20 MAY 2019.Pmd

20 MAY 2019.Pmd

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Moja – Tarehe 20 Mei, 2019 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo kikao cha 31. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nasikitika kuwatangazia kifo cha mwanasiasa mkongwe na kiongozi aliyepata kuhudumia kwa muda mrefu hasa kule kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Ally Juma Shamhuna. Waheshimiwa Wabunge, katika uhai wake, marehemu Ally Juma Shamhuma amepata kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo hizi zifuatazo; amepata kuwa Mkurugenzi wa Mifugo, amewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, amewahi kuwa Katibu Mkuu, Export Processing Zone Zanzibar, amewahi kuwa Waziri wa Mipango, amekuwa Waziri wa Nchi, Afisi ya Waziri Kiongozi, aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na wakati huo huo akiwa ni 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Naibu Waziri Kiongozi, katika uhai wake amekuwa Waziri wa Ardhi, Maji na Nishati na alipata kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali. Aidha, Marehemu Mheshimiwa Shamhuna kwa muda mrefu alikuwa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kutokea Zanzibar na baadhi yenu humu Wabunge mtamkumbuka marehemu Mheshimiwa Shamhuna kama Mbunge wa Bunge la Katiba na alikuwa Mjumbe wa Kamati namba 8 kwenye Bunge la Katiba, Kamati ambayo nilikuwa Mwenyekiti wake. Kwa niaba yenu Waheshimiwa Wabunge, tunatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Tunatoa pole kwa Wazanzibari wote na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia kifo hicho na tunamuomba Mwenyezi Mungu aihifadhi roho yake mahali pema peponi, amina. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Abdallah Ulega. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali. Swali la kwanza linaelekezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, litaulizwa na Mheshimiwa 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Tauhida Cassian Galoss. Mheshimiwa Tauhida uliza swali lako tafadhali, kwa niaba yake. Na. 252 Mgogoro Kati ya Kituo cha Polisi Bububu na Soko MHE. ASHA ABDULLAH JUMA (K.n.y. MHE. TAUHIDA CASSIAN GALOSS) aliuliza:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua mgogoro wa muda mrefu kati ya kituo cha polisi Bububu na soko dogo la wananchi lililopo karibu na kituo hicho? (b) Je, kiutaratibu umbali kati ya kituo cha polisi na makazi ya wananchi ni hatua ngapi? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Engineer Hamad Masauni tafadhali. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tauhida Cassian Galoss, Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, si kweli kuwa kuna mgogoro wa kiwanja kati ya wananchi na Jeshi la Polisi katika eneo la kituo cha polisi Bububu. Ndiyo sababu wakazi wa eneo hilo ikiwemo wafanyabiashara wa soko hilo dogo hupata huduma za kiusalama katika kituo cha Bububu bila shaka yeyote. Aidha, kiwanja kilipojengwa kituo cha polisi Bububu na majengo mengine ya kituo yanamilikiwa kihalali na Jeshi la Polisi ingawa kuna kibanda cha kuuza samaki karibu na kituo hicho cha polisi kinachoitwa soko dogo la wananchi. Kibanda hicho kipo kati ya kituo cha Polisi Bububu na majengo mengine ya kituo. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, ni kweli upo utaratibu wa kuwepo kwa umbali kati vituo vya polisi, kambi za makazi ya askari ya wananchi. Hii ni kutokana na sababu za kiusalama kwa miundo mbinu ya Jeshi la Polisi. Aidha, kutokana na changamoto za makazi na ujenzi holela mijini. Uvamizi wa maeneo sehemu mbalimbali na kuongezeka kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu zisizo rasmi imesababisha maeneo mengi ya vituo vya polisi kuingiliwa na kusogeleana na makazi ya wananchi. SPIKA: Mheshimiwa Asha Abdullah Juma nimekuona. Swali la nyongeza. MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kupata nafasi hii, nashukuru sana Mheshimiwa Waziri wa majibu yako mazuri lakini nitakuwa na suala moja la nyongeza. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa muingiliano umekuwa mkubwa na watu wamekuwa wengi, kwanini hiki kituo kisitafutiwe sehemu nyingine, kikajengwa huko, kikawa na nafasi kubwa kikaelekea kama kituo kweli cha polisi kuliko pale kilivyokaa, hakijapendeza wala haifai. Huku kituo, huku soko, nafikiri Serikali ifikirie kukihamisha kikapate nafasi kubwa zaidi na majengo ya kisasa yaliyokuwa bora zaidi. Ahsante. SPIKA: Swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani, tunaomba majibu Mheshimiwa Engineer Hamad Masauni tafadhali. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na hoja ya kuhamisha kituo hiki kwa sababu ya ufinyu wa nafasi kiusahihi ni kwamba eneo la kituo lile ni kubwa mno, labda Mheshimiwa Mbunge tukipata nafasi tukatembelee ili nimuoneshe. Ni juzi tu hapa kuna eneo ambalo liliwahi hata kupewa mwekezaji na kutokana na maelekezo ya Mheshimiwa Rais ya kwamba maeneo ya vyombo vya usalama yabakie kwa matumizi ya vyombo hivi tulitoa maelekezo na kuhakikisha kwamba tumemhamisha yule mwekezaji. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, lakini utakumbuka pia hata eneo ambalo liko pembeni ya kituo cha polisi ambacho kimetumika kama soko kama alivyozungumza kwenye swali la msingi ni eneo pia la polisi ukiachia mbali eneo la nyuma ambalo ni kubwa. Kwa hiyo, kimsingi kuhamisha kituo hiki kwa sababu ya ufinyu wa eneo nadhani haitakuwa sahihi kwa sababu kuna eneo la kutosha. Cha msingi ni kuendelea kutoa wito kwa wananchi kutumia nafasi yao yoyote ya kuvamia maeneo ya polisi kuacha maeneo ya polisi yaendelee kutumika kwa ajili ya shughuli za kiusalama. SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Paulina Gekul, uliza swali lako tafadhali. MHE. PAULINA P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri kwanza nikushukuru kwa kutupatia zile 150,000,000 ambazo zimetusaidia kujenga majengo ya polisi katika eneo la Bagara Ziwani na nyumba zinakamilika. Mheshimiwa Spika, sasa eneo hilo halijawahi kufidiwa, wananchi hawajawahi kufidiwa tangu 2004, polisi wanajenga majengo yao, wananchi hawajalipwa fidia tangu 2004. Nini kauli ya Serikali juu ya wananchi hawa ambao wametoa eneo kwa polisi lakini hawajapatiwa fidia mpaka leo? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Engineer Masauni tafadhali. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa tunachukua pongezi kama Serikali kutokana na kazi ambayo inaendelea nchi nzima maeneo mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za askari polisi. Mheshimiwa Spika, la pili nimpongeze yeye binafsi kwa kufuatilia kwa karibu hii kadhia ya wananchi wake kutolipwa fidia. Hata hivyo, naomba nimhakikishie kwamba jambo hilo nimelichukua na tutalifanyia kazi na baadaye tutarudi kwake kuweza kumpatia majibu ya hatua ambazo zimefikiwa na 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) changamoto gani kama zipo na nini mikakati ya Serikali katika kukabiliana na changamoto hizo ili hatimaye wananchi hawa waweze kupata fidia stahiki. SPIKA: Bado tupo Wizara hiyo hiyo Waheshimiwa Wabunge, swali lifuatalo litaulizwa na Mheshimiwa Rehema Juma Migilla. Mheshimiwa Rehema. Na. 253 Polisi Kukamata Bodaboda na Kutoa Baadhi ya Vifaa MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Pamoja na jitihada za vijana wengi kujiajiri wenyewe kwa kuendesha bodaboda wamekuwa wakisumbuliwa na polisi kwa pikipiki zao kukamatwa mara kwa mara:- Je, kwa nini pikipiki zao zinapokamatwa na wanapoenda kuzichukua hukuta baadhi ya vifaa kama betri hazipo? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, kwanini pikipiki zikikamatwa betri zinaibiwa? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rehema Juma Migilla, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168 iliyorejewa mwaka 2002 inampa mamlaka Askari Polisi kusimamisha chombo chochote barabarani na kukikagua kubaini kama kina makosa na hatimaye kukizuia na kukamata. Chombo cha moto kinapokamatwa hutunzwa kituoni kwa mujibu wa mwongozo wa Jeshi la Polisi Namba 229. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, inapotokea kielelezo kimeharibiwa uchunguzi hufanyika na hatua kuchukuliwa kwa waliohusika na upotevu huo. SPIKA: Umeridhika? MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini naona majibu haya yamejibiwa kisiasa kuliko uhalisia wenyewe ulioko huko kwa waendesha bodaboda. Mheshimiwa Spika, ni ukweli ulio hai kabisa bodaboda hawa wamejiajiri wenyewe na wanafanya kazi katika mazingira magumu na wamekuwa wakisumbuliwa sana na polisi especially hawa PT. Wanawakamata na wakishawakamata hata uchunguzi wa kina haufanyiki na sometimes wanawabambikizia makosa. Wanapowabambikizia makosa wanawaaambia watoe hela, wasipotoa zile hela pikipiki zao zinapelekwa polisi. Zikifika polisi, pindi wanapotaka kuzichukua wanakuta baadhi ya vitu kama betri, mafuta na hata wakati mwingine wanakuta hadi gamba zimebadilishwa na tunaelewa kabisa polisi ni mahali ambapo pana usalama

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    240 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us