NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI Kikao cha Nane – Tarehe 4 Februari, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Tunaendelea na Kikao chetu cha Nane katika Mkutano huu wa Pili wa Bunge la Kumi na Moja. Orodha ya Shughuli zetu za leo mnayo. Katibu! HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha (Mapitio ya Nusu Mwaka 2015/2016 [Monetary Policy Statement (The Mid-Year Review 2015/2016)] 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 92 Watumishi Wasio na Sifa Katika Vituo vya Afya na Zahanati Nchini MHE. RIZIKI S. MNGWALI aliuliza:- Kumekuwa na tatizo sugu nchini kwa baadhi ya vituo vya afya na zahanati kuwa na watumishi wasio na sifa za utabibu:- Je, Serikali inatumia vigezo gani kuwapeleka watumishi wasio na sifa katika zahanati na vituo vya afya? MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri (TAMISEMI). Subiri kidogo Mheshimiwa Waziri. Waheshimiwa Wabunge, jana tulipewa taarifa kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu leo hatakuwepo Bungeni kwa sababu yupo nje ya Dodoma. Kwa mujibu wa Kanuni zetu yeye ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni na Serikali imo humu. Mheshimiwa Waziri Mkuu anapokuwa hayupo Dodoma, anaweza kuwa ofisini lakini yupo, anapokuwa nje ya Dodoma, Kanuni zinataka awepo Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Kwa leo Mheshimiwa William Lukuvi ndiye Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Tunaendelea, Naibu Waziri TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo. (Makofi) NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), napenda kujibu swali la Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu ambao unatumika kuajiri watumishi wa kada za afya ni kuwapanga moja kwa moja kwenye vituo vya kazi kadiri wanavyohitimu na ufaulu wa masomo yao. Aidha, ili kuhakikisha watumishi wasio na sifa hawaajiriwi, Serikali imekuwa ikafanya zoezi la uhakiki wa vyeti vyao kabla ya kusaini mikataba ya ajira. Hivyo, endapo Mheshimiwa Mbunge anazo taarifa za kuwepo kwa watumishi wa afya wasio na sifa atusaidie kupata taarifa hizo ili tuweze kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi wa afya, zipo baadhi ya zahanati na vituo vya afya ambavyo vina watumishi wenye sifa tofauti na muundo. Serikali kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) inaendelea kushughulikia changamoto hii ambapo tayari mikoa tisa yenye upungufu mkubwa zaidi wa watumishi imetambuliwa na kupatiwa kipaumbele cha kuwaajiri watumishi wa afya. Vilevile Serikali imepanga kuangalia maeneo yenye mlundikano wa watumishi ili kuweka uwiano wa watumishi baina ya zahanati na vituo vya afya vilivyopo mijini na vijijini. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Riziki. MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi na kwa niaba ya wananchi wa Mafia niulize maswali ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoa majibu ambayo hayatoshelezi sana, namuuliza Mheshimiwa Waziri kama ataichukulia kesi ya Mafia kuwa ni special case ambayo inahitaji kushughulikiwa kwa haraka? Hili liko katika zahanati ya Chemchem ambapo zahanati imepewa jukumu la kuwa kituo cha afya kwa maana ya kushughulikia vijiji zaidi ya kimoja lakini ina mhudumu wa afya badala ya tabibu ambaye anahudumia wananchi. Je, analichukulia jambo hili kuwa ni suala la dharura na kwa hiyo atupatie tabibu haraka iwezekanavyo? Mheshimiwa Mwenyekiti, ataichukulia pia kama ni special case Zahanati ya Chunguruma ambapo pamoja na kumuweka Mkunga mwenye sifa lakini ni mwanaume. Je, atatupelekea haraka Mkunga mwanamke katika Zahati ya Chunguruma ili wanawake wa Mafia wapewe huduma stahiki? Ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nataka tu niwakumbushe Kanuni zetu bado ni wageni, Kanuni ya 44(4) haituruhusu kusoma maswali unauliza tu moja kwa moja. NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeisikia changamoto hii na umezungumzia Zahanati ya Chechem na Chunguruma. Kama nilivyosema pale awali, ni kweli, ukiangalia Mafia ina Hospitali ya Wilaya na tuna zahanati takriban 16. Changamoto yake ni kwamba zinazo-function vizuri ni zahanati tano. Kwa hiyo, tuna upungufu mkubwa zaidi katika zahanati zipatazo 11. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili nini cha kufanya sasa, ndiyo maana Wilaya ya Mafia sasa hivi imepewa kibali cha kuajiri watumishi wapatao 18 lakini katika hilo kipaumbele cha awali ni kuajiri Clinical Officers ili ku-cover maeneo yale ambayo tunaona kuna watu ambao hawastahili kufanya hizo kazi lakini 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) kutokana na changamoto iliyopo wanafanya kazi ambazo ziko nje ya kada yao. Kwa hiyo, tunalifanyia kazi hilo suala hilo na tunaishukuru Ofisi ya Utumishi imeshatupatia kibali. Si muda mrefu sana baada ya ajira hiyo watumishi hao wataweza kufika katika zahanati hizo ili waweze kutoa huduma. