Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Saba – Tarehe 18 AprilI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. PEREIRA AME SILIMA) Taarifa ya mwaka na hesabu za Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwa mwaka 2009/2010 [The Annual Report and Accounts of the Institute of Finance Management for the year 2009/2010]. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIITAA (TAMISEMI): Taarifa ya Matoleo yote ya Gazeti la Serikali Pamoja na Nyongeza zake Yaliyochapishwa tangu Kikao cha mwisho cha Mkutano wa Bunge uliopita. MASWALI NA MAJIBU Na. 82 Mgogoro wa Viwanja-Wananchi wa Manispaa ya Bukoba MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Uko mgogoro mkubwa wa viwanja kati ya wananchi na Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ambapo wananchi zaidi ya 800 walilipa fedha zao ili wapatiwe viwanja tangu mwaka 2002 na sasa ni miaka kumi imepita hawajapatiwa viwanja hivyo na Halmashauri hiyo haionyeshi juhudi za kutoa viwanja badala yake wananchi hao wanaambiwa kulipia gharama zaidi za wakati huu:- Je, Serikali inatoa kauli gani kwa Halmashauri hiyo ili iweze kuwapatia wananchi hao haki yao ya kupata viwanja hivyo walivyokwishalipia tangu mwanzo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba upo mgogoro uliojitokeza katika baadhi ya wananchi waliochangia fedha zao kutopatiwa viwanja katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Mwaka 1996 Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ilipitisha Azimio kuwa wananchi wanaohitaji viwanja katika eneo la Kyabitembe kwa ajili ya makazi, biashara na huduma za jamii wachangie gharama za upimaji ambazo zilikuwa ni shilingi 50,000/- kwa high density , shilingingi 60,000/- kwa medium density na shilingi 70,000/- kwa low density . Maeneo ya taasisi yalichangiwa shilingi 100,000/- hadi 200,000/-. Baada ya upimaji wananchi wote walipatiwa viwanja na hapakuwa na mgogoro. Mheshimiwa Naibu Spika, zoezi la uchangiaji liliendelea mwaka 2003, 2004, na 2005 katika maeneo ya Kyabitembe II , Rwazi/Rwome, Kiteyagwa na Kibuye ambapo jumla ya shilingi 58,562,600/= zilichangwa na wananchi 1,049. Hata hivyo, eneo pekee ambalo viwanja vilipimwa ni Kyabitembe II sawa na viwanja 476. Eneo hili halikuwa na makazi ya watu lakini walijitokeza wananchi na kudai maeneo hayo wanayamiliki kimila hivyo walitaka kulipwa fidia kwanza ndipo upimaji uweze kufanyika. Halmashauri ilisitisha upimaji na hivyo kuzua mgogoro na wananchi hao wakidai fedha walizochangia jumla ya shilingi 58,562,600/= Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba imeingia ubia na shirika la dhamana na uwekezaji Tanzania (UTT) na kupatiwa shilingi bilioni 2.9 kwa ajili ya kupima viwanja 5000 ambavyo vitauzwa kwa wananchi wote. Hii ni sehemu ya mkakati wa Serikali kutatua mgogoro kati ya wananchi waliochanga fedha zao na Halmashauri. Azimio limetolewa na Halmashauri kupitia Kamati ya Fedha , Uongozi na Mipango iliyokaa tarehe 16/11/2011 na Baraza la Madiwani lililokaa tarehe 16/4/2012 kwamba wananchi wote waliochangia fedha lakini hawakupata viwanja, wauziwe viwanja kwa bei ya punguzo sawa na fedha zilizochangwa kwa wakati huo na kwa thamani ya sasa. Aidha, watakaoshindwa kulipa warudishiwe fedha zao kwa thamani ya sasa. Vikao hivyo vimepitisha Azimio kuwa ili kupata thamani ya sasa ya fedha zilizochangwa kwa wakati huo riba ya asilia tano itawekwa kila mwaka kuanzia kwenye mwaka waliochangia hadi sasa. (Makofi) MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimepokea majibu ya swali langu kutoka kwa Waziri. Kwanza napenda kusema kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba imewatapeli wananchi wa Manispaa hiyo, siyo kuwatapeli tu, lakini pia inaendeleza kufanya dhuluma kutokana na majibu niliyoyapata hapa. Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumwuliza Waziri, si kweli kwamba wananchi wa Manispaa ya Bukoba walichangia upimaji, ukifuatilia fomu zilizojazwa kutokana na fedha walizochanga zinaonesha wazi wazi kwamba yalikuwa ni maombi ya viwanja, ninashangaa kwa miaka kumi wananchi wamekuwa wakidai viwanja vyao na mpaka sasa hawapatiwi, naomba Waziri kwa sababu jambo hili nilishakueleza hata wakati unafanya majumuisho ya ziara yako utamke utawasaidiaje wananchi wapate viwanja vyao. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, ukitazama mkataba ulioingiwa na Manispaa kutokana na mkopo walioupata kutoka UTT ni mkopo wa kibiashara, huwezi ukauza viwanja 5000 chini ya milioni sita ili kulipa deni. