NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Arobaini na Tisa – Tarehe 16 Juni, 2017 (Bunge Lilianza Saa 03:00 Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Katibu! NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaanza na Ofisi ya Rais – T AMISEMI, Mheshimiwa Bonnah Moses Kaluwa, Mbunge wa Segerea sasa aulize swali lake. Mheshimiwa Shangazi! Na. 399 Kuanzisha Shule za Kidato cha 5 na 6 – Segerea MHE. RASHID A. SHANGAZI (K.n.y MHE. BONNAH M. KALUWA) aliuliza:- Katika Jimbo la Segerea zipo shule kumi na moja za sekondari za Serikali ambapo wanafunzi wa shule hizo wanafaulu vizuri kwa kupata daraja la I, II na III na kuwa na sifa ya kujiunga kidato cha tano. Kwa mfano mwaka 2015 wanafunzi zaidi ya 400 walifaulu kwenda kidato cha tano, 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) lakini katika Jimbo la Segerea hakuna hata shule moja ya kidato cha tano licha ya kuwa na maeneo ya kujenga ya kutosha katika shule za sekondari za Kinyerezi, Magoza na Ilala. Je, Serikali ina mpango gani madhubuti wa kuanzisha shule za kidato cha tano na sita katika maeneo ya shule zilizotajwa ili kuwapunguzia wanafunzi hao adha ya usafiri wanayopata kwa kufuata shule mbali? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bonnah Moses Kaluwa, Mbunge wa Segerea kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina jumla ya shule za sekondari za Serikali 49 zikiwemo shule sita kongwe. Kati ya shule hizo, saba ni za kidato cha tano na sita. Halmashauri inaendelea kuboresha miundombinu ya shule ya sekondari Juhudi ili iwe na Kidato cha tano na sita. Aidha, katika mpango wa muda mrefu Halmashauri imepanga kuanzisha shule sita za kidato cha tano na sita kuanzia mwaka 2017 hadi 2022. Mpango wa Serikali ni kuhakikisha shule hizo zinakuwepo katika kila tarafa nchini. Mheshimiwa Mwenyekiti, shule za kidato cha tano na sita ni za kitaifa ambapo zinachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini, ndiyo maana wanafunzi 400 kutoka Jimbo la Segerea wamechaguliwa kwenda shule mbalimbali nchini. MWENYEKITI: Mheshimiwa Shangazi. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuna maswali mawili ya nyongeza. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Kwa kuwa kama tunavyofahamu Jiji la Dar es Salaam linazidi kupanuka na maeneo ya pembezoni zipo sekondari nyingi ambazo mwisho wake ni kidato cha nne; na kwa kuwa katika Jimbo la Segerea hasa katika eneo la Kinyerezi na Kipawa, bado hakuna Sekondari za kidato cha tano na sita. Je, Serikali haioni kwamba ni wakati sahihi sasa wakupeleka hizi shule za kidato cha tano na sita katika maeneo ya pembezoni? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa swali hili linafanana kabisa na kule Lushoto, hasa Jimbo la Mlalo. Tunazo Tarafa tano katika Halmashauri yetu ya Lushoto, lakini ni Tarafa nne pekee ndio zenye sekondari ya kidato cha tano. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka Tarafa ya Umba na Mlola nazo zipate sekondari za kidato cha tano? Ahsante sana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwa ufupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba Jiji la Dar es Salaam linapanuka, na shule nyingi nyingine zimejengwa pembeni mwa Jiji la Dar es Salaam especial maeneo ya kule Mbondole, Zingiziwa na maeneo mengine. Kwa hiyo nimesema kama ni ile mikakati wa Kiserikali, kwa sababu Halmashauri wenyewe wana mkakati wa kujenga takribani shule sita mpya za sekondari. Sisi Serikali katika hilo tutawaunga mkono shule hizi, na mara baada ya kukamilishwa kwake tutaweza kuzisajili. Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kubwa vijana wetu ambao wanapata nafasi baada ya kumaliza kidato cha nne waweze kupata nafasi ya kidato cha tano na sita. Kuhusu suala la shule za kule Mlalo, Mheshimiwa Shangazi kama mtakuwa mmeianzisha hii mipango kule Mlalo katika Halmashauri yenu ya Lushoto, naomba nikuhakikishie kwamba Serikali haitosita kushirikiana nanyi. Kwa sababu hata nilipokuwa ziarani kule mlinipeleka shule moja ya 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) sekondari ambayo mmeniambia kwamba watoto wanafaulu kwa kiwango kikubwa sana. Kwa hiyo Serikali itaungana na ninyi, lakini ni mara tu baada ya kuanza michakato hii mliyoianza ya ujenzi wa sekondari za kidato cha tano na sita. Serikali tutaungana na hilo ili kuwafanikisha wananchi wa Mlalo na Wilaya ya Lushoto kwa ujumla ili waweze kupata fursa hii ya elimu ya kidato cha tano na cha sita. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbatia halafu Mheshimiwa Amina. MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Lengo la Nne la Maendeleo Endelevu ya Dunia linasema elimu bora sawa shirikishi kwa wote ifikapo mwaka 2020/2030. