Bunge La Tanzania ______

Bunge La Tanzania ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 11 Agosti, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. MUSTAFA H. MKULO): Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Benki ya Uwekezaji Tanzania kwa Mwaka ulioishia Tarehe 31 Desemba, 2005 (The Annual Report and Accounts of the Tanzania Investment Bank Limited for the Year ended 31st December, 2005) NAIBU WAZIRI WA MIPANGO, UCHUMI NA UWEZESHAJI: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. MHE. ADAM K. A. MALIMA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI): Maoni ya Kamati ya Fedha na Uchumi kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji kwa Mwaka wa Fedha Uliopita pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI: Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, pamoja na Maoni kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. SPIKA: Kabla ya kumwita mwuliza swali la kwanza kwa leo natangaza tu kwamba kama ilivyo kawaida wageni tutawatangaza mara baada ya kipindi cha maswali . 1 MASWALI NA MAJIBU Na. 385 Kuboresha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro MHE. DR. OMARI M. NIBUKA aliuliza: - Kwa kuwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ilijengwa wakati wa Mkoloni kwa kukarabati na kuboresha majengo yaliyokuwa ya kituo cha Jeshi wakati huo na kwa kuwa idadi ya vitanda hospitalini hapo ni ndogo kulinganisha na idadi ya wagonjwa wanaolazwa hapo na wakati mwingine hospitali hupokea majeruhi wa ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara: - (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuiboresha hospitali hiyo ili ilingane na wakati wa sasa? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuleta Daktari Bingwa wa Mifupa ili wananchi wapate huduma ya kufaa na ya haraka? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dr. Omari Mzeru Nibuka, Mbunge wa Morogoro Mjini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo: - (a) Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiboresha majengo ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na vifaa vya kutolea huduma mwaka 2004/2005 na 2005/2006 kama ifuatavyo:- (i) Kitengo cha Watoto: Serikali ilikarabati wodi ya watoto na kuweka vitanda 40 na kufanya idadi ya vitanda kuongezeka ikilinganishwa na ilivyokuwa hapo awali. Wodi hiyo imekarabatiwa kwa jumla ya Sh.30,000,000/= na vyumba vya Wauguzi na Madaktari vimeongezwa. (ii) Kitengo cha Wagonjwa wa Akili:Kwa mwaka 2005/2006 ukarabati ulifanywa katika jengo hili kwa kuweka paa jipya na marekebisho haya yamefanywa kwa jumla ya Sh.32,000,000/= . Aidha, kwa mwaka wa fedha 2006/2007 Awamu ya Pili ya ukarabati itahusisha kuweka umeme, kupaka rangi na ununuzi wa samani na vifaa kwa gharama ya Sh.28,000,000/=. Mheshimiwa Spika, kwa kupitia wahisani wa AXIOS Foundation chini ya Mpango wa Udhibiti wa UKIMWI, hospitali imekarabati kitengo cha wagonjwa wa nje kwa jumla ya Sh.11,000,000/=, kitengo cha maabara kwa jumla ya Sh.17,000,000/= pamoja na kufunga viyoyozi. Ukarabati wa kliniki ya mama na mtoto unaendelea kwa 2 gharama ya Sh.10,000,000/=. Pia, vimenunuliwa vifaa vya maabara vyenye thamani ya Sh.10,000,000/=. Mheshimiwa Spika, kupitia wahisani wa Elizabeth Glacier Paediatric Aids Foundation (EGPAF) hospitali imeongeza ukubwa wa kitengo cha wagonjwa wa nje kwa gharama ya Sh.70,000,000/= kazi hiyo bado inaendelea. Hivi sasa Serikali inaendelea kuwasiliana na wafadhili wa Sight Savers International kwa ajili ya kujenga kliniki ya macho. Vile vile, Serikali inafanya juhudi za kupata fedha za ujenzi wa chumba cha upasuaji cha kisasa kitakachokidhi mahitaji ya kuhudumia wagonjwa na majeruhi. (b) Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Hospitali ya Mkoa wa Morogoro haina Daktari Bingwa wa Mifupa. Hivyo, Serikali inajitahidi kutafuta Daktari wa fani hiyo ili asaidiane na Daktari Bingwa wa Upasuaji aliyepo. Tatizo hilo ni la nchi nzima kulingana na ufinyu wa Madaktari wa fani hiyo. MHE. DR. OMARI M. NIBUKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Lakini pia ningependa nimshukuru Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri na yenye kuleta faraja. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri amezungumza kwamba hospitali ile imefanyiwa ukarabati wa wakati kwa wakati. Lakini kama unavyofahamu, suala la ukarabati maana yake haligeuzi miundombinu ya majengo. Kwa ukubwa wa hospitali ile vitanda havitoshi kulingana na idadi ya wagonjwa katika hospitali ile na kwa kufahamu kwamba Hospitali ya Mkoa wa Morogoro hakuna Hospitali ya Wilaya, hospitali ile inatumiwa kama Hospitali ya Rufaa na Hospitali ya Mkoa kwa hiyo itakuwa ina wagonjwa wengi kiasi ambacho haiwezi kukidhi haja. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri haoni kwamba ni wakati muafaka kwa kujenga majengo mapya kwa sababu eneo bado lipo ili angalau kuiongeza Hospitali ya Mkoa wa Morogoro iendane na wakati uliopo sasa? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. SELINA O. KOMBANI): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kwamba ni kweli Hospitali ya Morogoro ni finyu na eneo lake ni dogo. Lakini kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba, Serikali kwa kutambua hilo ndiyo maana inatenga fedha kila mwaka ili kukarabati na kuongeza majengo katika eneo hilo. Kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, wafadhili mbalimbali wanatafutwa ili kuboresha hospitali hii mara kwa mara na kwa mwaka huu Serikali imetenga pia Sh.75,000,000/= kwa ajili ya ukarabati na matengenezo madogo madogo na kuongeza vitanda katika hospitali hiyo. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge ashirikiane na Uongozi wa Mkoa kuhakikisha kwamba zile fedha ambazo zimetengwa na 3 Serikali zifanye yale mambo muhimu ambayo yataiwezesha Hospitali ya Morogoro kukidhi au kupunguza matatizo yaliyopo katika hospitali hiyo. (Makofi) Na. 386 Huduma za Benki – Itigi MHE. JOHN P. LWANJI aliuliza: - Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mji wa Itigi una wafanyakazi wengi kwa mfano katika Taasisi kama St. Gasper Hospital, Sekondari, Reli Shule za Msingi, Misitu na kwa kuwa kuna wakulima na wafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Itigi wenye vipato vizuri vya fedha kutokana na Mifugo, Alizeti, Tumbaku, Mbao, Asali, Nta na Machimbo ya Gesi:- Je, ni lini Serikali itaweka huduma za benki Itigi Mjini ili kuokoa muda na gharama za usafiri wa kwenda Manyoni Mjini kila siku kufuata huduma za Benki kitu ambacho pia kinavutia majambazi? NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. MUSTAFA H. MKULO) alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa John Paul Lwanji, Mbunge wa Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo: - Mheshimiwa Spika, Sera ya Serikali ni kujiondoa katika shughuli za kibiashara. Hivyo, haiwezekani kwa Serikali kutoa ahadi ya lini huduma za Benki zitafikishwa Itigi. Serikali inachofanya ni kuweka mazingira muafaka kwa Sekta Binafsi kufanya shughuli hizo. Hivyo, wananchi wote wakiwemo wale wa Itigi wanahamasishwa kujiunga pamoja na kuanzisha Benki au Taasisi ya Fedha. Benki Kuu iko tayari kupokea ombi la kuanzishwa Benki au Taasisi ya Fedha kutoka kwa wananchi wa Mji wa Itigi. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu inayohitajika katika kuweka mazingira ya kiuchumi, sheria na miongozo imara itakayowawezesha wananchi kuungana na kuanzisha Benki au Taasisi za Fedha katika maeneo yao. Mheshimiwa Spika, wakati Bunge lako Tukufu likipitisha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 swali kama hili lilijitokeza. Tuliahidi kufanya kikao na Benki Kuu na Mabenki. Kikao hiki kilifanyika mwishoni mwa Mei, Mabenki yote yamekubali kutazama suala hili na wataleta taarifa yao kwa Waziri wa Fedha mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2006. Ni mategemeo yangu kwamba kutakuwepo na pendekezo la kuweza kusaidia sehemu ambazo hazina Benki. MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha, napenda kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa miaka michache iliyopita CRDB iliwahi kufika Itigi na kuangalia hali ya uchumi ya wananchi wa Itigi na Tarafa nzima ya Itigi na wakaona kwamba wana uwezo mzuri wa kiuchumi na wakaona kwamba kuna uwezekano wa kufungua Benki, 4 lakini mpaka leo hawajafanya hivyo. Je, Wizara iko tayari kutusaidia kuwashawishi hawa watu wakafungua Benki? NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. MUSTAFA H. MKULO): Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika swali la msingi, CRDB ni mojawapo ya Benki 30 ambazo tulikutana nazo pamoja na Wizara ya Fedha na Benki Kuu na CRDB pia iliahidi kuangalia, si sehemu ya Itigi tu, lakini kuna maeneo mengi ambayo wameomba wapelekewe huduma za Benki. Ni matumaini ya Serikali kwamba ifikapo tarehe 31 Oktoba, 2006 Benki Kuu itakuja na taarifa Serikalini ya kuonyesha jinsi gani Mabenki yanaweza kujiandaa kushiriki sehemu ambazo pengine hakuna faida kama vile wanavyopata sehemu ambazo sasa hivi wapo. Na. 387 Mahitaji ya Benki Simanjiro MHE. DORAH H. MUSHI aliuliza: - Kwa kuwa Mji wa Mererani una wakazi wengi wakiwemo wachimbaji wakubwa (Tanzania One) na wachimbaji wadogo wadogo, Tanzania Africa Ltd, wafanya biashara wa madini ya Tanzanite, vikundi vya uzalishaji vya akinamama kama SACCOS, CEDHA na Pride Tanzania, lakini hakuna huduma ya Benki na vikundi vyote hivyo vinahitaji huduma hiyo na kwa sababu huduma hiyo haipo hivyo hulazimika kuifuata Arusha Mjini ambapo ni mbali sana:

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    138 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us