MKUTANO WA TATU Kikao Cha Ishirini Na Nane

MKUTANO WA TATU Kikao Cha Ishirini Na Nane

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Nane - Tarehe 25 Mei, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. MWENYEKITI: Ahsante. Katibu! NDG. CHARLES MLOKA - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Maswali, tunaanza na swali la kwanza linaelekezwa kwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI na linaulizwa na Mheshimiwa Joseph Leonard Haule, Mbunge wa Mikumi. 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Na. 229 Ujenzi wa Daraja Kata ya Ruhembe MHE. JOSEPH L. HAULE aliuliza:- Serikali ilifanya tathmini na kuona umuhimu wa kujenga daraja kwenye Kata ya Ruhembe kwa shilingi milioni mia sita lakini mpaka sasa shilingi milioni 100 tu zimepelekwa kwenye Halmashauri ya Kilosa. Je, ni lini kiasi cha shilingi milioni 500 kilichobakia kitapelekwa ili kukamilisha daraja hilo na kuwasaidia wananchi wa Ruhembe wanaozunguka umbali mrefu ili kupata mahitaji yao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Leonard Haule, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha zilizoidhinishwa na Serikali katika bajeti ya mwaka 2014/2015, kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Ruhembe zilikuwa ni shilingi milioni 300 fedha zilizopokelewa hadi Juni, 2015 zilikuwa shilingi milioni 100 ambazo zilitumika kwa ajili ya usanifu wa ujenzi wa daraja hilo. Mkandarasi aliyeomba fedha hizo anahitaji shilingi milioni 600 na hivyo kusababisha mradi huo kutotekelezeka. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya mwaka 2016/2017, zimetengwa shilingi milioni 700 ambazo zitatumika kujenga daraja hilo na kuchonga njia inayounganisha daraja hilo. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Haule! MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza naishukuru sana Serikali kwa kutenga bajeti ya daraja hili la Ruhembe kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017. Hata hivyo, kutokana na kilio na mateso makali pamoja na vifo vya watu wa Ruhembe ambao wamekuwa wakilia kwa muda mrefu, Serikali ipo tayari kuleta pesa hizi kule Mikumi katika robo ya kwanza ya mwaka 2016/2017? MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri upo tayari kutenga? 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nimesema hapa tumetenga shilingi milioni 700 na hii milioni 700 Mheshimiwa Joseph Haule anachosema ni kweli, katika lile daraja tumepoteza watu wengi sana, takribani watu wanane hivi kwa mujibu wa takwimu nilizozipata na mtu mmoja ambaye tumempoteza pale ni mtumishi wa Serikali katika Ofisi yetu ya TAMISEMI. Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba, jambo hili sisi wengine tunalifuatilia na tunalijua vizuri sana. Ndiyo maana tumeona katika suala zima la bajeti, mwaka jana waliomba shilingi milioni 600, lakini kilichopitishwa Hazina ilikuwa ni shilingi milioni 300 na ilikuja milioni 100 peke yake. Katika msisitizo mwaka huu tukaona ile milioni 700 lazima irudi katika bajeti kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo. Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linatugusa sana kwa sababu, wananchi pale wakitaka kuvuka kufika ng‟ambo ya pili ni mpaka watembee au wazunguke karibu kilometa 20. Tatizo ni kubwa, ndiyo maana ofisi yetu sasa imefanya harakati za kutosha kuhakikisha tunawasiliana na wenzetu wa TANROAD na hivi sasa nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunapewa daraja la mudam lile la chuma kupitia ofisi ya TANROAD, si muda mrefu sana angalau liweze kufungwa wakati tukisubiri mpango mrefu kuhakikisha daraja lile linajengwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kufanya hivyo sasa angalau tutapunguza kilio cha watu wa eneo lile na imani yangu kubwa ni kwamba, watu wa TANROAD kuanzia wiki hii sasa muda wowote watakwenda kulifunga ili kuondoa tatizo kwa wananchi wa eneo lile. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Lubeleje swali moja la nyongeza. MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali ya nyongeza. Kwa kuwa katika kipindi hiki cha mvua barabara nyingi sana zimeharibika, mfano, Wilaya ya Mpwapwa; Kata za Matomondo, Lembule, Mlima, Bereje, Mkanana, Londo, Chamanda, Majami mpaka Nana kule. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa kutenga fungu la kutosha kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo kwa sababu zinapitika kwa shida? MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri kwa kifupi. NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAMISEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi na Mheshimiwa Lubeleje hivi karibuni tumekwenda Wilaya ya Mpwapwa pale kutembelea kuangalia baadhi ya huduma zikiwemo huduma za afya, huduma ya shule, takribani wiki mbili na nusu zilizopita. 