini na kwamba baadhi ya Wajumbe wa Bodi, wanatoka maeneo ambayo ni mbali na zilipo shule na hivyo kuchochea mfumuko wa gharama za kuwahudumia wanapokuja kwenye mkutano wa Bodi. Je, ni kwa nini Serikali isingeona umuhimu wa kuainisha zaidi vigezo vya Wajumbe wa Bodi watokane na maeneo ambayo wananchi au wana jamii waweze kushiriki katika kuwachagua ili waweze kuteuliwa kwenye hizi Bodi, badala ya kumwachia Mwalimu Mkuu, kuteua watu ambao yeye anadhani wanafaa kufanyanao kazi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dr. Raphael Chegeni, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, labda kwanza nieleze kwamba ilikuwaje, halafu na sasa ikoje. Mheshimiwa Spika, zamani aliyekuwa anawateuwa wajumbe wa Bodi, alikuwa ni Waziri mwenye dhamana, yaani maana yeke ni kwamba Profesa Maghembe ndiye angekuwa anawateuwa, lakini sasa alichofanya amekasimu madaraka yale yakawa yanapitia kwa ma-REO.Wale Wakuu wa Shule walioko pale walichoagizwa ni kwamba wahakikishe, na hapa nimeisoma, kwamba wale wanaowateuwa na wale wanaowapendekeza ambao hatimaye watapelekwa mpaka kwa Mheshimiwa Waziri, wawe ni watu wanaotoka katika maeneo yale na ni watu ambao wanaweza wakapatikana. Mheshimiwa Spika, sasa msisitizo ambao anauweka hapa, mimi ninauona. Kwa sababu ukisema wajumbe wa Bodi kama ni wa Manyara wakatoka Mtwara, ukawaleta pale ukaanza kuwasafirisha kuwapeleka pale ni kazi ngumu. Lakini nafikiri ninachoweza kukiona hapa ni kwamba Mheshimiwa Mbunge, ana pointi kubwa na anachosema ni kwamba tuhakikishe kwamba wanatoka katika Mkoa uleule. Lakini hata kama wanatoka katika Mkoa uleule anachosisitiza yeye ni kwamba watoke pale karibu na shule ili waweze kuisaidia shule. Mimi ninalichukua hili na ninajua kwamba tutafanya mawasiliano na Mheshimiwa Waziri wa Elimu, ili tuweze kuona kwamba hilo linafanyika kama anavyoshauri. MHE. JUMA H. KILLIMBAH: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, sasa hivi kuna wingi wa shule hizi za Sekondari hasa kwenye maeneo ya Kata. Na kwa kuwa, mara nyingi uteuzi kama anavyoeleza, utaratibu wa kuchukua watu wanaotoka maeneo yaliyo karibu na wanaopatikana katika Mkoa huo uko sahihi, lakini liko tatizo moja kubwa juu 4 ya uelewa wa wajibu wao katika kufanya shughuli katika Bodi hizo. Na mara nyingi wanaonekana kuburuzwa na walimu kwa sababu hawaelewi wajibu. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inawaelimisha ili kuondoa hiyo tofauti iliyopo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Killimbah, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, labda hili nalo nilisemee. Ni kwamba kwanza kabisa ushauri unaotolewa hapa, ukimpleka mtu anayeingia katika Bodi ya Shule, minimum qualification walao awe amemaliza Form IV. Ukifanya hivyo inakusaidia sana uelewa, kwa sababu hata kama utapeleka watu wa pale ni lazima uwe na watu ambao wataelewa watakapoeleweshwa. Lakini mara kwa mara, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na TAMISEMI, tumekuwa tunatoa Semina kwa ajili ya wajumbe hawa ili waweze kuongeza uelewa wao. Kwa hiyo, hili analolisema Mheshimiwa Killimbah, tunakubaliana na yeye na tutafanya hivyo. Lakini suala la qualification hapa kwa wajumbe, nalo ni muhimu pia. (Makofi) MHE. SIJAPATA F. NKAYAMBA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Kata nyingi sasa hivi zina Sekondari na zote zimeshafikia Form IV. Na kwa kuwa, wanafunzi wanapoanza Form I, huwa wanaambiwa wapeleke meza na viti. Je, vile viti vingine huwa vimeenda wapi? SPIKA: Amechomekea tu, lakini labda Mheshimiwa Waziri wa Elimu; maana hili sasa limekuwa mahususi mno. (Makofi/Kicheko) WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nijibu swali la nyongeza. Lakini pia napenda nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa majibu mazuri ambayo ameyatoa katika masali ya awali yaliyoulizwa juu ya suala hili.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    224 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us