1. SEHEMUA: UFAHAMU Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu mawali yanayofuata. Huenda katika bara zima la Afrika, Kenya ndiyo nchi yen ye uwanja mpana sana wa aina ya muziki. Kenya ina makabila zaidi ya arobaini na kila kabila lina aina yake ya muziki. Hata hivyo, kwa muda mrefu sana wakenya hawakuuenzi muziki wa kikenya. Katika miaka ya sabini na themanini muziki uliovuma sana nchini ulikuwa ule wa kutoka taifa la kidemokrasia la Kongo au Zaire, kama ilivyojulikana wakati huo. Wanamuziki wa kutoka huko walivuma sana hapa nchini na hata vikundi vingi vya kutoka huko vilipiga kambi nchini humu na kubobea katika muziki huku ikiwa ndiyo njia yao ya kuzumbua riziki. Siku hizo wanamuziki kutoka Zaire walienziwa sana hapa nchini na walikuwa na soko kubwa sana la muziki wao hapa. Haikuwa ajabu kuwapata wakenya wakiimba muziki wa kizaire bila hata ya kujua maana ya maneno waliyokuwa wakiimba. Mwanamziki Franco ndiye aliyetambulika sana hasa kwa muziki wake taratibu na sauti yake nzuri iliyowaongoa watu wengi. Kila alipozuru Kenya kuimba wafuasi wake wengi walimiminika ili kumsikiliza na kuufurahia muziki wake. Popote alipoenda watu walifurika na kulipa pesa nyingi zilizotozwa kama kiingilio. Umaarufu wake ulikuwa kiasi kwamba kila alipozuru mji wa Kisumu, mashabiki wake waliuvunja ukuta wa uwanja wa mpira ili kupata kuingia. Wengine waliovuma ni Sam Mangwana, Tabu Ley, Mbilia Bel, Kanda Bongoman na Pepe Kalle. Hata hivyo katika miaka ya tisini, wingu jipya la muziki lilianza kuvuma kwani muziki wa kizaire ulianza kupoteza mvuto wake kwa wakenya. Waimbaji wengi hawakuweza kuvutia mashabiki kama ilivyokuwa awali na wengi walikata guu kukanyanga Kenya kwani pesa walixopata haiikuwa nyingi. Wingu hili Ulikuwa la wakenya kuanza kuuenzi muziki wao wenyewe. Wengi hasa vijana waliuonea fahari muziki wa Kenya na wakajitenga na nyimbo za kutoka Zaire. Muziki wa Kenya ukaanza kukua na hata kutawala katika vyombo vya habari kama redio, runinga na hata magazetini. Hapo ndipo kulipotokea vijana barobaro waliouteka uwanja wa muziki kwa vishindo. Vijana hawa ambao walifana sana katika muziki wa kufoka waliweza kujidhihirisha kama wanamuziki bora na wakawa na wafuasi wengi miongoni mwa vijana. Kwa mara ya kwanza, muziki ukaanza kuchukuliwa kama taaluma nyingine yoyote ambayo mtu angeweza kuitegemea ili kuzumbua riziki. Hapo ndipo kukatokea muziki wa genge na kapuka ulioasisiwa na vijana kutoka jijini Nairobi kama Jua Cali, Nonini, Jimwat, Bamboo, Nameless, Pilipili, Lady S, Jaguar na wengine. Muziki wao uliweza kuteka nyoyo za vijana kwa maana unaimbwa kwa lugha ya "Sheng" ambayo ni mchanganyiko wa Kiingereza na Kiswahili. Muziki huu ulichukua mtindo wa kufoka ambao unatumiwa sana na wanamuziki wengi wa Kimarekani ambao unawapendeza sana vijana. Isitoshe, vijana hawa waliimba muziki uliosheheni mambo yanayowahusu vijana. Muziki wa genge na kapuka hauwavu'tii tu vijana pekee bali hata