Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 29 Juni, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU): Randama ya Makadirio ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge maswali, tunaanza na Ofisi ya Waziri. 1 Na. 99 Halmashauri za Ushetu na Msalala Kuanza Kazi MHE. GODFREY W. ZAMBI (K.n.y. MHE. JAMES D. LEMBELI) aliuliza:- Kati ya Halmashauri tatu katika Wilaya ya Kahama ni Halmashauri moja tu ya Mji wa Kahama ndiyo imepata Hati ya kuanza kazi:- (a) Je, ni lini Halmashauri za Ushetu na Msalala zitaanza rasmi? (b) Kwa kuanzishwa kwa Halmashauri ya Ushetu na Msalala. Je, ni nini hatma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kahama? (c) Je, wapi yatakuwa Makao Makuu ya Halmashauri hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa James Daudi Lembeli, Mbunge wa Kahama, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, taratibu za kuanzisha Halmashauri za Msalala na Ushetu zinafanywa kwa mujibu wa Sheria Na. 7 ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 2 1982 kifungu cha 7 (1- 4) kinachoeleza kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa atatangaza kusudio la kuanzisha Halmashauri katika Gazeti la Serikali na magazeti ya kawaida na atatoa siku sitini (60) kwa wadau kuwasilisha kwa maandishi maoni, ushauri, au pingamizi kuhusiana na uanzishwaji wa Halmashauri hizo. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza tarehe 18 Juni, 2012 wakati najibu swali Na. 25 lililoulizwa na Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige, kwamba Halmashauri za Msalala na Ushetu ni miongoni mwa Halmashauri mpya ambazo zipo katika hatua ya uhakiki wa maeneo ya kijiografia (geographical boundaries) kwa maana ya mgawanyo wa Tarafa, Kata, Vijiji na Vitongoji/Mitaa ili kuweza kutangaza. Hivyo Halmashauri za Msalala na Ushetu zitaanza rasmi sambamba na Halmashauri nyingine mpya zinazotarajiwa kuanzishwa baada ya kukamilika kwa taratibu za uanzishaji wake kwa mujibu wa Sheria. (b) Mheshimiwa Spika, mwaka 2011, Serikali ilitangaza kuigawa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama katika Halmashauri zingine tatu za Msalala, Ushetu na Halmashauri ya Mji wa Kahama. Halmashauri ya Ushetu itajumuisha eneo lote la Jimbo la Uchaguzi la Kahama ukiondoa eneo la Halmashauri ya Mji wa Kahama. Halmashauri ya Msalala inayopendekezwa itajumuisha eneo lote la jimbo la Uchaguzi la Msalala. Kwa maelezo hayo ni dhahiri kuwa baada ya kuanza kwa Halmashauri hizo tatu, hapatakuwapo 3 tena na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, kutakuwepo na Wilaya ya Kahama tu. (c) Mheshimiwa Spika, pamoja na mambo mengine, lengo la Serikali kuzigawa au kuanzishwa Halmashauri mpya ni kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi. Hata hivyo, jukumu la kujua wapi yawepo Makao Makuu ya Halmashauri ni la Uongozi wa Halmashauri husika ukishirikiana na wananchi wake. MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake. Lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza kama ifuatavyo:- Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri anasema Halmashauri za Ushetu na Msalala zitaanza mara baada ya kukamilika taratibu. Sasa naomba kujua hizo taratibu zitakamilika lini maana inawezekana zikawa mwaka mmoja, mwaka mzima hizo taratibu zitakamilika lini ili wana Usheti na Msalala waweze kupata huduma kama alivyosema Waziri tunataka tuwasogezee huduma hizo. Mheshimiwa Spika, suala la pili kwa sababu tuna Halmashauri pia nyingi sana katika nchi za miji midogo ambazo zimeanza nyingine miaka minne mitano ikiwepo Halmashauri ya Mji Mdogo wa Vwawa kule Mbozi. Je, hiyo Halmashauri yenyewe itaanza lini sambamba na Halmashauri zingine ambazo ziko katika hatua ya Miji Midogo? 4 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, hizi Halmashauri ninazozingumza hapa pamoja na zile nyingine ambazo zinazungumzwa haziwezi kuanza bila ya kupitia kwenye huu mchakato ninaouzungumza hapa. Juzi nilijibu hapa na naomba nirudie na kusema hapa sasa hivi tunayo timu ambayo imeundwa pale TAMISEMI ambayo inazunguka katika maeneo yote mapya ambayo yanakusudiwa kuanzishwa. Nia na shabaha ya mpango ule ni kufananisha yale yaliyoandikwa katika makaratasi ambayo yamekuja kama mapendekezo na hali halisi iliyoko pale kwenye ground. Mheshimiwa Spika, kuanzisha Halmashauri hapo unaanzisha kwa ajili ya watu na watu ni lazima waseme sisi tuko tayari Halmashauri hii ianze na lazima useme vijiji vitakavyoingia mle ni hivi. Useme mitaa itakayoingia mle ni hii, Tarafa zinazoingia mle ni hizi na Kata zinazoingia mle ni hizi na wote waafiki waseme kwamba naam barabara!!! Atatangaza