Tarehe 9 Mei, 2019

Tarehe 9 Mei, 2019

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 9 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. ASHA MSHIMBA JECHA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2018/ 2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. QAMBALO W. QULWI – NAIBU MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Kuhusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea. Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Manyoni Magharibi sasa aulize swali lake. Na. 196 Serikali Kuzipatia Waganga Zahanati za Jimbo la Manyoni Magharibi MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Wananchi wa Manyoni Magharibi kwa kushirikiana na Serikali kupitia miradi mbalimbali ikiwemo TASAF wamejenga zahanati katika Vijiji vya Gurungu, Sanjaranda, Kitopeni, Ipande, Doroto, Itagata, Kalangali, Makale, Mwamagembe na Kintanula, lakini mpaka sasa zahanati hizi hazina Waganga:- Je, ni lini Serikali itazipatia zahanati hizo Waganga, ili wananchi wapate huduma kufuatana na sera yake? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA)alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika kwa Mwaka wa Fedha 2017/ 2018 na 2018/2019 Serikali imeajiri watumishi 8,444 wa afya katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambapo watumishi 46 walipangwa kwenye vituo vya afya na zahanati katika Jimbo la Manyoni Magharibi. Zahanati za Gurungu, Sanjaranda, Kitopeni, Ipanda, Doroto, Itagata, Kalangali, Makale, Mwamagembe na Kitanula zimepatiwa Waganga na wataalam mbalimbali wa afya ambao wanatoa huduma hadi hivi sasa. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya vituo vya afya vya kutolea huduma za afya sambamba na kuajiri wataalam wa afya kwa awamu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Yahaya Massare, swali la nyongeza. MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali na tumeona kweli Serikali sasa imeonesha nia ya kupunguza kadhia hii ya watumishi wa kada ya afya. Nina maswali madogo mawili ya nyongeza:- Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, dhamira ya Serikali, lakini na wananchi katika Jimbo la Manyoni Magharibi, Halmashauri ya Itigi ni kujikwamua, wameanza kutumia nguvu zao katika kujenga zahanati na vituo vya afya katika vijiji vyao, lakini nguvu zao zinaonekana kuisha. Je, Serikali iko tayari sasa kuwasaidia wananchi wa vijiji ambao wameanza kujenga zahanati kwa nguvu zao? 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika swali ambalo niliuliza mwaka jana kipindi kama hiki majibu ya Serikali ilikuwa yameonesha kwamba na Hansard iko hapa ninayo kwamba, Serikali ilikuwa imetenga milioni 600 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, lakini hadi tunapozungumza leo hii bajeti nyingine ya Wizara ya TAMISEMI ilishasomwa, hospitali hii bado hatujaletewa pesa. Je, Serikali iko tayari sasa basi kupeleka hizi pesa ambazo iliahidi na wananchi walisikia kwamba zitapelekwa katika Halmashauri ya Itigi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na nimpe pole sana kwamba, alipata ajali mbaya hivi karibuni, lakini pamoja na kwamba, alikuwa na machungu ya maumivu aliweza kuwakumbuka wananchi wake wa Manyoni na akaanza kuandika swali hili ambalo nalijibu hapa leo. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nijibu maswali ya nyongeza mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, sisi Serikali tunahimiza wananchi na wenyewe Waheshimiwa Wabunge wamekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wananchi kushiriki kujenga vituo vya afya na zahanati na kuna maboma mengi. Naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, jitihada na nia ya Serikali iko palepale, kadri ambavyo uwezo utapatikana tutapeleka fedha za maboma, lakini pia kupeleka wataalam na vifaa tiba ili kuweza kuboresha huduma za wananchi wetu katika maeneo yao na hii itakuwa ni kwa nchi nzima. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, anauliza habari za hospitali yake ya Itigi; naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaendelea kuliangalia hili kulingana na uwezo wa Serikali. Kama mwaka huu bajeti hii haikupelekwa katika eneo lake la Hospitali ya Itigi kama alivyotaja Mheshimiwa Mbunge, basi tunalichukua kulifanyia kazi ili wakati ujao aweze kupata fedha na kuweza kupata huduma na kuboresha hospitali yake ya wilaya. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa swali la nyongeza. MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Nitangulize kutoa shukrani za wananchi wa Bagamoyo kwa juhudi kubwa ya Serikali katika kuboresha huduma ya afya. Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Bagamoyo kwa muda mrefu sana wamehangaika na ujenzi wa zahanati katika Vijiji viwili, kimoja cha Buma Kata ya Kilomo, kingine Kitame katika Kata ya Makurunge. Hivi sasa zahanati ya Makurunge imekamilika na Buma wakati wowote tutamaliza, tunamalizia ujenzi wa choo. Swali langu kwa Mheshimiwa Waziri, je, ni lini tutaweza kupatiwa watumishi na vifaa tiba katika zahanati hizi kwa kuzingatia kwamba, kwa muda mrefu wananchi hawa hawajapata huduma? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Bagamoyo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshaomba kibali maalum kwenye Ofisi, Wizara ya Utumishi cha kuajiri Madaktari, Waganga na Wauguzi. Naomba nimwahidi 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mbunge kwamba, maeneo yote ambayo zahanati zimekamilika na vituo vya afya ambavyo vinajengwa nchi nzima na hospitali za wilaya na pale palipo na upungufu mkubwa tutazingatia maeneo hayo ikiwepo na eneo lake la Bagamoyo na zahanati mbili ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Venance Mwamoto, swali la nyongeza. MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, Wilaya ya Kilolo inapitiwa na barabara kuu (High Way) kutoka Tanzania kwenda Zambia, lakini pia ni barabara ambayo ukitoka Mikumi ni mpakani na Ruaha Mbuyuni mpaka ukifika Ilula ni kilometa zaidi ya 200, lakini hapo hakuna kituo cha afya. Mara nyingi accidents zimekuwa zikitokea, wananchi wa Mbeya, Malawi, Zambia, wamekuwa wakipata matatizo na wamepoteza maisha kwa sababu, inabidi waende wakatibiwe Iringa Mjini ambako ni mbali; na kwa kuwa, wananchi sasa wa Ruaha Mbuyuni wameonesha nia ya kujenga Kituo cha Afya, je, Serikali itakuwa tayari kuwasaidia kwa haraka ili kuokoa maisha ya watu ambao wamekuwa wakiyapoteza pale? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge Venance Mwamoto, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwa swali mojawapo la nyongeza hapa, hivi leo asubuhi kwamba, ni nia ya Serikali kuendelea kuboresha huduma za afya na 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja yatazingatiwa katika kuboresha. Kama wananchi wamechukua juhudi za kuanza ujenzi tunawapongeza sana, sisi kama Serikali tuko pamoja nao na mimi hivi karibuni nitaenda kutembelea Jimbo la Mheshimiwa Mwamoto. Hivyo nitaomba tutembelee eneo hili tuone juhudi za wananchi ili tuweze kutia nguvu katika eneo hilo. Ahsante sana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Paschal Haonga, swali la nyongeza. MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Mji Mdogo wa Mlowo ulioko Wilaya ya Mbozi una wakazi wapatao elfu 70 na zaidi, lakini bahati mbaya sana mji huu una zahanati tu ambayo inahudumia watu hao zaidi ya 70,000. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kujenga kituo cha afya ili kuweza kuwahudumia wale wananchi ambao ni wengi na wanapata tabu sana na wanasumbuka wakati wa kupata matibabu? NAIBU SPIKA:

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    380 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us