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu wanafunzi wamefaulu wengi sana ambao wanatakiwa waende kidato cha tano na hasa Shule za Sayansi; lakini kuna tatizo kubwa la wanafunzi wanakwenda kwenye shule hizo hakuna maabara kabisa. Serikali Awamu ya Nne ilianza hili suala la maabara. Je, nini jukumu la Serikali kwa haraka iwezekanavyo kuhakikisha shule zote za Sayansi zinakuwa na maabara za kisasa ili tujenge Tanzania yenye uwezo wa sayansi na teknolojia? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba wanafunzi wamefaulu wengi sana mwaka huu, ni kama takribani asilimia 27 ya waliofanya mtihani. Na malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ilikuwa kwamba tuwe tunapeleka wanaofaulu hawa wafike asilimia 20, isipungue asilimia 20. Kwa hiyo, utaona kazi nzuri imefanywa na Serikali, lakini nichukue nafasi hii kuwapongeza sana walimu wa nchi hii kwa kazi waliofanya na kusababisha ufaulu huu mkubwa. (Makofi) 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kushughulikia kiasi cha wanafunzi 93,018 ambao wamefaulu kwenda kidato cha tano, tumejipanga vizuri tumepeleka kiasi cha shilingi 22,000,000,000 ili kuhakikisha kwamba tunajenga maabara. Fedha hizi zimekwenda toka kama miezi mitatu iliyopita. Ujenzi unaendelea katika shule zote za A-level na hasa zitakazochukua wanafunzi wa combination za sayansi. Ujenzi huo tunahakika kabla shule hizi hazijaanza kupokea wanafunzi utakuwa umekamilika. Kwa sasa hivi tumetawanya watu kutoka ofisini pale Idara ya Elimu, karibu kila Mkoa tumepeleka maafisa wawili kwenda kuhakikisha kwamba wanasimamia kwa haraka ili shule hizi ziweze kukamilika. Kila shule ambayo tutakuwa tunapeleka wanafunzi zitakuwa na maabara zote zinazostahili. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tumeshachukua hatua, tumepeleka fedha hizo na nipende kumshukuru Mheshimiwa Mbunge, kama kuna shule ambayo ipo katika eneo lako basi mtusaidie Waheshimiwa Wabunge wote, kwa sababu fedha zimepelekwa na ziwe kwenye Halmashauri zetu, tusimamie tuwe karibu tuhakikishe kwamba shule zile zinakamilika kabla ya tarehe moja mwezi wa saba. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Amina. MHE. AMINA S. MOLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. MWENYEKITI: Aah! Mheshimiwa Waziri wa Elimu, nilikuwa sijakuona uko mwisho huku, samahani. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Sambamba na majibu mazuri kabisa yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ningependa pia kumpa taarifa Mheshimiwa James Mbatia kwamba Serikali pia imeshanunua vifaa vya maabara kwa ajili ya shule hizo, kwa hiyo ujenzi utakapokamilika vifaa vipo na wanafunzi watapata vifaa. Nakushukuru. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Tumalize na Mheshimiwa Amina. MHE. AMINA S. MOLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada nzuri zinazofanywa na Serikali za kusambaza vifaa saidizi kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inajenga shule moja ya mfano ambayo itawajumuisha watoto wenye ulemavu pamoja na watoto wengine ambao hawana mahitaji maalum, ili basi shule hiyo iweze kuwasaidia kwa kiwango kikubwa watoto wenye mahitaji maalum? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Elimu. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kutoa taarifa kwenye Bunge lako Tukufu kwamba Serikali inakamilisha mapitio ya michoro kwa ajili ya shule maalum ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali ni kujenga shule ya Kisasa ambayo itakuwa ni ya bweni, shule ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo shule hiyo itajengwa kwenye maeneo ya Chuo cha Ualimu cha Patandi ambacho ni chuo mahususi kwa ajili ya kufundisha walimu wenye mahitaji maalum. Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi huo utaanza mara moja mara baada ya kukamilisha mishoro kwa sababu fedha kwa ajili ya ujenzi zipo. MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swali lake. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 400 Matumizi Mabaya ya Sheria ya Tawala za Mikoa MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Sheria ya Tawala za Mikoa Sura ya 97 inawapa mamlaka ya kipolisi Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwatia nguvuni watu wa muda wa saa 48, lakini sheria hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kutoa amri za kukamata Wabunge, Wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na hata watumishi wa umma wakiwemo
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages181 Page
-
File Size-