watu wenye umri wa makamo. Hivi sasa wengi wa waimbaji hawa wanautegemea muziki kuwapa pato na si Eleza maana ya msamiati ufuatavyo, kama ulivyotumiwa katika kifungu hiki. ( alama 4) (i) kubobea ' (ii) lliyowaongoa (iii) muzikiwa kufoka (iv) Kuzumbua 2. Muhutasari soma kifungu hiki kish aujibu maswliyanayofuata Mungu ameumba wanawake wote na hisia za uzazi na kila mwanamke huwa na hamu na ghamu ya kumkopoa mwana wake mwenyewe, kumpakata, kumnyonyesha na kumlea kwa vitanga vya mikono yake hadi ukubwani. Ni nadra sana kupata mwanamke asiye na hisia za uzazi. Mjo wa mtoto hubadilisha maisha ya mama milele kwani humbidi kila wakati kumwazia maslahi yake. Hata hivyo, japo kicheko cha mtoto ni anga la nyumba, kutojitayarisha kwa kuja kwa mtoto hufanya maisha yawe na ugumu. Sharti mama mjamzito ajiweke tayari kwa kumpokea yule malaika na ni jukumu la mume pamoja na jamii kurnsaidia mjazito yule. Sharti mjamzito awe amejitayarisha vilivyo kuibeba mimba na kuilea vizuri hadi kujifungua. Ni muhimu sana mama awe tayari kiakili na kihisia kwa sababu katika miezi tisa ya ujauzito mama hupitia mabadiliko mengi ya kimwili na kihisia. Tamaa ya chakula hubadilika na kuna baadhi ya vyakula ambavyo huvikataa huku akivipenda vingine kupindukia. Kukua vizuri kwa mtoto hutegemea sana hali ya afya na hisia za mama. Mama anopokaa katika mazingira yanayomhuzunisha kila mara basi mtoto huathirika. Mimba ina majukumu, matarajio na wajibu mwingi unaohitaji mtu kuwa tayari kwa mimba ile. Kwa hivyo, mama akiwa katika ndoa nzuri yenye furaha na mapenzi ya dhati basi mimba ile itakuwa bila matatizo. Hii ni kumaanisha kuwa iwapo mimba ilikuwa ya ajali huenda mjamzito hajaikubali na ujauzito ule huwa na change moto chungu nzima. Watafiti wanadai kuwa akiwa tumboni mtoto aweza kujua hisia za mamake kwa hivyo mama akifurahi yeye hufurahi na vivyo hivyo mama akihuzunika pia mwana huhuzunika. Pia, sharti mzazi awe na uwezo wa kiuchumi wa kushughulikia mimba na mtoto pia atakapozaliwa. Kinyume na- ijivyokuwa hapo awali, kupata mtoto kuna gharama kuu ( b ) Elez a mamb o ambay o mwanamk e mjamzit o anafa a kuzingatia . ( Manen o 55-60 ) ( alam a 5 ) Matayarish o Jib u 3 . Matumiz i y a lugh a ( a ) To a mfan o mmoj a wa : ( alam a 2 ) ( i ) kizui o - kwamiz a ( ii ) Kimadend e 7 ( ii ) Nomin o ( o ) Elez a matumiz i y a kiambish i 4 ku ' katik a sentens i ziftiatazo : ( alam a 2 ) ( i ) kuchez a kuzur i hutuzw a ( ii ) Mwalim u anakyjt a ( p ) Mshazar i hutumiw a katik a kuteng a tarehe , mwez i n a mwaka . Onyesh a matumiz i mengin e matat u y a mshazar i ( alam a 3 ) ( q ) Bainsish a mofim u katik a neno : ( alam a 2 ) Wataend a 5 4 . Isimujami i ( alam a 10) ( a ) Nin i maan a y a usanifishaj i 1 0 Elez a sabab u nn e zilizochangi a usanifishaj i w a lugh a y a Kiswahil i ( alam a 8 ) HU U NDI O UKURAS A W A MWICH O ULIOPIGW A CHAPA . .
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages9 Page
-
File Size-