Bajeti Ya Wizara Ya Mambo Ya Nje Na

Bajeti Ya Wizara Ya Mambo Ya Nje Na

YALIYOMO YALIYOMO ................................................................................. i ORODHA YA VIFUPISHO .........................................................iii 1.0 UTANGULIZI..................................................................... 1 2.0 MISINGI YA SERA YA TANZANIA KATIKA UHUSIANO WA KIMATAIFA ................................................................ 7 3.0 TATHMINI YA HALI YA UCHUMI, SIASA, ULINZI NA USALAMA DUNIANI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 ......................................................................... 9 3.1 Hali ya Uchumi............................................................... 9 3.2 Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ................................. 10 4.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 ............ 17 Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 .......... 20 Mapato............... ...................................................................... 20 Fedha Zilizoidhinishwa............................................................. 21 Fedha Zilizopokelewa na Kutumika ......................................... 21 4.1 Kusimamia na Kuratibu Masuala ya Uhusiano Baina ya Tanzania na Nchi Nyingine .......................................... 22 4.1.1 Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ......................... 22 4.1.2 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Afrika.................. 23 4.1.3 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Asia na Australasia ................................................................... 31 4.1.4 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Mashariki ya Kati………………. ........................................................ 37 4.1.5 Ushirikiano wa Tanzania na Nchi za Ulaya na Amerika..........................................................…………40 4.2 Kuratibu Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa ...................................................................... 50 4.3 Kufuatilia na Kusimamia Utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa na Hati za Makubaliano ............................... 83 i 4.4 Kuratibu Masuala ya Itifaki, Uwakilishi na Huduma za Kikonseli....................................................................... 87 4.4.1 Ziara za Viongozi wa Kitaifa na Mashirika ya Kikanda na Kimataifa Kutoka Nje ya Nchi ...................................... 87 4.4.2 Ziara za Viongozi wa Kitaifa Nje ya Nchi ..................... 95 4.4.3 Kuanzisha na Kusimamia Huduma za Kikonseli.......... 97 4.5 Uratibu wa Watanzania Wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) .................................................................... 99 4.6 Elimu kwa Umma ....................................................... 100 4.7 Utawala na Maendeleo ya Watumishi........................ 102 4.7.1 Uteuzi wa Viongozi .................................................... 102 4.7.2 Mafunzo ..................................................................... 103 4.7.3 Upandishaji Vyeo ....................................................... 103 4.7.4 Kubadilisha Kada Watumishi ..................................... 104 4.7.5 Uhamisho................................................................... 104 4.8 Kuratibu na Kusimamia Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Wizara na Taasisi Zilizo Chini ya Wizara........................................................................ 104 4.8.1 Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Wizara ........ 104 4.8.2 Utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi Zilizo Chini ya Wizara........................................................................ 105 5.0 CHANGAMOTO ZILIZOPO NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA ..................................................... 112 6.0 SHUKRANI.................................................................... 113 7.0 MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022 ..................................................................... 117 8.0 MALENGO YA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022 .................................. 119 9.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022 ......................... 122 10.0 HITIMISHO.................................................................... 124 ii ORODHA YA VIFUPISHO AfCFTA - African Continental Free Trade Area AfDB - African Development Bank AICC - Arusha International Conference Centre APRM - African Peer Review Mechanism CFR - Centre for Foreign Relations Common Market for Eastern and COMESA - Southern Africa DRC - Democratic Republic of Congo EAC - East African Community EPA - Economic Partnership Agreement km - Kilometa kV - Kilovolt United Nations Multidimensional MINUSCA - Intergrated Stabilization Mission in the Central African Republic United Nations Organization MONUSCO - Stabilization Mission in the Democratic Republic of Congo. iii MW - Megawatt Organisation of African, Carribean and OACPS - Pacific States OSBP - One Stop Border Post Southern African Development SADC - Community TEHAMA - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano United Nations Educational, Scientific UNESCO - and Cultural Organisation United Nations Development UNDP - Programme United Nations Industrial Development UNIDO - Organisation United Nations Interim Force in UNIFIL - Lebanon Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu UVIKO-19 - unaosababishwa na Virusi vya Korona iv 1.0 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo katika Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 na pia lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. 2. Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu siku ya leo. Kwa kuwa Hotuba hii ya Bajeti ni ya kwanza nikiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, napenda kumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuongoza Wizara hii. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa nitafanya kazi kwa uwezo wangu wote na kwa kudra za Mwenyezi Mungu nitatekeleza majukumu yangu ipasavyo katika kuleta maendeleo ya Taifa letu. 1 3. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwamba, tarehe 17 Machi, 2021 Taifa lilipata msiba mzito wa kuondokewa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, tarehe 24 Julai, 2020 tulimpoteza Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na tarehe 17 Februari, 2021 tuliwapoteza Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mheshimiwa Balozi Mhandisi John William Hebert Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Naomba kutumia nafasi hii kuungana na Waheshimiwa Mawaziri wenzangu waliotangulia kuwasilisha Hotuba zao kutoa pole kwa Mheshimiwa Rais, familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla kwa misiba hii mizito. Wizara yangu inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa viongozi hawa katika kukuza taswira ya nchi yetu kimataifa na mahusiano ya kidiplomasia baina yetu na nchi mbalimbali. 4. Mheshimiwa Spika, natumia nafasi hii pia kutoa shukrani za dhati kwa nchi marafiki na jumuiya ya kimataifa kwa kuonesha mshikamano, kutufariji na kushiriki nasi katika kipindi cha majonzi makubwa kwa Taifa letu. 2 5. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba kutoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa uamuzi wake wa kuitisha kikao rasmi cha Baraza Kuu la Umoja huo kwa ajili ya kumuenzi na kumkumbuka Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichofanyika tarehe 16 Aprili, 2021 Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Kupitia kikao hicho, Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa zilielezea mafanikio makubwa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyopatikana chini ya Uongozi wa Hayati Dkt. Magufuli katika kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, maji, afya, nishati na miundombinu ya usafirishaji. Tunawashukuru sana. 6. Mheshimiwa Spika, vilevile, naomba kutoa pole kwako na Bunge lako Tukufu kufuatia vifo vya Waheshimiwa Khatibu Said Haji aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Konde, Zanzibar aliyefariki tarehe 20 Mei, 2021; Mhandisi Atashasta Justus Nditiye aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoa wa Kigoma, aliyefariki tarehe 12 Februari, 2021; na Martha Jachi Umbulla aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, aliyefariki tarehe 21 Januari, 2021. Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu mahala pema peponi. Amina. 3 7. Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa na kwa moyo mkunjufu napenda kutumia nafasi hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, nawapongeza Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), kwa kuaminiwa na kuendelea kushika nafasi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuna imani na uongozi mpya ulioingia madarakani kuendelea kudumisha amani na Muungano wetu, kusukuma mbele gurudumu la maendeleo na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na jumuiya ya kimataifa. 8. Mheshimiwa Spika, nampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mheshimiwa Othman

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    132 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us