Waziri mwenye dhamana ataweka kwenye ukuta, atawapa siku 60 waseme kama wanataka kuanzisha Halmashauri hizo au hawataki. Mheshimiwa Spika, ndiyo maana inaniwia vigumu, lakini nataka niseme hapa kama mlivyosikia katika hotuba zote Waziri wa Nchi atakaposimama hapa na Waziri Mkuu ataeleza hili la mchakato unaendelea hapa. Habari ya Kahama au Ushetu pamoja na Msalala wala hakuna debate tena. Kwa sababu ni 5 jambo ambalo linajulikana kwamba tunaanza, lakini kwa kuzingatia hili ninalosema. Mheshimiwa Spika, sasa anazungumzia habari ya Vwawa. Vwawa nimefika pale naifahamu. Nilieleza juzi nilipokuwa nazungumza habari ya Itigi na wale wengine. Tunachowaomba Waheshimiwa Wabunge wote ambao mmeomba muwe na Mamlaka za Mji Mdogo wote kabisa na kina Lwanji ahakikisheni kwamba mnatuletea. Juzi nimekwenda kutafuta Mheshimiwa Godfrey Zambi tukakuta kwamba kweli wanakiri Mkoa wa Mbeya pamoja na wale wengine wote kwamba zile documents hazikufika zimefika ofisini kwetu. Kwa hiyo, nawaomba sana wote hata wewe Mheshimiwa Spika kama una mji wako mdogo unataka kuanzisha wewe tuletee hizo takwimu hapa. SPIKA: Mimi nina mji mkubwa lakini hamjui kama kuna vijiji 44. Ndiyo hilo tu. MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nilikuwa naomba niulize swali moja dogo la nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa kuwa baadhi ya Halmashauri hapa nchini ambazo zimetangazwa na Serikali kwamba ziweze kuanza nyingi baadhi zimeshakamilisha vigezo vyake kama Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Kwa kuwa katika majibu yako ya msingi umeeleza kwamba itabidi 6 kuweza kusubiri Halmashauri zote ambazo zimeanzishwa ziweze kukidhi vigezo. Je, hatuoni kwamba ni kuwachelewesha maeneo mengine ili suala zima la kusogeza huduma kwa wananchi kutokana na kutokuanzishwa Halmashauri ambazo tayari zimeshakidhi vigezo, Serikali inatoa kauli gani? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, hii Halmashauri ya Kasulu, Masasi, Nzega, Handeni wala tusizungumzie, yaani nawaambia kabisa tusizungumze kwa sababu hizo najua kabisa kwamba zinakuja, hizi zilishakuwa zimetamkwa kutoka kule nyuma. Ninachosema hapa kama kuna watu ambao tunawasema hivyo tunavyosema halafu watachelewa hawakuleta treni imepita, itakuwa imekwenda. Mheshimiwa Spika, nina hakika hataweza kusema kwamba mimi naanzisha hapa kama hatujajiridhisha hapa kwamba hivi tunavyosemwa na wananchi wameridhika na jambo hilo linalosemwa. Hii itatuondolea migogoro ambayo tunayo katika Tanzania ya mahali unaanzisha maeneo ya utawala kesho unakuta watu wanalalamika kusema kwamba sivyo. Nataka nikuthibitishie kwamba sisi hapa tumeshaeleza na kwamba tunawasiliana kwa karibu sana na Halmashauri zote hii ni pamoja na zile Halmashauri 19 ambazo zitaanzishwa baadaye. 7 Kwa sasa hivi Mheshimiwa Rais alichofanya ameanzisha Wilaya na ameteua Wakuu wa Wilaya na Mikoa mipya ili wasaidie kusimamia mchakato huu tunaozungumza hapa. Kwa hiyo unaweza ukaiona kabisa dhahiri nia ya Serikali ya kutaka kufanya kazi hii lakini kwa kufuata taratibu hizi ambazo nimesema hapa za kisheria. SPIKA: Ahsante hili suala limejibiwa sana sana. Na. 100 Barabara Toka Ihumwa – Chuo Kikuu Hombolo MHE. DKT. DAVID M. MALLOLE aliuliza:- Mji wa Dodoma unakua kwa kasi sana na uwepo wa Vyuo Vikuu hivyo inalazimu miundombinu ya barabara iwekwe vizuri ili kufikia Vyuo hivyo kwa urahisi:- Je, Serikali ina mikakati gani ya kuweka lami kwenye kipande cha barabara inayotoka Ihumwa hadi Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo? NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa David Mciwa Mallole, Mbunge wa Dodoma Mjini, kama ifuatavyo:- 8 Mheshimiwa Spika, barabara ya Ihumwa – Hombolo ni sehemu ya barabara ya Ihumwa-Hombolo- Gawaye-Mayamaya yenye jumla ya urefu wa kilometa 55.75. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo, Serikali ilipandisha hadhi mwaka 2009 kuwa barabara ya Mkoa. Katika mwaka wa fedha 2010/2011, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Mkoa wa Dodoma, iliifanyia matengenezo ya kawaida, muda maalum pamoja na matengenezo ya madaraja barabara hiyo yenye gharama ya jumla ya shilingi 58,632,150.00. Pia katika mwaka wa fedha 2011/2012, barabara hiyo imefanyiwa matengenezo ya kawaida, muda maalum pamoja na matengenezo ya madaraja yenye gharama ya jumla 122,632,440.00. Hali kadhalika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, jumla ya shillingi 269,190,000.00, zimeombwa ili kuifanyia matengenezo ya aina hiyo kwa mwaka unaofuata. Mheshimiwa Spika, kutokana na ufinyu
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages716 Page
-
File Size-