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nimeona changamoto ya barabara katika maeneo yale, lakini nimesema katika kila mgawanyo wa halmashauri una fungu lake. Jukumu letu kubwa ni hii bajeti iliyotengwa, ikishapatikana basi iende kuweka miundombinu, kwa sababu utengaji wa bajeti ni jambo moja na utekelezaji wa bajeti ni jambo lingine. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sasa hivi Ofisi ya Rais, TAMISEMI tutajielekeza kuhakikisha pesa yote iliyotengwa angalau iweze kufika katika maeneo kwa ajili ya kuhakikisha miundombinu inarekebishwa. Kwa hiyo, Mheshimwa Lubeleje kwa sababu na mimi nilifika kule nimeona hali jinsi gani ilivyo naomba tushirikiane kwa pamoja kuangalia kile kitakachowezekana tuweze kukifanya ili mradi wananchi wa Mpwapwa waweze kupata huduma ya miundombinu ya barabara. MWENYEKITI: Ahsante. Kwa sababu ya muda tunaendelea na swali linalofuata, linaulizwa na Mheshimiwa Deogratias Francis Ngalawa, Mbunge wa Ludewa. Na. 230 Ujenzi wa Daraja Kata ya Ruhembe MHE. DEOGATIAS F. NGALAWA aliuliza:- Serikali ilitoa ahadi ya kutengeneza barabara ya lami toka Itoni – Njombe – Manda na upembuzi yakinifu tayari umeshafanyika. Je, ni lini ujenzi huo utaanza hasa ikizingatiwa kuwa barabara hiyo imekuwa kero kubwa hasa kipindi cha masika lakini pia ni muhimu kwa sababu ya ujiio wa miradi ya makaa ya mawe Mchuchuma na chuma cha Liganga? NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Deogratias Francis Ngalawa, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa barabara ya Itoni – Ludewa hadi Manda yenye urefu wa kilometa 211.4 kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa barabara yameshaanza ambapo kwa sasa barabara inafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, usanifu wa kina kwa sehemu ya barabara yenye urefu wa kilometa 50 kuanzia Kijiji cha Lusitu hadi Kijiji cha Mawengi umekamilika na taratibu za kumpata mkandarasi wa kujenga sehemu hii ya barabara zipo katika hatua za mwisho. Ujenzi wa kiwango cha zege wa sehemu ya Lusitu hadi Mawengi umepangwa kuanza katika mwaka wa fedha 2016/2017. Mheshimiwa Mwenyekiti, usanifu wa kina wa sehemu ya barabara iliyobaki, unatarajiwa kukamilika Julai, 2016. Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kulingana na upatikanaji wa fedha. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ngalawa. MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Juu ya suala la upembuzi yakinifu wa barabara hii limeshakuwa ni la muda mrefu sana. Bahati nzuri tayari hata Mkandarasi alishapatikana na tayari hilo tangazo lilishatolewa toka Desemba, 2015. Sasa leo hii mnapozungumza kwamba, process za kumpata mkandarasi zinaendelea ni mkandarasi gani tena mwingine huyo? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, imeshakuwa ni kawaida kwa Serikali kuwa inatoa utaratibu wa kwamba hiki kitu kitashughulikiwa muda fulani, lakini matokeo yake muda unapita na hicho kitu kinakuwa hakijafanyika. Sasa ningependa kujua kwa sababu 2016/2017 ni muda mrefu, ni muda ambao unachukua miezi 12, wananchi wa Ludewa wangependa wajue ni lini hasa itaanza? MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa nilizonazo kama ambavyo nilisema katika jibu la msingi mkandarasi yupo katika hatua ya mwisho kupatikana. Vilevile ujenzi wa barabara hii atakumbuka kwamba, alisaidia sana Bunge limepitisha bajeti ya Wizara yetu na katika bajeti ile kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hii, kwa hiyo, ujenzi utaanza katika mwaka ujao wa fedha unaoanza tarehe Mosi, Julai. MWENYEKITI: Ahsante. Swali moja la nyongeza Mheshimiwa Paresso. MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Huko nyuma takribani kama miaka sita sasa kumewahi kutolewa ahadi ya kujengwa baadhi ya barabara katika Mji wa Karatu kwa kiwango cha lami na ahadi hii imekuwa ni ya muda mrefu na mara nyingi tumeuliza hapa Bungeni. 5 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ituambie ahadi ile ilikuwa tu ni kuwahadaa wananchi ili watoe kura au mmeshindwa kutekeleza? Tunaomba jibu. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwa kifupi sana. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi zote za Serikali zinaonyesha dhamira

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    262 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us