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa sasa swali? MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Naibu Spika swali, wananchi wale watalipwaje asilimia tano ambayo kwa mtu aliyelipa elfu arobaini ni elfu ishirini kwa miaka kumi, utawasaidiaje wananchi hawa waweze kupata fedha zao kama hawakupata viwanja kwa thamani ya sasa na kwa riba inayoendana na biashara kwa sababu Halmashauri inaonekana wanafanya biashara. NAIBU SPIKA: Ahsante umeshaeleweka, Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwa ufupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika, mimi Bukoba nimekwenda na hili jambo analozungumza Mheshimiwa Mbunge ninalifahamu. Nilikwenda kule kwa sababu ya boti ambalo lilileta maneno na yeye ndiye alileta jambo hili hapa, tukaenda nalo kama tulivyokwenda na wala sitaki nimpuuze Mbunge hapa kwa jambo analozungumza. Ametaka tusaidie Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ili iondoke katika tatizo hili na ninamwomba Mbunge anisikilize vizuri. Mheshimiwa Naibu Spika, hili jambo limekuwa mis- handled miaka kumi iliyopita, hata ukiwatafuta hawa waliohusika wengine hawapo, Halmashauri ikafika mahali ikaachana na hilo eneo moja kwa moja, wakafika mahali wakapata viwanja elfu tano ili kweza kupima hivyo viwanja elfu tano wakaomba mkopo kutoka UTT wa bilioni mbili na point tisa (bil. 2.9) wakapata. Wamekwenda kupima viwanja elfu tano. Anachozungumza hapa anasema miaka kumi iliyopita mtu alilipa shilingi elfu hamsini na mimi nikasema ni kweli, sasa elfu hamsini iliyolipwa tukaulizana kwamba shilingi elfu hamsini kwa leo ni sawa na shilingi ngapi ili anapokwenda kuchukua kile kiwanja apate punguzo la kiasi hicho ili aweze kupata kiwanja. Mheshimiwa Conchesta, dada yangu anasema kwamba twende tukawape wananchi wale viwanja vile bure, swali tunawapa bure na huu mkopo uliochukuliwa unakwenda kulipwa na nani? Wamekutana juzi tarehe 16 tumetoa maelekezo kama Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa tukawaambia wakae watuondoe hapo tuliposema. It is my judgment kama Deputy Minister ninayefanya kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba kama mkikataa jambo hili hamtaondoka katika mgogoro ule itakuwa ni vurugu, namna pekee ya kuondoka katika jambo lile ni kukubali sasa wananchi wale waseme kwamba mimi kama sitaki kiwanja bei itakuwa ni kubwa nirudishieni hela zangu kwa thamani ya sasa. Mheshimiwa Naibu Spika, sauti hii ni msisitizo tu mzee wangu wala siyo ugomvi hapa. Lakini mimi nataka niisaidie Serikali nimezungumza na Kagasheki Mbunge wao, nimezungumza mimi na Mkurugenzi Mtendaji, nimezungumza na baadhi ya wale waliopo kule na wote wanaona kwamba hii ndiyo njia pekee ambayo itatuondoa katika jambo hili. (Kicheko ) Mheshimiwa Naibu Spika, ninakuomba Conchesta Dada yangu toa msaada shirikiana na Halmashauri yako nenda sasa ukazungumze na wananchi wapewe viwanja vile wavichukue, hakuna namna nyingine ya kisayansi ya kuondoka katika tatizo hili bila kufanya kama nilivyosema. ( Makofi ). MHE. OMARY A. BADWEL: Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa miji mipya imeendelea kukumbwa na migogoro ya viwanja ikiwemo Mji wa Bahi na wananchi wa Bahi tayari walishamwandikia barua Waziri Mkuu kutaka awasaidie kutatua mgogoro uliopo baina yao na Halmashauri yao juu ya viwanja pale Mji wa Bahi. Je, ofisi ya Waziri Mkuu sasa inatoa tamko gani kusaidia mara moja Halmashauri ya Bahi imalize mgogoro wa viwanja wao na wananchi wa Bahi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri tena Bahi nimekwenda na nimekaa na wananchi na hao wananchi wamekuja mpaka ofisini. Mheshimiwa Badwel alikuwa kabla ya kuja hapa alikuwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Wameshindana kule wakaja ofisini, tukaketi nao. Wale wananchi wakaja pale nikawaambia maandamano hapa sitaki, lakini tukaelewana. Nikawapa mimi watu wangu wamekwenda nao kule wameshindana mimi kiwanja changu kilikuwa hiki, mimi nilitaka nipewe hiki, eneo nililokuwa nakaa ni hili nilitaka nipewe hili, tukafika mahali mpaka nikamwambia Mkurugenzi kwamba jambo hili liishe. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nilishasema hapa Serikali haitapuuza mawazo ya Wabunge, kama Mheshimiwa Badwel anasema bado tatizo hili lipo saa saba nitakaporudi ofisini kwa kibali cha Waziri wangu Mheshimiwa Mkuchika nitawaita Halmashauri waje tena pale ofisini, na Mheshimiwa Badwel saa saba kamili tukutane pale ofisini halafu tumalize jambo hili. NAIBU SPIKA: Ahsante sana, bado tupo Wizara hiyo hiyo tunaelekea Singida swali la Mheshimiwa Mohamed Gulam Dewji. Na. 83 Ukarabati wa Majengo ya Sekondari ya Mwenge MHE. DIANA M. CHILOLO (K.n.y. MHE. MOHAMED G. DEWJI) aliuliza:- Shule ya Sekondari ya Mwenge ni miongoni mwa shule
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages277 Page
-
File Size-