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika hili tumejielekeza, asubuhi tulikuwa tunawasiliana na RAS wetu wa Mkoa wa Pwani. Changamoto ya jiografia ya Mafia utakuta watumishi wengi sana wakipangwa wengine wanasuasua kufika. Tumeelekezana na RAS wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha watumishi wote wanaotakiwa kufika Mafia hasa katika sekta ya afya waweze kufika ili wananchi wote wanaotakiwa kupata huduma waweze kupata huduma. Lengo letu kama Serikali ni kuhakikisha afya hasa ya mama na mtoto inalindwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya kwamba mhudumu mwanaume ndiye anayetoa hiyo service, tumelichukua hili. Nadhani ni angalizo kwa sisi watu wa Serikali japokuwa watu wa afya hasa Madaktari kazi zao wanafanya sehemu zote lakini tunatoa kipaumbele kwa akinamama. Inawezekana magonjwa mengine anapohudumiwa na baba inakuwa ni changamoto kubwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tulichukue hili na nimwelekeze RAS wetu wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha kwa haraka anafanya juhudi iwezekanavyo kupeleka Madaktari au wahudumu wanawake katika zahanati hii ambayo inaonekana ina changamoto kubwa ili hata mtu akienda katika zahanati ile akiwa mwanamama aone kwamba sitara yake imesitirika. Nashukuru sana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Jitu Soni. MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuiuliza Serikali, je, katika maeneo ambapo sisi kama wananchi na viongozi tumejitahidi, kwa mfano, Kituo cha Afya Magugu tumeweza kuwekeza vifaa mbalimbali ambavyo ngazi hiyo haina mpango au kwa mpango wa Serikali haipeleki wataalam wa aina hiyo, kwa mfano, tuna ultra-sound na vifaa vya macho. Je, Serikali itakuwa tayari mahali ambapo sisi wananchi tumewekeza vifaa mbalimbali ituletee wataalam wa ngazi hiyo? Kwa mfano, Kituo cha Afya Magugu watuletee Madaktari wa Upasuaji wa Macho na wa Ultra-sound kwa sababu vifaa vyote tunavyo na havitumiki. Inabidi tuombe wataalam kutoka mkoani wawe wanakuja mara moja kwa wiki kutusaidia. Je, Serikali itakuwa tayari kutusaidia wataalam hawa? MWENYEKITI: Vifaa wanavyo wanataka wataalam. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nikiri miongoni mwa Wabunge ambao wanafanya kazi kubwa ni Mheshimiwa Jitu Soni. Mwaka juzi nilikuwa ni shahidi Detros Group ya Arusha imesaidia vifaa vyote kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Magugu. Kwa hiyo, juhudi hii amefanya Mbunge akashirikiana na wadau wenzake kutoka Arusha lakini kusaidia Mkoa wa Manyara. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikiri katika mgao wa mwaka huu zoezi kubwa tunalokwenda kufanya, juzi nilijibu swali hapa kwamba mwaka huu mkakati wa Serikali ni kuajiri watumishi wapya wa afya 10,780. Katika watumishi hao wapya ambao tunakwenda kuwaajiri, naomba nikuambie Mheshimiwa Jitu Soni; Kituo cha Afya cha Magugu kitapewa kipaumbele kwa sababu wananchi wa Manyara, Babati Vijijini mmefanya kazi kubwa, lengo letu akinamama wapate huduma bora pale. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya. NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi nitoe tu majibu ya ziada kwamba Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jami ipo kwenye mchakato wa kutengeneza utaratibu wa kuwasainisha mikataba maalum watumishi wote ambao wataajiriwa kuanzia sasa kwa kipindi maalum, kama miaka mitatu ama miaka mitano ili wasiondoke kwenye maeneo ya pembezoni kama ilivyo kwenye Kituo cha Afya cha Magugu. Na. 93 Tatizo la Kudidimia kwa Ardhi kwenye Makazi ya Watu MHE. ALI HASSAN OMARY KING aliuliza:- Tatizo la Mazingira ni tatizo mtambuka na tumeona jinsi Serikali ilivyojipanga kutatua tatizo hili kwenye maeneo tafauti:- Je, Serikali imejipanga vipi kutatua tatizo la mazingira linalojitokeza la kudidimia kwa ardhi kwenye makazi ya watu? NAIBU WAZIRI WA MUUNGANO NA MAZINGIRA (MHE. LUHAGA J. MPINA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ali Hassan King, Mbunge wa Jang’ombe, kama ifuatavyo:- 5 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuwa kumejitokeza tatizo la kudidimia kwa ardhi na nyumba za makazi ya watu kwa vipindi na maeneo tofauti katika maeneo ya Zanzibar hususani 1998 na 2015. Kufuatia matukio haya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliunda timu ya wataalam kutoka sekta mbalimbali ili kufanya utafiti wa kina na kubaini chanzo cha tatizo hili chini ya utaratibu
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages165 Page
-
File Size-